Kwakweli hiki kinachoendelea sio sawa, hivi ndugu hawana msemo kwenye huu msiba, hawa watu inabidi wampe heshima marehemu.
Mjomba kwa kweli leo wamemchosha, hakuna ubaya watu kutoa salamu zao za mwisho lakini sio kumuweka nje siku nzima kama walivyofanya leo.
Kuna ubaya gani baada ya kutua Dodoma wangemtia kwenye chopa kesho wakamzungusha mitaa michache, wakatoa masaa kadhaa ya kuagwa uwanjani tena watu wapite mbali na jeneza (kuondoa bottleneck) zoezi liwe la haraka sio kama walivyofanya uhuru leo.
Yaani siku nzima wanamzungusha hilo sidhani kama ni sahihi.