GPSA: Tuhuma za ufisadi, matumizi mabaya ya madaraka na mengineyo


Amen


Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Ni zenu mlioondolewa na sasa mazingira hayaruhusu.


Sent from my iPhone using JamiiForums
Sijawahi kufanya kazi serikalini kwahiyo sijui utaratibu wenu wa kuwa shughulikia wafanyakazi wanaovunja sheria za wazi "conflict of interest" inakuwaje watu mmewabaini wana kampuni binafsi za kugomboa mizigo na mna ushahidi walikuwa wanazipa kazi kwa kutumia vyeo vyao halafu mkaamua kuwahamisha maeneo ya kazi badala ya kuwafungulia mashitaka?
 
Mimi sio sehemu hiyo but I am telling you the truth. Na usiniamini, tunaomba serikali ifanye Survey juu ya malalamiko. There is nothing personal
Kweli kaka hilo ndio la msingi
 
Hapa ndio hata mimi namshangaa, huyu mzee yawezekana kabisa na yeye anahusika kwa hiyo anaweweseka maana utetezi wake hauna mashiko kabisa...ukiona andiko la FRAME-19 amesema wazi na ametaja wamiliki wa kampuni.

Huyu mzee alikuja kuzima mjadala tatizo hakujipanga Kama waleta tuhuma amekuja na hoja dhaifu na amejikuta anachochea Moto zaidi
 
Tafiti zinaonyesha kuwa mafanikio ya taasisi yanategemea kwa kiasi kikubwa tabia za mtu mwenye dhamana ya kufanya maamuzi yanayohusu wafanyakazi wa taasisi husika.

Kiongozi akikosa sifa, ni vigumu walio chini yake kufanya wajibu wao.
Migogoro, kutokuelewa, hujuma, utegeaji, kukosa hamasa ni baadhi ya athari zinazoweza kuzaliwa na
uongozi usio na sifa.

Ingawa tunaweza kusema mengi yanayohusu wajibu wa mfanyakazi lakini bila kiongozi kuwa na sifa, itakuwa vigumu kupata ufanisi unaotakiwa kupatikana.
 
Umenipa jina lingine la kufuatilia "Hamza", hebu dodosa kidogo nini amefanya kabla sijaingia mitamboni kupata data zake...uko nyuma ya keyboard na TAKUKURU wanakufatilia funguka
Huyu mzee nilitaka kumjibu Imebidi nimuache, maana nimegundua kaja kuzima mjadala akiwa hana data au yumo kwenye hii kashfa.

Huyu "Hamza" anaemzungumzia Alikuwa meneja masoko..Kuna kesi ya kimajungu ilitokea pale wakamtoa ( hili nalo ni la kuchunguzwa), Akakaimishwa bwana mdogo nadhani anaitwa Peter..

Kinachotokea Sasa wanahisi kila mtu Aliyekuwa anajua madili na upigaji wao, lakini hii haitasaidia acha tuiokoe taasisi yetu Kama na sisi tunaoandika nyuma ya keyboard tunahusika tukamatwe...Kwa hiyo mzee jakatugu tulia, usipanick utakufa kwa presha.

Nakubaliana kabisa na mwambega kuchunguzwa huyu ndiye Papa wa Ufisadi wote pale GPSA, akifuatiwa na DBSS Hawa wengine akina CEO ndio wanajifunza na akiachwa nao watakuwa mapapa...wafanyiwe kazi
sasa
 
Mkuu mleta mada Kama umemuelewa vizuri hajasema Kama posho haitoshi, anazungumzia namna gani jinsi hizi posho zinavyolipwa kimajungu...

Nimejaribu kuongea na rafiki zangu walioko pale na wote wamesema ni kweli, malipo hayako standard, yaani ni Kama hisani ya mtu tu hivyo anaamua akupe au asikupe itategemea na siku hiyo kaamkaje.

