Gwajima anaendelea kumshikia bango Makonda, adai amekimbia nchi kama Magufuli alivyotabiri

Gwajima anaendelea kumshikia bango Makonda, adai amekimbia nchi kama Magufuli alivyotabiri

Muda utasema,
Nilikutana na mzee moja amefanya kazi na Hayati Mwl. Nyerere; sasa huyo mzee yeye alikuwa anaiita serikali hivi siri- kali (Top - Secret) utaelewa tu kadili muda unavyoenda.

Maana akili zingine siyo za "tit for tat" zinaelewa taratibu.

Basi sawa, let's wait and see huo muda ukifika!!
 
Hizo sifa alizompa mh rais ni za kinafki kupita maelezo.
Wanausalama msimlee huyu mchungaji feki.
 
  • Thanks
Reactions: SDG
Mhalifu hapo ni Nani sasa!? Mmemsachi, mmempima mmemkuta msafi kama Si hivyo angekuwa ndani!! Hapo mhalifu ni Bashite aliemsingizia.

Je, una elewa kuwa Gwajima anaripoti kituo kikuu cha polisi kila baada ya muda Fulani?

Yaani, yuko chini ya uangalizi?

Sasa, huo uangalizi ni wa kitu gani?

Utaelewa tu muda ukifika.

Serikali, haikurupuki elewa hivyo.
 
Huyu nae katushosha badala ahubiri habari njema za kwenda Mbinguni watu waokoke yeye kutwa kuingiza mambo yake binafsi madhabahuni kwa Bwana ,ama kweli mtawatambua kwa matendo yao
Kwa hiyo unataka amfichie Daudi maovu yake?
 
Je, una elewa kuwa Gwajima anaripoti kituo kikuu kila baada ya muda Fulani?

Yaani, yuko chini ya uangalizi?

Sasa, huo uangalizi ni wa kitu gani?

Utaelewa tu muda ukifika.

Serikali, haikurupuki elewa hivyo.

Like you said time will tell let's wait and see!! All I know hajapandishwa mahakamani!! Kama Ana kitu chochote kile wangeshamfungulia mashtaka serikali ina mkono mrefu Ila mbele ya macho yangu he is innocent until proven otherwise!! Ila jiulize Kama he has to report huko polisi, Na Kama Ana magumashi ya kiaina Na bado anajiamini hivi anapata wapi hizo nguvu!!?
 
Unamchokaje mtu anaishi kwake analala kwake, anakula kwake, hakupigii simu wala kukubugudhi kwa namna yoyote mmemchoka je ungekuwa unaishi naye nyumba moja ungekuwaje?
Kwahiyo watu wanaokuchosha wewe hua unaishi nao, wanalala kwako, wanakula kwako, wanakupigia simu na kukubughudhi kwa namna mbali mbali? Basi moderator akikupiga ban walau mara 1 kwa wiki hutakiwi kuchoshwa nae maana hajakidhi vigezo vya kukupelekea kuchoka? Bogus!
 

Akizungumza leo kanisani kwake, Ubungo, jijini hapa, Gwajima alidai kosa la kwanza la Makonda ni kughushi cheti ambacho kinaonyesha yeye ni Paul Makonda wakati akifahamu kuwa yeye ni Daudi Bashite.

Askofu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima ametaja makosa ya kisheria yaliyomfanya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,Paul Makonda kukimbilia Afrika Kusini.

Akizungumza leo kanisani kwake, Ubungo, jijini hapa, Gwajima alidai kosa la kwanza la Makonda ni kughushi cheti ambacho kinaonyesha yeye ni Paul Makonda wakati akifahamu kuwa yeye ni Daudi Bashite.

“Kosa hilo kwa mujibu wa Gwajima ni kifungo cha miaka saba.Kosa jingine ni kula kiapo cha ukuu wa wilaya na ukuu wa mkoa akisema yeye ni Makonda wakati akijua yeye ni Bashite,” alisema

Gwajima alisema kosa la hilo la kula kiapo na cheti feki ni kifungo cha miaka mitatu.

Kosa jingine alisema ni kupokea mshahara na posho kwa jina la Makonda wakati akifahamu si yeye na kuongeza kuwa kosa hilo likithibitika atatakiwa kurudisha mishahara na posho zote alizochukua.
 
Nasikia neno la leo limetoka katika kitabu cha Kubenea.

Haaaa haaaaaa mbavu zangu jamaniii.
Nimecheka sana. Eti kitabu cha Kubenea.
Ndiyo dini uchwara na bishop uchwara.

Kweli, kazi bado tunayo kama Taifa kwa dini kama hizi kibwetele wa Uganda watu wengi hawatamwepuka aisee .

😀😱😀
 
Like you said time will tell let's wait and see!! All I know hajapandishwa mahakamani!! Kama Ana kitu chochote kile wangeshamfungulia mashtaka serikali ina mkono mrefu Ila mbele ya macho yangu he is innocent until proven otherwise!! Ila jiulize Kama he has to report huko polisi, Na Kama Ana magumashi ya kiaina Na bado anajiamini hivi anapata wapi hizo nguvu!!?


Ndiyo maana basi serikali, huwa ina hatua za uchunguzi na upelelezi pana mambo mengine yanachukua miaka unafikili kuwa serikali imekuacha au hauna hatia ila baada ya miaka hata 10 wanakufata taratibu unawekwa mikono salama
 
Yani anamtaka rais afanye maamuzi kwa wakati, huku akimtajia takwimu mbalimbali, akizuga anamsapoti.

hizi ni sifa za kinafki.
 
Back
Top Bottom