EWGM's
JF-Expert Member
- Jul 22, 2013
- 1,521
- 2,112
Najua Mchungaji Josephat Gwajima upo hapa JF
Tumepata taarifa jumapili ijayo kuna wageni watatoka Kolomije village kuja kuongea na familiya ya wana Ufufuo,tumesikia wengine ni waalimu waliomfundisha Mh makonda na wengine ni wanakijiji.
Naomba nikuombe neno moja,samehe na kusahau kwa kuwa ndio tulioitiwa,waendao katika mwili hawawezi kumpendeza Mungu,wewe ni MTU mkubwa katika jamii na unaheshimika,hivi unaweza kufundisha somo LA kumsamehe adui yako?
Naomba uwe mfano wa kuigwa ili usipoteze kondoo unao waongoza,kumbuka maneno ya Yesu,akulazimishae kutembea maili moja tembea nae mbili,na akuny,ang,anyae koti mwachie na shati.
Kuna Nyakati Hata Binadamu Anachukizwa Na Visa Vya Watu Waovu, Kama Ni Kweli Makonda Alitumia Vyeti Vya Kughushi Na Akapata Nafasi Anayoitumia Kufanya Uovu Kwa Watu Hivyo Anastahili Kukemewa Kwa Kauli Moja Na Watu Wote Wenye Mapenzi Mema Na Imani Kwa Mungu.
Pia Wachungaji Wana Nafsi Kama Binadamu Wa Kawaida, Na Shambulio La Mchungaji Ni Shambulio La Kanisa. Hata Yesu Akiwafundisha Watumishi Wake Somo La Imani Kupitia Pale Alipoona Njaa Wakati Anaelekea Mjini (Bethania) Akaona Mti Kando Ya Njia Akauendea Na Asione Kitu Juu Yake Ila Majani Tu Akakemea Yasipatikane Matunda Kwako Tangi Leo Hata Milele. Mti Ukanyauka Mara.
Kwa Tafsiri Rahisi Yesu Alitegemea Matunda Kwenye Mti Ule Na Alipokuta Hamna Kitu Akashikwa Na Hasira Akakemea Mti. Lakini Akatumia Kitendo Kile Kufundisha Imani. Sasa Makonda Anafundishwa Nguvu Za Wachungaji Ili Atambue Nguvu Ya Imani Kwa Mungu Aliye Mkuu Asiwe Anapenda Kuchafua Makanisa Kwa Manufaa Yake Binafsi.
Hata Yesu Alipatwa Na Hasira Pale Ekalu La Bwana Lilipogeuzwa Soko Watu Wakawa Wanafanya Biashara, Yasiyo Ya Haki na Wizi. Ndiyo Maana Aliwafukuza Pale Si Mahali Pake Pa Kufanya Mambo Yale. Hata Makonda Ile Ofisi Aliyopewa Ni Kwa Huduma Wala Si Visasi Na Kuweka Watu Polisi Kiholela Holela Tu. Mamlaka Na Ofisi ZaSerikali Lazima Ziheshimiwe