Hadithi: Kesi ya Mzee Mnyoka

Hadithi: Kesi ya Mzee Mnyoka

KESI YA MZEE MNYOKA 15

Dokta Kimei Sasa aliona Sasa Hakuna namna isipokuwa kumueleza mkuu wake wa kituo kuanzia mwanzo mpaka mwisho,...


Alitoka na kumuacha Mzee Mnyoka pale kwake Kisha akaenda hospitali usiku ule ule,


Alifika na kukuta tayari madaktari wenzake wameshafika na kumpiga jicho la "mbona umechelewa"

Alisogeza kiti na kukaa pole pole huku mkuu wao akiendelea kusikiliza taarifa ya daktari wa zamu,

"So nilitoka theater na kwa bahati tukapata mgonjwa wa OPD mmoja ambaye alikua na kesi ya heart attack , kwahiyo nikawa namuattend, Sasa nilikua natoka kukagua kwenye hims maana mgonjwa alikua anaatend hapa, ili nichukue details zake ndio umeme ukakata, nikajua genereta itawaka Kama siku zote, na kweli ikawa inawaka Ila Sasa umeme ukawa hauji ndio nikaongea na James hapo akampigia fundi, ambaye alisema afuatwe , so James akamfuata na akaja akarebisha anasema alikuta kitu Kama pipi kwenye main switch ambayo ilitengeneza maji maji na kupiga shot,


Sasa Ile narudi kule wodini ndio kwenye emergency room nakuta Mzee Omari ambaye analala na Mzee Mnyoka akasema haonekani"


Dokta Ali alikua Sasa anaongea..

"Dokta Kimei, halafu Kimei, kwanza umechelewa, lakini pia tupo Kwenye kikao wewe uko bize na smartphone yako, bila kujua haya mabalaa yote Ni wewe ndio chanzo"

Alisema Sasa daktari mkuu , Dokta Lightnes huku akimuangalia dokta Kimei,.

"Hapana mkuu nasikiliza Sana na hapa na naomba uangalie simu yako"

Dokta Kimei alisema kwa upole..

Dokta Light , Sasa alichukua simu yake na kuona ujumbe mfupi,


"Sorry mkuu najua Mgonjwa alipo Ila naomba tuongee wawili"

Ilikua Ni sms kutoka kwa dokta kimei,


"Okay Sasa turudi tukapumzike, atakayepata taarifa zozote za Mzee Mnyoka Basi atume kwenye group la staff haraka"

Dokta Lightnes Sasa alisema huku akiwaruhusu madaktari wake kuondoka,.

"Kimei Baki"
Dokta Lightnes alisema Sasa,


Baada ya kuhakikisha wamebaki wawili tu Sasa Dokta Kimei aliongea...

"Mkuu samahani Sana kabla ya yote,"

Alisema Sasa Kisha akamuhadithia mwanzo mpaka mwisho kuhusu Mzee Mnyoka,...

Dokta Lightnes Sasa alivuta pumzi ndefu,
"Kimei unajua sikutegemea ungefanya huu upuuzi, Mimi Ni mkuu wako, you should let me know, Sasa suppose wangemuua unadhani ungeulizwa wewe.? No, na ujue Ni kwa vile tu nilikua nakuamini Ila umenidisapoint Sana"

Alisema dokta Lightnes


*********

Oscar alishika kitasa Cha mlango pole pole na kujaribu kukivuta na mlango ukafunguka,..


Alitokea kwenye korido ndefu na kwa bahati mbaya hakuwahi kufika pale zaidi ya kuishia kwenye stoo tu, hivyo alienda kwa hisia tu,..

Ni wakati anataka kusogea ndipo akasikia hatua za watu wakiwa wanakuja kuelekea alipo, Oscar Sasa alishachelewa kurudi alipotoka hivyo akarudi hatua moja na Kisha akasimama pembeni ya mlango wa kuingilia ukumbini Kama wafanyavyo walinzi...

Alivaa Kofia yake Kisha akasimama wima,


Mbinu yake ilisaidia kwani wale jamaa walipita huku wakimtolea ishara ya salamu TU kwa kunyoosha mkono, Oscar aliamua Sasa kwenda kule walikotokea na baada ya hatua kadhaa alipigwa na mshangao ....


Aliona ngazi za kushuka kuelekea chini!


Sasa alijipongeza kwa ugunduzi wake huo, siku moja alisikia sauti Kama za mashine hivi, bila shaka zilikua zinatoka maeneo haya, aliwaza Sasa akishuka hizo ngazi kwa haraka,

Alifika sehemu na kukuta mgawanyiko wa ngazi akaamua kubahatisha kuchukua mojawapo,..


Sasa kwa mbali aliona maabara kubwa ya kisasa huku watu kadhaa wakiwa Kwenye nguo Nyeupe wakiendelea na kazi zao Kama kawaida, alijaribu kuangalia Kama Kuna camera zozote hakuona,


Akapiga hatua moja hivi Kisha akatoa kitu Kama kishikizo Cha chuma akaweka kwenye kola ya koti lake akasogea zaidi kwa Kunyata kuelekea kwenye maabara hiyo....


"Kumbe hawa jamaa Wana maabara yao kwa maana kila kitu wanafanya hapa"

Oscar aliwaza,

Hakutaka kupoteza muda pale alirudi mpaka Kwenye Ile njia na kuchukua njia nyingine ya upande wa kulia, alitembea pole pole kwa tahadhari kubwa na Sasa akatokea kweye uwazi mkubwa na kumuona Mlinzi mmoja akiwa amesimama Vyema na bunduki yake,..
Oscar Sasa alivua lile begi lake na kulishikilia mkononi,

Halafu akatembea kwa haraka kuelekea kule alipo yule Mlinzi,

"Simama!"
Aliamriwa kusimama na akasimama,


"Nawahisha mzigo boss" Oscar alisema huku akijifanya kupita..


"Mzigo? Mzigo gani!"?


Mlinzi aliuliza

"Umetoka kwenye Gari, napeleka kwa bosi alisahau" Oscar alidanganya...

"Okay naomba kibali"

Oscar alielewa alitakiwa kutaja Neno la Siri, hivyo kuzubaa kokote kule kungemaanisha kukamatwa kwake,..

"Acha utani Basi jamaa, mzigo huu unachelewa ujue"

Oscar aliongea Sasa huku akijaribu kupita ..


Sasa yule Mlinzi akashindwa kuvumilia,

"Ukisogea hatua moja nakupasua kichwa"

Alisema yule Mlinzi huku akimuweka chini ya ulinzi Oscar ....


"Oya man unazingua Sasa ujue" Oscar aliongea huku akimsogelea yule Mlinzi

"Oya sitanii hatua moja nakupasua kweli"

Yule Mlinzi Sasa aliongea

"Huyu boya anaweza kuniua kweli, usicheze na mjinga atakupasua jicho"

Oscar aliwaza Sasa akiwaza namna ya kumuwahi yule jamaa,...

"Okay chukua Basi hili begi, peleka wewe"

Oscar alisema huku akinyoosha mkono, Ni Kama yule Mlinzi alizubaika hivi akawa anasogea kuelekea alipo Oscar,

Kwa Kasi ya ajabu Oscar alichomoa kisu na kumrushia shingoni , yule mlinzi akaanguka pale pale ,.
Kwa haraka alimvuta na kumuweka pembeni, akapiga hatua na kuelekea mbele ambapo Sasa alikuta mlango mkubwa wa vioo Wenye maandishi makubwa .

"MEETING ROOM"

"Wako humu bila shaka"

Oscar aliwaza huku akifikiria Jambo la kufanya.


***************


" Kwahiyo Sasa mmepanga kufanya Nini?" Dokta Lightnes aliuliza

"Walisema ndani ya wiki moja zoezi lao litakuwa limeisha kabisa"

Kimei aliongea,

"Sasa hapa mambo yameshaharibika kakae nae Kwanza huko Nyumbani kwako" lightness aliongea,


Kimei hakuwa na jinsi zaidi ya kukubaliana na mkuu wake Kisha akaondoka,

*********
Lengo la Oscar ilikua Ni kufahamu wahusika hivyo kufanya ukorofi wowote ingekuwa shida,

Alirudi nyuma ili Tena kuona Kama Kuna sehemu yoyote ya kupitia akakosa,.

Mwishowe alirudi mpaka juu kabisa akatafuta sehemu akajibanza na kutulia kusubiria watoke, hata hivyo hakukaa dakika nyingi kengele ya hatari ikaanza kulia mle ndani huku walinzi wakipita na silaha huko na huko,

"Shit wameona Ile maiti itakuwa" Oscar alijisemea Sasa akiwaza namna ya kutoka salama mle ndani,

Alitembea kwa kujificha Mara nyingine alijifanya mmoja wao ,

Kwasababu ambazo hakuzielewa sehemu Ile ya chini hakukua na kamera zozote hivyo Oscar alifanikiwa kutokea juu bila kuonekana, alitafuta sehemu ya dari juu akajibanza na Sasa akawashuhudia waheshimiwa wakiwa wanatoka huku wakiwa wamezunguukwa na walinzi wao,


Oscar Sasa alipigwa na mshangao,


"Aisee Kumbe!"
Aliwaza huku Sasa akihisi kazi yake itakuwa imeisha kabisa....

"Mvamizi hajatoka nje ya jengo yupo humu humu"

Mmoja wapo wa walinzi alisema akimuambia mr Bill,


"Safari hii nataka asitoke humu"

Nataka ndani ya dakika kumi mniletee huyo mtu akiwa hai hapa,....


Mr Bill aliongea huku akiwa anatetemeka kwa hasira,

Wakuu wake akina Tito Kimbikile walimuona kuwa amezembea katika nafasi yake lawama zote walimpa yeye, Ni kwa bahati siku hiyo Mr Johnson hakuwepo, hivyo kikao Cha siku hiyo alikuwepo Askofu Majimbi na Tito Kimbikile tuu,
 
KESI YA MZEE MNYOKA 16

SAA 9:14 usiku


Oscar akiwa pale juu alimuona Askofu Majimbi na Tito Kimbikile, ilikua Ni ngumu kuendelea kushikilia pale juu, na hivyo aliomba waondoke Haraka pale chini ili aweze kuondoka, aliendelea kushikilia pale huku akiomba Mungu Mlinzi yoyote asipige jicho pale juu,


"Nilishauri tuweke kamera huku chini mkanipinga, oneni Sasa tunavyotolewa jasho"

Alisema Majimbi,

"Acha ubishi Askofu, kumbuka kamera zinatumia mfumo wa komputa kujiendesha, na kama ujuavyo kutokana na teknolojia Sasa hivi mtu anaweza kuingilia mfumo huu na kuona kila kitu, believe me tungekuwa na camera huku chini tusingefik.......

