Kwanza, uwanja wa Mkapa ndiyo uwanja rasmi wa Simba. Kama ambavyo Berkane wametupeleka huko Morocco ndani ndani kuwafuata badala ya kuchezea pale Casablanca, vivyo hivyo Simba ina haki ya kucheza katika uwanja wake wa nyumbani.
Pili, taa za uwanja wa Amaan hazina quality nzuri. Uwanja wa Amaan unapendeza zaidi kwa picha za kwenye mwanga wa jua. Wamekataa mechi kuchezwa saa 10 na hii ni njia nyingine ya kuwabeba waarabu.
Tatu, Simba inapoteza mapato makubwa sana kwa kuhamishiwa mechi. Fainali kwa Mkapa ingeingiza karibia shilingi bilioni 1. Mechi ikichezewa Zanzibar haiingizi hata nusu ya pesa hizo.
Nne, Zanzibar ni mamlaka tofauti kisoka pamoja na kwamba kisiasa tunashare huu muundo wa muungano wa magazijuto. Hii haileti usawa wa kiushindani kwa timu zote mbili.
Tano, uwanja wa Mkapa una historia ndefu na Simba. Ingependeza historia hiyo ikaandikwa kwa Simba kucheza fainali yake pale na siyo uhamishoni kama wakimbizi.
Sita, sababu ya kuhamisha mechi kisa mvua siyo nzito kihivyo. Tumeshuhudia mechi zinachezwa hadi kwenye snow/barafu ndiyo ije kuwa sababu za mvua. Hii sababu hauwezi kuitumia kuinyima timu na mashabiki wake kuiona timu yao katika mechi ya kihistoria kama hii.
Ikishindikana, mechi iahirishwe hadi mvua zitakapokata ila CAF wajue hata kipindi cha kiangazi, mvua kunyesha siku Simba inacheza ni jambo ambalo haliepukiki!