Hachafuliki: Tunampenda Rais Dikteta na Kichaa Aliyefanya haya

Na ukiwa na akili huwezi kumuona mwenye akili mwenzako
Unaona lakini unaangalia mapungufu zaidi.

Ndiyo maana Nyerere alivyowalalamikia Watanzania wanaangalia mabaya yake sana badala ya mazuri yake, nilimuona hana akili.

Tunatakiwa kuangalia mabaya ili tuyarekebishe, mazuri hayahitaji kurekebishwa sana kama mabaya.
 
Hata kina Stalin, Hitler, Idd Amin na madikteta wengine walifanya maendeleo ya vitu ila tunawakumbuka kwa ukatili wao. Binadamu atakukumbuka kwa hisia ulizomwachia nafsini na sio vitu ulivyomwachia. Kama uliumiza nafsi yake atakukumbukwa kwa maumivu uliyompa. Kwa mfano Mbowe ni kiongozi bora wa CHADEMA kuwahi kutokea ila anaweza akakumbukwa kama kiongozi wa hovyo endapo anguko la CHADEMA litatokea mikononi mwake. Magu atakumbukwa na maskini wengi kwa jinsi alivyokuwa anawafurahisha kwa kuwaumiza matajiri na watumishi wa umma. Maskini wengi hufurahia sana maumivu ya watu waliofanikiwa kiuchumi. Magu alilifahamu hilo ndo maana akaweza kukamata wajinga/maskini wengi.
 
Kwa hiyo vipindi vingine walioua walijulikana, kipindi chake ndio likaja neno "wasiojulikana"? Tofauti iko wapi kama wote waliua?
Kipindi chake hakutaka mkosoaji alibambikia watu kesi, kuminya wapinzani, kupendelea chato.
 
Kama mnajua alifanya hayo yote msingesimama kwenye Majukwaa na kuanza kupiga kelele kwa kumsifu Mama! Mama kajenga barabara,Mama kaleta Maji,Mama kajenga Hospitali,Mama kajenga madaraja,nk kumbe Mengi kafanya Magu!
 
Anamsifia kichaa nae ni kichaa
 
Naunga mkono hoja.Hivi kichaa anawezaje kufanya yote hayo manzuri
 
Vijana wako jobless ten years. sababu ni yeye, wengine umri wa kustaafu wanahesabu vidole tu. Tena bado mwanga wa kuajiriwa haupo.
 
For all haters, I salute you brother!
 
Hata wafanyeje😎
 
Kwa hiyo unataka mazuri uyaangalie katika awamu Moja tu hebu Anza na mbaya toka awamu ya kwanza Hadi tulipo Ili ueleweke zaidi.
 
Hakuna utawala usiomwaga damu!
Ukweli kwamba hakuna utawala usiomwaga damu haimaanishi kuwa watawala kumwaga damu ni kitu kizuri, tukikubali tu.

Kama vile ilivyo kwamba hakuna mtu asiyeumwa haimaanishi kuumwa ni kitu kizuri, tukikubali tu.
 
Umeongea kweli yote Mkuu.
Wenye akili tumeelewa.
Bahati mbaya, haya yote sidhani kama yameongelewa kwenye Kitabu cha Ka-flag
 
Kwa hiyo unataka mazuri uyaangalie katika awamu Moja tu hebu Anza na mbaya toka awamu ya kwanza Hadi tulipo Ili ueleweke zaidi.
Kwani wapi nimetetea awamu yoyote? Unaleta Whataboutism fallacy.

Mabaya ya Magufuli ni matokeo ya mabaya ya Nyerere.

Nyerere alichukua sheria za kikoloni akazirithi, akazitumia yeye. Jaji Nyalali kaziandika sheria 40 kandamizi.

Nyerere kafunga wapinzani wake kwa indefinite detention. Nyerere kapiga marufuku vyama vya siasa vya upinzani, miaka ya 1960s. Nyerere kalambisha asali za ubalozi kina Christopher Kassanga Tumbo tangu miaka ya 1960s.

Magufuli kaendeleza.

That does not make either right.

They are both wrong. Two wrongs do not make a right.
 
Samia ameumiza Watanzania wengi zaidi kuliko Rais yoyote.

Wengi wametekwa, kuna wangapi wameuwawa? ameuza maliasili nyingi za Taifa, waulize Wamasai, familia ya Kibao, Soka.

Sera zake zimepandisha Kodi, tozo, being ya umeme, vifaa vyao ujenzi, chakula, mafuta na kuwafanya Watanzania wengi makini zaidi.

Amewakumbatia wezi, mafisadi wote anawaambia kuleni kwa urefu wa kamba zenu.

Vilio kila sehemu wizi, uporaji wa viwanja mashamba, nyumba za maskini kila sehemu pamoja na ubakaji umeshamiri, uchomaji masoko, umeshamiri.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…