Hadi sasa kuna uwezekano wa 75% wa fainali ya Simba vs Berkane kurudishwa Uwanja wa Mkapa

Kweli we mbumbumbu yaani caf wapoteze mda wao kujadili ujinga wakati viwanja vipo tayari
 
Nitakuwa mtu wa mwisho kuamini kuwa mechi ya pili ya fainali ya Simba vs Berkane itachezwa Zanzibar.

Ndiyo, kuna uzembe mkubwa umefanyika katika ukarabati wa uwanja wa Mkapa na wachache tumekuwa tunapigia kelele hili suala kwa muda mrefu.

Ndiyo, kuna watu tulio nao hapo hapo Tanzania wana matamanio yao binafsi ya kisiasa au ya kimpira ya kutaka fainali ichezwe Zanzibar. Hili nililitabiri muda mrefu.

Ndiyo, kuna watu tunao katika maeneo mbalimbali ambao hawataki Simba ifanye vyema wameweka mikono yao ili Simba ipate ugumu katika harakati hizi za ubingwa wa CAF. Tukumbuke pia upotevu mkubwa wa mapato na kuingia gharama za ziada kwa Simba unaotokana na haya yanayofanyika kuinyima haki ya kutumia uwanja wa Mkapa.

Kilichofanyika kupeleka mechi Zanzibar ni hujuma ya waziwazi dhidi ya Simba iliyoshirikisha watu wetu wa ndani. Ni kama imepatikana "perfect storm" ya watu wa ndani na nje wamekutana katika nia na lengo moja. Inakuwa rahisi sana kulitekeleza jambo katika mazingira hayo.

Pia tukumbuke alichosema aliyekuwa Kocha wa timu ya Taifa Amrouche wakati wa AFCON, sisi tukaweka unyonge mbele na kuona kulinda mahusiano ya kidiplomasia ni muhimu kuliko hadhi na maslahi ya nchi yetu. Haya yote ni matokeo yake.

Kama kweli serikali haina mkono katika hili basi ionyeshe nguvu na ushawishi wake kwa kufanya kila inaloweza kurudisha fainali uwanja wa Benjamin Mkapa. Kinyume cha hapo, hizi hasira na manung'uniko yatabaki mioyoni mwa wapenzi na mashabiki wa Simba na hakuna anayejua watakuja kuzitoa vipi na wakati gani.

Tukumbuke, issue siyo kuchukua ubingwa. Issue ni mashabiki wa Simba wanataka haki yao ya kuishuhudia kwa macho yao timu yao ikibeba ubingwa huo katika uwanja iliyotengeneza nayo historia kwa miaka mingi. Haki hii haiwezi kupokonywa kirahisi kama baadhi ya watu wanavyodhani.

Narudia tena. Pamoja na juhudi za watu fulani fulani wa ndani na nje ya Tanzania kushinikiza hili la Zanzibar, na pamoja na kwamba nililiona mapema likifanyiwa kazi, nitakuwa mtu wa mwisho kuamini fainali hii itakwenda kuchezewa huko.
Kwani shida iko wapi timu ikicheza Aman Zanzibar! Mbona mechi na Stellenbosch ilichezwa kule.
 
Uwanja ushapangwa na maandalizi ya mechi ya mkondo wa pili yashaanza sidhani kama caf bado wanajadili suala la uwanja wa mechi ya pili sio rahisi kama mnavyofikilia kubadili tu uwanja Kila muda kama vile wanabadili nguo!
 
Magori anawaaminisha kuwa atapambana na kuwajulisha kila kitu na mechi inakuja kwa mkapa
 
Nitakuwa mtu wa mwisho kuamini kuwa mechi ya pili ya fainali ya Simba vs Berkane itachezwa Zanzibar.

Ndiyo, kuna uzembe mkubwa umefanyika katika ukarabati wa uwanja wa Mkapa na wachache tumekuwa tunapigia kelele hili suala kwa muda mrefu.

