Gwajimanized na Samialization ya Siasa Zetu: Serikali Imelikuza la Gwajima

Gwajimanized na Samialization ya Siasa Zetu: Serikali Imelikuza la Gwajima

Na. M. M. Mwanakijiji

Sielewi kwanini suala la Askofu Gwajima limefanywa kubwa mno kivile. Hakuna jambo lolote ambalo alilisema kwenye kile kikao chake na waandishi wa habari tunaloweza kusema lilikuwa ni kubwa mno kiasi cha kuonekana "kuchochea" wananchi dhidi ya serikali. Suala la matukio ya utekaji yamekuwepo Tanzania kwenye mazingira ya kisiasa na kiuhalifu tu. Kwamba, kuna mtu serikalini amekereka sana inashangaza!

Yaani, kweli kabisa serikali imepata taarifa toka kwa Gwajima kuwa kuna watu zaidi ya 80 wametoweka kwenye mazingira ya kutatanisha? Kwamba, baadhi ya waliotoweka au kuuawa ni watu wenye mirengo ya kisasa za upinzani? Kweli kabisa, Jeshi la Polisi, TISS na vyombo vingine vya usalama havijui uwepo wa matukio haya?

Hivi, kulikuwa na ugumu gani wa kumuita Gwajima kama walivyofanya kwa wanasiasa wengine na kutaka awape ushirikiano? Mbona haya yamekuwa yakifanyika mara kwa mara? Naamini Gwajima amefanya kosa moja kubwa ambalo linanifanya nisimuonee huruma moja kwa moja; afanye analotakiwa kufanya nalo ni kujiuzulu Ubunge na UCCM lakini pia, kama anataka kuingia kwenye siasa basi hana budi kujivua Uchungaji ili asichanganye mahubiri ya kanisa na malalamiko ya kisiasa...

Zaidi...


View: https://www.youtube.com/watch?v=i1W5Qcmlibw&lc=UgxBxMwrQwEzDpB8uCl4AaABAg

Kwa maoni yako ukiwa kiongozi wa dini hutakiwi kukosoa na kukemea maovu yanayoonekana kushamiri kwenye jamii unayoiongoza kiroho?

Kuna shehe mmoja maarufu wa msikiti wa Temeke aliyewahi kuwa shehe wa mkoa wa Dar es salaam Al Hadi kama sikosei Kila mara alikuwa anatoa matamko ya kisiasa hukuwahi kutoa kauli hizi au kwa kuwa anasifia watawala?

Siasa ni mahusiano ya jamii na uchumi ( social economy relation) unamtengaje raia na masuala yanayohusu maisha yake kwa mfano?

Gwajima hana kosa, kama Raia ametumia haki yake kutoa maoni ambayo wengi ikiwemo wewe tumekosa ujasiri wa kukemea na kuyasema. Hana kosa labda kama hupendezwi na haki ya kuishi ya watanzania
 
Hakuna cha uongo alichosema Gwajima. Na hakuna kipya alichokisema.

Alichofanya yeye ni kuongeza tu sauti dhidi ya hayo matendo.

Na kwa kweli mpaka sasa hakuna aliyezipangua hoja zake kwa kutumia hoja na taarifa za ukweli.

Yeye katoa hoja. Wao wamemjibu kwa kutumia nguvu.

Ukweli huuma.

Na labda, ukweli unaposemwa na mtu wa ndani, huuma zaidi….
You nailed it, lakini mtoa Uzi ana majibu yake maana kwanza anajaribu kudowanplay impact ya utekaji nchini.

Kauli kwamba Kuna wengine waliishia sema ni kijinga, serikali ilitakiwa kuja na majibu siyo kiongozi mkuu kuja na vijembe na michambo wakati wananchi wanaona hali halisi.
 
Naamini Gwajima amefanya kosa moja kubwa ambalo linanifanya nisimuonee huruma moja kwa moja; afanye analotakiwa kufanya nalo ni kujiuzulu Ubunge na UCCM lakini pia, kama anataka kuingia kwenye siasa basi hana budi kujivua Uchungaji ili asichanganye mahubiri ya kanisa na malalamiko ya kisiasa...
Kwani siasa ni nini hadi Gwajima na viongozi wengine wa siasa hawaruhusiwi?

Askofu Bagonza amejibu swali hili mara nyingi tu, mbona hamuwasemi TEC na barua zao nyingi tu za kukemea? Au wanaogopwa? Maana imebaki kuwashambuloa akina father Kitima
 
Jamaa huyu mwanzisha thread tangu uchaguzi wa 2015 uishe akili hazijamkaa sawa. Ni wale watu wanafurahi kuona mtu ambaye alitofautiana naye kimawazo, anaishi maisha ya tabu na dhiki hata kama hana kosa. Ni diktekta mmoja uchwara wa hatari sana. Hivi kweli mauaji yanayoendelea ni kitu cha kawaida?
Mpuuzi huyu wa kupuuzwa na wengine wanaomuunga tena wako humu jukwaani ambao maisha ya wanayetofautiana mtazamo siyo muhimu
 
M.M long-time !

