Habari mbaya: Uwanja wa Uhuru Dar, Watu 45 wapoteza maisha kutoka na msongamano

Habari mbaya: Uwanja wa Uhuru Dar, Watu 45 wapoteza maisha kutoka na msongamano

Salaam Wakuu,

Kuna habari mbaya ya watu wengi kufariki wakati wakiaga mwili wa hayati Magufuli.

Inadaiwa baadhi ya watu wamepelekwa Hospitali ya Temeke wengine wakiwa wamepoteza maisha na wengine kuzimia.

Nmempigia Mganga Mkuu wa Hospitali ya Temeke kumuuliza juu ya vifo hivi, baada ya kujitambulisha tu, akanikatia simu. Hivyo nmeshindwa kujua Idadi kamili.

Hapa chini ni baadhi ya watu waliotajwa kupoteza maisha kenye msongamano Uwanja wa Uhuru Temeke Dar es Salaam



TANZIA!
TUNASIKITIKA KUTANGAZA KIFO CHA MWALIMU JANE NGONDE (MWALIMU MKUU WA S.M MGEULE) KILICHOTOKEA LEO MCHANA UWANJA WA BENJAMIN MKAPA ALIPOKUWA AKISHIRIKI KUTOA SALAMU ZA MWISHO. TARATIBU ZA MAZISHI ZINAFANYIKA NA TUTAENDELEA KUJULISHANA. AIDHA TUNAITAARIFU KAMATI YA MAAFA- UVEMI KUENDELEA NA TARATIBU ZETU. R. I.P

Nyingine:

TANZIA: Mboka Nsobi Minga amefiwa na mkewe Lidia Shomari Minga ambaye leo tarehe 21/3/2021 asubuhi akiwa mzima wa afya alikwenda uwanjani kuaga mwili wa Hayati John Joseph Pombe Makufuli. Kifo chake kimesababishwa na kukanyagwa na umati wa watu uwanjani hapo. Mwili wake umehifadhiwa hospitali ya Temeke. Msiba upo Kilwa road Barracks
View attachment 1731031
Lidia Shomari
Corona si mchezo mkuu
 
Hao ni physical victims wa msongamano. Sijui viral victims wa msongamano itakuwaje maana barakoa hazikupewa nafasi yake?

Mungu aliponye hili taifa liondokane na usukule wa hii miaka 5 iliyopita na awarudishie waja wake fahamu zao wajitambue kuwa wao ni binadamu hai wanaoishi!
Dah
 
Mipango mibovu huzaa maafa na simanzi. Kama wakubwa wanaoratibu hawakutafakari na kutathmini kutokana na matukio haya basi tutegemee wengi kuathirika na kuagwa kwa mpendwa wetu.
 
mleta mada tuwekee vyeti vyao vya vifo tuamani tasrifa zako kama vinasomeka wamekufa kwa msongamano.

Si vizuri kutangaza kifo cha mtu bila kuambatanisha death certificate
Wazee wa kuficha maradhi kazini, halafu kifo kina waumbua.
 
Hv unadhn ana akili huyu zombi????
Kwa hiyo ajali zikitokea barabarani polisi wakitoa taarifa huwa na death certifacate?

Watu walioko eneo la tukio au ndugu zao wasiseme neno mpaka death certificate?
 
Hv unadhn ana akili huyu zombi????
Jamaa lina roho mbaya na kikatili katili sana. Ukimsoma hapo analalamika why taarifa za waliokufa au kuumizwa zitangazwe? Anaamini ktk usiri ili aje awalaumu wanyetishaji huku akigombea maiti ambayo alificha maradhi yake! Yehodaya Atakuwa Madelu huyu siyo bure.
 
Kweli Watanzania, tunajijua wenyewe....., utakuta hapo pia walikuwepo wazazi wanawapeleka pia watoto wao, mtu unabana wenzako, unakimbia na kuwakanyaga eti ili uende kuaga mtu aliyeondoka..., si kwanza uwaage hawa unaowakanyaga ?
 
@GENTAMICINE alionya hapa mchana akitumia neno inaweza tokea stampede na kusababisha vifo naona maneno yake yametimia.
 
Watu wangu wanaangamizwa kwa kukosa maarifa Mimi nilishangaa kina Mama na watoto huko kwenye misongamano
Kuna mmoja jana alikuwa na kichanga kama cha miezi miwili, walimkandamiza, yaan ni aliminywa firigisi na utumbo mi nilijua anakufaa haloo usiombe [emoji848][emoji848] mi na rafiki yangu tukamnyang'anya mtoto..alivyochoropoka hapo tukamnasa vibao vitatu tukamrudishia mtoto wake, alikuwa anatafuta upenyo wa kurudi home, maana si kwa ukunga ule kwa mminyo wa kufa mtu
 
Kuna mmoja jana alikuwa na kichanga kama cha miezi miwili, walimkandamiza mi na rafiki yangu tukamnyang'anya mtoto..alivyochoropoka hapo tukamnasa vibao vitatu tukamrudishia mtoto wake, alikuwa anatafuta upenyo wa kurudi home
Hivi hawana wanaume hawa wanawake maana majority wamevaa Madera wanaenda kutafta sifa za kijinga kuzurula na watoto wadogo. I'm sure hapo uhuru wamekufa wengi
 
Stampede! kulikuwa na Dalili zote watu wanasombwa na Maloli huku uwanja mdogo

Sasa maambukizi wanaenda mitaani kwenye misiba 🙁
 
Back
Top Bottom