Gwajimanized na Samialization ya Siasa Zetu: Serikali Imelikuza la Gwajima

Gwajimanized na Samialization ya Siasa Zetu: Serikali Imelikuza la Gwajima

, kama anataka kuingia kwenye siasa basi hana budi kujivua Uchungaji ili asichanganye mahubiri ya kanisa
Hili Jambo alizingatie Sana.Na wale WA mfano WA the late mama lwakatare wasikimbilie vitu maalum Tu ya kaisari yabaki kuwa ya kaisari na ya MUNGU yabaki kuwa ya MUNGU..Watumishi wabaki na kofia moja Tu inawatosha.
 
Na. M. M. Mwanakijiji

Sielewi kwanini suala la Askofu Gwajima limefanywa kubwa mno kivile. Hakuna jambo lolote ambalo alilisema kwenye kile kikao chake na waandishi wa habari tunaloweza kusema lilikuwa ni kubwa mno kiasi cha kuonekana "kuchochea" wananchi dhidi ya serikali. Suala la matukio ya utekaji yamekuwepo Tanzania kwenye mazingira ya kisiasa na kiuhalifu tu. Kwamba, kuna mtu serikalini amekereka sana inashangaza!

Yaani, kweli kabisa serikali imepata taarifa toka kwa Gwajima kuwa kuna watu zaidi ya 80 wametoweka kwenye mazingira ya kutatanisha? Kwamba, baadhi ya waliotoweka au kuuawa ni watu wenye mirengo ya kisasa za upinzani? Kweli kabisa, Jeshi la Polisi, TISS na vyombo vingine vya usalama havijui uwepo wa matukio haya?

Hivi, kulikuwa na ugumu gani wa kumuita Gwajima kama walivyofanya kwa wanasiasa wengine na kutaka awape ushirikiano? Mbona haya yamekuwa yakifanyika mara kwa mara? Naamini Gwajima amefanya kosa moja kubwa ambalo linanifanya nisimuonee huruma moja kwa moja; afanye analotakiwa kufanya nalo ni kujiuzulu Ubunge na UCCM lakini pia, kama anataka kuingia kwenye siasa basi hana budi kujivua Uchungaji ili asichanganye mahubiri ya kanisa na malalamiko ya kisiasa...

Zaidi...


View: https://www.youtube.com/watch?v=i1W5Qcmlibw&lc=UgxBxMwrQwEzDpB8uCl4AaABAg

Mimi ninachojua Mwenyekiti kasema tuyakatae Magwajima kisha likafuata hilo kufutiwa usajiri na jana tu katuma salamu kuhusu dini za ushetani
 
Sielewi kwanini suala la Askofu Gwajima limefanywa kubwa mno kivile. Hakuna jambo lolote ambalo alilisema kwenye kile kikao chake na waandishi wa habari tunaloweza kusema lilikuwa ni kubwa mno kiasi cha kuonekana "kuchochea" wananchi dhidi ya serikali. Suala la matukio ya utekaji yamekuwepo Tanzania kwenye mazingira ya kisiasa na kiuhalifu tu. Kwamba, kuna mtu serikalini amekereka sana inashangaza!
Okay
 
Jamaa huyu mwanzisha thread tangu uchaguzi wa 2015 uishe akili hazijamkaa sawa. Ni wale watu wanafurahi kuona mtu ambaye alitofautiana naye kimawazo, anaishi maisha ya tabu na dhiki hata kama hana kosa. Ni diktekta mmoja uchwara wa hatari sana. Hivi kweli mauaji yanayoendelea ni kitu cha kawaida?
Nadhani hujamwelewa sana
 
Hata Mzee Kibao masikini mmemuuwa kwa kumdhalilisha sana haipendezi kabisa

Hii tabia ya kuwadhalilisha binadamu wenzio na baadaye kuwauwa Mungu atajibu soon
Ndio huko sawa, sasa mimi nausika vipi na hizo lawama zako

Kila mru alaumu kwa karata zake
 
Yes anapiga kimya as if hao wanaopotea si kitu ....
Kuna level ya hali ya juu ya serikali kutokujali raia, kuna dereva mmoja anashikiliwa South Sudan (alipe faini). Serikali kimya. Pesa za vitu vya hovyo hovyo za kina Diamond zipo ila rare situation ya raia kawekwa bond is up to family.
Diamond katafuta pesa kwa jasho na kujitoa kwa hali ya juu, inakera na kusikitisha kuona akili za kiunaharakati zikimuhusisha na upuuzi wa siasa zetu. Ni mtanzania kama mimi na wewe na anao uhuru wa kuwa na mienendo anayoona inamfaa yeye na wote wanaomzunguka.

Situation ya huyo dereva ni ya kushughulikiwa na wizara ya mambo ya nje na sio kuweka kundi moja na raha za Diamond.

