Gwajima anapaswa kupigwa vita na vyama vyote

Wapinzani wa bongo na wafuasi wao ni wapuuzi sana. Viongozi wenu wanawahadaa ni vijimisemo vya rejareja kama vile "siasa haina rafiki wala adui wa kudumu". Matokeo yake mnabaki kutapatapa na personalities za watu ambazo hubadilika kila uchao.

Way back 2015 mliposaliti demokrasia na harakati za kweli mkishirikiana na mamluki akiwemo huyo Gwajima mlimwona jembe kweli. Mlimtumia kumdhihaki Dr. Slaa aliyeamua kusimamia misingi ya upinzani kwa wakati ule. Mkamtukuza huyo Gwajima ambaye wiki chache tu kabla alikuwa Arusha akimnadi Lowassa wa ccm na akaweka bayana asiyemtaka Lowassa akalambe ndimu.

Picha lenu na Gwajima likaendelea alipoanza minyukano na mkuu wa mkoa msiyempenda. Mlichekelea kweli. Sasa kibao kimegeuka ameanza kuwang'ata mnabaki kutapatapa mitandaoni. Kesho akija upinzani mtatafu sabuni mumtakase tena! Bure kabisa.
 
Hao nao utakuta wanajiita wafuasi wa demokrasia. Kila mtu anao uhuru wa kogombea na akachaguliwa.
 
Hivi huyu jamaa aliwahi kusambaza ujumbe unaousu ukabila vile? Sikumbuki vizuri. Ila nadhani ni mkakati fulani ivi maana sio yeye peke yake hata Bashite atakuwa mitaa ya Kigamboni pale. Mtamuelewa tu mzee baba taratiiibu
 
Kwa Vita vya ufisadi ni vya chadema peke yake
 
Akiwa upande wa Chadema walisema hauwezi tenganisha siasa na dini,

leo yupo CCM wanasema anachanganya siasa na dini.

MTIFUANO
 
Gwajima ni mtanzania anazo haki ya kugombea ubunge. Kuwa kiongozi kama mchungaji, padri au shekhe kakuondoi sifa zake za kutumikia wananchi, wala kuamua mustakabli wake wa maisha. Mifano ipo mingi sana kama ya Kina Dr.Fr.Slaa, Mch.Natse (Karatu), Fr.Mwanjelwa (mbeya vijijini), Mch.Msigwa (Iringa Mjini), Fr.Supa (Dodoma Mjini), Mch.Chakwela (Rais Malawi), Sheck Hasan Fereji (Geita), Maalim Seif Sharif Hamadi (Waziri Kiongozi -SMZ) nk. Katiba haisemi ukiwa kiongozi unapoteza haki zako za kiraia.
 
Sasa huwezi amini ukiambiwa yeye yupo ndani ya system, nchi ina mambo mengi sana hii.
 
Kuhusu gwajima kuwala kondoo wake,mi sioni tatizo ilimradi wamekubaliana tu,
Kuhusu utapeli,,hapa tunamuonea tu baba askofu,,hakuna kazi isiyo na malipo na kila mtu atakula ofisini kwake,
 
Kila aliye maarufu sasa hivi anataka kuwa mbunge
Shida ni kwamba siasa Tanzania kumeifanya ndio sehemu pekee ya kupiga hela ndani ya muda mfupi hivyo kila mtu anataka akapige hela
 
Cheo cha uchungaji kapewa na nani? Na hili kanisa lake lina matawi nchi ngapi au ni dini kaivumbuwa yeye mwenyewe tu
 
Ni aibu sana kuwa na kiongozi wa namna yake.
 
Kuhusu ugombea wa huyu Tapeli, iwapo Chadema wataamua kufanya lolote lile ili siwe mshindi na hata mgombea, wataungwa mkono na wana CCM wengi sana. Hata mgombea wao anaweza pita kwa kura za wana CCM, wasioridhishwa na viongozi wa chama chao
 
Umesoma vzr nilichokiandika? Nikuonyeshe vipi kanisa la MSIGWA wakati nimekwambia wachungaji huwa HAWANA Makanisa yao binafsi?
Wakati mwingine kuvamia vitu usivyovijua? Hebu nenda kwa Mzee wa Upako ukamwambie lile kanisa na wewe linakuhusu asipokutimua na panga! Haya makanisa ni mali za watu kalagabaho!
 
Binafsi namuunga mkono Gwajima. Jamaa ana convincing power ya ajabu. Na atashinda. Hayo mengine kwani anawabaka? Si wanakubali wenyewe ? Kuhusu uchungaji hiyo ni fursa tu. Kwa Tanzania ukifa masikini basi uliamua mwenyewe tu.
Kwanza mimi nawashangaa wanaomkejeli Gwajima sasa hivi! Si ndio hawa walikuwa wanawahi siti za mbele kanisani kwa Gwajima ili kusikiliza anapomshambulia Makonda?
Si ndio hawa hawa ambao Gwajima alikuwa mshenga wao wa kumleta Lowasa Chadema?

Sasa tofauti ni ni nini?

Alafu kuhusu suala la uzinzi, vipi kwa mwenyekiti wao anaezini, kulewa hadi kuanguka kisha anasingizia selikali?

Kumbe wafuasi wa chadema ninwajinga na wanafiki kiasi hiki?

Vipi kama Gwajima angetangaza kugombea jimbo la Mwanaccm kupitia chadema? Wangemtukana hivihivi?

Sent from my SM-T585 using JamiiForums mobile app
 
Gwajima kama atapitishwa basi kigezo itakuwa Usukuma wake na si kinginecho.
 
Huyo mcheza ngono hana nafasi kati ya watanzania waadilifu
Hizo Ngono si zilionekana tuu kwenye Mitandao? Wana chi wengi hawawezi kuziona na hazirhusiwi kuoneshwa Hadharani wakati wa Kampeni. Zitaishia Tu mtandaoni.
 
Uzinzi Nani asiyezini? Wakianza kuorodhesha Server zitajaa. Cha Msingi hawajarekodi picha za Uzinzi wao. Halafu huyu ni tofauti na Wengine Kwa kuwa hatutegemei Mlokole kuwa Mzinzi ni Mtumishi wa Bwana Dhambi zote wameacha.
 
Uzinzi Nani asiyezini? Wakianza kuorodhesha Server zitajaa. Cha Msingi hawajarekodi picha za Uzinzi wao. Halafu huyu ni tofauti na Wengine Kwa kuwa hatutegemei Mlokole kuwa Mzinzi ni Mtumishi wa Bwana Dhambi zote wameacha.
Unajidanganya Gwajima hana tofauti yeyote na kina Mbowe au Magufuli,
Kikubwa acheni kumhofia Gwajima hapo Kawe

Sent from my SM-T585 using JamiiForums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…