Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 34,256
- 44,597
Na. M. M. Mwanakijiji
Sielewi kwanini suala la Askofu Gwajima limefanywa kubwa mno kivile. Hakuna jambo lolote ambalo alilisema kwenye kile kikao chake na waandishi wa habari tunaloweza kusema lilikuwa ni kubwa mno kiasi cha kuonekana "kuchochea" wananchi dhidi ya serikali. Suala la matukio ya utekaji yamekuwepo Tanzania kwenye mazingira ya kisiasa na kiuhalifu tu. Kwamba, kuna mtu serikalini amekereka sana inashangaza!
Yaani, kweli kabisa serikali imepata taarifa toka kwa Gwajima kuwa kuna watu zaidi ya 80 wametoweka kwenye mazingira ya kutatanisha? Kwamba, baadhi ya waliotoweka au kuuawa ni watu wenye mirengo ya kisasa za upinzani? Kweli kabisa, Jeshi la Polisi, TISS na vyombo vingine vya usalama havijui uwepo wa matukio haya?
Hivi, kulikuwa na ugumu gani wa kumuita Gwajima kama walivyofanya kwa wanasiasa wengine na kutaka awape ushirikiano? Mbona haya yamekuwa yakifanyika mara kwa mara? Naamini Gwajima amefanya kosa moja kubwa ambalo linanifanya nisimuonee huruma moja kwa moja; afanye analotakiwa kufanya nalo ni kujiuzulu Ubunge na UCCM lakini pia, kama anataka kuingia kwenye siasa basi hana budi kujivua Uchungaji ili asichanganye mahubiri ya kanisa na malalamiko ya kisiasa...
Zaidi...
View: https://www.youtube.com/watch?v=i1W5Qcmlibw&lc=UgxBxMwrQwEzDpB8uCl4AaABAg