Watanzania tuna hulka mbovu sana, kutaka kumpangia mtu maisha yake binafsi. Hatujui Diamond kahatarisha mangapi mpaka kufika hapa alipo lakini kwa sababu ya wivu wetu tunahisi tunayo haki ya kumsengenya.
 
serikali ilikuwa inatafuta mbinu ya kuzika Ajenda ya no reforms no election na swala la Lissu

hakika wamefanikiwa
Kama lengo ndio hilo basi wamekosea sanaaa, maana no reform no election na hii hoja zinaendana vinaya mno, na wanazid kuwapa cdm platform
 
Dr Martin Luther King Jr hakujivua uchungaji ili kutetea haki huko USA

Desmond Tutu hakujivua uaskofu ili kutetea haki huko South Africa

Gwajima hatakiwi kujivua haki zake za kikatiba ikiwemo uhuru wa kuabudu na kueneza dini na pia wajibu wake wa kiraia wa kukemea yasiyofaa katika nchi.

Alichokifanya Gwajima hakina tofauti na wanachokifanya maaskofu wa kikatoliki wanapotoa nyaraka za kukemea maovu kama vile utekaji watu au kutaka demokrasia iheshimiwe.

Hii dhana ya kutuaminisha kuwa Gwajima alikuwa sahihi pale ila alikosea pengine, ni dhana inayopandikizwa mdogomdogo ili kuvunja polepole kazi nzuri ya kutetea uhai wa watu aliyofanya Gwajima.

Uhai wa watu siyo kitu cha mchezomchezo lazima kiheshimiwe na kipambaniwe madhabahuni au kwenye jukwaa la kisiasa. Everywhere!
 
Gwajima mbona hajaituhumiu serikali?
Lakini si kamsema Samia Suluhu Hassan, ambaye ndiye Mwenyekiti wa CCM, na Rais wa nchi; ambaye serikali iliyopo iko chini yake?
Samia ndiye anayeteua na kutengua hao wakuu wa vitengo aliowazungumzia Gwajima.
Sasa utasemaje kuwa Gwajima "hajaituhumu serikali"?
 
Umeongea VIZURI sana mwanakiijji,ila Kuna kitu umesahau,tofauti ya waongeaji wengine ambao wamekuwa wakikosoa utekaji na uhalifu NCHINI,Gwajima yeye amekuja moja kwa moja kuihusisha hoja yake ya utekaji mamlaka za juu ya nchi hii...yaani akimaanisha kwamba Mamlaka za Uteuzi zinatoa baraka kwa watekaji...huo ni UCHOCHEZI...

Pia,maongezi Hayo anayafanyia kanisani,badala ya kanisa kuendelea na shughuli zake za kufufua WAFU na kuponya wagonjwa anafanya KAZI ya kuichamba SERIKALI.
 
Lakini si kamsema Samia Suluhu Hassan, ambaye ndiye Mwenyekiti wa CCM, na Rais wa nchi; ambaye serikali iliyopo iko chini yake?
Samia ndiye anayeteua na kutengua hao wakuu wa vitengo aliowazungumzia Gwajima.
Sasa utasemaje kuwa Gwajima "hajaituhumu serikali"?

Hilo wanajifanya hawajaliona...

Gwajima moja kwa moja kaituhumu serikali na kuihusisha na utekaji.

Mbaya zaidi mashambulizi hayo anayafanyia kanisani,anaachwa VIPI?
 
Naamini Gwajima amefanya kosa moja kubwa ambalo linanifanya nisimuonee huruma moja kwa moja; afanye analotakiwa kufanya nalo ni kujiuzulu Ubunge na UCCM lakini pia, kama anataka kuingia kwenye siasa basi hana budi kujivua Uchungaji ili asichanganye mahubiri ya kanisa na malalamiko ya kisiasa...
Kwani uko bungeni kaingia kwa kofia ya uaskofu? Si mwanasiasa pia?

Ukisiliza alichoongea kabla ajaaanza kuongea alijitambulisha kwa nafasi zake, nanukuu alisema yeye ni askofu, mbunge , mnec au kuna nec ya kiaskofu? Ila aliendelea kusema ile siku alikuwa anaongea kama mtanzania.
 
Hilo wanajifanya hawajaliona...

Gwajima moja kwa moja kaituhumu serikali na kuihusisha na utekaji.

Mbaya zaidi mashambulizi hayo anayafanyia kanisani,anaachwa VIPI?
Ni lazima niseme wazi.
Hukuelewa nilicho andika.
Haiwezekani, na hakuna siku yoyote ambayo wewe na mimi tunaweza kuwa na msimamo unaoafikiana katika jambo la nchi yetu. Kwa maana hiyo huwa sisomi chochote toka kwako humu JF.
 
Jamaa huyu mwanzisha thread tangu uchaguzi wa 2015 uishe akili hazijamkaa sawa. Ni wale watu wanafurahi kuona mtu ambaye alitofautiana naye kimawazo, anaishi maisha ya tabu na dhiki hata kama hana kosa. Ni diktekta mmoja uchwara wa hatari sana. Hivi kweli mauaji yanayoendelea ni kitu cha kawaida?
Hivi.. umesahau kabisa watu walisema "mama hatufokei"?
 
Kwanini mtu wa dini akihoji ionekane siasa lakini akisifia inakua sio siasa? Bado kosa la Gwajima halijawekwa bayana
Aliwasema nje ya kanisa....angehubiri yale majina 23 na mapendekezo yake kanisani au angezungumza Bungeni ambako ana kinga..
 
Back
Top Bottom