"

Tito alikatishwa maongezi ghafla,

"Mkuu tuondokeni Sasa juu kuko clear"

Alisema Sasa jamaa mwingine ambapo walianza kupanda ngazi kurudi juu huku Tito akisisitiza Bili afanye kazi ya kumkamata huyo mtu kabla ya usiku kwisha,

Oscar Sasa alitambaa taratibu kupanda akiacha hatua kadhaa baina yao,.


Alipita kwenye njia yake ya mwanzo na kutokea kule store Kisha akatoka nje ,


Kwa tahadhari kubwa alitambaa chini kwa chini, huku akizidi kuliacha jengo, na baadae akasimama na kupotelea msituni....


Alifika mafichoni mwake na kuchukua vifaa vyake vyote Kisha akapotea,


"Imeisha hii!"


Oscar alijisemea huku akikiacha Kijiji cha Kinjeki, alifurahi kuona amemaliza kazi yake salama kabisa.


***************


Dokta Kimei alimueleza mama Monica kuwa Mzee Mnyoka alipata mstuko mfadhaiko na akajikuta ametoka nje ya hospitali Ila yupo mahali salama, Mama Monica alilazimisha kumuona mumuwe usiku ule ule, dokta Kimei hakuwa na kipingamizi alienda nae

*************

Dar es salaam


Oscar alifika kwa bosi wake Mr Allan, ambapo alitoa taarifa zote ikiwemo wahusikia aliofanikiwa kuwaona pamoja na ramani ya pale,


"Kazi nzuri Oscar, hatukutegemea ungefanya kwa wepesi kiasi hiki,..

Kwasasa unaweza kwenda kupumzika na wakati wowote kutoka Sasa hivi utakwenda rasmi kwa ajili ya kazi,..

Tunasubiri activation kutoka kwa mkuu, akitoka kwenye mkutano, kwasasa tutakuwa tunaangalia nyendo za Tito, na Majimbi kwa karibu,...

Tunaamini hawawezi kufanya chochote ndani ya muda mfupi, hivyo mheshimiwa akitoka tu kazi itaanza ndani ya siku tatu au nne zijazo,.

Sasa unaweza kwenda"


Mr Allan alimalizia huku akimpa mkono Oscar,

************

Dar es salaam saa 9 alasiri

Oscar alikua nyumbani kwake amejipumzisha wakati alipopigiwa simu hii

"Ndio, nimekuelewa"

Alisema baada ya kuongea kwa dakika kadhaa na upande wa pili ,


Sasa baada ya simu hii alijisikia kuchangamka, mwenyewe alishachoka kukaa kaa tu Bila kazi,

Simu hii aliitegemea , ingawa ni Kama iliwahi hivi, hata hivyo tofauti na matarajio yake mpango kidogo ulibadilika, na Sasa alitakiwa kukutana na Mr Allan, jioni Ile saa moja ili apewe mpango mzima,

Na hatimaye safari hii aliambiwa atafute mwenza katika kazi hii, hivyo alijishauri, na hatimaye akaona amchukue jamaa yake wa siku zote,

Baada ya kuweka vitu vyake sawa Oscar alitoka nje ya nyumba yake Kisha akachukua boda boda,


"Twende mpaka Banana"


Oscar alisema huku akiweka sawa jacket lake...

**********

Kijijini Kinjeki siku hiyo hiyo

Frank aliegesha Gari lake huku akivuta pumzi ndefu,

Hakujua amuambie Nini Mr Bill,


Ni kweli alijitahidi kumuua Mzee Mnyoka Ila Sasa Mzee Alitoweka hospitali, pamoja na kufanya jitihada zake kwa siku mbili hakufanikiwa kumuona,


"Asipoelewa Basi"
Alipiga usukani wa Gari yake Kisha akafungua mlango na kutoka nje,


Alipita vibarua wakiendelea na kazi zao moja kwa moja Hadi kwa Bosi wake,


"Sema, naona unakodoa macho tuu"

Mr Bill aliongea huku akipanga mafaili yake mezani,


"Mkuu, nimemkosa yule Mzee"
Frank aliongea,


"Kwahiyo unataka Sasa nikupigie makofi nikupongeze kwa kumkosa au?"

Mr Bill aliongea kwa jazba,


"Sikiliza nashindwa kuwavumilia, juzi mpuuzi mmoja katuvamia hapa, Tena mbele ya wageni, na ameua Mlinzi mmoja na hajakamatwa, wewe nawe kwenda kumaliza kazi ya dakika mbili tu unanijia hapa baada ya siku 4 Tena ukiwa umeshindwa, task ndogo tu, una akili kweli? Hebu toka mbele yangu,..


Mfuate mpuuzi mwenzako huko mkaendelee kujaza vifua vyenu"

Mr Bill aliongea,


Frank alitoka zake na kurudi juu,

Alienda moja kwa moja kwa Tony ambaye alikua anapanga mizigo,


"Oya man vip"

Oscar alimstua Tony,

"Dah we boya umenistua kinyama"

Tony aliongea Sasa akisalimiana na swahiba wake huyo,

Baada ya story mbili tatu, Frank alimueleza kuhusu kushindwa kwa zoezi zima la kummaliza Mzee Mnyoka,


"Pole jamaa yangu, Ni Kama mkosi juu ya mkosi juzi Kuna boya katuvamia hapa Basi ndio Kama ulivyoona Carlos haelewi chochote humu ndani, "

Tony aliongea...
 
KESI YA MZEE MNYOKA 16

SAA 9:14 usiku


Oscar akiwa pale juu alimuona Askofu Majimbi na Tito Kimbikile, ilikua Ni ngumu kuendelea kushikilia pale juu, na hivyo aliomba waondoke Haraka pale chini ili aweze kuondoka, aliendelea kushikilia pale huku akiomba Mungu Mlinzi yoyote asipige jicho pale juu,


"Nilishauri tuweke kamera huku chini mkanipinga, oneni Sasa tunavyotolewa jasho"

Alisema Majimbi,

"Acha ubishi Askofu, kumbuka kamera zinatumia mfumo wa komputa kujiendesha, na kama ujuavyo kutokana na teknolojia Sasa hivi mtu anaweza kuingilia mfumo huu na kuona kila kitu, believe me tungekuwa na camera huku chini tusingefik.......

"

Tito alikatishwa maongezi ghafla,

"Mkuu tuondokeni Sasa juu kuko clear"

Alisema Sasa jamaa mwingine ambapo walianza kupanda ngazi kurudi juu huku Tito akisisitiza Bili afanye kazi ya kumkamata huyo mtu kabla ya usiku kwisha,

Oscar Sasa alitambaa taratibu kupanda akiacha hatua kadhaa baina yao,.


Alipita kwenye njia yake ya mwanzo na kutokea kule store Kisha akatoka nje ,


Kwa tahadhari kubwa alitambaa chini kwa chini, huku akizidi kuliacha jengo, na baadae akasimama na kupotelea msituni....


Alifika mafichoni mwake na kuchukua vifaa vyake vyote Kisha akapotea,


"Imeisha hii!"


Oscar alijisemea huku akikiacha Kijiji cha Kinjeki, alifurahi kuona amemaliza kazi yake salama kabisa.


***************


Dokta Kimei alimueleza mama Monica kuwa Mzee Mnyoka alipata mstuko mfadhaiko na akajikuta ametoka nje ya hospitali Ila yupo mahali salama, Mama Monica alilazimisha kumuona mumuwe usiku ule ule, dokta Kimei hakuwa na kipingamizi alienda nae

*************

Dar es salaam


Oscar alifika kwa bosi wake Mr Allan, ambapo alitoa taarifa zote ikiwemo wahusikia aliofanikiwa kuwaona pamoja na ramani ya pale,


"Kazi nzuri Oscar, hatukutegemea ungefanya kwa wepesi kiasi hiki,..

Kwasasa unaweza kwenda kupumzika na wakati wowote kutoka Sasa hivi utakwenda rasmi kwa ajili ya kazi,..

Tunasubiri activation kutoka kwa mkuu, akitoka kwenye mkutano, kwasasa tutakuwa tunaangalia nyendo za Tito, na Majimbi kwa karibu,...

Tunaamini hawawezi kufanya chochote ndani ya muda mfupi, hivyo mheshimiwa akitoka tu kazi itaanza ndani ya siku tatu au nne zijazo,.

Sasa unaweza kwenda"


Mr Allan alimalizia huku akimpa mkono Oscar,

************

Dar es salaam saa 9 alasiri

Oscar alikua nyumbani kwake amejipumzisha wakati alipopigiwa simu hii

"Ndio, nimekuelewa"

Alisema baada ya kuongea kwa dakika kadhaa na upande wa pili ,


Sasa baada ya simu hii alijisikia kuchangamka, mwenyewe alishachoka kukaa kaa tu Bila kazi,

Simu hii aliitegemea , ingawa ni Kama iliwahi hivi, hata hivyo tofauti na matarajio yake mpango kidogo ulibadilika, na Sasa alitakiwa kukutana na Mr Allan, jioni Ile saa moja ili apewe mpango mzima,

Na hatimaye safari hii aliambiwa atafute mwenza katika kazi hii, hivyo alijishauri, na hatimaye akaona amchukue jamaa yake wa siku zote,

Baada ya kuweka vitu vyake sawa Oscar alitoka nje ya nyumba yake Kisha akachukua boda boda,


"Twende mpaka Banana"


Oscar alisema huku akiweka sawa jacket lake...

**********

Kijijini Kinjeki siku hiyo hiyo

Frank aliegesha Gari lake huku akivuta pumzi ndefu,

Hakujua amuambie Nini Mr Bill,


Ni kweli alijitahidi kumuua Mzee Mnyoka Ila Sasa Mzee Alitoweka hospitali, pamoja na kufanya jitihada zake kwa siku mbili hakufanikiwa kumuona,


"Asipoelewa Basi"
Alipiga usukani wa Gari yake Kisha akafungua mlango na kutoka nje,


Alipita vibarua wakiendelea na kazi zao moja kwa moja Hadi kwa Bosi wake,


"Sema, naona unakodoa macho tuu"

Mr Bill aliongea huku akipanga mafaili yake mezani,


"Mkuu, nimemkosa yule Mzee"
Frank aliongea,


"Kwahiyo unataka Sasa nikupigie makofi nikupongeze kwa kumkosa au?"

Mr Bill aliongea kwa jazba,


"Sikiliza nashindwa kuwavumilia, juzi mpuuzi mmoja katuvamia hapa, Tena mbele ya wageni, na ameua Mlinzi mmoja na hajakamatwa, wewe nawe kwenda kumaliza kazi ya dakika mbili tu unanijia hapa baada ya siku 4 Tena ukiwa umeshindwa, task ndogo tu, una akili kweli? Hebu toka mbele yangu,..


