Gwajima: Taifa tumekosa maono, inakuwaje kujenga reli kabla ya kuchimba chuma? Waziri Mwigulu ampinga

Bidhaa nyingi zinazozalishwa nchini sasa hivi ziko out of reach or means kwa wananchi wenzetu because of prices? ukiwauliza manufacturers wanalalmika taxes?
hizo chuma zingetolewa bure?
 
Bidhaa nyingi zinazozalishwa nchini sasa hivi ziko out of reach or means kwa wananchi wenzetu because of prices? ukiwauliza manufacturers wanalalmika taxes?
hizo chuma zingetolewa bure?
Sasa kama mashine zote na spares zote zinatoka nje unategemea nini kwa bidhaa zake. Na kwanini hatuzalishi hizo mashine humu? Hatuna chuma. Hakuna aliyesema kitatolewa bure.
 
Ok tuseme ana hoja kwanini iwe chuma tu? Pamba, dhahabu, almasi, Tanzanite, korosho na mengine mengi tu kwanini tusiwe na viwanda vyetu tuuze product sio raw materials. Kwani ukiwa na chuma ndio utajenda reli. Hapa tuna mbao kibao lakini furniture tunanunua toka nje kwanini? Kuuza raw materials haikufanyi kuuza bidhaa bora hatuna uwezo huo vibiriti vyetu mpaka kiwake umemaliza njiti 30. Nakubaliana na yeye kama nchi ni lazima tuwe na vision, tunataka kuwa nini wauzaji au watengenezaji.
 
Sasa kama mashine zote na spares zote zinatoka nje unategemea nini kwa bidhaa zake. Na kwanini hatuzalishi hizo mashine humu? Hatuna chuma. Hakuna aliyesema kitatolewa bure.
na wale watakao zalisha hizo machine au parts watapunguza bei zakuuza? logic here ni the tax structures are to high??
 
Sasa Mwigulu hiyo vision 2025 ndio mpango wa muda mrefu? Unajua tofauti ya short na long term Plans? Miaka 25 huwezi kuita long term ni makosa! Projections za miaka angalau 50 ijayo would suffice. Inakupa maono ya jinsi mnavyotegemea nchi iwe!
 
na wale watakao zalisha hizo machine au parts watapunguza bei zakuuza? logic here ni the tax structures are to high??
Hujui kuwa kitu kinachoagizwa na kinachozalishwa ndani kodi zao ni tofautu kabisa?
 
Watu wanamjibu Gwaji boy personal,,, ila hawajibu hoja zake...

But Gwajima ana point nzuri sana,, ni kukaa na kuiweka sawa tu... na Viongozi hawaipendi kwasababu wanaona itawabana...
 
Kama chuma kinapatikana, uzalishaji unaanza halafu kwenye tenda kunawekwa kipengele cha kutumia chuma kutoka ndani ya nchi.
Kwa maneno mengine gharama inapungua, pia biashara na ajira vinaongezeka.
Mbona sukari ya ndani ina bei kuliko na nje? hatujiulizi kwanini? nchi hii inashida kwenye mifumo ya tax sio attractive nchi inatoza kodi kubwa sana haivutii ni rahisi kuwa na kiwanda china kuliko hapa ndio maana unakuta bidhaa za ndani zinabei kuliko za nje pamoja na ushuru. Nchi ina cheap labour lakini kwanini viwanda vinashindwa kushindana mp
 

Kuna mambo ni magumu kufanyia uamuzi bila ku-dig deeper..., na katika hili suala tuakiacha Siasa kuna ingredients mbili za muhimu za kufahamu...

Je Production cost ya Tani moja ya Chuma mpaka inakuwa tayari ni kiasi gani ?
Je Tani hio ikinunuliwa inaponunuliwa mpaka kuletwa hapa ni kiasi gani ?
Je uchimbaji na utayarishaji wa hicho chuma hapa mpaka kinaenda sokoni kitaleta faida ya kiasi gani kama tukiuza bei sawa na washindani wetu ?

Hapo ndio naweza kuchangia vizuri nini kifanyike nikipata hizo data....

Nadhani ni vema kumalizia na Msemo wa Adam Smith

It is the maxim of a every prudent master of a family, never to attempt to make at home what it will cost him more to make than to buy.
 
Hayuko sahihi. Nikueleze kwa kirefu kidogo. Kwanza nchi kuwa na madini ya chuma ni kitu kimoja na kuyachimba na,kuyabadilisha kuwa aina,kadhaa za chuma ni suala,lingine linalotegemea kiwango cha teknolojia nchi ilichonacho. Hicho kinachoitwa chuma kitaslam kinaitwa iron ore, ambapo ukishachimba unayeyusha na kupata pig iron, baada ya hapo kama una teknolojia unaweza kutengeneza aina kadhaa za steel na alloys zake. Sio kuwa maadam ni chuma basi unajengea tu reli au na mabehewa. Pili bidhaa kuzalishwa ndani ya nchi sio factor ya kufanya bidhaa hiyo iwe cheap; kuna bidhaa zinatoka Kenya kuletwa Tanzania lakini zinauzwa rahisi kuliko bidhaa hizo hizo zinazozalishwa Tanzania.

