Hayuko sahihi. Nikueleze kwa kirefu kidogo. Kwanza nchi kuwa na madini ya chuma ni kitu kimoja na kuyachimba na,kuyabadilisha kuwa aina,kadhaa za chuma ni suala,lingine linalotegemea kiwango cha teknolojia nchi ilichonacho. Hicho kinachoitwa chuma kitaslam kinaitwa iron ore, ambapo ukishachimba unayeyusha na kupata pig iron, baada ya hapo kama una teknolojia unaweza kutengeneza aina kadhaa za steel na alloys zake. Sio kuwa maadam ni chuma basi unajengea tu reli au na mabehewa. Pili bidhaa kuzalishwa ndani ya nchi sio factor ya kufanya bidhaa hiyo iwe cheap; kuna bidhaa zinatoka Kenya kuletwa Tanzania lakini zinauzwa rahisi kuliko bidhaa hizo hizo zinazozalishwa Tanzania.
Nchi kama Korea na Japan ni watengenezaji wakubwa duniani wa meli, mabehewa na bidhaa zingine za vyuma lakini kwao hakichimbwi chuma. Switzerland wanatengeneza best chocolate lakini hawalimi cocoa. Ili nchi izalishe bidhaa bora lazima iwe na teknolojia yake sio kuzalisha kitu under licence au kujenga kiwanda cha kuunganisha bidhaa mfano magari au mgeni toka nje anajenga kiwanda ambacho kinazalisha hatua fulani ya bidhaa kisha nchi inatamba kuwa ina viwanda. Huwa nawauliza watu kuwa kuna,mtu mweusi anajua kugeuza,mchanga/udongo kuwa machine?
Pia nchi inaweza kuzalisha bidhaa lakini isiwe na comparative advantage hivyo bidhaa hiyo inaweza isiweze kushindana hata katika soko lake la ndani na bidhaa toka nje.
Sio lazima materials yatoke ndani ya nchi, mradi unapofanywa kuna manufaa ya,moja kwa moja kama vibarua na yasio ya,moja kwa moja kama supply ya vyakula na vitu vingine hivyo kuchochea ukuaji wa shughuli za,kiuchumi kutokana,na mradi huo mmoja tu.
Hicho chuma hata kikichimbwa bado ni iron ore tu inaweza kuwa aina ya chuma kinachohitajija kwa ujenzi wa reli ni lazima kiwe kimetengenezwa hatua kadhaa za process eg stainless steel, cast iron nk.kila mkataba unapofungwa kinachotakiwa ni quality output hivyo huwezi kulazimisha materials ya kazi yatoke nchini kwako, na hata yakitoka nchini kwako materials hayo yanauzwa kwa,bei ya soko hayatolewi bure kwa sababu kampuni inayozalisha hicho chuma inauza kwa faida na bei yake inaweza ikawa iko juu na kampuni inayojenga reli ni nyingine hivyo hizi ni kampuni mbili tofauti hivyo hazina uhusiano wa baba na mtoto.
Uchumi uko complex sio kama baadhi ya watu waanavyodhani.