Wewe ni mkomavu, mambo umeyaeleza kwa akili.
Na hilo la mwisho sijui maiti kufanyaje, mi nimeshuhudia huo mkasa.
Tumeweka kambi njiani kupumzika ili kesho tuendelee na msafara wa kusindikiza maiti tukielekea kwao kuzika, jamaa likamchukua mfiwa, yaani mke wa marehemu na kufanikiwa kwenda kumlala, huku maiti ya mume ikiwa ndani ya gari!
Hilo lilinifikirisha sana namna ya kuziweka kwenye uzani akili za mjane wa marehemu, kwamba alikuwa na utulivu gani wa akili kupelekea kuridhia kitendo hicho, au alikuwa na chuki na marehemu mumewe, sikupata jibu.
Hili la Baltasar naona ni cha mtoto, bila kufanya mambo ya kiGwajima asingelijulikana kudadeki.