Hili jambo wengi hawawezi kulijua, wazungu wanapotoa nafasi kama hizo kwa wahamiaji na hata scholarships wanalenga kupata pia cheap labour, yaani wanakuwa wanahisi kuna uhaba wa watu wa kufanya casual works......ila sisi kwa umaskini wetu tunaona ni bonge la fursa sawa na kuokota dodo chini ya mwarobaini.
Nyumisi: Nilidhani umeelimika!bado thinking yako iko twisted, unaposema cheap labour sijui una maana ipi! Hivyo mtu aliyekuja soma US, sio kutoka Tanzania tu au nchi yoyote kama professional,yeye analipwa kidogo sawasawa na mzawa!
Nauliza unajua unachokisema? Nilimtembelea recently Mtanzania ambaye alikuwa BOT akaja kusoma huku, baada ya kuwa na experience amewekwa kuwa mkuu wa kitengo fulani katika IT company, mshahara alioutaka yeye baada ya kuangalia wenzake wanalipwa nini IBM,dau alilotaka walimpa,siwezi kuweka hapa maana hatuaamini!
Sasa narudi kwenye mfano binafsi, my son ni IT person, alipokuwa semester ya mwisho yeye na wenzake wawili walikuwa approached na Institution fulani, waliopoajiriwa, yeye Mtanzania, mmoja kutoka Nepal na kijana mzungu wa hapa wote walianza na scale moja! Maana shirika liliwaonyesha entry level package.
Sasa sijui habari hizi mnaokoteza wapi?
Anyway, let say nikubali argument yako, nimetoka Tanzania nakuja kusoma US, mshahara wangu Tanzania ni $ 1500/ Baada ya ku graduate, shirika la US likaona nafaa, na kunilipa mara tano ya Tanzania, na position hiyo hiyo yuko mzawa analipwa more than me, kwa hiyo unashauri nirudi nyumbani kuchukua $1500/ yangu sababu ya uzalendo! Uzalendo upi hasa!
Hivi huo uzalendo mnaouzungumza hapa mbona hatuuoni ukifanya kazi na kubadili nchi?
Mnaishia kulalamika juu ya tozo, ukosefu wa maji, umeme, mbona huo uzalendo uliowakimbiza ulaya umeshindwa kubadili nchi!
Hebu acheni porojo!