Mfuate mpuuzi mwenzako huko mkaendelee kujaza vifua vyenu"

Mr Bill aliongea,


Frank alitoka zake na kurudi juu,

Alienda moja kwa moja kwa Tony ambaye alikua anapanga mizigo,


"Oya man vip"

Oscar alimstua Tony,

"Dah we boya umenistua kinyama"

Tony aliongea Sasa akisalimiana na swahiba wake huyo,

Baada ya story mbili tatu, Frank alimueleza kuhusu kushindwa kwa zoezi zima la kummaliza Mzee Mnyoka,


"Pole jamaa yangu, Ni Kama mkosi juu ya mkosi juzi Kuna boya katuvamia hapa Basi ndio Kama ulivyoona Carlos haelewi chochote humu ndani, "

Tony aliongea...
Well
 
KESI YA MZEE MNYOKA 17

"Pita iyo nyumba hapo Kama unaenda kanisani, halafu ingia kulia niache hapo"

Oscar alikua anamuelezekeza boda boda ..


Oscar alishuka jirani na kwa rafiki yake George ambaye Mara kadhaa walifanya kazi pamoja,


Kama ilivyo kawaida yake Oscar hakupitia Mlangoni, alizunguuka nyuma ya nyumba Kisha akavaa gloves zake na kwa Kasi ya ajabu akaruka na kujivingirishia ndani ya geti,

Ilikua Ni saa 10 alasiri , kwa ratiba za George alijua lazima atakua nyumbani,

Oscar alinyata huku akitabasamu kwa mzaha wake huu anaomfanyia rafiki yake, aliendelea mpaka mlango wa nyuma na kuufungua Kisha akapitiliza sebuleni,

TV ilikua imewashwa hivyo akahisi lazima jamaa yake huyo hatakua mbali,


Alisogea kwenye friji na kutoa juice kisha akajimiminia juice Ni wakati huo Sasa simu yake ilitikisika kuonyesha ishara ya ujumbe mfupi,

"Karibu home broo, vipi siku hizi umeacha pombe? Mbona umechukua juisi?"


Ulikua Ni ujumbe mfupi kutoka kwa George,..ikionyesha kuwa alikua anamtazama akiwa mahali fulani,


"Okay umeshinda"

Oscar alisema kwa sauti ..

"Tangu wale maboya walipoingia na kuchukua TV yangu niliboresha mfumo wa ulinzi hapa, "

George aliongea akitokea chumbani...

************

Mzee Mnyoka alirudi zake kijijini akiwa na afya njema, Kama ilivyo kawaida wanakijiji walimiminika nyumbani kwa Mzee Mnyoka kumjulia Hali,


Mpaka Sasa mkewe alidhani mumewe kweli alisumbuliwa na presha tu,

Wasingeweza kukaa kwa dokta kimei kwa muda wote, hivyo baada ya kulala siku moja tu Mzee Mnyoka Sasa alipewa "semina elekezi" ya namna kuishi kijijini huku pia akipewa mbinu na mikakati ya kukabiliana na wale watu endapo watataka kumdhuru,

Na hata hivyo serikali iliahidi kumlinda kwa kipindi chote hiki ambacho oparesheni ya kuwatia nguvuni wahujumi ikiwa inasukwa,

Ni katika mikakati hii pia Mzee Mnyoka aliweza kupewa simu janja, na kifaa kingine kidogo ambacho alitakiwa kutembea nacho kila sehemu,.
Kwa maelezo yao walimuambia Mzee Mnyoka kuwa hata ikitokea atatekwa Basi asiwe na wasi wasi watajua alipo....

Hivyo mzee Mnyoka kwa umahiri mkubwa akakishonea kidubwasha hicho kwenye mkanda wake mwenyewe alikiita hirizi,


Mzee Mnyoka alitakiwa kutoa taarifa atakazohisi zingesaidia hususani mienendo ya kule mgodini,


**************


Oscar akiwa na George walitoka Kama wanaenda Gongo la mboto Kisha wakafika banana, wakavuka upande wa pili wakapaki Gari yao nje ya kanisa la washindi ,

Kwa mtu yoyote aliyewaona alijua Ni washirika ambao walienda kwenye ibada pale winners chapel,

Oscar alitoa mkoba Kisha wakaingia lango la kabisa Hilo huku sauti za nyimbo vikiendelea Kama kawaida,..

Walipanda kwenye upande wa juu Kisha wakawa Kama wanaotafuta viti vya nyuma kabisa, halafu wakatokea mlango wa nyuma na kushuka Tena ngazi kurudi chumba Cha chini,

Baada ya dakika moja alitokea binti
"Mchungaji anawasubiri kabla ibada haijaanza"

Alisema yule msichana Sasa huku akiwakaribisha ofisini kwa "Mchungaji"


Oscar alimuangalia George Kisha wakakonyezana wakaingia ndani,

Walipita chumba Cha kwanza Kisha wakaingia ndani na kumkuta Mr Allan akiwa amekaa kwenye kiti chake Cha kuzunguuka,

Sasa George alishindwa kujizuia na kutoa kicheko kabisa,

"Tuko kazini George hebu kua Basi!"

Alisema Mr Allan nae akitabasamu huku akiwapa Mikono,


"Kwasasa nataka mmoja wenu tumpandikize kwa waziri Tito, baada ya kushauriana na wenzangu tumeona lazima watuhumiwa wakamatwe wakiwa na vidhibiti hivyo kwa Sasa Oscar fanya mipango yako nataka kuona baada ya wiki moja uwe karibu Sana na Tito, halafu siku yoyote Tito akienda kule mgodini ndio tukamalize kazi kule, tunataka kumkamata kule kule akiwa Kwenye hiyo maabara yake uchwara, "

Alisema Mr Allan,
**************************************
Mgodini-Kinjeki

"Yule Mzee amerudi sasa tunasubiri oda yako mkuu"

Frank alimwambia Mr Bill,

"Kwahiyo umeona hapa ndio itakuwa rahisi sio?"

Kazi kupenda vitu rahisi tu,
Hebu tulia kwanza huyo mzee tutadili nae kidiplomasia tu mpaka mwenyewe ataomba poo hapa,

Carlos aliongea Sasa,

Ni kweli mikakati ilipangwa kimya kimya kumfanya Mzee Mnyoka mwenyewe akimbie kile Kijiji kwa ridhaa yake,

***************

Mzee Mnyoka alikuwa na shamba lake la kahawa, na alivuna Mara moja kwa mwaka, hapo zamani waliuza kahawa bila kuwa na hati yoyote Wala nyaraka,

Lakini baada ya wizi kushamiri Sasa ili kuuza kahawa ilimpasa mkulima kwanza kuandikiwa na kiongozi wake wa Dini hati ya uaminifu, pili, mkulima angeenda na hati hiyo kwa kiongozi wake wa Kijiji ambapo angeandikiwa barua ya utambulisho ambayo Ingemfanya mkulima kuuza kahawa yake,



Mzee Mnyoka alitumia mauzo hayo ya kahawa kila mwaka kusomesha watoto wake, hususani James ambaye alikua kidato cha tano,


Siku hii Mzee Mnyoka alienda kwa Padri John kwa ajili ya kuandikiwa hati ya uaminifu ili aweze kwenda ofisi ya Kijiji kupata hati ya kuuza ndipo Sasa Jambo la kushangaza zaidi linatokea,


"Nzee Nyoka siwezi andika, wewe bado iko na kesi huko"

Padri John Sasa aliongea huku akikataa kata kata kumuandikia Mzee Mnyoka,

"Padri, lakini si unajua wazi Ile kesi nilitengenezewa? Padri? Hata wewe unaamini Mimi kweli niliiba ng'ombe?"

Mzee Mnyoka Sasa alipigwa na butwaa,


"Nzee Nyoka wewe nenda malizana na serikali, kesi naisha, Mimi andikia wewe hati safii"


Padri John aliongea,



Mzee Mnyoka Sasa hakuamini macho na masikio yake! Padri huyu huyu ambaye alikua msaada na tegemeo lake Leo hii anakataa kumsaidia Tena kumuandikia tu barua ili auze kahawa yake?

"Naenda kwa mwenyekiti!"
Mzee Mnyoka alijisemea akitoka


***************


Oscar na Swahiba wake George walitoka kwa Mr Allan , na kupitia njia zile zile na kutoka nje,

Wakiwa ndani ya Gari Sasa ndipo story zikanoga,.

" Yaani Mzee anajifanya Mchungaji kabisa kumbe bonge la jasusi!"

George Sasa aliongea huku akicheka,...


"Tena pale tumewahi, umkute Sasa jumapili akiwa anaombea mapepo! Yaani nakuambia utasema umemuona Askofu Gwajima wa ufufuo na uzima, kumbe Ni mtu mmoja hatari anaweza kukuvunja mbavu ukimuendea vibaya"
Oscar alisema Sasa,.


"Halafu waumini wake wanajua wamepata bonge la Mchungaji..."


George aliongea,

"Ah yule Mzee kiboko mi nakuambia, Ni Noma"

Oscar alisema Sasa wakimalizia mitaa kadhaa kurudi kwa George,

"Sasa kuhusu Tito mi nitamalizana nae, kuanzia leo Mimi na wewe hatujuani kabisa, kuhusu mawasiliano nadhani kila mmoja anajua namna ya kumpata mwenzake, kanuni Ni zile zile, "

Oscar alisema huku akishuka kwenye Gari kurudi kwake
 
KESI YA MZEE MNYOKA 18

"Mzee Mnyoka wewe sio mgeni hapa Kijijini na Jambo la ajabu kabisa wewe ndio ulikua mstari wa mbele kutunga hii sheria kuwa mtu asiuze kahawa bila utambulisho wa kiongozi wake wa Dini, Sasa nakushangaa unavyokomaa eti nikupe barua, au Mzee Mnyoka unataka nivunje sheria?" Mwenyekiti aliongea huku akimtazama Mzee Mnyoka

"Lakini kesi si iliisha na mahakama ilionyesha Sina hatia?"
Mzee Mnyoka aliuza,

"Sikiliza Mzee Ile Ni mahakama, Ina utaratibu wao, na sisi kijijini tuna utaratibu wetu, hata Kama mahakama itaona huna hatia, bado sisi Kama Kijiji tunaweza kukuwajibisha,

Na Jambo la kukushauri tu Mzee Mnyoka, tafuta utaratibu mwingine wa kupata hela Ila nataka nikuhakikishie kahawa hutauza mpaka kesi yako iishe"

Mwenyekiti aliongea kwa majigambo,

"Sikiliza mwenyekiti Mimi na wewe tunafahamu ukweli wote, kuwa sikuwahi kuiba hata kuku hapa Kijijini, hivyo siwezi kuhukumiwa kwa kosa ambalo sijafanya! Na kwanza kesi hiyo imeisha"
Mzee Mnyoka alijitutumua

"Sasa kesi imeisha wapi? Je nikikuuliza una hati yoyote ya kutoka mahakamani inayosema wewe huna hatia?"

