Gwajima amcharukia Diamond

Gwajima amcharukia Diamond

Kesho kinyago cha mpapule lazima ajifiche nyuma ya fuvu liliko kwenye studio yake..Baba mchungaji lazima amtie ngeu kesho
 
hivi kwenye haya mashairi ya huu wimbo mpya wa chibu nionyesheni neno lililomtaja huyo gwajima[emoji116]

Nasema walau nina kidogo na mashabiki wananiambia mbona hausemi chochote
Ah, si uko nao siku zote ama ulezi unafanya uogope
Ah na media pande zote wanalalama kiongozi atoke
Ah nchi inaingia matope niende wapi na mimi mtoto wa wote,
Yaani lawama, acha nikae kimya, niongee, kimya (ooh ninyamaze mimi)
Nikae kimya nisemee (kimya) mama kaniambia (acha nikae kimya)
Ooh nifunge mdomo, mimi bado mdogo nisiseme (kimya)
Verse
Ni mengi majaribu najaribu kuepuka yasije nicost
Japo mengine swadakta mengine hayana maana
Rafiki kipenzi wa karibu hata nyimbo yake sikuweza ipost
Ila alipokamatwa iliniumiza sana mitandaoni kila kona
Uongo na ukweli unashonwa kila nyumba inanong’ona, ahh, ooh Tanzania
Mara kibembe Dodoma wabunge pinzani wamegoma juzi akapotea na Roma
Ohh Tanzania
Najaribu kunyamaza Makame hataki ohh ananiambia walau nina kidogo
Nyumbani nafungwa geti niende kwa Mangi kununua super gate
Napewa za chini ya kapeti kuna redio imevamiliwa eti
Ehh, napita kwenye magazeti nakuta lundo la watu wameketi
Ehh badala ya kutafuta senti wanabishana tu mambo ya vyeti
Acha nikae kimya (nisiongee ) nikae kimya (ninyamaze kabisa)
Nikae kimya (ulimi koma) kimya (usije kuniponza) acha nikae kimya
(nifunge bakuli langu) nikae kimya (nikojoe nikalale) kimya
Mimi bado mdogo sana mama kanimbia
Bridge
Najiuliza wapi (wapi) najiuliza wapiii, tunakwenda wapi
Wapi, kila siku maneno, wapii, hatuwajengi jamaa
Mimi na wewe ni taifa moja, Kambarage baba mmoja
Sasa tofauti za nini tushikamane tukaijenge Tanzania
Inaonekana masikio hayasikii vizuri. Rudia tena kuusiliza. Hujanishawishi mimi ambaye nimeusilikiza full. Gwajima ametajwa mwanzo wa wimbo.
 
Huyu jamaa ni mnafiq tena anawawaibiatu waumini, sijawahi ona mchungaji wa sampuli hii kabisa! Ila akae akijua atamalizia kubaya!.
 
Hii thread inatembea fasta zaidi ya matokeo ya uchanguzi mkuu wa rais 2015
 
Huyo mchungaji asambaze injili ya bwana, Yesu alitukanwa na kukashifiwa sana na warumi, mafarisayo na watu wasio mcha Mungu lakini hakunyanyua kinywa chake kusambaza umbeya.

Huo wimbo wa Diamond nimeusikiliza kwa umakini sana, Chibu kajaribu kuwa neutral sana sana sana. Asingeweza kuimba zaidi ya alivyoimba. Kipande cha Gwajima anasema "Mara nasikia Konda, Gwajima ugomvi umekolea". Sasa hapo Chibu kamchafua wapi Gwajima.

Chibu anasema asimame wapi, yeye mtoto wa pande zote, anasema wazi kila akijaribu kunyamaza moyo unakataa, msikilize kwa makini anasema media zote wanataka kiongozi atoke, nchi inaingia matope (hapa yupo wazi kabisa kua japo Konda ni mlezi wao lkn uwepo wake ni kama nchi imeingia matope).

Gwajima hawezi kumshusha Diamond hata afanye nini. Dogo yupo strong kuliko Gwajima anavyodhania. Dogo anajenga misikiti na kurudisha fadhila kwa jamii, yeye Gwajima hata kanisa lake kashindwa kujenga anasalisha watu uwanjani.
Yaani pale anaposema amefanya utafiti,
 
Nadhani ajajua kuwa kabla ya hili mondi kashapitia vizingiti vingi

Kushindana Na mswahili utapata shidaa
 
Hiyo heading nimeipenda mkuu, unafaa kuwa mhariri wa gazeti![emoji1]
 
Back
Top Bottom