GPA ya 5 - Anazurura mtaani; we are not serious!

Leo nilikua namwambia kijana wangu kwamba.

Shule itampa maarifa, lakini kusoma hakumpi guarantee ya kufanikiwa.

Lakini nilimwambia kwamba.

Akishaipata elimu, atakua namaarifa. Ili afanikiwe anapaswa kuwa mwenye bidii na nidhamu
Kupata maarifa napo ni kufanikiwa ndugu.
 
Kwa mtazamo wangu tumechelewa kujua umuhimu wa pass za juu katika kupaisha Taifa kiuchumi nk

Hivi inakuwaje mwanafunzi amemaliza Chuo amepata GPA ya 4.8 au kwa wenzetu wa Arts wanapata hadi GPA 5 naye yupo mtaani hana ajira?
Shida sio GPA, siku hizi waajiri wanaangalia vitu vingi. Mnaweza mkaenda kuomba kazi watu wawili wenye madaraja tofauti, akachukuliwa mwenye daraja la chini na yule wa daraja la juu akaachwa. Na sehemu zingine ukienda, huulizwi hata hivyo vyeti unafanyiwa interview tu na kuanza kazi. Vyeti siku hizi havina ishu sana, kiutendaji mtu wa second class anaweza akawa better zaidi ya mtu aliyepata first class ndio mana siku hizi wanaangalia criteria nyingi ukiachana na hayo mambo ya vyeti
 
Kama ni hivi supp zifutwe tu
 
Mtaani elimu ya veta Ina thamani kuliko ya chuo kikuu
I think you are too theoretical as well,fanya uchunguzi kidogo tembelea hata gereji chache na maeneo ya site hao watu wa VETA wa siku hizi ni weupe kuliko unavodhani....
 
I think you are too theoretical as well,fanya uchunguzi kidogo tembelea hata gereji chache na maeneo ya site hao watu wa VETA wa siku hizi ni weupe kuliko unavodhani....
Lakini angalau bora waanze na theoretical then awawezi pata shida kwenye practical
 
Binafsi toka nizaliwe sijawahisikia gpa ya5points ya juu kabisa nliwahisikia ni 4.8
 
Hizo GPA ya 5 mnapataje Nyie vitoto vya sasa? Unajua maana ya GPA 5 Points.

Maskini Tanzania! Ni ya chuo gani hiyo GPA?
Namfahamu rafiki angu UDSM certificate alitoka with distinction about 4.7 ila hakuwa na connection angesoma degree direct. Akaenda OUT LLB akapiga GPA ya Tano na hakupewa tuzo ya mwanafunzi bora. Dizzle anatafuta pesa yupo mtaani since 2018,aende law school ila he is seriously and tallented
 
Lazima tutofautishe MTU aliyesoma full time na OUT
 
Lazima tutofautishe MTU aliyesoma full time na OUT
OUT anashida gani? Anajisomesha mwenyewe ka kuku wa kienyeji. Hangiii na act kwenye mtihani by that time... hana course work kwamba itamuongezea alama... hamjui lecture kwamba atamuhonga
 
Na wew unamuacha aendelee kuzurura?? You are not siriazi
 
😂😂😂Binadam bhan
 
OUT anashida gani? Anajisomesha mwenyewe ka kuku wa kienyeji. Hangiii na act kwenye mtihani by that time... hana course work kwamba itamuongezea alama... hamjui lecture kwamba atamuhonga
Thubutuu. Eti kuku wa kienyeji
 
Aliesoma sio wa kumdharau ipo siku yake tu naamini kabisa ndugu
 
Kwa mtazamo wangu tumechelewa kujua umuhimu wa pass za juu katika kupaisha Taifa kiuchumi nk

Hivi inakuwaje mwanafunzi amemaliza Chuo amepata GPA ya 4.8 au kwa wenzetu wa Arts wanapata hadi GPA 5 naye yupo mtaani hana ajira?
Ajira za Wahadhiri kila siku zinatangazwa kwanini haombi?? Hata leo ukiingia kwenye website ya Sekretarieti ya ajira utaona matangazo ya nafasi za Wahadhiri.

Au yeye ndo hayupo serious na kuomba kazi?
 
4.7 LLB NA LLM ? HUELEWEKI. HAKUNA GPA ZA 5 MASOMO YA ARTS UDSM KASOME PS TUKUONE
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…