Hadi sasa kuna uwezekano wa 75% wa fainali ya Simba vs Berkane kurudishwa Uwanja wa Mkapa

DELETED ACCOUNT

JF-Expert Member
Joined
Mar 25, 2010
Posts
9,805
Reaction score
15,476
Nitakuwa mtu wa mwisho kuamini kuwa mechi ya pili ya fainali ya Simba vs Berkane itachezwa Zanzibar.

Ndiyo, kuna uzembe mkubwa umefanyika katika ukarabati wa uwanja wa Mkapa na wachache tumekuwa tunapigia kelele hili suala kwa muda mrefu.

Ndiyo, kuna watu tulio nao hapo hapo Tanzania wana matamanio yao binafsi ya kisiasa au ya kimpira ya kutaka fainali ichezwe Zanzibar. Hili nililitabiri muda mrefu.

Ndiyo, kuna watu tunao katika maeneo mbalimbali ambao hawataki Simba ifanye vyema wameweka mikono yao ili Simba ipate ugumu katika harakati hizi za ubingwa wa CAF. Tukumbuke pia upotevu mkubwa wa mapato na kuingia gharama za ziada kwa Simba unaotokana na haya yanayofanyika kuinyima haki ya kutumia uwanja wa Mkapa.

Kilichofanyika kupeleka mechi Zanzibar ni hujuma ya waziwazi dhidi ya Simba iliyoshirikisha watu wetu wa ndani. Ni kama imepatikana "perfect storm" ya watu wa ndani na nje wamekutana katika nia na lengo moja. Inakuwa rahisi sana kulitekeleza jambo katika mazingira hayo.

Pia tukumbuke alichosema aliyekuwa Kocha wa timu ya Taifa Amrouche wakati wa AFCON, sisi tukaweka unyonge mbele na kuona kulinda mahusiano ya kidiplomasia ni muhimu kuliko hadhi na maslahi ya nchi yetu. Haya yote ni matokeo yake.

Kama kweli serikali haina mkono katika hili basi ionyeshe nguvu na ushawishi wake kwa kufanya kila inaloweza kurudisha fainali uwanja wa Benjamin Mkapa. Kinyume cha hapo, hizi hasira na manung'uniko yatabaki mioyoni mwa wapenzi na mashabiki wa Simba na hakuna anayejua watakuja kuzitoa vipi na wakati gani.

Tukumbuke, issue siyo kuchukua ubingwa. Issue ni mashabiki wa Simba wanataka haki yao ya kuishuhudia kwa macho yao timu yao ikibeba ubingwa huo katika uwanja iliyotengeneza nayo historia kwa miaka mingi. Haki hii haiwezi kupokonywa kirahisi kama baadhi ya watu wanavyodhani.

Narudia tena. Pamoja na juhudi za watu fulani fulani wa ndani na nje ya Tanzania kushinikiza hili la Zanzibar, na pamoja na kwamba nililiona mapema likifanyiwa kazi, nitakuwa mtu wa mwisho kuamini fainali hii itakwenda kuchezewa huko.
 
😂😂😂 Upuuzi tu... Kwa mkapa mkacheze na bodi ya ligi
 
Kwa hili namuunga mkono Mama😂😂 Mitano tena,Ametekeleza Na fainali ikachezwe Zanzibar kukuza uchumi wa blue
 
Kiongozi, hivi unajua pia CAF wiki iliyopita walisitisha uwanja kutumika kwenye Mashemeji derby hapo Kenya na kuelekeza uwanja ufungwe usitumike kwajili ya maandalizi ya michuano inayokuja? Matokeo yake mashemeji derby ikaihirishwa. CAF hawewezi ruhusu uwanja wa mkapa utumike tena kwa sasa kwakua kuna michuano mikubwa inakuja mbele hapa, Simba wajiandae tu kwenda zanzibar mapema hii itawasaidia kuliko kuwa na imani na mkapa stadium tena,
 
Yaani unalinganisha mashemeji derby na fainali ya CAF?
 