1. Serikali haijalikuza . Ni tatizo linaloisumbua jamii kwa sasa .Wasiojulikana wana nguvu zaidi ya vyombo vya dola, nani yu salama! Mjadala wa Wananchi kupitia Bunge umezuiliwa na Spika Tulia. Gwajima tofuati na wengine ameongea kwa uwazi ''ya moyoni' kama msemaji wa Wananchi.

2. Serikali haijalikuza, bali imekosa Watu wanaofahamu ku deal na situation wakidhani hoja inaweza kutekwa, pigwa rungu, risasi na maji ya washawasha. Hawafahamu hoja inajibiwa kwa hoja na hubaki hewani na mioyoni bila shurti na daima.

3. Wasio na ufahamu ndani ya serikali ni Short sighted, hawajui wa deal vipi na situation iliyopo.
Pili ni long sighted hawajui madhara ya siku za mbeleni. Mfano, wamefungia Kanisa , je Sheikh X akisema ya Gwajima watafungia misikiti? Viongozi wana set bad precedent bila kujijua.

4. Kwamba ajiuzulu , hapana! Ni vema 'revolt' ikianzia ndani ya CCM. Angesema CHADEMA au ACT ingeonekana ni wale wanaotumiwa na mbeberu. Kutoka ndani ya CCM inaeleza jamii jambo fulani halipo sawa. Inaeleza ''resentment'' katika jamii
 
Kinachonichekesha na kunikasirisha ni pale wale waliokaa kimya wakati Gwajima anaropoka. Wale waliomsifia na kumshangilia wakati anaropoka hadi kusema Serikali imepata mtemi wake, leo ndio wanakuja na vifalsafa vya ajabu ajabu;
Mara ooh, ashughulikiwe Gwajima sio Kanisa!
Mara ooh, sasa waumini wake watasalia wapi!

Mara ooh, Serikali imechukua hatua kali sana!

Kwani, wakati anaropoka, hamkujua kitachomtokea na kumuonya? Sisi tulioonya mapema si mlituona mapimbi? Sasa Kiko wapi?
Naona hapa ni level ya juu ya upumbavu, kama alikuwa anaropoka na wewe kwa akili yako ukaona anaropoka, kuwa hakuna utekaji, upoteaji na mauaji ya watu basi mahali salama kwako ni Mirembe.
 
Gwajima mbona hajaituhumiu serikali?
Yenye mamlaka ya kuchunguza na kubaini wauaji yako kwa nani kama siyo serikali?

Anayeteua viongozi wa vyombo vya ulinzi wa usalama ni nani? Huwezi kusoma between the lines au una agenda maalum?
 
"Watu kama hao ni manabii wa uongo, ni wafanyakazi wadanganyifu ambao wanajifanya kuwa mitume wa Kristo. Na hii si ajabu, kwa sababu hata shetani hujigeuza aonekane kama malaika wa nuru. Kwa hiyo si ajabu kama malaika wake shetani nao wanajigeuza waonekane kama watumishi wa haki. Mwisho wao utakuwa sawa na matendo yao" -(2 Wakorintho 13-15)
Wakati mwingine inabidi tuwe na kipimo cha kupima afya ya akili, Gwajima ametoa hoja ambazo inabidi zijibiwe, badala ya kumjibu mnamshambulia binafsi.

Hapa umetuonyesha mapungufu yake?
Great minds discuss ideas
Simple minds discuss events
And foolish minds discuss people.

Kama mna akili hata ya kuazima jibuni hoja zake
 
unga kanisa. Chukua Ubunge. Chukua kadi ya chama. Aende anakotaka kwenda. Kiburi. Dharau. Mdini. Mtovu wa nidhamu. Mbaguzi. Anajificha kwenye “dini na haki” pale anapoona inamfaa yeye. Mnafiki! Tapeli mkubwa mcheza picha za ngono

Hakuna kanisa la ufufuo na uzima!! Ni utapeli mtupu wacha leo utapeli huo umakizike. Angekuwa anafufua angemfufua Magufuli aliyempa kura za Halima Mdee na kumleta Bungeni. Kwanza wananchi wa Kawe ametutapeli sana. AFUNGIWE tu TAPELI mkubwa
Ni tapeli kweli tunakubali, jibuni hoja zake nyie watekaji na wauaji.

Au mmejiunga na Idi Amin Mama kujibu mipasho na michambo badala ya hoja?

