DELETED ACCOUNT
JF-Expert Member
- Mar 25, 2010
- 9,805
- 15,476
Kiongozi, hivi unajua pia CAF wiki iliyopita walisitisha uwanja kutumika kwenye Mashemeji derby hapo Kenya na kuelekeza uwanja ufungwe usitumike kwajili ya maandalizi ya michuano inayokuja? Matokeo yake mashemeji derby ikaihirishwa. CAF hawewezi ruhusu uwanja wa mkapa utumike tena kwa sasa kwakua kuna michuano mikubwa inakuja mbele hapa, Simba wajiandae tu kwenda zanzibar mapema hii itawasaidia kuliko kuwa na imani na mkapa stadium tena,Nitakuwa mtu wa mwisho kuamini kuwa mechi ya pili ya fainali ya Simba vs Berkane itachezwa Zanzibar.
Ndiyo, kuna uzembe mkubwa umefanyika katika ukarabati wa uwanja wa Mkapa na wachache tumekuwa tunapigia kelele hili suala kwa muda mrefu.
Ndiyo, kuna watu tulio nao hapo hapo Tanzania wana matamanio yao binafsi ya kisiasa au ya kimpira ya kutaka fainali ichezwe Zanzibar. Hili nililitabiri muda mrefu.
Ndiyo, kuna watu tunao katika maeneo mbalimbali ambao hawataki Simba ifanye vyema wameweka mikono yao ili Simba ipate ugumu katika harakati hizi za ubingwa wa CAF. Tukumbuke pia upotevu mkubwa wa mapato na kuingia gharama za ziada kwa Simba unaotokana na haya yanayofanyika kuinyima haki ya kutumia uwanja wa Mkapa.
Kilichofanyika kupeleka mechi Zanzibar ni hujuma ya waziwazi dhidi ya Simba iliyoshirikisha watu wetu wa ndani. Ni kama imepatikana "perfect storm" ya watu wa ndani na nje wamekutana katika nia na lengo moja. Inakuwa rahisi sana kulitekeleza jambo katika mazingira hayo.
Pia tukumbuke alichosema aliyekuwa Kocha wa timu ya Taifa Amrouche wakati wa AFCON, sisi tukaweka unyonge mbele na kuona kulinda mahusiano ya kidiplomasia ni muhimu kuliko hadhi na maslahi ya nchi yetu. Haya yote ni matokeo yake.
Kama kweli serikali haina mkono katika hili basi ionyeshe nguvu na ushawishi wake kwa kufanya kila inaloweza kurudisha fainali uwanja wa Benjamin Mkapa. Kinyume cha hapo, hizi hasira na manung'uniko yatabaki mioyoni mwa wapenzi na mashabiki wa Simba na hakuna anayejua watakuja kuzitoa vipi na wakati gani.
Tukumbuke, issue siyo kuchukua ubingwa. Issue ni mashabiki wa Simba wanataka haki yao ya kuishuhudia kwa macho yao timu yao ikibeba ubingwa huo katika uwanja iliyotengeneza nayo historia kwa miaka mingi. Haki hii haiwezi kupokonywa kirahisi kama baadhi ya watu wanavyodhani.
Narudia tena. Pamoja na juhudi za watu fulani fulani wa ndani na nje ya Tanzania kushinikiza hili la Zanzibar, na pamoja na kwamba nililiona mapema likifanyiwa kazi, nitakuwa mtu wa mwisho kuamini fainali hii itakwenda kuchezewa huko.
Yaani unalinganisha mashemeji derby na fainali ya CAF?Kiongozi, hivi unajua pia CAF wiki iliyopita walisitisha uwanja kutumika kwenye Mashemeji derby hapo Kenya na kuelekeza uwanja ufungwe usitumike kwajili ya maandalizi ya michuano inayokuja? Matokeo yake mashemeji derby ikaihirishwa. CAF hawewezi ruhusu uwanja wa mkapa utumike tena kwa sasa kwakua kuna michuano mikubwa inakuja mbele hapa, Simba wajiandae tu kwenda zanzibar mapema hii itawasaidia kuliko kuwa na imani na mkapa stadium tena,
Sio blue,ni buluuKwa hili namuunga mkono Mama😂😂 Mitano tena,Ametekeleza Na fainali ikachezwe Zanzibar kukuza uchumi wa blue
Mazoea yana tabu....Sio blue,ni buluu
Utani tu, ndio Wanavyouita KWA kiswahili. Uchumi wa buluuMazoea yana tabu....
Kuna watu naona nati zimeachia. Yan fainali ifananishwe na mashemeji derby...na Zaid fainali ikaangaliwe na mashabiki elfu 12.Yaani unalinganisha mashemeji derby na fainali ya CAF?
Mbona imeshapelekwa sasa zanzibar kama ni hivyo?,Kuna watu naona nati zimeachia. Yan fainali ifananishwe na mashemeji derby...na Zaid fainali ikaangaliwe na mashabiki elfu 12.
Hoja yako ni muflis kwa sababu hata Amman Stadium itatumika kwenye mashindano ya Chan.Rudi tena na sababu nyingine.Kiongozi, hivi unajua pia CAF wiki iliyopita walisitisha uwanja kutumika kwenye Mashemeji derby hapo Kenya na kuelekeza uwanja ufungwe usitumike kwajili ya maandalizi ya michuano inayokuja? Matokeo yake mashemeji derby ikaihirishwa. CAF hawewezi ruhusu uwanja wa mkapa utumike tena kwa sasa kwakua kuna michuano mikubwa inakuja mbele hapa, Simba wajiandae tu kwenda zanzibar mapema hii itawasaidia kuliko kuwa na imani na mkapa stadium tena,