GPSA: Tuhuma za ufisadi, matumizi mabaya ya madaraka na mengineyo

Ndugu zangu Wa GPSA msilie sana, mataasis ya umma mengi yameoza na hayana tija, tatizo kubwa ni mifumo mibovu ya serikali kutazama mienendo ya taasis zake kuanzia utendaji mpk nidhamu.

Hata vyombo ambavyo vingeisaidia serikali kama Takukuru na CAG nao wananunulika. Mi nimeshamuachia Mungu, hakuna marefu yasiyo na ncha
 
Basi nikajua hii taasisi ina mahela kumbe hamna kitu?
Poleni aisee
Mkuu hiyo taasisi ina pesa nyingi tangu zamani na mpaka sasa. Kwenye kunufaika watu wanaanza wakubwa wa vitengo, hawa wa kawaida mpaka awe na connection au anajua kutumia mianya ya kula(gap).

Ukiwa mfanyakazi wa kawaida kwa hapo na hujui mifumo wala magepu lazima upauke.
Kwa sasa Gpsa imepiga hatua kiutendaji, hiyo mianya naamini ipo sana kwa sababu ya kutokuwepo sheria za kuwabana wakuu na uhaba wa watalaamu baadhi ya idara.

Ushauri kwa majukumu ya Gpsa inabidi nafasi kama za wakurugenzi wasiteuliwe, iwe inatangazwa mtu mwenye vigezo aombe na akipata apewe dira na malengo ya taasisi. Akishindwa kufikia basi atakuwa hastaili na itasaidia kupata watu wataoleta mabadiliko na ufanisi mkubwa wa taasisi.
 
CEO wa sasa hivi sil alikuwa mwalimu wa mzumbe university amesoma phd yake Sua
CEO wa
 
CEO mpya anachapa kazi na kuwanyoosha mpaka mnaweweseka. Sehemu yoyote akija CEO mpya mchapakazi na kuparekebisha wazee wa mirija lazima wachachawe ndio kinachotokea hapa



Sent using Jamii Forums mobile app
 
Waswahili sisi ni wabobezi wa fitina na majungu, kuna mtu anatafutwa, mtujuze mkifanikiwa, acheni roho mbaya, si mna vikao vya wafanyakazi na mnayo Board of Directors, pelekeni huko malalamiko yenu, shubamit
Sio rahisi kihivyo, labda uwe umejitoa muhanga sana. Na system iliopo kwa maandishi ya humu ni ya kulindana ndani kwa ndani kwa baadhi ya watu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Usinihusishe na upuuzi wa kijinga mkuu, mimi nimesema kile nilichokishuhudia pale kipindi nikiwepo tena hata huyu CEO alikuwa hayupo alikuwa Mwambega kipindi hicho, acha kutetea vitu kwa mambo ya kipumbavu..labda kama umeguswa
mpaka naondoka mimi meneja wangu wa mkoa alifukuzwa kazi kwa ajili ya ufisadi, alihamisha mapato ya taasisi kuwa fedha zake binafsi.
 
CEO mpya anachapa kazi na kuwanyoosha mpaka mnaweweseka. Sehemu yoyote akija CEO mpya mchapakazi na kuparekebisha wazee wa mirija lazima wachachawe ndio kinachotokea hapa



Sent using Jamii Forums mobile app
Unajibu kirahisi sana mkuu, madai yaliyoleta hapa ni makubwa nashauri vyombo vya usalama vipite pale ili kama hawa walioleta madai nao walihusika ila mianya yao imezibwa, kwa uchunguzi wao watajua na hatua stahiki zichukuliwe...
Tusifiche maovu kwa kutetea pasipo na maana
 

Twende Taratibu Mkuu acha Ukali, kila mtu akihoji mnasema ameguswa. Nauliza hivi

Mbona kuna ID ya mwenzako hapo imesema huyo Mwambegu sijui alikua na yy Fisadi japo kastaafu? Na ww si ulikuwepo kipindi hiko hiko haukuona Madudu yake? Meneja anafukuzwa huyo Mzee alibaki vp?

Na wewe unahusika uchunguzwe
 
Kuna ID hapo kama tatu hii nahisi ni za mtu huyo huyo mmoja amefungua mpya ili kuongezea uzito wa hoja yake ionekane wengi wanaujua ubaya wa GIPUSA!
ndugu yangu, humu sidhani kama kuna watu wanajuana, watu wameleta malalamiko.. unataka kuyafunika kwa maneno mepesi yasiyo na msingi
 
wewe jamaa umenifanya nicheke, mimi nilikuwa na maamuzi gani mbele ya CEO wangu? ndio, nakubaliana na wewe na mimi pia nichunguzwe kama nahusika ni vema nikapata haki yangu sahihi
 
aiseeee wahusika fanyieni kazi hizi taarifa ipasavyo!hatuhitaji watu wajione wao ndiyo kilakitu kwenye mali ya uma.
 
Mkuu hiyo ofisi haina hela sasa hasira ni za nn mdogo angu yupo hapo makao makuu na anasaka uhamisho aende popote lkn sio gpsa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nlishawahi kufuatwa na jamaa flani back in 2008, alipewa connection na shemeji yangu, nikamvutia waya dingi Mjeda akaniambi "NISITHUBUTU KUSIKIA UMEINGIA HUKO, SOMETIMES MAISHA YA HUKO NI UTUMWA INATEGEMEA NA KITENGO, KAMA ULIKATAA JESHI PAMBANA HUKOHUKO URAIANI"
 
jakatugu utetezi wako unasubiriwa huku
 
Hivi PPRA na GPSA wanafanya kazi tofauti?
 
Mkuu jakatugu sijaona uhuni wowote na wewe kama kiongozi haufai kabsa. Eti ni wivu kwa kukosa UCEO. SERIOUSLY.
Boss hii ukichomoka, we jembe .

Sent using myLG leon
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…