KESI YA MZEE MNYOKA 21
Mzee Mnyoka Sasa alipata taarifa kuhusu mwenendo wa kesi yake,
"Ni taratibu zile zile Mzee Mnyoka, nitakupa hati ya shtaka lako, Kama utakubali Basi, halmashauri ya nidhamu itakujadili ndani ya wiki moja, halafu tutaitisha kamati kwa ajili ya kutoa maamuzi, lakini Kama utakanusha, Basi, tutaunda tume ya uchunguzi ambayo itabidi ifuatilie kwa undani Kama uliiba ngo'mbe ama la, lakini tume hiyo pia haitaishia hapo, kumbuka Kijiji kina watu wengi, kwahiyo hata Kama wataona huna hatia, bado kamati inaweza kushauri uchukuliwe hatua maana kwanini utajwe wewe na sio mwanakijiji mwingine?"
Mtendaji wa Kijiji Alikua akimpa maelezo Mzee Mnyoka,
"Wewe nipe hiyo hati na nataka nijibu hapa hapa"
Mzee Mnyoka aliongea Sasa huku hasira zikizidi kumpanda,
"Hapana, kanuni zinasema unatakiwa kujibu ndani ya siku 14 sio lazima leo!"
Mtendaji alimuelewesha Mzee Mnyoka,
"Wewe nipe"
Mzee Mnyoka alisema akipokea hati yake ya shitaka na kutoka nje ya Ofisi ya Kijiji,
Siku zote uongo ukisemwa Sana bila kukanushwa Basi hugeuka kuwa kweli,
Hivyo taratibu wanakijiji wakaanza kumuona Mzee Mnyoka Kama mwizi kweli, zaidi ya hapo waliona Mzee Mnyoka kuwa Kama mtu mwenye mtazamo tofauti na viongozi wa Kijiji,
Taratibu hata marafiki zake Mzee Mnyoka walianza kumteta,
Hata hivyo yeye aliendelea na maisha yake huku akitafuta namna ya kutoka kwenye jinamizi la kuzuiwa kuuza mazao yake,
"Hawataniweza"
Mzee Mnyoka Sasa alijisemea akitabasamu, Kuna Jambo lilimjia kichwani,
***********
"Yeah ni kweli niliibadilisha aisee, nilikua nakunywa juisi kwa bahati mbaya, ilimwagika kidogo juu ya Ile bahasha ya mwanzo, sikuona Kama Ni busara Sana kuleta bahasha yenye maji maji Ndio nikaona niibadilishe, hata hivyo si Ni karatasi tu za kawaida Mzee baba? "
Oscar alimjibu Ima,
Huku akionyesha kutokua na wasi wasi,
"Ndio ujifunze Sasa kuwa makini, mjomba"
Alisema Ima huku akiendelea na kazi zake,
Oscar alitoka Kisha akaingia kwenye Gari, alienda mbele kidogo Kisha akapaki pembeni kidogo ya njia na kutoa simu yake,
"Hey hebu angalia Kuna kitu nakutumia uniambie kinahusu Nini "
Oscar aliongea baada ya simu yake kupokolewa
"Sawa bosi"
Ilisikika upande wa pili,
Oscar alitoka nje akijifanya kuangalia angalia Gari lake Kama Kuna hitilafu hivi lakini lengo lilikua Ni kupoteza maboya Kama Kuna mtu alikua akimfuatilia, lakini kwa uhalisia alikua anasubiri simu ya kupewa maelezo kuhusu nyaraka alizotuma,
Baada ya dakika kumi hivi simu yake iliita,
Aliitazama mpigaji na Mara moja akaweza sikioni na kuingia ndani ya Gari,
"Hizo Ni taarifa za mgodi wa UreFact za mwezi wa 5, mwaka huu,
Zinaenda kwa CEO wa iyo kampuni Mr Johnson Zagris Ping, wa uingereza,
Ni Kama kiambata Ina maana Kuna barua nyingine ambayo imeandikwa kwa juu yake"
Alimalizia upande wa pili,
"Sawa endelea kuangalia hizo items Kama zinahusiana na nini, halafu baadae nitakua ukumbi wa Julius Nyerere mlimani city utaniletea maelezo
Maana simu hii haitapatikana "
Oscar alimalizia Kisha akatoa line yake na kuiweka sehemu anayojua yeye,
Kisha akawasha Gari na kuondoka..