Ndugu mbumbumbu kubali Matokeo, Mechii imeshapangiwa uwanja kule CAF hakuna Mguto.
Uwanja wa Aman upo katika viwanja vilivyo chaguliwa na Simba endapo kiwanja chaguo la kwanza kitakua na Hitilafu.
Kubadili uwanja kunahusisha wadau wengi wa mechi iyo aiwi kama kubadili chupi.
Usije kufikiri Kuna husisha Simba na Berkane pekee.
 
Mbumbumbu fc pambaneni mpate Matokeo uwanjani, Nje ya uwanja mmesha zibitiwa.
kwasasa watendaji wakuu wote wa CAF wapo Morocco kuandaa fainali ya kwanza kupokea wageni kutoka sehemu mbalimbali Duniani.
Msihangaike kuwatafuta viongozi wa CAF hawana tena muda wa kujadili uwanja wa mechi
wakimaliza mechi ya kwanza wanaelekea Zanzibar kuandaa mechi ya pili.
Mkumbuke Kuna mechi nyingine ya CAF champion league inawahitaji watendaji aoao kwa maandalizi
 
Kiongozi, hivi unajua pia CAF wiki iliyopita walisitisha uwanja kutumika kwenye Mashemeji derby hapo Kenya na kuelekeza uwanja ufungwe usitumike kwajili ya maandalizi ya michuano inayokuja? Matokeo yake mashemeji derby ikaihirishwa. CAF hawewezi ruhusu uwanja wa mkapa utumike tena kwa sasa kwakua kuna michuano mikubwa inakuja mbele hapa, Simba wajiandae tu kwenda zanzibar mapema hii itawasaidia kuliko kuwa na imani na mkapa stadium tena,
Hoja yako ni muflis kwa sababu hata Amman Stadium itatumika kwenye mashindano ya Chan.Rudi tena na sababu nyingine.
 
Haki ya Mungu aliyetuloga watanzania uchawi wake utakuwa mkali sana. Kwenye hili sakata wanalaumiwa CAF kwa kosa gani? Au makamu wa raisi wa CAF analaumiwa kwa kosa gani? Una zaidi ya TZS B 23 mkononi kwa takribani miaka miwili umeshindwa kuzifanyia kazi halafu ghafla jana baada ya kutangazwa kuhamishwa mechi ndio watu wanakurupuka kukagua uwanja mara mbili na wengine wanatoa matamko huko. Sijui hao viongozi wanatuonaje sisi watanzania na mbaya zaidi wanafikiri CAF inaendeshwa kiswahili swahili. Na watanzania wengi wameingia mkenge na kuanza kupeleka lawama kwa CAF.

Wahusika wangetimiza wajibu wao na kutengeneza uwanja mapema kwa viwango vinavyotakiwa na CAF kusingekuwa na shida yoyote kwani hata huyo makamu wa raisi wa CAF anayetajwa tajwa kama mbuzi wa kafara angeshindwa kufanya figisu. Kwa hiyo kabla ya kukimbilia kwenye hujuma ni bora kwanza kujichunguza wenyewe kuanzia viongozi wa juu wa serikali mpaka mkandarasi ili yoyote yule aliyehusika kwa njia moja au nyingine awajibishwe ili kutengeneza uwajibikaji huko mbele ya safari. Lakini hiki kinachoendela cha kutafuta mbuzi wa kafara kwa uzembe unaonekana wazi wazi basi tutegemee tukio kama hili kutokea tena huko mbele ya safari.

Mwisho uwanja wa Mkapa uwe kwa ajili ya mpira tu hayo mashindano mengine sijui ya nini na hata matamsha mengine ambayo sio muhimu sana serikali iyatafutie viwanja vingine kuanzia sasa. Na tukipenda sifa mambo yanapoenda vizuri basi tuwe waungwana kupokea lawama mambo yakienda kombo tusipepese macho hapa.

Ni mtizamo tu
 
Back
Top Bottom