Habari nzuri kwa makampuni ya Mabasi: CATL wazindua battery yenye lifespan ya miaka 15!

Habari nzuri kwa makampuni ya Mabasi: CATL wazindua battery yenye lifespan ya miaka 15!

Mad Max

JF-Expert Member
Joined
Oct 21, 2010
Posts
26,961
Reaction score
77,890
Watengenezaji wakubwa wa battery za magari ya umeme CATL jana (tar 13 Sept) wamezindua battery Tectrans Bus Edition kwaajili ya mabasi ya umeme yenye lifespan ya miaka 15 au Kilometa Mil 1.5 na warranty ya miaka 10 au kilometa Million 1.

Hii battery ina energy density ya 175 Wh/kg ambayo ni kubwa kulizo zote katika segment ya mabasi, na iko rated IP68 waterproof na inaweza kuvumilia masaa 72 ikiwa imezama kwenye maji.

CATL wameingia mkataba na makampuni ya mabasi ya Yutong Bus, Golden Dragon, and Dongfeng Motor kwaajili ya mass production.
images (2).jpeg

Hawa CATL ndio watengenezaji wakubwa wa battery za magari kwani wanachangia market share ya 37% au zaidi katika hii sector kwa mwaka 2024 na inazidi kupanda kwa kasi sana.

Hizi battery zinaweza kuchajiwa hadi 60% kutoka 0% kwa chini ya dakika 12 tu, kwahiyo ule muda wa kuchimba dawa unatosha kabisa kupata chaja ya kutosha. Pia full charge inakupa range hadi ya kilometa 500!
images (3).jpeg

Makampuni ya mabasi wanaweza kuangalia gharama za uendeshaji, wakifananisha mafuta na EV bus na kuamua kushift.
 
Mafuta yatashuka bei sana... wacha tuone.

Maana sahivi EV zinakuja kwa Kasi.

Nchi inatakiw iweke mikakati kuandaa mazingira ya kupokea EV.. hasa vyanzo vya kuchaji na ufundi wake.

Matajiri wamekosa washauri, wawekezaji hawana mazingira rafiki, Wananchi hawana elimu.
 
CATL ni kampuni ya kichina kama sikosei hawa wachina Wana balaa kubwa Sana kwenye magari ya UMEME.
Huku kwenye mabus ya UMEME ndiyo watakuwa wameua soko la mafuta Kwa kiwango kikubwa Sana maana wafanyabiashara wa mabus wataagiza Kwa wingi kama station za kuchajia zitakuwa nyingi Tanzania
 
Kwa safari ndefu kilomita mil 1.5 bus inazikata ndani ya mwaka na nusu
Million 1.5 km

1,500,000 km

Dar to Dodoma ni 500 km

Kwenda kurudi 1000 km

So ni trip (to&fro) 1,500

Kama kwa siku unaenda na kurudi same bus

Ni sawa na siku 1,500

Mwaka una siku 365

Sawa na miaka 4.

Kama kwa siku ni trip moja.

Miaka 8.
 
Mafuta yatashuka bei sana... wacha tuone.

Maana sahivi EV zinakuja kwa Kasi.

Nchi inatakiw iweke mikakati kuandaa mazingira ya kupokea EV.. hasa vyanzo vya kuchaji na ufundi wake.

Matajiri wamekosa washauri, wawekezaji hawana mazingira rafiki, Wananchi hawana elimu.
Matajiri wa mafuta wanahaha, matumbo joto
 
Way to Go. Japo naona gari na bajaji za gesi wanavyopata tabu na serikali badala ya kuweka incentive au policy huduma ipate wawekezaji wengi. Hata vituo vya kawaida waweke.

Sema ndio hivyo tatizo ngozi kwenye 10% tunanunulika kirahisi.
 
Back
Top Bottom