Tofauti na taasisi zingine posho zikiwepo unajua kabisa kila mwezi lazma kiasi flani kitaingia bank Kama posho unakuwa huna wasiwasi, pale Hawa jamaa zangu wanasema kwenye mapipo waangalia sura na kwamba uko upande gani wa kujipendekeza ndio unakadiriwa cha kupewa au usipewe kabisa kwa kisingizio cha kutoa wahi kazini lakini humohumo Kuna wengine wanapewa japo hawawahi...hiki ndicho kinachozungumzwa hapa na sio kwamba posho haitoshi.

Hawa jamaa wakaendelea kusema, watumishi wa hii taasisi baada ya kufanya kazi kwa weledi wamegeuka kuwa watumwa wa posho, yaani wako radhi uwakute mpaka saa12 wako online tu ofisini bila kazi maalum za kiofisi wakihofia kuondoka ambapo itawafanya wasilipwe posho na hii ni kulingana na viongozi walivyoweka mpangilio wa hizi zinazodaiwa ni EX. duty tofauti kabisa na taasisi zingine zinavyofanya malipo haya.

Jamaa anasema posho zimegeuka janga la kuwa-stress badala ya kuwa-motivate ili wafanye kazi kwa bidii...hiki ndicho kinachozungumzwa....!!

Parabora
 
Mh! Kama ni hivyo basi bado tuna safari ndefu sana.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Basi nikajua hii taasisi ina mahela kumbe hamna kitu?
Poleni aisee
 
nyie wabunge naona mmekuja kutikisa kiberiti kabla hamjaenda zimba kuwachana mafisadi....
 
Kwahyo watu waendelee tu kujipigia vitu vya umma kwakutokufata procedures are you serious?

Sent using Jamii Forums mobile app
Kuleta hizi taarifa JF ndiyo procedure? Jiongeze Mkuu.
Alitakiwa apeleke PCCB bila wao kujua, hapa wanaharibu ushaidi kwasababu wanajiandaa sasa na kuweka mambo sawa
 
Unajua maana ya whistle blower mtu Hadi kuleta hapa seems huko Takukuru kume fail wanakula nao sahani moja upigaji, kuandika wenye mamlaka watapitia na kufatilia kuliko kwenda huko Takukuru maana bila amri ya Raisi hawafanyi ndo kwanza wataenda kuomba rushwa
Kuleta hizi taarifa JF ndiyo procedure? Jiongeze Mkuu.
Alitakiwa apeleke PCCB bila wao kujua, hapa wanaharibu ushaidi kwasababu wanajiandaa sasa na kuweka mambo sawa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Niko hapa duniani na huyo mume hata Sina na siwezi loga mtu mzima eti atulie for which purpose, pia siamini mafanikio katika nguvu za Giza naamini kwenye ubunifu na utendaji ulio bora
Unauliza swali as if hauishi duniani? Mbona mnaenda kwa waganga kuloga waume zenu sasa unashangaa mtu kuloga alinde cheo chake

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kuna ID hapo kama tatu hii nahisi ni za mtu huyo huyo mmoja amefungua mpya ili kuongezea uzito wa hoja yake ionekane wengi wanaujua ubaya wa GIPUSA!
 
Kuna ID hapo kama tatu hii nahisi ni za mtu huyo huyo mmoja amefungua mpya ili kuongezea uzito wa hoja yake ionekane wengi wanaujua ubaya wa GIPUSA!

Bora na ww umelishtukia jambo hilo Mkuu, kuna mmoja naona ni Hasira za kuhamishwa hapo maana anasema alikua Mgavi 2015 akapelekwa Mkoani. Ina maana uchafu wa hiyo Taasisi yao ni kwa miaka hii tu wakati yeye Mgavi hakukua na uchafu?



Hapa kunaweza kuwa na Ukweli pia kukawa na MAJUNGU kwa kiasi kikubwa. Fanyeni Kazi Umbea acheni
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…