Nchi kama Korea na Japan ni watengenezaji wakubwa duniani wa meli, mabehewa na bidhaa zingine za vyuma lakini kwao hakichimbwi chuma. Switzerland wanatengeneza best chocolate lakini hawalimi cocoa. Ili nchi izalishe bidhaa bora lazima iwe na teknolojia yake sio kuzalisha kitu under licence au kujenga kiwanda cha kuunganisha bidhaa mfano magari au mgeni toka nje anajenga kiwanda ambacho kinazalisha hatua fulani ya bidhaa kisha nchi inatamba kuwa ina viwanda. Huwa nawauliza watu kuwa kuna,mtu mweusi anajua kugeuza,mchanga/udongo kuwa machine?
Pia nchi inaweza kuzalisha bidhaa lakini isiwe na comparative advantage hivyo bidhaa hiyo inaweza isiweze kushindana hata katika soko lake la ndani na bidhaa toka nje.

Sio lazima materials yatoke ndani ya nchi, mradi unapofanywa kuna manufaa ya,moja kwa moja kama vibarua na yasio ya,moja kwa moja kama supply ya vyakula na vitu vingine hivyo kuchochea ukuaji wa shughuli za,kiuchumi kutokana,na mradi huo mmoja tu.

Hicho chuma hata kikichimbwa bado ni iron ore tu inaweza kuwa aina ya chuma kinachohitajija kwa ujenzi wa reli ni lazima kiwe kimetengenezwa hatua kadhaa za process eg stainless steel, cast iron nk.kila mkataba unapofungwa kinachotakiwa ni quality output hivyo huwezi kulazimisha materials ya kazi yatoke nchini kwako, na hata yakitoka nchini kwako materials hayo yanauzwa kwa,bei ya soko hayatolewi bure kwa sababu kampuni inayozalisha hicho chuma inauza kwa faida na bei yake inaweza ikawa iko juu na kampuni inayojenga reli ni nyingine hivyo hizi ni kampuni mbili tofauti hivyo hazina uhusiano wa baba na mtoto.

Uchumi uko complex sio kama baadhi ya watu waanavyodhani.
 
Upo off point na Mbunge, either hujamwelewa kabisa!! Yeye anachojaribu kusema ni kuwa shambani kwetu tayari Kuna nyanya na zinaweza kuvunwa na kuivishwa, hivyo katika kupika chakula inatakiwa ujitahidi utumie nyanya zako ulizovuna shambani!! Sasa swali lake ni iweje tukimbilie kununua nyanya Kwa jirani ilihali za kwetu zingeiva na kutumika kupunguza hasara hii kubwa ya manunuzi!? Tena Kwa Dola kutoka nje!!
 
Hili suala amewahi kuongea ZZK kitambo kidogo. Sijui kama kuna watu walimueleawa. Yaani chuma kwanza, reli ndo ifuate.
 
Mimi nimejibu kama mchumi tena professsional yeye amezungumza kama layman asiyeelewa abc za uchumi

Mimi nimechangia kama,mchumi yeye amazungumza kama layman .
 
Hii habari ya comparative advantage ipo kumfanya mzalisha raw materials aendelee hivyo maisha yote, na anaetumia materal hayo kuzalisha bidhaa ghali aendelee hivyo. Ina usanii ndani yake. Ghana wamekuwa na mpango wa kuzalisha chokleti nchini mwao. Viwanda kadhaa vimeshaanzishwa na vinafanya kazi. Leo kwa kiasi Tz tunaweza safisha dhahabu, zamani walisema, kama wewe, "Mtu mweusi hawezi." Hao unasema hawachimbi chuma ila wanazalisha meli unawaangalia leo, huko nyuma walinunua iron ore kila kona na kufua chuma. Chuma ndiyo msingi wa viwanda.

Ukiweka factor za uzalishaji sawa, bidhaa za ndani zinakuwa na bei ya chini kuliko za nje. Na wenzetu wakati wanakua walizilinda bidhaa zao za ndani hata dhidi ya za bei ya chini kutoka nje.
Ipo hivi, ingefaa sana tujitosheleze kwa chuma. Ingefaa sana reli yetu tungejenga kwa chuma chetu.
 
Unapoandika mambo mengi, inaonyesha fika umeelimika, je huoni umuhimu wa wewe kushauri kuendeleza raw material ya ndani uliyonayo na kuzalisha ajira ya kiwanda huku ukiwa tayari na soko la kujiuzia chuma!? Fikiria reli ya tazara, kulikuwa na viwanda kama Mang'ula kule ifakara, huona saving ilikuwa kubwa!! Tunapochambua hoja tuweke na uzalendo Sio story TU!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…