Mwenyekiti aliongea Kisha akaendelea,

"Wewe Rudi zako nyumbani fanya utaratibu mwingine wa kupata pesa, subiri uchunguzi ufanyike kwa upya Kama huna hatia itajulikana tu, ingawa Sasa siwezi kukuhakikishia kuwa Ni lini"

Mwenyekiti aliongea huku akinyanyuka kuonyesha kuwa mazungumzo yake yametosha

*********
Dar


Waziri Tito alipenda Sana kujiachia sehemu mbali mbali za jiji siku ambazo hakua na ziara za kikazi au vikao vya bunge, kwanza alikua waziri kijana hivyo aliutumia vizuri ujana wake, Waziri Tito alikua na msemo wake kuwa "tunaishi leo tu"

Hivyo kila "leo " aliitumia vizuri Sana, tofauti na mawaziri wengi yeye alitembea na walinzi Binafsi na nyumbani kwake alilindwa pia,


Siku hii ya leo Tito aliamua kumtoa out mkewe pamoja na binti yake Joyce,

Alikua na kawaida hiyo ingawa sio Mara kwa Mara ,

Baada ya kumaliza mizunguuko yao walipitia kwenye duka moja la nguo ,

Walipaki Gari Kisha Tito na familia yake walishuka wakiwa na Mlinzi mmoja kwenye Gari,

Wakati wote umbali wa mita Kama 150 kulikua na Gari ndogo ambapo ndani yake

Alikuwemo dereva Peke yake,


Hakushuka kwenye Gari mpaka pale Tito na na familia yake walipokua wanatoka,


Mtu huyo alitoa simu yake mfukoni Kisha akatamka Neno moja tu,

"Now"

Akimaanisha "Sasa" Kisha akafungua mlango wa Gari na kutoka nje, akiwa anaelekea kule kwenye duka,

Ni wakati huo wakatokea vijana wawili walionekana Kama wahuni hivi na kuanza kumfanyia fujo Waziri Tito,

Sasa Mlinzi wake Alianza kuwatisha ikiwemo kuwatolea bastola, hata hivyo vijana wale walizidi kutoa maneno ya kejeli na matusi kwa waziri,

"Unakula nchi tu, unauza twiga huko sisi watanzania wengine tunabaki kuwa maskini , kazi kula Bata tu na kutembea na wasichana wadogo"

Walizidi kuongea wale vijana huku Sasa wakianza kushika Ile mifuko ambayo mkewe Tito na binti yake walikua wameshika,

Watu walianza kusogea eneo la tukio huku kelele zikirindima,

Ni wakati Sasa yule mtu aliyekua kwenye Gari nae akasogea...


Waziri Tito sasa alichanganyikiwa hakujua namna ya kuepuka lile zogo bila kuharibu Ile sura yake kwa jamii alijilaumu Sana kuwepo maeneo Kama Yale,

Vijana wale Sasa walianza kuvuta Ile mifuko, yule Mlinzi Sasa alikua akijishauri, alimuangalia bosi wake ambaye alimtingishia kichwa kumkatalia kuwa asitumie bastola, ndipo Sasa akarudisha bastola yake kiunoni,

Kisha akawasogelea vijana wale kibabe,

"Aisee huyo Ni waziri tafadhali naombeni muondoke, "
Yule Mlinzi aliongea Sasa akiwasogelea,

Ni wakati anasogea ndipo Sasa wale vijana wakakaa mkao wa mapigano kwa ajili ya kukabaliana na Mlinzi...

Tito alimuamini Sana Mlinzi wake, hivyo alijua vijana wale wangepata adabu ya kutosha,

Mlinzi wa Tito alikua anafikiri awaachie ngeu tu kidogo Kisha amuwahishe bosi wake kabla "waandishi" hawajaanza kutoa simu zao,


Hivyo hakutaka hata kukunja ngumi au kukaa mkao wowote, aliwasogelea tu,


Kumbe alikosea Sana! Hakika alikosea Sana,
Maana Sasa wale vijana walijirusha hewani kwa mtindo wa samasolti Kisha kwa pamoja wakaachia mateke yao na kutua kifuani kwa Mlinzi ambaye kwakuwa hakutegemea akajikuta Yuko chini huku damu zikimtoka
Yule mtu Sasa alishuhudia kila kitu ambapo Sasa aliingia Kati Kati ya lile duara Kisha akamfuata mtoto wa Tito Joyce,

"Nishikie hii simu, let me handle this"

Alisema Sasa yule mtu Kisha akawasogelea wale vijana pale walipokua wanamsulubu Mlinzi



*************


Mzee Mnyoka Sasa alirudi Nyumbani akiwa na mawazo mengi, Hali ya uchumi kwake ilikua sio nzuri,

Kipato pekee kilichokua na uhakika kwake ilikua Ni zao la Kahawa, Mzee Mnyoka alikua na uwezo wa kuhifadhi kilo zaidi ya 70 kwa mwaka,

Kwa Bei ya shilingi elfu tatu na Mia tano kwa kilo Mzee Mnyoka angeweza kumlipia mtoto wake ada ya mhula wa pili pamoja na michango mingine,


Hivyo Jambo Hili lilimkosesha amani kabisa,


Kulikua na uwezekano wa kumpa jirani yake auze badala yake lakini kulikua na kiwango kwa muuzaji mmoja asingeruhusiwa kuuza zaidi ya kilo 80

"Lakini mbona sijafanya kosa lolote?"

Mzee Mnyoka aliwaza bila kupata majibu,

Ni wakati anatafakari ndipo alikuja balozi wake wa nyumba kumi,

Bwana Ali ,

Alimletea barua yake kutoka huko kwenye serikali ya Kijiji

"Yah HATI YA MASHTAKA,

Kwa barua hii unajulishwa kuwa umefunguliwa hati ya mashtaka kuhusu wizi wa Ng'ombe mnamo mwezi juni tar 4 mwaka 2016,""

Hivyo unatakiwa kufika hapa Ofisi ya Kijiji tar 10 jumatatu ijayo kwa ajili ya kupata utaratibu wa mashtaka yako"

Ilisema sehemu ya barua hiyo..
Mzee Mnyoka Sasa alichanganyikiwa,

Alijua utaratibu kesi ulivyo,

Mwanakijiji akishapata hati ya shtaka asingewe kupata fursa yoyote pale Kijijini mpaka kesi yake itakapoisha,


Zaidi Sana vikao vya kesi huchukua hata miezi mitatu,

"Dah"

Mzee Mnyoka alisema akimuonyesha mkewe Ile barua,


*******


"Hey wajomba mnajua kabisa huyo Ni waziri lakini mnajitia machizi si ndio?"

Yule jamaa aliongea huku akiwa anawakabili Sasa,

Muda huo Sasa waandishi uchwara walishawasha simu zao
"We Nani kwani, "

Alisema yule mhuni mmoja huku akiruka teke ambalo yule jamaa alilikwepa kirahisi tu,


Kisha kwa Kasi ya ajabu akaruka teke moja na kumpasua kidogo kwenye paji la uso, yule mwenzake nae akaja akakutana na ngumi Kali iliyompeleka chini,

Sasa waziri Tito alijisikia kumhusudu huyu jamaa kutokana na uwezo wake wa kupigana,

Ndani ya dakika tatu wale jamaa walikua chini wakivuja damu,

Yule mtu alimnyanyua yule Mlinzi na kumpangusa huku wale jamaa wakiamka na kujikongoja kukimbia,

Alimfuata Joyce na kuchukua simu yake,

Kisha akapiga hatua kuondoka,


"Kijana subiri kidogo"

Alisema Sasa waziri Tito huku wakisogea pembeni

"Asante kwa kuniokoa"

Vipi unaitwa Nani?

"Oscar"

Alijibu yule jamaa
 
KESI YA MZEE MNYOKA 19

Mzee Mnyoka Sasa maji yalianza kupanda taratibu kutoka magotini,

"Mbona Kama Kuna kitu sikielewi hapa, mbona kesi iliisha kule Mzee Mnyoka, na hata hakimu alisema huna kosa?"

Mama Monica nae alishangaa,


"Hata Mimi nashangaa mke wangu, hawa jamaa Kuna Jambo wanalitafuta bila shaka"

Mzee Mnyoka Sasa aliona apate ushauri wa dokta Kimei, alimpigia na kumueleza kuhusu kuzuiliwa kwa Kahawa yake ,

"Ngoja niangalie namna ya kukusaidia Mzee Mnyoka baadae nikitoka kazini Kuna rafiki yangu anahusika na mambo ya kilimo nadhani anaweza kukusaidia, unajua shida Mzee Mnyoka siku hizi wameshusha Sana mamlaka mpaka Kwenye ngazi ya Kijiji, wenyeviti na watendaji wana Nguvu mno,

Na busara Mara nyingi Ni kukaa nao, angalia siku hizi sisi wenyewe hata kwenye utoaji huduma, mtendaji wa Kijiji lazima ahusike moja kwa moja ngoja nikitoka tutawasiliana Mzee wangu"

Alisema dokta Kimei akikata simu,....



Ni kweli Mzee Mnyoka alijua wazi hata Kama simu ingetoka huko juu bado njia za kupita Ni zile zile,

Hata hivyo sehemu pekee ambayo ni rahisi Ni kupitia kwa Padri John ambae angemuandikia na kumuwekea muhuri wa kanisa,


"kwani Padri John nae wamemfanya Nini?"

Mzee Mnyoka aliwaza akielekea chumbani kwake

********

"Sawa Oscar tafadhali Sana Kama hutajali naomba unisindikize nyumbani, naomba Sana"


Waziri Tito aliongea kwa upole,.


Joyce alijiuma uma meno yake huku akimpiga jicho Oscar la "kumuomba"

Awasindikize,

Oscar alienda kwenye Gari lake na kulipaki pale dukani Kisha akaingia kwenye Gari la waziri,


"Hawa jamaa wanakula Raha Sana"

Tito aliwaza wakati Gari Hilo la waziri likikata mitaa kuelekea maeneo ya Mbezi beach,

Ambako mawaziri wengi walipenda kuishi badala ya makazi yao rasmi ya kiofisi kule Dodoma,.