***********
Jioni Ile Oscar alikua amemsindikiza Tito pale mlimani kwenye ukumbi wa JK Nyerere,
Tito alikua Ndio mzungumzaji Mkuu katika huku akitarajiwa kuulizwa maswali na wanafunzi wa chuo kikuu mada ilikua Ni namna gani wananchi wananufaika na rasilimali za nchi hususani madini na gesi,
"Serikali inafanya jitihada kubwa, katika kuhakikisha kila mmoja ananufaika na rasilimali hizi, majengo mnayoyaona, vifaa mnavyoviona sehemu mbali mbali, vyote Ni faida ya rasilimali zetu, mbali na kodi chanzo kingine kikuu Cha mapato Ni madini na gesi zinazopatikana nchini,"
Tito alikua anatoa hotuba yake , Kisha akaendelea na kumaliza kwa dakika 15 Kisha akaruhusu maswali,
Wanafunzi waliuliza maswali mengi lakini mwishowe mwanafunzi mmoja akasimama na kuuliza swali
"Mheshimiwa Kuna madai kuwa baadhi ya viongozi ikiwemo wewe mnashirikiana na wageni, katika kutorosha Mali za nchi nje, kwa maslahi Binafsi, na zaidi Sana serikali inakosa mapato yaliyokusudiwa , Hili unalizungumziaje?"
Mwanafunzi huyo aliuliza huku akipigiwa makofi na wenzake,
Tito hakutegemea swali Hili sura yake ilibadilika, moja kwa moja alijua Kuna maadui zake "wasiomtakia mema" Ndio wamepanga watu wa kuuliza maswali ya kumkomoa, hasa ikizingatiwa mkutano ule ulirushwa mubashara,
"Kwanza ufahamike viongozi wote sio Tito pekee yake, kila kiongozi anatakiwa afanye majukumu yake kwa mujibu wa kanuni na taratibu za nchi, "
Tito alijibu swali huku akionyesha kukereka,
Baada ya mkutano wakiwa Kwenye Gari sasa Tito alishindwa kuzuia hasira zake,
"Wamemtuma yule dogo kunichafulia najua wanataka hii nafasi Sasa ngoja niwatumie salamu"
Tito alisema na bila kujali Kama Oscar anasikia ama la alitoa simu yake na kubonyeza namba kadhaa,
"Yule ngedere aliyetumwa kuuliza swali la kijinga mmalize usiku huu huu ili wapate salamu"
Aliongea Tito Huku aking'ata meno yake kwa hasira,
Sasa Oscar alijisikia Kama Yuko ndotoni!
Hakika hakuamini masikio yake,
*******************************************
Mzee Mnyoka alikumbuka Jambo fulani hivi ,
Aliingia Sasa chumbani kwake,
"Pengine hawa jamaa wanahisi Mimi nitaogopa kujieleza Sasa ngoja,"
Mzee Mnyoka aliingia ndani kwake Kisha akavaa miwani yake na kuanza kujibu Ile hati ya mashtaka,
Aliandika hoja nyingi huku akimalizia na maswali
"Mahakama ilichunguza na kuona Sina hatia, je kwa Sasa mmepata ushahidi wa kunitia hatiani?
_je wakati naiba huyo ng'ombe Nani alishuhudia?
Huyo ng'ombe nilimpeleka wapi baada ya kumuiba?
Sasa naomba Sana kesi hii itolewe maaumuzi mapema, na pia muweze kutoa ushahidi wa Mimi kufanya huo wizi,"
Mzee Mnyoka alimalizia hoja zake na kupeleka kwenye ofisi ya kijiji
Siku ile Ile,
Mtendaji alisoma hoja za Mzee Mnyoka Kisha akamwambia aondoke huku akimsindikiza na maneno,
"Mzee Mnyoka unajifanya mjuaji Sana wewe, Ila hapa umefika, kumbuka ofisi hii haingiliwi katika maamuzi yake"
Mzee Mnyoka Hakujali aliondoka zake..
*********
Oscar alijifanya kuunga mkono hoja,
"Yeah yule dogo katumwa Ni vizuri kumshughulikia kweli," Oscar alisema
"Yeah vijana wa siku hizi akipewa elfu tano tu amtukane kiongozi tayari anafanya tu bila kufikiria madhara yake"
Tito alisema,
"Huyo jamaa uliyemtuma anaweza kazi lakini?"
