Goli la Simba dhidi ya Azam ASFC 2021

Goli la Simba dhidi ya Azam ASFC 2021

Sio kwamba unamuogopa mnyama
😀😀😀
Mimi napenda ladha ya soccer kwa mshindi anayeshinda vizuri na kila mmoja anaridhika. Mshindi na aliyeshindwa.

Ujanja ujanja na ghiriba .....
 
Mkuu yanafungwa sana lakini marefa huwa hawafanyi distraction.... ikitokea anapiga filimbi ku align
Iangalie vizuri clip iliyotupiwa kwenye uzi huu. Hii clip ni ya mechi nyingi. Kuna mechi moja wachezaji walikuwa wanamzonga mwamuzi na free kik ikapigwa refa akakubali goli na mpira ukawekwa kati. Kuna nyingine golikipa alikuwa ameegemea goli ili aanze kuwapanga wachezaji wake na fasta free kik ikapigwa akabaki ameegemea goli wakati nyavu zinatikisika!!
 
😀😀😀
Mimi napenda ladha ya soccer kwa mshindi anayeshinda vizuri na kila mmoja anaridhika. Mshindi na aliyeshindwa.

Ujanja ujanja na ghiriba .....

IMG-20210626-WA0060.jpg
 
Kwanini mpira

1. Ukimgonga referii unarudi kwake aukabidhi kwa wahusika

2. Kwanini mchezaji akiwa offside japo hajagusa mpira lakini kama kamcheza kipa kwa maana moja ama nyingine inaitwa distraction

Tunaongelea refarii kuwacheza Azam yaani distraction
Refa ndo aliwafuata wachezaji wa wa Azam au wao ndio wakimfuata refa?
Labda tuangalie na sheria 17 zinasemaje
 
😀😀😀
Mimi napenda ladha ya soccer kwa mshindi anayeshinda vizuri na kila mmoja anaridhika. Mshindi na aliyeshindwa.

Ujanja ujanja na ghiriba .....
Kwenye football kitu kama hicho ni ngumu, pamoja na VAR, goal line technology, marefa watano
 
Lile bao hakuna kosa kwa upande wa Simba wala Mwamuzi, ni akili kubwa ya Wachezaji wa Simba kwenye hatua kama zile

Rejea Simba dhidi ya Nkana kwenye Klabu bingwa Afrika, move ya faulo ilikuwa kama ile, Wachezaji wa Nkana walipoteza concentration, Simba wakawahi kuweka (Quick thinking)

Azam au Mtu yoyote ambaye ni Mwanasoka ajue inapotokea faulo yoyote lazima kwanza ukazibe mpira, zibeni mpira huku wengine wanaongea na Mwamuzi

Wenzetu Ulaya ile mali hata akichezewa faulo anawahi kuidaka kwanza ikae eneo lake, wengine kwenye ukuta na wengine wanakaa karibu na mpira

Sasa Azam wengine wapo kwa Mwamuzi na wengine wanajipanga, wakaacha mpira kwa Simba, ni akili ya haraka Simba wakaitumia kufunga lile bao, hizo ndio akili za Wazoefu

Kilichotokea ni kuendelea kujifunza, kukomaa na kujua nini kinahitajika kwa wakati ganiView attachment 1830891

Mpe credit Jr.Farhanjr,umeicopy kwa page yake ukaileta kama ilivyo na ukamute kutoa credit,unless uwe ni wewe ndiyo mwenye Original post kule IG [emoji3][emoji3]
 
Mpe credit Jr.Farhanjr,umeicopy kwa page yake ukaileta kama ilivyo na ukamute kutoa credit,unless uwe ni wewe ndiyo mwenye Original post kule IG [emoji3][emoji3]
Huyo mwenyewe uliemtaja ka-copy.
Original author ni Kumwembe.
 
1. Sasa refarii alikuwa anajadili nini nawachezaji?

2. Kujadiliana na wakinga ukuta tuseme refarii kachangia kuwahujum?

3. Kwanini refa aingilie nakuwapa maelezo azam.... alitaka wapange ukuta? Alitaka wasogee nyuma?

Please
 
Faulo ilipulizwa.Maana yake mchezo umesimama.

Ili mchezo uendelee lazima refarii aruhusu tena.


Mazingira yale ya mpira hata kama ni kwiki thinking'i siyo sahihi.

Ingekuwa refarii haongei na mtu sawa.

Ila mchezaji mmojawapo wa Azam yupo na refarii,wanaongea.

Hata kama kanuni zinaruhusu jambo hili siyo sahihi.

Kipyenga kipulizwe.

Pale ni karibu na goli,ukuta uwekwe

Wenye faida na pigo wapige mpira.

Mazingira ya namna ile yanatengeneza maamuzi yasiyo sahihi kwa waamuzi,wengine wanaweza kuzuia ile 'move' ya mpira na kuamuru upigwe tena.

Wengine wakaacha lililoanza liendelee.Yaani tunaruhusu maamuzi ya 'utashi' badala ya maamuzi ya sheria.
 
Back
Top Bottom