Habari Njema Kutoka Barrick Gold kwa Watanzania, Tunaanza Kufaidi Rasilimali Zetu, Donge Nono la Dola Milioni 100 zalipwa

Habari Njema Kutoka Barrick Gold kwa Watanzania, Tunaanza Kufaidi Rasilimali Zetu, Donge Nono la Dola Milioni 100 zalipwa

Mzeebaba bado namind Barrick kulipa mpunga wametukata mdomo sisi upinzani tulishajipanga kuangusha mabomu kwa mkulu kama wangegoma
Sasa mtu ulisema kakudhulumu buku mi nikakwambia huyo buku hakulipi tukabishana weee halafu akaja kukulipa sh5 katika buku na bado unajisifia!!! Hivi dola bilioni190 hadi dola milioni300 ni sawa kweli?
 
Najua jukwaa hili lina wataalamu mbalimbali. Na ninajua kuwa pia kuna watu wa serikali huwa wamo humu na huwa wanafuatilia yanayojadiliwa humu.

Mtu muungwana ni yeye yule atoae ushauri kwa kuzingatia Uzalendo. Na mtu muungwana kwa upande wa pili ni yeye yule apokeaye ushauri na kuufanyia kazi.

Lengo ni kujenga nchi yetu pendwa. Maendeleo hayana vyama.

Karibuni.


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mbona hizo hela ni kidogo sana aisee,yaani sisi hapa ofisini ni budget ya mwaka .Sasa million 100 mpaka kwenye magazeti tunaandika?duuu safari ya Tz ni ndefu.

Ila sawa angalao hicho wametoa ila bado aisee wametupiga sana ujue hakuna kodi nyingine watatoa kwa next 5 years zaidi ya hizo mil 300.

Na tukicheza kwenye hiyo kanuni mpya share ya yetu inaweza kuwa ni hela hiyo hiyo ikawa moja toa moja sifuni.
 
Tunashukuru kwanza zimelipwa na zimefika hazina sasa swala la nini kifanyike kwa matumizi ya hizo hela Serikali ina wataalamu na wabobezi pia washauri wataoweza kutoa maoni na wapi na kuna uhitaji mkubwa kiasi gani.

Kwa maana hatuwezi hatuwezi kusema ziende mashuleni wkt kuna Afya pia upande mwingine tuna Maji.

Hivyo naamini wahusika watakaa na kufanya maamuzi yaliyo sahihi kwa maendeleo ya TAIFA TEULE TANZANIA.
 
Blood of Jesus,

1. Ujenzi wa daraja linalounganisha kigongo busisi mkoa wa mwanza
2. SGR kutoka mwanza kwenda singida
3. Ujenzi wa bwawa la kuzalisha umeme la Julius nyerere.
4. Ujenzi wa barabara kutoka kahama kwenda geita
5.ujenzi wa barabara kutoka mugumu Serengeti kwenda tarime mkoa wa Mara.
6. Ujenzi wa mradi wa maji kutoka tabora , kwenda singida na dodoma,maji yanayotoka ziwa Victoria.
7. Endelea kuongeza....
 
Mbona hizo hela ni kidogo sana aisee,yaani sisi hapa ofisini ni budget ya mwaka .Sasa million 100 mpaka kwenye magazeti tunaandika?duuu safari ya Tz ni ndefu.Ila sawa angalao hicho wametoa ila bado aisee wametupiga sana ujue hakuna kodi nyingine watatoa kwa next 5 years zaidi ya hizo mil 300.Na tukicheza kwenye hiyo kanuni mpya share ya yetu inaweza kuwa ni hela hiyo hiyo ikawa moja toa moja sifuni.
Samahani mkuu, nimesoma bilioni 250, sijui hii milioni 100 imekuja vipi? Naomba kueleweshwa mkuu.
 
Back
Top Bottom