Ndiyo, kuna watu tulio nao hapo hapo Tanzania wana matamanio yao binafsi ya kisiasa au ya kimpira ya kutaka fainali ichezwe Zanzibar. Hili nililitabiri muda mrefu.

Ndiyo, kuna watu tunao katika maeneo mbalimbali ambao hawataki Simba ifanye vyema wameweka mikono yao ili Simba ipate ugumu katika harakati hizi za ubingwa wa CAF. Tukumbuke pia upotevu mkubwa wa mapato na kuingia gharama za ziada kwa Simba unaotokana na haya yanayofanyika kuinyima haki ya kutumia uwanja wa Mkapa.

Kilichofanyika kupeleka mechi Zanzibar ni hujuma ya waziwazi dhidi ya Simba iliyoshirikisha watu wetu wa ndani. Ni kama imepatikana "perfect storm" ya watu wa ndani na nje wamekutana katika nia na lengo moja. Inakuwa rahisi sana kulitekeleza jambo katika mazingira hayo.

Pia tukumbuke alichosema aliyekuwa Kocha wa timu ya Taifa Amrouche wakati wa AFCON, sisi tukaweka unyonge mbele na kuona kulinda mahusiano ya kidiplomasia ni muhimu kuliko hadhi na maslahi ya nchi yetu. Haya yote ni matokeo yake.

Kama kweli serikali haina mkono katika hili basi ionyeshe nguvu na ushawishi wake kwa kufanya kila inaloweza kurudisha fainali uwanja wa Benjamin Mkapa. Kinyume cha hapo, hizi hasira na manung'uniko yatabaki mioyoni mwa wapenzi na mashabiki wa Simba na hakuna anayejua watakuja kuzitoa vipi na wakati gani.

Tukumbuke, issue siyo kuchukua ubingwa. Issue ni mashabiki wa Simba wanataka haki yao ya kuishuhudia kwa macho yao timu yao ikibeba ubingwa huo katika uwanja iliyotengeneza nayo historia kwa miaka mingi. Haki hii haiwezi kupokonywa kirahisi kama baadhi ya watu wanavyodhani.

Narudia tena. Pamoja na juhudi za watu fulani fulani wa ndani na nje ya Tanzania kushinikiza hili la Zanzibar, na pamoja na kwamba nililiona mapema likifanyiwa kazi, nitakuwa mtu wa mwisho kuamini fainali hii itakwenda kuchezewa huko.

Mtume (SAW) alijiwa na muumini akaulizwa kati ya wazazi wangu 2 yupi Bora zaidi?
Akajibiwa MAMA YAKO
Halafu nani anaefuata kwa ubora? akajibiwa MAMA YAKO akaulizwa tena anaefuata nani? akajibiwa MAMA YAKO,akaulizwa kisha nani? akajibiwa BABA YAKO.

Lowassa alitaja vipaumbele vyake kwenye Kampeni yake ya kuwania Urais 2015
ELIMU
ELIMU
ELIMU
Na Simba walipochagua viwanja vya nyumbani. kiwanja no.1 na 2 angechagua
1. MKAPA
2. MKAPA
Lakini kwa Umbumbumbu no.2 walichagua AMAN COMPLEX halafu mnawalaumu CAF si kuwaonea huko.
 
Yaani fainali ya michuano ya caf waingie watazamaji 10000 utakuwa utoto sana
Hata uwanja wa Berkane unaotumika katika mechi ya kesho hauna hadhi ya kuchezewa fainali ya mashindano makubwa kama haya. Embu imagine mechi ya pili ya kukabidhiwa kombe ingekuwa uwanja kama ule.
 
Shida ya watanzania wengi ni unafiki. Mambo yakiwa mazuri sifa zinaenda kusikostahili yakija mambo mabaya lawama nazo zinapelekwa kusikostahili.

