Gwajima: Kutakuwa na Ugeni wa mzee kutoka kijiji cha KOROMIJE


Mfuasi mwingine wa Gwajima huyu.

Hahahaaaaa.
 
Nadhani huyu mtumishi wa Mungu ni mnafiki sana. Nadhani hata huduma yake iko ukingoni.
Safi sana muda wote umesema unadhani! , unadhani! vizuri umekuwa mkweli kuwa huna uhakika!
 
hapana ndugu...ngwajima ni binadamu kama wengine ana hisia, hasira, kutotaka kuaibishwa, na sifa zote za binadam...uweke pembeni uchungaji..tumchue yeye kama yeye kama mtu alie aibishwa sana....kama ni kweli anahusika na madawa wamfunge kama inavo wataka kisheria ila kama ilikua kuwachafua na kushusha heshima za watu walizo tengeneza miaka mingi basi anacho kifanya huyu bwana kwa kaka daudi mashite ni sahihi kabisa...
1. kila siku tambua malipo ni duniani hapa hapa
2. muosha huoshwa
3. na tatu insu ya vyeti ni nyeti, watu wengi wamesoma na wanastahili wadhfa mbalimbali lakin hawajazipata kwa sababu zimezibwa na wale ambao ndugu zao wananguvu serikalin na kwenye maofisi mengi sana TZ kwa kutumia vyeti vya kuunga ungaaa........

INAUMA SANA UMESOMA UMEFAURU VIZURI ALAFU KAZI HUPATI KIRAHISI WAKATI HUOHUO UNA MUONA MTU UNAE MJUA ALIKUA KIAZI TU CLASS NA MITIHANI ALIFELI NDO AMEKAA KWENYE KITI CHA ENZI AMBACHO ILITAKIWA UKAE WEWE......

KILA MTU APATE ANACHO STAHILI....................
 
Jamaa amecheza faulo ndani ya 18 alafu amepuliza kipenga mwenyewe na kutoa red mwenyewe na kuweka penalty mwenyewe na kufunga mwenyewe hii ndio shaolin soccer isee!
 
Acheni kuchukulia msamaha na neema ya Mungu kuwa ni Upumbavu! Paulo anawaambia wagalatia!
 


 

Aisee!

Kazi ipo kubwa mno kuliko hata navodhani.
 
Mnaosema Gwajima asamehe, kumbukeni hata Mungu husamehe wale tuu wanaomuomba msamaha, Daudi inabidi ajitokeze amuombe radhi mtumishi wa Mungu kwa kumsingizia uwongo, kisha akiri kuiba cheti na aombe radhi, otherwise jino kwa jino
 
Hao waumini wake wakapimwe akili maana sio bure, mtu unakua unalipa nauli kwenda kufuata umbea na sio neno la kukujenga kiroho? sasa vyeti vya Mkuu wa mkoa ndio vitawapeleka Mbinguni? Kwa hizi akili maendeleo yatachelewa sana kuja!

Wacha hayo maendeleo yachelewe kuja aisee, kwani yalikuwa wapi zaidi ya miaka 50 ya uhuru yamepita. Sasa hivi ni mwendo wa sarakasi
 
GWAJIMA NI KANJANJA WA DINI LAKINI KTK HILI LA MAKONDA NAMUUNGA MKONO KWA ASILIMIA MIA ILI CCM IFE NA ITEKETEE KABISA.... SHENZY KABISA.
 
katika viongozi wote wa dini niliowahi kuwasikia na kuwaona,hakuna mpuuzi na mtu wahovyo kamma huyu bwana ,anaacha kuhubiri neno la mungu anageukia kwenye mipasho na hao mazuzu wake utamsikia wanamshangilia,
 
Fungua macho hili ni pambano dogo ndani ya vita kubwa
A tiny battle in a big war
Vipofu hao, hata wakifungua hawaoni kitu, UNAJUA ULE USEMI, ai wish acudubi yule, ndio ulichochea mafuta. Sasa acudu bi ndo refa, mchezo unaendelea, kadi nyekundu imekua ngumu kuitoa wakati aliomba kushika kipenga. Mie simo!!
 
Hao waumini wake wakapimwe akili maana sio bure, mtu unakua unalipa nauli kwenda kufuata umbea na sio neno la kukujenga kiroho? sasa vyeti vya Mkuu wa mkoa ndio vitawapeleka Mbinguni? Kwa hizi akili maendeleo yatachelewa sana kuja!
Huyo aliyemshuku kumtwisha mzigo hakujua kwamba ana waumini na alitegemea kondoo wake watamwelewaje mtukufu wao?Gwajima anajisafisha ili waumini wake wazidi kutambua kwamba ni msafi.Hakuna ubaya kama anatafuta namna ya kurejesha imani ya waumini.
 

Umeongea ukweli mtupu. Jambo lingine hayo mambo ya Mungu rahisi sana kuyasoma, lakini kutekeleza ni issue aisee. Hivi unalala selo (rumande) bila hatia, unadhalilishwa bila hatia. Acha inauma sana. Kuna kanisa fulani mahali fulani viongozi walikuwa kwenye kikao wakahitilifiana kuhusu agenda fulani, sasa kumbe walikuwa na mgogoro wao nje ya kanisa. Aisee walipandishiana, mwingine akaweka mkoba chini akamwambia mtu mwingine amshikie mkoba kwanza, na ukristo anauweka pembeni kwanza, huyu mkorofi lazima amuonyeshe yeye ni nani, wakazichapa baadaye wakaamuliwa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…