DOKEZO Habari hii ikufikie Waziri wa Afya, ubabe wa Hospitali ya Muhimbili utaniua

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
Waziri wa Afya ninaandika hili kwa uchungu mkubwa na majuto ya kujitawala, mimi ninaumwa nilikwenda hosipitali ya mkoa nikafanya X-Ray na Ct-Scan, kisha nikapewa rufaa kwenda Muhimbili.

Nimeenda Muhimbili tarehe 9/11/2023 nikiwa na CD ya Ct-Scan ili daktari aicheze kuona tatizo langu, daktari hawezi kuicheza mpaka niipeleke ICT eti waikopi waiweke kwenye mfumo wa Muhimbili!

Na ili waikopi ninatakiwa nilipe sh 86,000/=? Bila hivyo nikae na CD yangu nikafilie mbali, sina hela hiyo na pia sioni uhalali wa malipo hayo kwani hiyo CD ukiweka kwenye kompyuta inafunguka haihitaji uchawi wowote ule.

Mhe. Waziri walionipa CD hiyo ni hospitali ya Serikali na niligharamia hiyo Ct- Scan kwa ajili ya madaktari wajue tatizo langu na si kwa ajili yangu binafsi ya kutengeneza Bongo muvi, hiyo CD kwangu mimi ni nyangarakasha kwani sina utaalamu wa kuisoma na nimeingia hasara ya kufanya Ct- Scan.

Kwaheri kuonana ni majaliwa.
Mungu atusaidie, huduma za afya za Tanzania zinatia kinyaa mpaka basi. Watanzania tupo tupo tu, hakuna kiongozi yoyote mwenye kujali maisha ya watanzania. Tunaishi kwa kudra za Mungu tu, ila kwamba kuna msaada wowote wa serikali ni uongo!!

Mzazi anakufa na mtoto kisa 160,000/=. Wakati huo huo kuna nyumbu inazunguka na punda na baiskeli kuipamba CCM na serikali yake. Ni wendawazim tu wanaweza kuelewa haya maigizo.
 
Dah umenipa wazo kubwa sana ngoja nitafute watu wa It tufanye intergration
Yeah.. easy tu.. ingawa ktk lugha itawapa changamoto kiasi. Kuna namna ya kuondoa hiyo changamoto kwa kuinsert API's mbalimbali za translation.
 
Yeah mkuu n mbona inawwzekana maana hata AI zilizopo zinfanya kazi hizo hizo tu hii Project ulosema nimeipenda how to start it inawezekanaje kuifanya ?
 
Muhimbili kuna shida kubwa ...
Sijajua ni uchache wa watumishi au wingi wa wagonjwa?

Kuna shida kwanza ya mifumo ya computer.. Yaani data za wagonjwa.. Madaktari..uhasibu... Na vitengo kama Radiology ..havisomani ..

Data za mgonjwa ...akiambiwa nenda kitengo flani.. Kwa ajili LA tatizo lako..ukifika huko ukiwa umeshakaa foleni masaa 3 wanakujibu mbona hatukuoni kwenye mfumo wetu..

Kuna MTU alinidokeza kuna watumishi walionewa na kuondolewa kazini kwa kutoa huduma kwa wagonjwa ambao mifumo ya computer haisomani kwa shida za MTU wa IT ..

Yaani shinda ndani ya Taasisi inamuondoa mtumshi kazini ili wakija wakaguzi wapate sababu..yaani kuwatoa kafara watumishi kwa makosa yako mwenyewe ...
 
Waziri wa Afya ninaandika hili kwa uchungu mkubwa na majuto ya kujitawala, mimi ninaumwa nilikwenda hosipitali ya mkoa nikafanya X-Ray na Ct-Scan, kisha nikapewa rufaa kwenda Muhimbili.

Nimeenda Muhimbili tarehe 9/11/2023 nikiwa na CD ya Ct-Scan ili daktari aicheze kuona tatizo langu, daktari hawezi kuicheza mpaka niipeleke ICT eti waikopi waiweke kwenye mfumo wa Muhimbili!

Na ili waikopi ninatakiwa nilipe sh 86,000/=? Bila hivyo nikae na CD yangu nikafilie mbali, sina hela hiyo na pia sioni uhalali wa malipo hayo kwani hiyo CD ukiweka kwenye kompyuta inafunguka haihitaji uchawi wowote ule.