Baada ya dakika 40 walifika na Oscar alijifanya kuwa na haraka sana ya kurudi,


"Kijana hebu tafadhali uingie hata ndani tufahamiane, Mimi najua mjini hapa nakupotezea muda wako mwingi, tafadhali Sana"

Alisisitiza Tito

"Ni kweli Mzee hapa nilikua naelekea ofisini kwangu nilitoka tu kupata chakula kidogo ndio nikawa narudi"


"Unafanya kazi wapi kwani Kijana"

Tito Sasa aliuliza


"Nauza vifaa vya Music Mzee wangu,
Kama vile mixer, spika ,vinanda, magitaa n.k"

Oscar alijibu,

"Duka Ni la kwako? Au umeajiriwa?"

Tito aliuliza Sasa wakikaa kwenye bustani ndogo pale nje


"Nimeajiriwa tu na tupo wanne tunapeana zamu wawili asubuhi na wawili jioni"

Oscar alisema huku akimuangalia Tito,


"Okay Sasa nimekuelewa, wewe nenda huko ofisini kwako Ila kesho nitakuomba Sana ufike hapa nyumbani kama hutajali alisema Tito huku akitoa pochi yake..


Chukua hii upate nauli maana najua uliacha Gari yako pale, na bila shaka watakutoza parking fees"

Alisema Tito akitoa noti kadhaa za elfu kumi kumi,...

Oscar alizipokea kwa heshima Kisha akatoka nje ya Geti na kutoweka,

********


Sasa huko mitandaoni habari zilizagaa kila Kona,
Magazeti ya mitandaoni pamoja na vyombo vya habari walikuwa wanaripoti taarifa za "waziri wa Nishati Kushambuliwa"

Baadhi ya vipande vya video vilisambaa na Oscar akawa maarufu ghafla,


Wakati huo Oscar alikua mahali fulani akiwa na wale vijana,


"Ila ungetuua bosi, sio kwa mateke Yale!"


Alisema Sasa kijana mmoja,


"Nyie maboya mlitakiwa kabisa mkaze, tupigane kweli sio vile mateke mawili tu mnakua hoi"

Oscar alisema,.

"Okay imeisha hii mkaendelee na majukumu yenu, nikiwahitaji nitawatafuta"



Oscar alisema huku akiagana na vijana wake,


SAA mbili kamili,.

Habari Ile ilirushwa kupitia Azam 2,

Na watu wengi walimsifia Sana Oscar na waziri mwenyewe alikiri kuwa atafanya namna kijana yule awe karibu nae zaidi,..


"Yeah kwakweli nimefurahi kuona nchi yetu ikiwa bado na vijana wakakamavu Kama Oscar, lakini sio ukakamavu tu Bali pia uzalendo, unajua Sasa Kuna vijana wengi sio wazalendo, kumuokoa waziri Ni uzalendo mkubwa Sana, kwahiyo Mimi nitamtafuta Oscar"


Waziri alikua anahojiwa na Mtangazi wa runinga,..

Mr Allan nae hakua nyuma katika kufuatilia habari hii,.


"Good job Oscar!"

Alijisemea huku akizima TV yake...


****************************************

Mgodini Kinjeki


Shughuli ziliendelea Kama kawaida huku uzalishaji ukiendelea maradufu,

Faida Sasa iliendelea kuonekana,

Mawasiliano yalikua mazuri Kati ya mmiliki Bwana Johnson na wadau wenzake,


Ni Askofu Majimbi ndie ambaye alikataa kata kata kurudi Tena kule mgodini kutokana na seke seke la siku ile


Ni hapo Sasa Askofu Majimbi nae alivutiwa na Kijana Oscar ,

Baada ya kuona jinsi alivyompigania rafiki yake, Sasa aliona Kijana huyu angefaa kumuwakilisha yeye hususani safari za kule Mgodini,

Kwa maana hiyo alitaka atumie mgongo wa TiTo kwanza, maana isingekuwa Vyema kujitokeza kwake hapa mwanzoni,


"Vijana hao ukimpa nyumba na Gari dogo tu na uhakika wa hela ya kufanyia starehe unamtumia utakavyo"

Ilikua Ni sehemu ya gumzo kwenye simu Kati ya Askofu Majimbi na Waziri Tito wakimjadili Oscar,



"Vipi Kama atakataa?"


Tito aliuliza
"Hakuna kijana atakataa, huwezi kushindwa kumshawishi mheshimiwa Waziri"


Waliendelea kujadiliana


*********


"Hallo Mzee Mnyoka Sasa nimeongea na jamaa kwakweli Ni Kama nilivyohisi , amesema kesi hiyo lazima ishughulikiwe Kijijini, maana yeye akiwapigia huko Ni Kama anawafosi"

Dokta Kimei aliongea kwenye simu alimueleza Mzee Mnyoka,


Mzee Mnyoka Sasa alijisikia vibaya,

Ilikua imebaki wiki moja tu mwanae James arudi kutoka shuleni kwa ajili ya likizo , na hivyo ingempasa kumuandalia Pesa ya nauli ya kurudi pamoja na ada na vifaa kwa ajili ya mhula wa pili,


"Ee Mungu nisaidie"
Mzee Mnyoka alijisemea,


Yeye pamoja na mkewe walichanganyikiwa maana ilifikia hatua Sasa hata Pesa ya matumizi iliisha,.

Hata zile shilingi Mia tano ambazo alikua akimpa mtoto wake Mary aliyekua akisoma shule ya kata ya Kinjeki kidato cha pili Sasa alikosa,


Ndipo Sasa Mzee Mnyoka aling'amua kuwa lengo halikua kumnyanyasa yeye tu Bali Sasa familia yake yote ilikua hatarini,


Alienda Mara kadhaa kwa Padri lakini majibu yake yalikua Yale Yale,


"Siwezi kukupa hati mpaka kesi iishe"


Na Sasa Mzee Mnyoka uvumilivu ulikua unataka kumuishia

*********

Saa 12 na nusu Jioni Oscar alikua akigonga geti Nyumbani kwa Tito,

Baada ya kufunguliwa na Mlinzi, Mlinzi alimuelekeza Njia za kupita Hadi kufikia mjengo huo,

Ilikua Ni nyumba nzuri sana Kama zilivyo nyumba nyingi mtaa huo wa "wazito"

Mlinzi huyu alikua kwa ajili ya shughuli ndogo ndogo tu kama vile kuelekeza , kuuliza watu wanaokuja n.k,


Lakini mambo mengi hapo ya kiusalama yalikua katika mfumo wa teknolojia,

Oscar alipitiliza moja kwa moja na kubonyeza kengele ya mlangoni Sasa,


"Ohhh karibu Sana Kaka Oscar"
Ilikua Ni sauti ya Joyce alimkaribisha Oscar ndani,

"Asante Sana Joyce!"
Oscar nae alisema

"Lakini Jana sikukutajia jina langu, umenijuaje!?"

Joyce aliongea Sasa alimkaribisha Oscar sebuleni,


"Joyce bhana! Wewe ni mtoto wa waziri kwahiyo lazima ufahamike tu"

Oscar Sasa aliongea huku akiweka nukta, kana kwamba hataki kuongea Tena,

"Baba anakusubiri Sasa twende huku"

Alisema Joyce huku wakipanda ngazi Sasa kuelekea kwa waziri Tito Kimbikile

Walifika na waziri alionyesha Furaha yake wazi wazi!


Ilifika mahali Oscar akawa anajisikia kumuhurumia ,

Baada ya salamu na maongezi mafupi Sasa Tito akaanza mada yake!
 
Guys tusameheane hadithi hii ndio ya kwanza kuandika! Nikirefer kisa Cha kweli ambacho kilinitokea mwenyewe nikaongeza chumvi kwa kutumia fasihi,


Hadithi hii sikuihariri! Hivyo Kuna marudio mengi ya baadhi ya maneno kama vile "Sasa" na baadhi ya wahusika kujichanganya!

Bado Mimi ni mtunzi chipukizi kwa yeyote anataka kunipa support ikiwemo kunidhamini kutoa kitabu basi nitashukuru!!

Wengine wanaweza kuungana na mkuu Gily kuniwezesha bando!

Nawapenda sana!

Namba yangu ni 0746 mia mbili sitini na sita , mia mbili sitini na Saba!
 
Guys tusameheane hadithi hii ndio ya kwanza kuandika! Nikirefer kisa Cha kweli ambacho kilinitokea mwenyewe nikaongeza chumvi kwa kutumia fasihi,


Hadithi hii sikuihariri! Hivyo Kuna marudio mengi ya baadhi ya maneno kama vile "Sasa" na baadhi ya wahusika kujichanganya!

Bado Mimi ni mtunzi chipukizi kwa yeyote anataka kunipa support ikiwemo kunidhamini kutoa kitabu basi nitashukuru!!

Wengine wanaweza kuungana na mkuu Gily kuniwezesha bando!

Nawapenda sana!

Namba yangu ni 0746 mia mbili sitini na sita , mia mbili sitini na Saba!
Warry out bro, number coppied
 
Guys tusameheane hadithi hii ndio ya kwanza kuandika! Nikirefer kisa Cha kweli ambacho kilinitokea mwenyewe nikaongeza chumvi kwa kutumia fasihi,


Hadithi hii sikuihariri! Hivyo Kuna marudio mengi ya baadhi ya maneno kama vile "Sasa" na baadhi ya wahusika kujichanganya!

Bado Mimi ni mtunzi chipukizi kwa yeyote anataka kunipa support ikiwemo kunidhamini kutoa kitabu basi nitashukuru!!

Wengine wanaweza kuungana na mkuu Gily kuniwezesha bando!

Nawapenda sana!

Namba yangu ni 0746 mia mbili sitini na sita , mia mbili sitini na Saba!
Support tutaendelea kukup usijali kabisa. .
 
KESI YA MZEE MNYOKA 20
"Oscar Kama ujuavyo kutokana na kazi zetu hizi tunakumbana na ghiliba nyingi, lakini kwakweli Jana umenifurahisha Sana, na zaidi ya yote ulinisaidia Sana, kwakweli, hata hivyo nikaona ili kutoa shukran zangu kwako nimeona nikupe kazi! Sijui unalionaje Hilo?"

Tito Sasa aliongea kwa hamasa!

