Gwajima anapaswa kupigwa vita na vyama vyote

Nadhani Gwajima ana haki ya kugombea ubunge na havunji sheria yoyote.


Hizo ni tuhuma tu. Kuhusu picha za ngono ni utashi wa mtu tu kun'gamua maana angekuwa mcheza filamu hizo tusingeishia kuiona moja, bali tungeona nyingi.

Kikubwa nachoona wapinzani wake kama atapitishwa wanaenda kutumia Dini kumhukumu na kuwagawa wapiga kura.

Kwa hoja hii ni afadhali CCM watumie busara wasimpitishe...la sivyo watarajie kampeni za jimbo la Kawe kuendeshwa kidini. Na sio Gwajima atakayefanya hili bali ni wapinzani wake na hakuna namna ya kulizuia zaidi ya kutokumpitisha.
 
Hili jitu ni tapeli haswaa, wanaosali kwake mirembe inawahusu! watu gani hadi leo hawajaelewa wanaishi kwa kutapeliwa na mhuni. Ana Mungu gani huyu mtu. Unabii ameupata wapi!
 
Nani sio mzinzi humu
Tuache maneno ana haki ya kufombea ni mtanzania kama ilivyo kwa halima mdee, mbona tuhuma za usagaji za halima hamzisemi humu au ndio maadili hayo
Wewe ni mzinzi?
 
Gwajima kupata airtime kubwa katika sarakasi zake za “kiroho”, kijamii na kisiasa ni kielelezo kamili cha uovyo (mediocrity) wa nchi yetu na sisi wenyewe. Kwa kiwango cha bunge letu na siasa zetu leo hii, hakuna cha ajabu mtu kama Gwajima akiwa mbunge. Doesn’t really matter when any sob can make the grade! Mpaka sasa hili bunge ni bonge la embarrassment. Kila unapoangalia vikao vyake kwenye tv aibu unaona wewe!

Katika yote, hiyo tuhuma ya kunyanyasa kingono mabinti wadogo ndio mtihani kwa serikali na wasimamizi wa haki za binadamu. Kama kuna ukweli hapo, basi akiachwa kuingia bungeni itadhihirisha jinsi tulivyozidi kuzama kwenye maji taka.
 
Ukitaka kujua gwajima sio mtumishi ni mmliki genge la uhalifu angalia bodyguards wake pia angalia anavyoongea tu utapata kitu kingne dah! jamaa kamfanya mkewe zezeta zezeta.
Hili limelishuhudia kwa macho na masikio yangu, nimekutana na mama aliyesali kwa hilo kanisa lake kwa muda mrefu sasa sijui alishtuka nini akawa anahama hilo kanisa.........nakwambia akaanza kuugua na kila akiombewa mapepo yana manifesti kuwa yanatoka kwa........na yanamtaka arudi aendelee kuita watu wajae kanisani

tokea siku hiyo nikajua huyo anayejita askofu ana nguvu zingine zingine ndani yake
 
Binafsi namuunga mkono Gwajima. Jamaa ana convincing power ya ajabu. Na atashinda. Hayo mengine kwani anawabaka? Si wanakubali wenyewe ? Kuhusu uchungaji hiyo ni fursa tu. Kwa Tanzania ukifa masikini basi uliamua mwenyewe tu.
hamna kitu mbaya kama watu wanaotakiwa kuchungaa kondoo na kugeuka wafaidika wa hao kondoo.........
 
Umemsikia na NABII SHILLAH nae ametia nia kupitia CHADEMA?
ukisikia mtumishi wa mungu anagombea nafasi za kisiasa ujue huyo si mtumishi wa mungu tena, ni bora wajitangaze wameachana na utumishi wa mungu na sasa wanataka kutumikia ufalme mwingine
sijui mengi kumuhusi nabii SHILLAH ila kwa macho na masikio yangu huyo mwingine kupitia maombi aliyofanyiwa mama aliyehudumu kanisani kwake nimejiridhisha ana nguvu zingine zisizo za MUNGU aliye hai katika jina la YESU KRISTO
 
Gwajima aka BAUNSA hafai kupewa hata kura moja labda ya Mkewe na Yake mwenyewe tu.
 
Akikushindwa kiroho wanatumika bodyguards
 
Utiaji nia mwaka huu ni uchafu mtupu
Watia nia hawana maadili wamegeuza Ubunge kama Biashara ya Kuuza Maandazi
gwajima hastahili hata kuwekea watu mikono itakuwa kuwa mbunge ....

Nchi ipo shimoni kwenye kina kirefu

Watu ha wapo serious na maisha ya Mtanzania

Wamejitokeza wazinzi walevi wachawi waongo wanafiki wakosa elimu wakosa hekima busara na imani, manabii wa uongo wasanii(hata shule walihudhuria madarasa tu)
Someone has to come out aweke hii nchi kwenye mstari

Uongozi umekuwa wa kulipwa fadhila

Tukienda kwa mwendo huu basi miaka kumi hii tutalizika Taifa na kufunika kaburi kwa zege na nondo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…