Badala ya sasa hivi kukaa kuijadili CAF lingekuwa jambo la maana sana iwapo umma wa watanzania unaosononeka ungejulishwa ni wakina nani walizembea kwenye ukarabati wa uwanja ambao pesa nyingi zilishatolewa na ulitakiwa kukamilika kama sikosei mwaka jana mwishoni na hatua gani zimechukuliwa dhidi yao mpaka sasa.

Ninachositika mpaka sasa watanzania wametolewa kwenye reli na wote kama manyumbu wanailalamikia CAF na makamu wa raisi wa CAF. Kwa jinsi hii wahusika wamefanikiwa kuwaondoa watanzania kwenye hoja ya msingi ya juu ya wakina nani wamezembea kwenye ukarabati wa uwanja na kwenda kuchezezesha ngoma ya hovyo ya kuwapigia kelele CAF. Ukaguzi wa uwanja hufanyika kitaalamu na baadae mapendekezo ya marekebisho hupewa wahusika kuyafanyia kazi. Je wataalamu wetu waliyafanyia kazi mapendekezo ya marekebisho tuliyopewa na wataalamu wa CAF?. Na ikumbukwe kuwa sio rahisi hao wataalamu kuja kwako kukagua uwanja kila siku kwani wana ratiba maalumu.
 
Yaani unalinganisha mashemeji derby na fainali ya CAF?

Kwani mechi ya nusu fainali simba alichezea wapi na kwa sababu gani ?

Uwanja wa Amani caf waliambiwa na nani kama simba atautumia kuanzia nusu fainali na kwa sababu gani ?

Nusu fainali usitumie uwanja wa mkapa ila fainali unataka huyo huyo aliekukatalia kucheza nusu usitumie uwanja wa mkapa akuruhusu kilazima ucheze fainali kwenye uwanja aliukataa toka nusu
 
Kiongozi, hivi unajua pia CAF wiki iliyopita walisitisha uwanja kutumika kwenye Mashemeji derby hapo Kenya na kuelekeza uwanja ufungwe usitumike kwajili ya maandalizi ya michuano inayokuja? Matokeo yake mashemeji derby ikaihirishwa. CAF hawewezi ruhusu uwanja wa mkapa utumike tena kwa sasa kwakua kuna michuano mikubwa inakuja mbele hapa, Simba wajiandae tu kwenda zanzibar mapema hii itawasaidia kuliko kuwa na imani na mkapa stadium tena,
Katika sababu za CAF hakuna sababu inayosema Kuna michuano mkubwa inakuja mbele,acha kabisa kudanganya umma na upotoshaji wako.
Sababu kuu ni uwanja kukaa maji.
 
Kwani mechi ya nusu fainali simba alichezea wapi na kwa sababu gani ?

Uwanja wa Amani caf waliambiwa na nani kama simba atautumia kuanzia nusu fainali na kwa sababu gani ?

Nusu fainali usitumie uwanja wa mkapa ila fainali unataka huyo huyo aliekukatalia kucheza nusu usitumie uwanja wa mkapa akuruhusu kilazima ucheze fainali kwenye uwanja aliukataa toka nusu
Nusu fainali ilichezwa Znz kwa sababu uwanja ilikua unajaa maji,Kwa Sasa uwanja umetengenezwa haujai maji.
 
Kwani mechi ya nusu fainali simba alichezea wapi na kwa sababu gani ?

Uwanja wa Amani caf waliambiwa na nani kama simba atautumia kuanzia nusu fainali na kwa sababu gani ?

Nusu fainali usitumie uwanja wa mkapa ila fainali unataka huyo huyo aliekukatalia kucheza nusu usitumie uwanja wa mkapa akuruhusu kilazima ucheze fainali kwenye uwanja aliukataa toka nusu
Badala ya kutoa hoja unauliza maswali tena yasiyo na kichwa wala mguu.

Nami nikujibu kwa kukuuliza swali Ila langu litakuwa swali la maana lenye mantiki. Nani aliizuia Simba isicheze nusu fainali kwa Mkapa?
 