"Kwakweli Mzee itapendeza Sana, lakini Sasa mpaka nijue kazi yenyewe maana unajua Mzee Mimi Elimu yangu Ni ya kidato cha nne tu, na sikua na matokeo mazuri Sana, "

Oscar alisema,

"Hata usijali, maisha Ni zaidi ya kusoma Oscar, wangapi Wana PhD zao lakini wako mtaani tuu, usiogope,

Unajua sisi mawaziri tuna kazi nyingi, Kuna mahali naweza kuhitajika wakati mwingine hata kufuata hata nyaraka tu! Sasa nikiwa na mtu Kama wewe unaweza kunisaidia zile kazi ndogo ndogo Kama hizo, kwa maana fupi nataka uwe msaidizi, wangu"

Tito alisema

"Na itakuwaje yaani utaratibu mzima wa kazi"
Oscar aliongea Sasa,


"Kazi kubwa Ni kuzunguuka na Mimi utakuwa Kama mlinzi wangu wa pili Ila Sasa wewe utakua unaniwakilisha kwenye zile shughuli zangu za nje ya ofisi, mfano Nina mashamba yangu kule kiluvya, Nina Ranchi moja kule mlandizi n.k, Sasa Mimi siwezi kufuatilia kila kitu kwahiyo wakati mwingine nitakua nakutuma wewe tu na mambo mengine tutazidi kuwasiliana, na sitakua nakulipa mshahara, Bali kila kazi utakayokua unafanya nitakulipa, na wakati mwingine utakua free na Mambo yako"

Tito aliongea

"Basi Hakuna shida Mzee, niseme kwamba Mimi nimekubali na tunaweza kuanza kazi!"

Alisema Oscar

************

Mzee Mnyoka aliwaza na kuwazua Sasa alikosa majibu,

Na hatimaye shule zilifungwa na mtoto wake James akarudi nyumbani kwa ajili ya likizo,

Mdogo wake Mary alimueleza kila kitu Kaka yake kuhusiana na kesi na "majanga" yote yaliyomkuta Mzee wao,


"Ndio Ni kweli tuko na Hali ngumu kwasasa Ila Mambo yatakaa sawa tu utarudi shule bila shida"

Mzee Mnyoka alikua akimtoa hofu mwanae, aliamini Kuna "namna" ya kuondokana na haya maseke seke,

Ingawa hakujua Ni kwa namna gani,


"Maisha hayawezi kusimama kwa ajili ya Jambo Hili"

Mzee Mnyoka aliwaza ,


*************


Baada ya wiki moja



Oscar Sasa alikua karibu na familia nzima ya Tito,

Na Kuna siku nyingine alichelewa Sana na "majukumu" yake akiwa na Tito hivyo alipewa sehemu ya kulala,


Kwa ufupi familia nzima ya Tito ilimuamini,


Siku hii ya leo, Oscar alipewa kazi ya kutuma baadhi ya taarifa kwa njia ya barua Pepe,

Zilikua Ni nyaraka mbili,

Oscar alizipeleka tu kwenye sehemu ya kutolea huduma za mtandao "internet cafe"

Ambapo alitakiwa tu kumuuliza Bwana ima,

Kisha angempa zile nyaraka,


Oscar aliamua kujiongeza na kununua bahasha nyingine ya kaki, Kama Ile Ile Kisha akachana na kusoma

"UreFact
The products may 2016"

Kilikua Ni kichwa Cha habari,

Oscar aliamua kuzipiga picha Kisha akaweka kwenye bahasha nyingine na Ile akaitupa mbali,


Alifika sinza kumekucha kisha akapaki Gari na kuingia kuelekea kwenye jengo moja lililokua na milango miwili ya vioo

"IMA INTERNET CAFE"

maandishi yalisomeka,


Baada ya salamu Oscar alimuuliza Kisha akampa Ile bahasha na kumnong'oneza

"Imetoka kwa Tito"

"Okay poa, naituma chap"

Alisema Ima Kisha akachukua Ile bahasha na kuingalia kidogo,

"Sikiliza jomba,

Hii bahasha sio, na usirudie Tena kufungua bahasha za watu"

Ima alimwambia Oscar kwa sauti ya chini

"Mhhh jamaa amejuaje? Na bahasha ziko sawa hizi?"

Oscar aliwaza huku akitafuta jibu la kumpa..
 
KESI YA MZEE MNYOKA 21

Mzee Mnyoka Sasa alipata taarifa kuhusu mwenendo wa kesi yake,

"Ni taratibu zile zile Mzee Mnyoka, nitakupa hati ya shtaka lako, Kama utakubali Basi, halmashauri ya nidhamu itakujadili ndani ya wiki moja, halafu tutaitisha kamati kwa ajili ya kutoa maamuzi, lakini Kama utakanusha, Basi, tutaunda tume ya uchunguzi ambayo itabidi ifuatilie kwa undani Kama uliiba ngo'mbe ama la, lakini tume hiyo pia haitaishia hapo, kumbuka Kijiji kina watu wengi, kwahiyo hata Kama wataona huna hatia, bado kamati inaweza kushauri uchukuliwe hatua maana kwanini utajwe wewe na sio mwanakijiji mwingine?"

Mtendaji wa Kijiji Alikua akimpa maelezo Mzee Mnyoka,

"Wewe nipe hiyo hati na nataka nijibu hapa hapa"

Mzee Mnyoka aliongea Sasa huku hasira zikizidi kumpanda,


"Hapana, kanuni zinasema unatakiwa kujibu ndani ya siku 14 sio lazima leo!"

Mtendaji alimuelewesha Mzee Mnyoka,

"Wewe nipe"
Mzee Mnyoka alisema akipokea hati yake ya shitaka na kutoka nje ya Ofisi ya Kijiji,

Siku zote uongo ukisemwa Sana bila kukanushwa Basi hugeuka kuwa kweli,


Hivyo taratibu wanakijiji wakaanza kumuona Mzee Mnyoka Kama mwizi kweli, zaidi ya hapo waliona Mzee Mnyoka kuwa Kama mtu mwenye mtazamo tofauti na viongozi wa Kijiji,

Taratibu hata marafiki zake Mzee Mnyoka walianza kumteta,

Hata hivyo yeye aliendelea na maisha yake huku akitafuta namna ya kutoka kwenye jinamizi la kuzuiwa kuuza mazao yake,

"Hawataniweza"

Mzee Mnyoka Sasa alijisemea akitabasamu, Kuna Jambo lilimjia kichwani,

***********

"Yeah ni kweli niliibadilisha aisee, nilikua nakunywa juisi kwa bahati mbaya, ilimwagika kidogo juu ya Ile bahasha ya mwanzo, sikuona Kama Ni busara Sana kuleta bahasha yenye maji maji Ndio nikaona niibadilishe, hata hivyo si Ni karatasi tu za kawaida Mzee baba? "

Oscar alimjibu Ima,


Huku akionyesha kutokua na wasi wasi,

"Ndio ujifunze Sasa kuwa makini, mjomba"
Alisema Ima huku akiendelea na kazi zake,

Oscar alitoka Kisha akaingia kwenye Gari, alienda mbele kidogo Kisha akapaki pembeni kidogo ya njia na kutoa simu yake,


"Hey hebu angalia Kuna kitu nakutumia uniambie kinahusu Nini "

Oscar aliongea baada ya simu yake kupokolewa


"Sawa bosi"
Ilisikika upande wa pili,

Oscar alitoka nje akijifanya kuangalia angalia Gari lake Kama Kuna hitilafu hivi lakini lengo lilikua Ni kupoteza maboya Kama Kuna mtu alikua akimfuatilia, lakini kwa uhalisia alikua anasubiri simu ya kupewa maelezo kuhusu nyaraka alizotuma,

Baada ya dakika kumi hivi simu yake iliita,

Aliitazama mpigaji na Mara moja akaweza sikioni na kuingia ndani ya Gari,

"Hizo Ni taarifa za mgodi wa UreFact za mwezi wa 5, mwaka huu,

Zinaenda kwa CEO wa iyo kampuni Mr Johnson Zagris Ping, wa uingereza,

Ni Kama kiambata Ina maana Kuna barua nyingine ambayo imeandikwa kwa juu yake"

Alimalizia upande wa pili,

"Sawa endelea kuangalia hizo items Kama zinahusiana na nini, halafu baadae nitakua ukumbi wa Julius Nyerere mlimani city utaniletea maelezo

Maana simu hii haitapatikana "

Oscar alimalizia Kisha akatoa line yake na kuiweka sehemu anayojua yeye,

Kisha akawasha Gari na kuondoka..


***********

Jioni Ile Oscar alikua amemsindikiza Tito pale mlimani kwenye ukumbi wa JK Nyerere,

Tito alikua Ndio mzungumzaji Mkuu katika huku akitarajiwa kuulizwa maswali na wanafunzi wa chuo kikuu mada ilikua Ni namna gani wananchi wananufaika na rasilimali za nchi hususani madini na gesi,


"Serikali inafanya jitihada kubwa, katika kuhakikisha kila mmoja ananufaika na rasilimali hizi, majengo mnayoyaona, vifaa mnavyoviona sehemu mbali mbali, vyote Ni faida ya rasilimali zetu, mbali na kodi chanzo kingine kikuu Cha mapato Ni madini na gesi zinazopatikana nchini,"
Tito alikua anatoa hotuba yake , Kisha akaendelea na kumaliza kwa dakika 15 Kisha akaruhusu maswali,

Wanafunzi waliuliza maswali mengi lakini mwishowe mwanafunzi mmoja akasimama na kuuliza swali

"Mheshimiwa Kuna madai kuwa baadhi ya viongozi ikiwemo wewe mnashirikiana na wageni, katika kutorosha Mali za nchi nje, kwa maslahi Binafsi, na zaidi Sana serikali inakosa mapato yaliyokusudiwa , Hili unalizungumziaje?"
Mwanafunzi huyo aliuliza huku akipigiwa makofi na wenzake,


Tito hakutegemea swali Hili sura yake ilibadilika, moja kwa moja alijua Kuna maadui zake "wasiomtakia mema" Ndio wamepanga watu wa kuuliza maswali ya kumkomoa, hasa ikizingatiwa mkutano ule ulirushwa mubashara,

"Kwanza ufahamike viongozi wote sio Tito pekee yake, kila kiongozi anatakiwa afanye majukumu yake kwa mujibu wa kanuni na taratibu za nchi, "

Tito alijibu swali huku akionyesha kukereka,

Baada ya mkutano wakiwa Kwenye Gari sasa Tito alishindwa kuzuia hasira zake,


"Wamemtuma yule dogo kunichafulia najua wanataka hii nafasi Sasa ngoja niwatumie salamu"

Tito alisema na bila kujali Kama Oscar anasikia ama la alitoa simu yake na kubonyeza namba kadhaa,

"Yule ngedere aliyetumwa kuuliza swali la kijinga mmalize usiku huu huu ili wapate salamu"

Aliongea Tito Huku aking'ata meno yake kwa hasira,


Sasa Oscar alijisikia Kama Yuko ndotoni!


