Habari mbaya: Uwanja wa Uhuru Dar, Watu 45 wapoteza maisha kutoka na msongamano

Kaweka mfumo wa usiri unaoendelea mpaka sasa kwa hiyo haepuki lawama.

Lawama za mambo ya kimfumo hqziishi mtu akifa.

Baba ukishindwa kuelimisha wanao, hata ukifa utabaki na lawama tu.

Kifo chako si mwisho wa lawama kwako.
There you go!

Lawama ishapatikana.
 
Msiba huu wa kulia ni mama Janeth amepoteza mume na wanae wamepoteza baba sasa wewe mjamzito unajifanya una mahaba sana na marehemu kiasi unakokotana na wanao kujifanya una uchungu sana ili ukamuage,inatosha kuumia na kumlilia moyoni Watanzania kujipendekeza kutawamaliza.
 
Yani hii nchi miaka 60 ya uhuru ila ujinga ndo unaongezeka KWA kasi ya 5g licha ya kuwa na shule na vyuo. Hao wazee afya mgogoro na corona si wangetulia tu
Mkuu mambo mengine mimi nabaki kushangaa tu. Kweli akili za watanzania zina kasoro kubwa sana. Halafu tukisema hivi kuna wapumbavu wanasema tunaona wivu! Kwao watu wakifa na kuambukizana corona ni sawa tu. Jirani kwetu tumepata habari sasa hivi kuna dada mmoja kachukuwa mtoto wa jirani kaenda naye huko na wote wamefariki! Just imagine ni ujinga wa kiwango gani. Halafu watu kama hao unakuta wengi wameenda just for curiosity !
 
Polepole anahusika.. Jana alihamasisha wanaccm na wengine kujitokeza kwa wingi kwenda kuuaga mwili wa JPM... Umati niliouona leo kupitia TV 📺..sio ajabu hayo kutokea.
Kwaio hapa kisheria anaweza kupatikana na hatia, si ndio?
 
TANZIA
Habari za jioni Mates mwenzetu Mbasa Mtua amepata msiba mkubwa sana kwa kumpoteza mwanae mmoja watoto wa mdogo wake watatu na mtoto wa kaka yake mmoja baada ya kukanyagwa uwanja wa Taifa walipokwenda kumuaga JPM,na hadi sasa hawajui house girl yuko wapi,watoto waliongozana na mke wa mdogo wake,msiba uko kimara nyumbani kwao,tuwaombee wako kwenye wakati mgumu sana,mwenyezi mungu awapumzishe kwa Amani[emoji120]
 
Curious for nonsense
 
Jeshi,TPDF,wangeachiwa waendelee kuratibu utaratibu wa kuaga mwili wa Rais( kimsingi ndo wahusika), lakini kimbelembele cha Gondwe na RPC wake, na CCM ya Polepole ndo haya yakatokea.
Msiba wa Nyerere hatukusikia haya,ingawa umati ulikuwa mkubwa sana kuliko wa JPM wa kulazimisha vilio
 

Kwenye mikusanyiko ya watu wengi ni hatari sana kujumuika kama mwili wako sio strong,kama mwili wako ni MPESEMPESE bora utulie nyumbani.
 
Polepole anahusika.. Jana alihamasisha wanaccm na wengine kujitokeza kwa wingi kwenda kuuaga mwili wa JPM... Umati niliouona leo kupitia TV 📺..sio ajabu hayo kutokea.
Polepole hahusiki ,hivi MTU umeshafika Hadi uwanjani si tayari umeshaaga? Kwani ni lazima ukaone? Mbona waliosimama mabarabarani wamepunga mikono na wameridhika?. Hii ni shughuli ya kitaifa hivyo wingi WA watu hauepukiki. Wafanye taratibu mbadala.
 
Watoto walienda kufanya nini?.
 
Ukiangalia Hata wale waliokimbilia Ndege Pale airpot unajiuliza tuko serious kweli???

Unawezaje kuacha kitu kama kile je mtu akiingia pale na Nia ovu na bomu akaweka kwenye ndege??

au Nani ana uhakika wale wote ni watu wanaomboleza wengine sio...Ni Jambo la ajabu sana lile.Management ya Watu hawa imekua mbaya kabisa na hatari zaidi na zaidi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…