Habari nyeti na nasaha zangu kuhusu vijana watakaofanya kazi na DP World

Habari nyeti na nasaha zangu kuhusu vijana watakaofanya kazi na DP World

FaizaFoxy

Platinum Member
Joined
Apr 13, 2011
Posts
100,246
Reaction score
123,145
Vijana wa Kitanzania,

Msione tabu au uvivu kukisoma kilichopo chini, ni kwa manufaa yenu na ya Tanzania kwa ujumla.

Jana kuamkia leo ilibidi nifanye mawasiliano na Diaspora wa Tanzania waliopo Dubai. Nia na dhumuni ilikuwa ni kutafuta connection ya kuwatafutia vijana fursa za kazi ndani ya DP World.

Kwa bahati niliyeongea nae kwanza, kijana mwenzangu wa zamani, maarufu sana Dar au niseme Tanzania nzima, kwani alikuwa ni mcheza mpira wa kusifika enzi hizo.

Baada ya salaam na kuulizana ya hapa na pale nikamuuliza kuhusu DP World kama ana connection yoyote, kwanza kacheka akanambia wewe mtu zaidi ya wa kumi kuniuliza. Kwa ufupi, alikuwa na mtu tena mwema sana. Akanambia atanipigia baadae kidogo nimpe muda kidogo amtafute. Baada ya kama nusu saa akanistukiza kwa video conference call, akiwemo na huyo kijana ambae yupo jikoni, ndani ya Dubai World, hawa Dubai World ndiyo "mama" wa DP World. Tukaongea mengi sana.

Vijana wa Kitanzania watakao bahatika kupata kazi na DP World watafaidika na mengi. Kwa uchache:

1) Kutakuwa na kila aina ya ajira, wenye ujuzi na wasio na ujuzi watachukuliwa.

2) Mafunzo ya kazi ya mara kwa mara, ndani na nje ya nchi, yatatolewa kwa watakao pata kazi.

3) Uhamisho wa kituo cha kazi wa mara kwa mara kwa watakao ajiriwa.

4) Hatastahimiliwi mfanya kazi ambae hafati muda wa kazi na deadlines za assgnments.

5) Wenye kujua Kingereza kwa kusoma, kuandika na kuzungumza ndiyo watakuwa na chance kubwa.

6) Wenye kujua kutumia kompyuta kiwepesi chance zitakuwa kubwa.

7) Ukiwa mwongo kwenye cv au vyeti au kazini, hata ukishaajiriwa utaikosa kazi.

8) Wana policies and procedures kwa kila hatua ya kazi, ukikiuka hata kidogo ujue hauna kazi.

9) Visingizio (excuses) havina nafasi kabisa.

10) Rushwa aina yoyote kwa anaetoa au kupokea, ni "mmediate termination" hata kwa anaejaribu kugusia au kuzungumzia tu, haina mjadala.

Nimechoka kuandika kwa sasa, kuna mengi sana ntakuwa nayajazilia kidogo kidogo.

Mbele huko ntajulisha mpaka namna ya kupata kazi. Wapi pa kuanzia.

Nayafanya haya kwa nia njema kabisa, sitaki malipo, wala sitafuti kiki, hakuna tunaejuana humu isipokuwa wachache sana, tena wa karibu sana kwangu.

Uliza chochote hapa hapa jukwaa la wazi, sijibu PM.

Mwenyezi Mungu awe nasi. Nita update baadae lakini napokea maswali muda wote.


Update: podt #86 ina. Maelezo kamilibya namna ya ku apply.
FF
 
Hata mkataba wa gas ya mtwara sifa za fursa tuliambiwa zitakuwa kama hizi hizi. Leo hii tunaambiwa gas sio yetu! Tuliambiwa bomba la gas likifika Dar, mgao wa umeme utakuwa ni historia. Hivi leo tunalia kilio cha mbwa mdomo juu. Ogopa matapeli.
 
Back
Top Bottom