ANT DRUGS
JF-Expert Member
- Dec 20, 2013
- 5,578
- 7,055
Siyo B21 ni B31 mkuu.Haki ya Mungu aliyetuloga watanzania uchawi wake utakuwa mkali sana. Kwenye hili sakata wanalaumiwa CAF kwa kosa gani? Au makamu wa raisi wa CAF analaumiwa kwa kosa gani? Una zaidi ya TZS B 23 mkononi kwa takribani miaka miwili umeshindwa kuzifanyia kazi halafu ghafla jana baada ya kutangazwa kuhamishwa mechi ndio watu wanakurupuka kukagua uwanja mara mbili na wengine wanatoa matamko huko. Sijui hao viongozi wanatuonaje sisi watanzania na mbaya zaidi wanafikiri CAF inaendeshwa kiswahili swahili. Na watanzania wengi wameingia mkenge na kuanza kupeleka lawama kwa CAF.
Wahusika wangetimiza wajibu wao na kutengeneza uwanja mapema kwa viwango vinavyotakiwa na CAF kusingekuwa na shida yoyote kwani hata huyo makamu wa raisi wa CAF anayetajwa tajwa kama mbuzi wa kafara angeshindwa kufanya figisu. Kwa hiyo kabla ya kukimbilia kwenye hujuma ni bora kwanza kujichunguza wenyewe kuanzia viongozi wa juu wa serikali mpaka mkandarasi ili yoyote yule aliyehusika kwa njia moja au nyingine awajibishwe ili kutengeneza uwajibikaji huko mbele ya safari. Lakini hiki kinachoendela cha kutafuta mbuzi wa kafara kwa uzembe unaonekana wazi wazi basi tutegemee tukio kama hili kutokea tena huko mbele ya safari.
Mwisho uwanja wa Mkapa uwe kwa ajili ya mpira tu hayo mashindano mengine sijui ya nini na hata matamsha mengine ambayo sio muhimu sana serikali iyatafutie viwanja vingine kuanzia sasa. Na tukipenda sifa mambo yanapoenda vizuri basi tuwe waungwana kupokea lawama mambo yakienda kombo tusipepese macho hapa.
Ni mtizamo tu
CAF hawahusiki ni uzembe wa viongozi wetu.Mama anahujumiwa.