Hakika hakuamini masikio yake,

*******************************************

Mzee Mnyoka alikumbuka Jambo fulani hivi ,

Aliingia Sasa chumbani kwake,

"Pengine hawa jamaa wanahisi Mimi nitaogopa kujieleza Sasa ngoja,"

Mzee Mnyoka aliingia ndani kwake Kisha akavaa miwani yake na kuanza kujibu Ile hati ya mashtaka,


Aliandika hoja nyingi huku akimalizia na maswali

"Mahakama ilichunguza na kuona Sina hatia, je kwa Sasa mmepata ushahidi wa kunitia hatiani?

_je wakati naiba huyo ng'ombe Nani alishuhudia?

Huyo ng'ombe nilimpeleka wapi baada ya kumuiba?


Sasa naomba Sana kesi hii itolewe maaumuzi mapema, na pia muweze kutoa ushahidi wa Mimi kufanya huo wizi,"

Mzee Mnyoka alimalizia hoja zake na kupeleka kwenye ofisi ya kijiji
Siku ile Ile,


Mtendaji alisoma hoja za Mzee Mnyoka Kisha akamwambia aondoke huku akimsindikiza na maneno,

"Mzee Mnyoka unajifanya mjuaji Sana wewe, Ila hapa umefika, kumbuka ofisi hii haingiliwi katika maamuzi yake"

Mzee Mnyoka Hakujali aliondoka zake..


*********

Oscar alijifanya kuunga mkono hoja,

"Yeah yule dogo katumwa Ni vizuri kumshughulikia kweli," Oscar alisema

"Yeah vijana wa siku hizi akipewa elfu tano tu amtukane kiongozi tayari anafanya tu bila kufikiria madhara yake"

Tito alisema,

"Huyo jamaa uliyemtuma anaweza kazi lakini?"

Oscar akijaribu kumuuliza Tito

"Ah Pablo, Ni mzoefu Sana ameshafanya task Kama hizi Mara nyingi tu, unajua Oscar Dunia ya Sasa huwezi kukaa kwenye hizi nafasi zetu ukiwa "msafi" milele,

Usione wote hao unaona wanashine sio hivi hivi"

Tito aliongea kuhalalisha "ujahili" wake,

"Yeah wanasema siasa Ni mchezo mchafu"

Oscar aliongea Sasa na kila mmoja akakaa kimya,


Oscar alikua anataka kumuokoa yule dogo bila kustukiwa na Tito
Na hivyo alipanga tu akifika nyumbani ageuze chap kurudi chuoni Udsm,

********

Kijana swalehe Sasa alikua amezunguukwa na vijana wenzake wakijazana "upepo"

Kuhusu Hali ya siasa nchini,
"Dah mwanangu umeua , umemtia Jamba Jamba waziri, we Noma!"
Sasa yule kijana aligeuka maarufu ghafla jioni Ile,


Karibu na chuo kikuu mlimani Kuna stendi ya mabasi maarufu kwa jina la simu 2000 ama wenyewe walipenda kuita mawasiliano,

Ndani ya tax moja "Pablo" akiwa na mwenzake mmoja walikua tayari wanasubiri saa 12 ifike ambapo wanafunzi wengi walikua wakirudi maeneo ya chuo,

Tayari Pablo alikua na sura halisi ya "swalehe Issa" mwanafunzi wa mwaka wa pili ambaye alijizolea umaarufu ghafla kwa "kumgonga" waziri swali la kibabe,

Pablo alishapewa maelezo na bosi wake namna ya kummaliza bila kuacha alama zozote,

"Ila Tito nae, kwanini tumuue dogo kwa kesi ya kiboya Kama hii"

Aliongea Sasa mwenzake na Pablo huku akiendelea kuangalia Tena Ile video ya swalehe ,

"Ah sisi tunaangalia hela Bob"
Alisema Pablo huku akizima kipisi Cha bangi alichokua anavuta,

Waliongea Kisha wakavaa mavazi yao walioandaa Kisha wakasogea maeneo ya chuo,

Walishuka na kusogelea baadhi ya wanafunzi waliokua wanaingia getini,


"Aisee sisi tunatoka Pilika Online TV tulikua tunahitaji kufanya mahojiano na Swalehe Issa"
Pablo alisema huku akijifanya kuandaa camera yake na maiki,

"Aisee hapa hayupo Ila ngoja nimcheki rafiki yangu mmoja anasoma nae course moja anaweza kujua alipo"
Alisema mwanafunzi mmoja huku akibonyeza simu yake,

"Oi Mpigie Kipanya mwambie ana wageni wake kutoka Pilika Online TV hapa getini"
Aliongea yule mwanafunzi ,

"Oya anakuja, kumbe yupo nae Room"


Baada ya dakika 7 hivi swalehe au wenzake walipenda kumuita Kipanya alitokea akiwa na rafiki yake Mazinge,

Walisalimiana Kisha Pablo Sasa akatoa muelekeo

"Aisee sisi Ni Pilika Online TV, tuna deal Sana na masuala ya walimu na wanafunzi tumependa Sana jinsi ulivyowasilisha hoja zako, na tumeona tufanye na wewe mahojiano mafupi, lakini Kama hutajali tulitaka tufanyie ofisini kwetu sio mbali sana na hapa, Ni nyuma tu ya ubungo hapo ,kabla hujafika kwenye stendi ya mkoa"

"Ah Hakuna shida kabisa, twendeni"
Alisema Swalehe kwa furaha,

Hakutegemea Kama ipo siku angeweza kuhojiwa na mwandishi wa habari hakika alijiona mwenye bahati Sana,

Ni wakati anaingia kwenye Gari la akina Pablo Sasa alihisi harufu Kali ya bangi, wakati anataka kuongea ghafla akafunikwa na kitambaa puani, na katika kujitetea akahisi anakosa nguvu na kulegea Kisha akapoteza fahamu.....
 
KESI YA MZEE MNYOKA 22
Mnyoka Sasa alirudi nyumbani huku akiamini ule utetezi wake kidogo ungesaidia kuwatia Hamasa viongozi ya kuweza kumpa haki yake, kutokana na Hali ngumu ya maisha Mzee Mnyoka Sasa aliamua kuuza baadhi ya vitu vyake pale Ndani ili apate hela ya kujikimu, aliuza baskeli yake Phoenix kwa shilingi elfu 75,

Alimpa mkewe mama Monica elfu 35 na nyingine akabaki nazo,


Mzee Mnyoka Sasa aliacha kabisa kwenda kanisani hata Ile siku moja kwa mwezi, hakuona umuhimu Tena wa kukutana na Padri John,


Mtoto wake James nae aliamua kumsaidia baba yake kwa kufanya vibarua pale mgodini, James Sasa aliweza kurudi na shilingi elfu 15 au 10 kila siku, ambapo alimpa mama yake ahifadhi,

Mzee Mnyoka hakupenda mwanae afanye kazi pale Mgodini, lakini Sasa hakuwa na namna yoyote Ile,


Alijisikia vibaya kuona badala mwanae angekuwa twisheni huko , Sasa yupo na wavuta bangi, na majambazi pale mgodini,...



Hakuwa na namna zaidi ya kumsisitiza tu kuwa Makini,


"Mambo haya yataisha tu,"

Mzee Mnyoka alikua akimwambia mwanae


************

Oscar yeye aliwahi mapema kabisa akajichanganya na wanafunzi pale getini, alijua kuwa lazima Kuna watu watakuja kumchukua Swalehe hivyo alikua makini kutazama mtu ambaye angetoka na Swalehe,


Wakati Pablo na mwenzake wanaingia,


Huku wamevaa vizibao vya Pilika Online TV, Oscar aliwapiga jicho,

Kama mpelelezi mzoefu alihisi Jambo kwenye muonekano wa Pablo, jinsi alivyoongea na jinsi alivyokua Oscar alikataa kuwa huyu Ni mwandishi tu,


Na wakati Pablo anainama kutoa vifaa vyake kwenye begi, ndipo Oscar alifanikiwa kuona bastola kiunoni mwa Pablo,

"Kumbe Ndio wewe!"

Oscar alijisemea Sasa akirudi nyuma Hadi kwenye piki piki yake, aliyokuja nayo,


Alishajua hawawezi kufanya tukio pale, Ni kweli baada ya muda Pablo alitoka na mtu wake kazi ikawa ndogo tu kwa Oscar kuwafuatilia,


Gari haikuelekea ubungo badala yake walinyoosha Kama wanaelekea mwenge, na ilipofika barabara ya shekilango wakasimama kwenye mataa,

Oscar alikua karibu nao kabisa, na kutokana na msongamano jioni idadi ya piki piki na magari ilikua kubwa hivyo Pablo asingeweza kufikiri kufuatiliwa ,

Gari iliendelea ilipofika sinza madukani, wakachukua barabara ya Uzuri
Halafu walipofika kwamtogole Gari wakaingia kulia,

Mwendo wa dakika 6 hivi wakatokea kwenye nyumba moja, Oscar akajifanya kuwapita kidogo Kisha akasimama kwa mbali kidogo, ilishakua saa moja na dakika kadhaa na giza lilikuwepo kwenye sehemu ambazo Hakuna taa, Oscar alijibanza na Kunyata pole pole, hakukua na geti , Oscar alinyata tu kuelekea kwenye Ile nyumba Kisha akatega sikio,

"Ngoja nimpigie, kuwa tushampata dogo"

Alisema Pablo.
"Ndio tunae hapa tunakusikiliza,

Ehh,
Ndio,

Sawa"

Pablo alikua anaongea na Tito,


"Anasema tumalize kazi halafu tuhakikishe Hakuna anayegundua , "


Pablo alimwambia mwezake,

Sasa sikia tunamaliza kazi halafu tutajua pa kumuweka,



Ni wakati huo Sasa Oscar alishusha Kofia yake inayofunika uso Kisha akafungua mlango pole pole,
Kwa kasi ya ajabu aliwatokea na hakuwapa muda wa kutafakari aliachia risasi mbili na sekunde kadhaa Pablo na mwenzake wakawa maiti pale pale,


Sasa alijaribu kumuamsha Swalehe lakini bado alikua amepoteza fahamu, alimbeba na kutoka nae nje begani Kisha akakumbuka kumsachi, alitoa simu yake na bahati mbaya ilikua na nywilla, hivyo akatoa line moja na kuweka kwenye simu yake Kisha akajaribu kukadiria namba moja wapo ya mtu wa karibu Ni wakati anajaribu kupiga Mara simu ikaita,

"Oya Kipanya vipi mbona hurudi Mwana? Si unajua tuna assignment kesho..."

Oscar alimkatisha,


"Sikiliza njooni hapa kwa mtogole mwenye simu Yuko hapa amezimia, njooni mtakuta karibu na mnara hapa kushoto nje ya nyumba,



Yeah, ukishuka sinza madukani unachukua uzuri road, kwamtogole unaingia barabara ya kulia Kama mita 200 hivi kwenye mnara wa simu kushoto Kuna nyumba ya vigae haina geti hapo nje mtamkuta"

Oscar alirudi kwenye piki piki yake akasubiri baada ya nusu saa Sasa zilizifika piki piki zaidi ya 4 wakamchukua Swalehe,.