Shida ya watanzania wengi ni unafiki. Mambo yakiwa mazuri sifa zinaenda kusikostahili yakija mambo mabaya lawama nazo zinapelekwa kusikostahili.

Badala ya sasa hivi kukaa kuijadili CAF lingekuwa jambo la maana sana iwapo umma wa watanzania unaosononeka ungejulishwa ni wakina nani walizembea kwenye ukarabati wa uwanja ambao pesa nyingi zilishatolewa na ulitakiwa kukamilika kama sikosei mwaka jana mwishoni na hatua gani zimechukuliwa dhidi yao mpaka sasa.

Ninachositika mpaka sasa watanzania wametolewa kwenye reli na wote kama manyumbu wanailalamikia CAF na makamu wa raisi wa CAF. Kwa jinsi hii wahusika wamefanikiwa kuwaondoa watanzania kwenye hoja ya msingi ya juu ya wakina nani wamezembea kwenye ukarabati wa uwanja na kwenda kuchezezesha ngoma ya hovyo ya kuwapigia kelele CAF. Ukaguzi wa uwanja hufanyika kitaalamu na baadae mapendekezo ya marekebisho hupewa wahusika kuyafanyia kazi. Je wataalamu wetu waliyafanyia kazi mapendekezo ya marekebisho tuliyopewa na wataalamu wa CAF?. Na ikumbukwe kuwa sio rahisi hao wataalamu kuja kwako kukagua uwanja kila siku kwani wana ratiba maalumu.
Jambo kwanza la msingi ni kupambana kubakisha fainali Dar es Salaam.
 
yanga bingwa.jpg
 
Kwani shida iko wapi timu ikicheza Aman Zanzibar! Mbona mechi na Stellenbosch ilichezwa kule.
Kwanza, uwanja wa Mkapa ndiyo uwanja rasmi wa Simba. Kama ambavyo Berkane wametupeleka huko Morocco ndani ndani kuwafuata badala ya kuchezea pale Casablanca, vivyo hivyo Simba ina haki ya kucheza katika uwanja wake wa nyumbani.

Pili, taa za uwanja wa Amaan hazina quality nzuri. Uwanja wa Amaan unapendeza zaidi kwa picha za kwenye mwanga wa jua. Wamekataa mechi kuchezwa saa 10 na hii ni njia nyingine ya kuwabeba waarabu.

Tatu, Simba inapoteza mapato makubwa sana kwa kuhamishiwa mechi. Fainali kwa Mkapa ingeingiza karibia shilingi bilioni 1. Mechi ikichezewa Zanzibar haiingizi hata nusu ya pesa hizo.

Nne, Zanzibar ni mamlaka tofauti kisoka pamoja na kwamba kisiasa tunashare huu muundo wa muungano wa magazijuto. Hii haileti usawa wa kiushindani kwa timu zote mbili.

Tano, uwanja wa Mkapa una historia ndefu na Simba. Ingependeza historia hiyo ikaandikwa kwa Simba kucheza fainali yake pale na siyo uhamishoni kama wakimbizi.

Sita, sababu ya kuhamisha mechi kisa mvua siyo nzito kihivyo. Tumeshuhudia mechi zinachezwa hadi kwenye snow/barafu ndiyo ije kuwa sababu za mvua. Hii sababu hauwezi kuitumia kuinyima timu na mashabiki wake kuiona timu yao katika mechi ya kihistoria kama hii.

Ikishindikana, mechi iahirishwe hadi mvua zitakapokata ila CAF wajue hata kipindi cha kiangazi, mvua kunyesha siku Simba inacheza ni jambo ambalo haliepukiki!
 
Haya, CAF wameshaamua! Nendeni mkacheze Zanzibar. Na kama hamtaki kwenda kucheza Aman, fanyeni tu kususia huo mchezo. Mwisho wa siku Bodi ya ligi itawatetea.
 
Back
Top Bottom