Mhe. Waziri walionipa CD hiyo ni hospitali ya Serikali na niligharamia hiyo Ct- Scan kwa ajili ya madaktari wajue tatizo langu na si kwa ajili yangu binafsi ya kutengeneza Bongo muvi, hiyo CD kwangu mimi ni nyangarakasha kwani sina utaalamu wa kuisoma na nimeingia hasara ya kufanya Ct- Scan.

Kwaheri kuonana ni majaliwa.
Ilikuwa ni bora zaidi ungalimuona Mkurugenzi Mtendaji/ Mkuu wa Muhimbili mara baada ya kutoridhishwa na maelezo ya huyo daktari. Kama naye jibu lake halingalikuridhisha ndipo ungalipeleka kisiasa kwa huyo waziri wa afya au kwa Makonda kupata msimamo wa kisiasa.

Ni kweli mifumo ya hizo CD za CT scans zetu hazisomani. Na huwezi kuifungua hiyo CD kwenye komputa yako. Inabidi upate na ku install application ya hiyo CT scan kutoka kwa waliotengeza hiyo CT scan machine. Huko play store haiko.

Ni kweli pia kwamba hiyo hospitali ulikofanya hizo CT scans ingaliweza kutuma hizo scan images kwa radiologists wa Muhimbili moja kwa moja in case wakashindwa kuifungua hiyo CD.

Si kweli kwamba IT wakiweza kuifungua hiyo CD wataona siri ya mgonjwa kwani hawana utalaam wa kutafisiri hizo images. Mwenye utalaamu huo wa kuzitafisiri hizo images ni daktari bingwa wa radiology. Hata daktari wa kawaida ni ngumu kuzitafisiri kwa ufasawa.
 
Enzi za mwamba hu Uzi ungekuwa umeshafutwa Kwa gharama yoyote Ili watu kulinda kazi zao
 
Yeah mkuu n mbona inawwzekana maana hata AI zilizopo zinfanya kazi hizo hizo tu hii Project ulosema nimeipenda how to start it inawezekanaje kuifanya ?
Kiserikali ngumu maana mifumo si ipo chini ya serikali mtandao..

Kama private ni rahisi kwa kukaa na wataalam wa programming hasa machine learning and AI developers. utawapa requirements na wao watakushauri zaidi.

Ingawa hapa Tz wataalam wetu wengi ni viande watakulia hela tu.. na prefer ufanye outsourcing kwa watu wanaojielewa.
 
Mkuu hata hizi System tunazotumia sasa lazma kuna mtu alipeleka proposal unajua imachukua mda sana kutype na kusikiliza mgonjwa inakuwa ninkazi mara mbili bado unatakiwa na kwenye faili uandike lakini itakuwepo Voice recognition inaweza kuwa sawa sana
 
Watanzania tafuteni hela mjue huduma za afya ni gharama sana, la sivyo mtaendelea kulalamika kila siku. Matibabu siku hizi sio bure ni hela.
Acha hizo, vipimo nilivitaka mimi na nilifanya vipimo 4 vikiwemo X-ray na CT- Scan na vyote nililipia bila tatizo pamoja na gharama za matibabu, kinachonikwaza ni hiyo shs 86,000/= ya kuiingiza DVD ya CT Scan kwenye mfumo wa Muhimbili badala ya dakitari kuisoma kwenye kompyuta yake na kunitibu.
Hebu nieleweshe wapi nimeshindwa kulipia.
 
Mkuu hata hizi System tunazotumia sasa lazma kuna mtu alipeleka proposal unajua imachukua mda sana kutype na kusikiliza mgonjwa inakuwa ninkazi mara mbili bado unatakiwa na kwenye faili uandike lakini itakuwepo Voice recognition inaweza kuwa sawa sana
Unaweza tumia 3rd party system ambayo unaassociate na computer yako so mfumo unakuwa unasomana wa ofisi na hiyo program cha msingi uwe na Microphone nzuri na sehem isiyo na muingiliano na sauti zingine.