Kesho yake Tito alimuita Oscar


"Yule dogo ameshindikana, Pablo na mwenzake wamekutwa wameuwawa na dogo Yuko hospitali, Sasa sijajua kitu gani kimetokea Ila Sasa nakupa kazi hiyo wewe,
Kammalize huyo mpuuzi pengine akawa amejua kitu fulani "


Alisema Tito


"Yuko hospitali gani kwani"

Oscar alimuuliza Tito

"Sijajua bado lakini tutajua muda si mrefu, shida ni kuwa tayari wanasiasa wameshalichukulia Hili suala tayari, hebu ona,"
Tito aliongea akimkabidhi "tablet" yake aangalie video

"Sisi Kama upinzani tutasimama na Swalehe, tunajua wapo viongozi hawataki kukosolewa, Sasa Bwana mdogo aliuliza swali dogo tu lile tayari wanataka kumuua, tayari nishaongea na Kamanda wa mkoa atoe majibu kuhusu jaribio Hili la mauaji ya mwanafunzi"

Alisema Mheshimiwa Farida, mbunge wa Kawe, wa chama Cha upinzani, huku akiwa amezunguukwa na wanahabari

"Duh Sasa hapa Mzee itakua ngumu kidogo kwa siku hizi maana chochote kibaya kikimtokea dogo itaonekana Kuna mkono wa mtu hebu tufikirie njia nzuri zaidi"

Alisema Oscar akimrudishia simu yake,

"Ngoja nimpigie kamanda Niongee nae"

Alisema Tito Kisha akabonyeza simu yake Tena,

Aliongea kwa dakika tano Kisha akatabasamu,

"Imeisha hii twende zetu Oscar"

Alisema Tito huku wakielekea kwenye Gari

Simu ya Oscar ilitikisika kidogo kuashiria ujumbe mfupi umeingia,

"Leo ni uingereza vs Panama mechi ya kirafiki usikose mechi hii kwenye screen kubwa pale kinondoni Pub saa 1 usiku "

Oscar aliangalia namba iliyotuma iyo sms Kisha akatabasamu!

***********
Iliundwa kamati ndogo ya watu watatu kuchunguza kesi ya Mzee Mnyoka,


Walifika nyumbani kwake asubuh na mapema, walianza kumhoji mkewe Kisha wakahoji na majirani kuhusu tabia na mwenendo wa Mzee Mnyoka, Kisha wakamaliza na Mzee Mnyoka mwenyewe,

"Kiukweli sisi hatujui Kama uliiba au la , sisi tunachuguza tu kujua ukweli, Kisha tutapeleka taarifa yetu kwenye Ofisi ya Kijiji, usijali Mzee Mnyoka kamati itatenda haki, Kama hukuiba Basi usiwe na wasi wasi, Ila tu uelewe itachukua muda sana"

Alisema mwenyekiti wa kamati,

Mzee Mnyoka Sasa aliona huu Ni "uzwazwa" kusubiri kesi isiyo na macho Wala masikio halafu imsubirishe huku watoto wake wakishindwa kwenda shule!

Aliamua Sasa liwalo na liwe aliingia chumbani kwake na kujifungia Kisha akatoa simu yake Ile aliyokua ameificha Kisha akapiga namba fulani aliyoelekezwa,

Namba haikupatikana,

Ni wakati anataka kuirudisha ndipo ikaita,

"Mzee Mnyoka Kuna jipya? "

Ilisikika sauti ya upande wa pili,

Mzee Mnyoka alitambua sauti ya Oscar alimueleza kwa ufupi kuhusu zuio la kuuza kahawa yake kwa kesi ambayo alikua hahusiki nayo

"Nitajie majina ya hao viongozi wa Kijiji"

Alisema Oscar ,
Mzee Mnyoka alimtajia
"Okay Sasa Mzee Niko bize kidogo hawa wote watahusika baadae kwasasa kwa ajili ya mahitaji yako na watoto wako kwenda shule, tutafanya namna, nakushauri jifanye mjinga wasikilize wanachokuambia ili tusiwakurupushe kwa ajili ya Ile inshu yetu, niamini Mzee serikali inatambua mchango wako, sema lazima Kuna Mambo ya kiitifaki yanachelewesha , kesho kutwa utapata msaada wa Pesa unaohitaji

Alisema Oscar Kisha akakata simu,


Mzee Mnyoka aliirudishia sehemu yake Kisha akatoka kwa bahati mkewe hakuwepo,

********
Oscar Sasa alikua amemaliza kuongea na Mzee Mnyoka Kisha akapiga simu mahali fulani huku akitaja jina la Mzee Mnyoka na Kijiji alicho na baadhi ya vitu Kisha akaingia kwenye Gari kwenda Kinondoni Pub,


Alifika Kama saa moja kasoro hivi Kisha akatafuta kiti na kukaa,

Ni baada ya dakika tano alikuja machinga akiwa anauza mikanda ya suruali, na viatu vya kiume, Alikua akipita meza moja baada ya nyingine mpaka alipokua Oscar ,

Alitoa Ile mikanda na viatu na Kisha akatoa kiatu kimoja kumpa Oscar ajaribishe,


Oscar alichukua kile kiatu na kukitazama,.
"Nipe mwenzake"

Alisema Kisha akapewa mwenzake

Na akapeana mkono na yule "muuzaji"

"Asante broo"

"Boya wewe, muone Sasa"

Alijibu Oscar,

Kwani ndani ya viatu vile kulikua na ujumbe ambao Oscar alikua ameomba aletewe kuhusu zile nyaraka alizokua ameiba kwa Tito

Na huyu machinga hakuwa mwingine Bali alikua Ni rafiki yake George..
 
KESI YA MZEE MNYOKA 20
"Oscar Kama ujuavyo kutokana na kazi zetu hizi tunakumbana na ghiliba nyingi, lakini kwakweli Jana umenifurahisha Sana, na zaidi ya yote ulinisaidia Sana, kwakweli, hata hivyo nikaona ili kutoa shukran zangu kwako nimeona nikupe kazi! Sijui unalionaje Hilo?"

Tito Sasa aliongea kwa hamasa!

"Kwakweli Mzee itapendeza Sana, lakini Sasa mpaka nijue kazi yenyewe maana unajua Mzee Mimi Elimu yangu Ni ya kidato cha nne tu, na sikua na matokeo mazuri Sana, "

Oscar alisema,

"Hata usijali, maisha Ni zaidi ya kusoma Oscar, wangapi Wana PhD zao lakini wako mtaani tuu, usiogope,

Unajua sisi mawaziri tuna kazi nyingi, Kuna mahali naweza kuhitajika wakati mwingine hata kufuata hata nyaraka tu! Sasa nikiwa na mtu Kama wewe unaweza kunisaidia zile kazi ndogo ndogo Kama hizo, kwa maana fupi nataka uwe msaidizi, wangu"

Tito alisema

"Na itakuwaje yaani utaratibu mzima wa kazi"
Oscar aliongea Sasa,


"Kazi kubwa Ni kuzunguuka na Mimi utakuwa Kama mlinzi wangu wa pili Ila Sasa wewe utakua unaniwakilisha kwenye zile shughuli zangu za nje ya ofisi, mfano Nina mashamba yangu kule kiluvya, Nina Ranchi moja kule mlandizi n.k, Sasa Mimi siwezi kufuatilia kila kitu kwahiyo wakati mwingine nitakua nakutuma wewe tu na mambo mengine tutazidi kuwasiliana, na sitakua nakulipa mshahara, Bali kila kazi utakayokua unafanya nitakulipa, na wakati mwingine utakua free na Mambo yako"

Tito aliongea

"Basi Hakuna shida Mzee, niseme kwamba Mimi nimekubali na tunaweza kuanza kazi!"

Alisema Oscar

************

Mzee Mnyoka aliwaza na kuwazua Sasa alikosa majibu,

Na hatimaye shule zilifungwa na mtoto wake James akarudi nyumbani kwa ajili ya likizo,

Mdogo wake Mary alimueleza kila kitu Kaka yake kuhusiana na kesi na "majanga" yote yaliyomkuta Mzee wao,


"Ndio Ni kweli tuko na Hali ngumu kwasasa Ila Mambo yatakaa sawa tu utarudi shule bila shida"

Mzee Mnyoka alikua akimtoa hofu mwanae, aliamini Kuna "namna" ya kuondokana na haya maseke seke,

Ingawa hakujua Ni kwa namna gani,


"Maisha hayawezi kusimama kwa ajili ya Jambo Hili"

Mzee Mnyoka aliwaza ,


*************


Baada ya wiki moja



Oscar Sasa alikua karibu na familia nzima ya Tito,

Na Kuna siku nyingine alichelewa Sana na "majukumu" yake akiwa na Tito hivyo alipewa sehemu ya kulala,


Kwa ufupi familia nzima ya Tito ilimuamini,


Siku hii ya leo, Oscar alipewa kazi ya kutuma baadhi ya taarifa kwa njia ya barua Pepe,

Zilikua Ni nyaraka mbili,

Oscar alizipeleka tu kwenye sehemu ya kutolea huduma za mtandao "internet cafe"

Ambapo alitakiwa tu kumuuliza Bwana ima,

Kisha angempa zile nyaraka,


Oscar aliamua kujiongeza na kununua bahasha nyingine ya kaki, Kama Ile Ile Kisha akachana na kusoma

"UreFact
The products may 2016"

Kilikua Ni kichwa Cha habari,

Oscar aliamua kuzipiga picha Kisha akaweka kwenye bahasha nyingine na Ile akaitupa mbali,


Alifika sinza kumekucha kisha akapaki Gari na kuingia kuelekea kwenye jengo moja lililokua na milango miwili ya vioo

"IMA INTERNET CAFE"

maandishi yalisomeka,


Baada ya salamu Oscar alimuuliza Kisha akampa Ile bahasha na kumnong'oneza

"Imetoka kwa Tito"

"Okay poa, naituma chap"

Alisema Ima Kisha akachukua Ile bahasha na kuingalia kidogo,

"Sikiliza jomba,

Hii bahasha sio, na usirudie Tena kufungua bahasha za watu"

Ima alimwambia Oscar kwa sauti ya chini

"Mhhh jamaa amejuaje? Na bahasha ziko sawa hizi?"

Oscar aliwaza huku akitafuta jibu la kumpa..
Ukimaliza uje nikupe true story uwafikishie watanzania maana uko vizuri katika uandishi ndugu .
 
Back
Top Bottom