Oscar akijaribu kumuuliza Tito
"Ah Pablo, Ni mzoefu Sana ameshafanya task Kama hizi Mara nyingi tu, unajua Oscar Dunia ya Sasa huwezi kukaa kwenye hizi nafasi zetu ukiwa "msafi" milele,
Usione wote hao unaona wanashine sio hivi hivi"
Tito aliongea kuhalalisha "ujahili" wake,
"Yeah wanasema siasa Ni mchezo mchafu"
Oscar aliongea Sasa na kila mmoja akakaa kimya,
Oscar alikua anataka kumuokoa yule dogo bila kustukiwa na Tito
Na hivyo alipanga tu akifika nyumbani ageuze chap kurudi chuoni Udsm,
********
Kijana swalehe Sasa alikua amezunguukwa na vijana wenzake wakijazana "upepo"
Kuhusu Hali ya siasa nchini,
"Dah mwanangu umeua , umemtia Jamba Jamba waziri, we Noma!"
Sasa yule kijana aligeuka maarufu ghafla jioni Ile,
Karibu na chuo kikuu mlimani Kuna stendi ya mabasi maarufu kwa jina la simu 2000 ama wenyewe walipenda kuita mawasiliano,
Ndani ya tax moja "Pablo" akiwa na mwenzake mmoja walikua tayari wanasubiri saa 12 ifike ambapo wanafunzi wengi walikua wakirudi maeneo ya chuo,
Tayari Pablo alikua na sura halisi ya "swalehe Issa" mwanafunzi wa mwaka wa pili ambaye alijizolea umaarufu ghafla kwa "kumgonga" waziri swali la kibabe,
Pablo alishapewa maelezo na bosi wake namna ya kummaliza bila kuacha alama zozote,
"Ila Tito nae, kwanini tumuue dogo kwa kesi ya kiboya Kama hii"
Aliongea Sasa mwenzake na Pablo huku akiendelea kuangalia Tena Ile video ya swalehe ,
"Ah sisi tunaangalia hela Bob"
Alisema Pablo huku akizima kipisi Cha bangi alichokua anavuta,
Waliongea Kisha wakavaa mavazi yao walioandaa Kisha wakasogea maeneo ya chuo,
Walishuka na kusogelea baadhi ya wanafunzi waliokua wanaingia getini,
"Aisee sisi tunatoka Pilika Online TV tulikua tunahitaji kufanya mahojiano na Swalehe Issa"
Pablo alisema huku akijifanya kuandaa camera yake na maiki,
"Aisee hapa hayupo Ila ngoja nimcheki rafiki yangu mmoja anasoma nae course moja anaweza kujua alipo"
Alisema mwanafunzi mmoja huku akibonyeza simu yake,
"Oi Mpigie Kipanya mwambie ana wageni wake kutoka Pilika Online TV hapa getini"
Aliongea yule mwanafunzi ,
"Oya anakuja, kumbe yupo nae Room"
Baada ya dakika 7 hivi swalehe au wenzake walipenda kumuita Kipanya alitokea akiwa na rafiki yake Mazinge,
Walisalimiana Kisha Pablo Sasa akatoa muelekeo
"Aisee sisi Ni Pilika Online TV, tuna deal Sana na masuala ya walimu na wanafunzi tumependa Sana jinsi ulivyowasilisha hoja zako, na tumeona tufanye na wewe mahojiano mafupi, lakini Kama hutajali tulitaka tufanyie ofisini kwetu sio mbali sana na hapa, Ni nyuma tu ya ubungo hapo ,kabla hujafika kwenye stendi ya mkoa"
"Ah Hakuna shida kabisa, twendeni"
Alisema Swalehe kwa furaha,
Hakutegemea Kama ipo siku angeweza kuhojiwa na mwandishi wa habari hakika alijiona mwenye bahati Sana,
Ni wakati anaingia kwenye Gari la akina Pablo Sasa alihisi harufu Kali ya bangi, wakati anataka kuongea ghafla akafunikwa na kitambaa puani, na katika kujitetea akahisi anakosa nguvu na kulegea Kisha akapoteza fahamu.....