Nimeangalia hiyo video na Picha zinazotumwa kwenye mitandao kumuonyesha Mtumishi wa Mungu GWAJIMA akifanya mapenzi na mwanamke akiwa chumbani nimegundua ni zakutengenezwa..
Kwanza ifahamike, Mimi sio mshirika wa Gwajima wala siandiki ili kumtetea.Mimi ni mtaalamu wa maswala ya ICT, na nimefanyakazi nyingi sana za Photoshop na Editting za picha mbalimbali
Kwanza, nimefuatilia kuhusu hiyo video, ni kweli huyo ni Gwajima Ila hiyo sauti ya mwanamke inayosikika ni sauti iliyopenyezwa haitokani na uhalisia wa tukio
Pili, Hiyo picha inayomuonyesha Gwajima kwamba amelala juu ya mwanamke ni picha iliyotengenezwa, Ukiangalia maungo kati ya shingo na kichwa cha Gwajima kilipopachikwa utaelewa kuwa Gwajima hana shingo ndefu namna ile.Hicho kichwa kimekuwa croped kutoka katika ile video
Tatu, Mazingira ya video inayoonyeshwa na mazingira ya picha iliyotumwa hayaendani, angalia mapazia na background zimetofautiana kabisa
Nne, Ni swala la kujiuliza maswali ya logic tu ambayo yatakupa kujua Hilo tukio Si la kweli Bali kutengenezwa. Je ni nani ambaye Gwajima angekubali ampige picha wakati anafanya mapenzi?Kama huyo mwanamke ni mchepuko wake, Je Gwajima ni kwamba hana akili mpaka akubali kupigwa picha akiwa anafanya mapenzi? Hata kama angekuwa kweli yupo na mkewe au mchepuko, isingewezekana kukubali kupigwa picha, ajipige picha ili akamuonyeshe nani?
Hizi taarifa ni za uongo kabisa zenye lengo Si tu la kumchafua na Kumshushia heshima Gwajima Bali linachafua kanisa la Mungu kwa ujumla, hata kama Gwajima humpendi au sio mchungaji wako lakini kufurahia aibu na video hzi kwa Gwajima ikiwa ni Kuutukanisha Ukristo wako pia na kumtukana Mungu
Hivyo, Ikiwa kweli wewe ni mkristo wa kweli lazima utaukemea ushetani huu unaosambazwa na maajenti ya ibilisi kuuchafua ukristo kwa ujumla.Hivyo kushiriki kufurahia au kusambaza taarifa hizi chafu kwa kufurahia aibu hii kwa Gwajima ujue unashiriki kazi za shetani, na wewe ni mchafu wa namna hiyo hiyo
Shujaa CRM