GPSA: Tuhuma za ufisadi, matumizi mabaya ya madaraka na mengineyo

Waswahili sisi ni wabobezi wa fitina na majungu, kuna mtu anatafutwa, mtujuze mkifanikiwa, acheni roho mbaya, si mna vikao vya wafanyakazi na mnayo Board of Directors, pelekeni huko malalamiko yenu, shubamit
 
Hao watu ambao maslahi yao yanaguswa ni akina nani mzee jakatugu ?
 

Nakupongeza sana lili kwa kukubali kwamba ni wewe ndie ulienunua gari hilo, na ukaiachia wakala chamgamoto na mgogoro mkubwa ambao unaonakana ulichukua muda sana mpaka kukamilishwa swala hili.

Nashauri ungeachia mamlaka iliyopo kuchukua hatua kwa mujibu na pia tuendelee kutimiza wajibu wetu huko tulipo bila badala ya kuendelea kuvuruga taasisi na viongozi waliopelekwa na mamlaka. Tuwaache watimize wajibu wao badala ya kuendelea kuvuruga kwa kukosa nafasi ambayo tulikuwa tuna matarajio makubwa nayo
 
Hapa utabaki kuhisi tu kwa hoja nyepesi, Mimi na wewe hatujuani kabisa na naamini asilimia zote hatujawahi kuonana...

Mtahisi kila mtu ambaye aliwahi kukwamisha madili yenu.. Ila ukweli usemwe uchunguzi huru ufanyike wahusika wachukuliwe hatua kunusuru taasisi, wawe wamestaafu, wawe wako kazini, niwe Mimi sheria ifuatwe mkondo.

Na kwa vile mwenyewe unakili Kuna mkono wa upigaji kwenye ununuzi wa hili gari na wewe ulikuwepo TAKUKURU fanyeni kazi yenu wahusika wote wapate haki.

Hawa ndio wanaompa kazi ngumu raisi kuongoza hi nchi
 
Mkuu jakatugu mbona Kama unaniunganisha na mimi, wakati hata Tz sipo mimi nimeuliza tu.

Kama unakubali hii scandal ya gari ni kweli basi naweza kuamini kwamba hata mengine yana ukweli.. TAKUKURU msaidieni raisi wetu mpenda nchi na mzalendo.

Hapa mmepewa taarifa zote jamani mnangoja nini?
Yaani Mimi nikisikia mtu anaibia nchi yake najisikia vibaya, huku nchi za wenzetu nilipo ni aibu mtumishi au raia kuibia nchi yake akifanya hivo anaweza kujiua mwenyewe kwa sonona tu hata kabla hajajulikana.

Huko watumishi mnalipwa mishahara mikubwa na tena mnaifisadi.. kiukweli kiasi kinachokusanywa serikalini ni kidogo kuliko kinachoingia mifukoni mwa watu maana kila mtumishi ni mpigaji...

Nakuhurumia sana raisi wangu magufuli una kazi kubwa kuwaongoza watanzania waliozoea wizi
 
Waswahili sisi ni wabobezi wa fitina na majungu, kuna mtu anatafutwa, mtujuze mkifanikiwa, acheni roho mbaya, si mna vikao vya wafanyakazi na mnayo Board of Directors, pelekeni huko malalamiko yenu, shubamit
Naona alichokifanya ni sahihi kuleta hapa, kwenye hizo board Kuna kuundiana fitna na wanaweza wakafunika kombe ..Hapa Hadi magufuli mwenyewe zinaweza kumfikia
 

Mkuu sijakuunganisha, ila hao watu waliohamishwa nasi kwakuwa walikuwa wanafanya biashara na wahuni wa pembeni ndio wanaleta majungu humu. Baddhi yao walitarajia wangepewa nafasi ya juu ya taasisi ndio tatizo hilo kiongozi


Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Sawa mkuu, uchunguzi ufanyike wajulikane wakamwate....fisadi ni mtu mbaya sana katika nchi

Na wewe mkuu inaonekana ulikuwa unasapoti wizi, kwa nini hukuwaripoti mapema ukaacha wanaifilisi taasisi?
 
tulia hivyo hivyo,lazima uingie jela. Mnafikiri hiyo ofisi ni yenu?
 

