Ndugu zangu,
Kuna baadhi ya kikundi wanalazimisha kwa kufanya propaganda kuwa Tundu Lissu ni sawa na Raisi Magufuli, wanaenda mbali kwa kutaka ''mdahalo'', sijui nini na nini. Tuweke taarifa sawa, Tundu Lissu sifa zake ni hizi;
- Anagombea urais kutafuta ruzuku ya chadema ili angalau baada ya uchaguzi aweze kupata chochote
- Anaogombea urais ili kuwaridhisha wafadhili wake; mfano mzuri hata hadhira na mambo anayozungumza yanahusu wakenya na wazungu.
- Tundu Lissu anaamini miundombinu, hospitali,shule nk ni maendeleo ya vitu sio watu; sasa hapa kufanya naye mjadala wenye akili watakushangaa. Ni sawa na kumkimbiza kichaa.
Kwa hoja hizo tatu itoshe kusema inashangaza kuona baadhi ya watu wanaoamini kuwa Tundu Lissu anamaanisha analolofanya kiasi cha kumlinganisha na Rais John Magufuli ambaye ametekeleza kwa kufanya mambo makubwa kwenye ujenzi wa nchi. Magufuli anapaswa kufanya yafuatayo;
- Anapaswa kwa makini kutulia na kuona ni jinsi gani atatimiza manifesto (ilani) ya Chama cha Mapinduzi (CCM), ikumbukwe mambo mengi ametekeleza kuzidi matarajio (2015-2020) na sio kujadili mdahalo wa kujadili kuwa miundombinu ni maendeleo ya watu au vitu?
- Huyu ni mtu anayetumia akili kufikiri namna ya kuwaletea wananchi kwa kutumia rasilimali zilizopo na sio kufurahisha watu wa nje.
Aah itoshe kusema, Raisi Magufuli hahitaji kujieleza, yeye keshatenda. Ni jukumu la Lissu kuwaambia watanzani Je Barrick/Accacia wameshinda kesi MIGA?
Wasalaam.