Tuanzie hapa: Kuna utekaji au hakuna?
 
Hili Jambo alizingatie Sana.Na wale WA mfano WA the late mama lwakatare wasikimbilie vitu maalum Tu ya kaisari yabaki kuwa ya kaisari na ya MUNGU yabaki kuwa ya MUNGU..Watumishi wabaki na kofia moja Tu inawatosha.
Kwa nini umzibe mdomoni asitumie haki yake ya kikatiba? Akina Bagonza, TEC, sheikh Ponda, Al Hadi, father Kitima. Unamkumbuka Mtikila?

Two wrongs don't make a right, mfumo wa uovu ulimpa ubunge that's right. Wote kwenye mfumo hawatakiwi kurepent wabaki huko huko?

Jaribuni basi kutumia akili hata za kuazima basi mtumie kujibu hoja zake
 
Umeongea VIZURI sana mwanakiijji,ila Kuna kitu umesahau,tofauti ya waongeaji wengine ambao wamekuwa wakikosoa utekaji na uhalifu NCHINI,Gwajima yeye amekuja moja kwa moja kuihusisha hoja yake ya utekaji mamlaka za juu ya nchi hii...yaani akimaanisha kwamba Mamlaka za Uteuzi zinatoa baraka kwa watekaji...huo ni UCHOCHEZI...

Pia,maongezi Hayo anayafanyia kanisani,badala ya kanisa kuendelea na shughuli zake za kufufua WAFU na kuponya wagonjwa anafanya KAZI ya kuichamba SERIKALI.
Kwani akina Bagonza, TEC wanafanyia kwenye mikutano ya kisiasa?

Ukiwa CCM lazima ujichatue uwe chizy
Hilo wanajifanya hawajaliona...

Gwajima moja kwa moja kaituhumu serikali na kuihusisha na utekaji.

Mbaya zaidi mashambulizi hayo anayafanyia kanisani,anaachwa VIPI?
Wewe juha wa CCM alifanya press conference, hiyo ni Moja. Kanisani aliweka sawa maana ya GWAJINIZATION

Pili mbona nyie wote machawa wa CCM hakuna hata mmoja anayejibu hoja zake? Je hakuna utekaji upoteaji na mauaji ya Raia?

Ukisema kweli unaachwaje? Mnatakiwa kupimwa afya ya akili
 
Naona hapa ni level ya juu ya upumbavu, kama alikuwa anaropoka na wewe kwa akili yako ukaona anaropoka, kuwa hakuna utekaji, upoteaji na mauaji ya watu basi mahali salama kwako ni Mirembe.
Kwahiyo, Gwajima katibu tatizo?
 
Kwahiyo, Gwajima katibu tatizo?
Kaliweka wazi tatizo, na hapo tumewajua wasiojulikana, wanaoteka watu, kuwavunja miguu, kuwapoteza na kuwaua watanzania.

Maana wamekasirika kuwekwa wazi wanataka wamdhibiti, na wewe umewajua ila dhamira yako ndio inakusaliti unaogopa kupoteza ajira yako ya buku 7
 
Kaliweka wazi tatizo, na hapo tumewajua wasiojulikana, wanaoteka watu, kuwavunja miguu, kuwapoteza na kuwaua watanzania.

Maana wamekasirika kuwekwa wazi wanataka wamdhibiti, na wewe umewajua ila dhamira yako ndio inakusaliti unaogopa kupoteza ajira yako ya buku 7
Kaliweka wazi sawa. Kwahiyo, way forward ni nini?
 
Kaliweka wazi sawa. Kwahiyo, way forward ni nini?
Serikali ya wauaji iwajibike siyo kutaka kuzima sauti zinazopinga mauaji yao.

Na nyinyi CHAWA wa buku 7 muanze kupaza sauti kukemea leo ni CHADEMA kesho itakuwa ndugu yako
 
Wakati mwingine inabidi tuna kipimo cha kupima afya ya akili, Gwajima ametoa hoja ambazo inabidi zijibiwe, badala ya kumjibu mnamshambulia binafsi.

Hapa umetuonyesha mapungufu yake?
Great minds discuss ideas
Simple minds discuss events
And foolish minds discuss people.

Kama mna akili hata ya kuazima jibuni hoja zake
Hiyo ni level ya akili yako na Gwaji boy, usituweke kwenye level zenu ambazo ni imbecelic
 
Serikali ya wauaji iwajibike siyo kutaka kuzima sauti zinazopinga mauaji yao.

Na nyinyi CHAWA wa buku 7 muanze kupaza sauti kukemea leo ni CHADEMA kesho itakuwa ndugu yako
Wenyewe mbona wanuana???
 
Back
Top Bottom