Program itachukua sauti na kuibadiri yaan speech to text transformation. Sasa kuna mawili ipeleke moja kwa moja au itunze kwenye text file alafu ww baadae ndio u copy na kupaste ktk sehemu unazotaka (fields).

Mie niliintergrate mfumo wa autocompletion ktk computer yaan kila kitu inasuggest neno la kufata so nateremka chap chap.
 
Nina maswali kwako
Je uliambiwa kulipia hiyo fedha kwa mtu au kwa control number?
Je uliuona uongozi wa hospital kuulizia kuhusu uhalali wa malipo hayo?
Kiwango hicho cha shs 86,000/= ni kikubwa sana wakati hawajaitengeneza wao na hata wangeitengeneza wao bado ni kikubwa sana.
 
Waziri wa Afya ninaandika hili kwa uchungu mkubwa na majuto ya kujitawala, mimi ninaumwa nilikwenda hosipitali ya mkoa nikafanya X-Ray na Ct-Scan, kisha nikapewa rufaa kwenda Muhimbili.

Nimeenda Muhimbili tarehe 9/11/2023 nikiwa na CD ya Ct-Scan ili daktari aicheze kuona tatizo langu, daktari hawezi kuicheza mpaka niipeleke ICT eti waikopi waiweke kwenye mfumo wa Muhimbili!

Na ili waikopi ninatakiwa nilipe sh 86,000/=? Bila hivyo nikae na CD yangu nikafilie mbali, sina hela hiyo na pia sioni uhalali wa malipo hayo kwani hiyo CD ukiweka kwenye kompyuta inafunguka haihitaji uchawi wowote ule.

Mhe. Waziri walionipa CD hiyo ni hospitali ya Serikali na niligharamia hiyo Ct- Scan kwa ajili ya madaktari wajue tatizo langu na si kwa ajili yangu binafsi ya kutengeneza Bongo muvi, hiyo CD kwangu mimi ni nyangarakasha kwani sina utaalamu wa kuisoma na nimeingia hasara ya kufanya Ct- Scan.

Kwaheri kuonana ni majaliwa.
Je unafikili ni dactari yeyote anaouwezo wa kusoma majibu ya ct scan, wapo watu kwa kazi hii, kusoma kuona nini tatizo na kuandika report nini kinasumbua ,then dactari atatumia iyo report kufanya matibabu,

So kwamba iyo hata kwenye laptop inasoma sio hoja, nikutakie afya njema ila punguza malalamiko ,
 
Ripoti imeambatanishwa na DVD, aliyeisoma ni mtaalamu wa hispitali ya serikali.
Mimi bado sijapata mtu akithibitisha uhalali wa hiyo gharama ys shs. 86,000/= kwa ajili ya DVD kuingizwa kwenye mfumo wa Muhimbili, ili iweje!
 
Unaweza tumia 3rd party system ambayo unaassociate na computer yako so mfumo unakuwa unasomana wa ofisi na hiyo program cha msingi uwe na Microphone nzuri na sehem isiyo na muingiliano na sauti zingine.

Program itachukua sauti na kuibadiri yaan speech to text transformation. Sasa kuna mawili ipeleke moja kwa moja au itunze kwenye text file alafu ww baadae ndio u copy na kupaste ktk sehemu unazotaka (fields).

Mie niliintergrate mfumo wa autocompletion ktk computer yaan kila kitu inasuggest neno la kufata so nateremka chap chap.
Mkuu nataka unipe ABC nikaweke kwenye kakituo kangu Huko swekeni ili Niwarahisishie kazi..
 
Asante sana mkuu, nafikiri umeongea Point kubwa Sana ningekuwa karibu ungepata hata soda
CC:- Gentlemen_
Watu wanalaumu vitu kabla hawajauliza sababu.
Mara nyingi system admins kwenye taasisi nyeti au walipo watumiaji wengi wenye uelewa mdogo au uelewa mkubwa sana wa vifaa na mifumo ya ICT wana disable CD drive na USB ports kwa sababu za kiusalama wa mfumo(System).
Wanatoa access level kutokana na group flani Kama ilivyo muelezea mdau mmoja huko juu.

Mimi naona wangelaumu gharama kubwa za kuingiza hizo taarifa hapo ningewaelewa.
 
Back
Top Bottom