Kwani MSD ina Management nzuri. ? Kuna madudu mengi sana. Mkurugenzi wa MSD ni mwanasiasa mzuri anajua kuji politics, lakini je Mahospitali kuna dawa? Ukitaka kujua Management ya MSD waulize wakurugenzi wa Hospitals na vituo vya Afya.

Watu wanalipa hela na wanasubiri mwaka na dawa hazifîki na ikifika unakuta kuna shida ya specification.

Kifupi taasisi za Umma zina shida. Na Magufuli mwenyewe hawezi hata kama alitaka kuweza maana hana Contract performance na hawa ma DG wake na kama anazo basi hakuna sheria msumeno itayowatia hofu hawa watu .

Wangeweka sheria DG yeyote akiingia Kwenye kashfa ya Rushwa au akishindwa kazi anakwenda Jela for sure na account zake zote zinakuwa blocked kwa uchunguzi. Anachukuliwa passport etc etc ; wakifanya Mfano kama Hiyo seriously kwa watu 3 utaona muelekeo ;

shida sheria zetu hazipo serious ndio maana unakuta Mkurugenzi anajua anazingua na wala hajiuzulu anasikilizia upepo.

Na MaDG wote wanasalary nzuri, sio chini ya 14Ml. hadi 20 Mil kwa Mwezi, na kuiba wana iba manina, TZ bwana !
 
Utetezi wako unakinzana kidogo na kwa uandishi wako unaonekana ni mzee na una mda mrefu GPSA tusaidie kujua haya, FRAME-19 alisema Kitengo cha Ugomboaji DBSS na Mhasibu pale walikuwa na kampuni ya clearing na walikuwa Wana -divert mizigo yote inayotakiwa kupitia kwenye taasisi ya GPSA ikawa inapitia kwenye kampuni zao na Kitengo hicho kikachoka kwa kukosa mizigo kikaja kuokolewa na maagizo ya raisi, na hapa isingekuwa raisi haya mambo bado yangeendelea sio?...
Sasa na wewe unakubali hili kwamba hizi kampuni zilikuwepo zinafisadi Kitengo cha Ugomboaji, je ni za nani?

Na pia mkurugenzi wa zamani wa GPSA, Mwambega ametajwa unazungumziaje hili?
 

Ni zenu mlioondolewa na sasa mazingira hayaruhusu.


Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Baada ya kusoma huu Uzi Jana Leo bahati nzuri inkakutana na mtu Fulani yuko GPSA kaniambia mambo ambayo ni DBSS wanafanya hadi nikamuonea huruma, inaonekana huyo DBSS anajina la Sanga na kama mjuavyo Sanga wengi wako kwenye system za Usalama wa nchi kwahiyo analindwa sana pia anatumia sana Ulozi nasikia ni balaa sana sasa ukiangalia ulozi wa kabila la Wakinga (wananunua utajiri kama anao) basi hapo wa kumuweza ni Ikulu tu wengine mtapotezwa bure
 

We jamaa hoja zako dhaifu sana. Ukiwa unawaza kila anayekupinga ana maslahi binafsi utachelewa kujifunza. If i was in a position to decide; basi taasisi ya kwanza kuivunja ni GPSA!

Umezungumzia Clearing: Mimi nadhani hili tusibishane sana; serikali ifanye Survey kwa taasisi zote zinazohudumiwa na GPSA kwenye kufanya Cleaning.

Hilo ni janga na ninashangaa unaposema mna fanya vyema eneo hilo, ikiwa mzigo unaweza kukaa bandarini miezi 2 hadi 5 na nyie mpo, na mkiitoa mizigo mna sahau kukamilisha na baadhi ya Docs etc etc Yaani hilo eneo ndio mpo worst like you have never seen before.

GPSA is good for nothing, atafutwe Mkurugenzi aliyekuwa Serious bwana acheni mambo ya kipumbavu.
 

Nashukuru kuwa wewe ni sehemu ya watu wa clearing ambao mnakereka na maamuzi ya serikali kuipa GPsa nafasi


Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Kawashtaki PPRA ndiye regulator
 
Kwa nilivo usoma huu Uzi nilijua ufisadi umekoma nchi hii kumbe bado umetaradadi, ni vile tu media imebanwa, Kuna haja ya hizi tuhuma kufanyiwa kazi na wahusika wawajibishwe immediately

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…