Hadithi: My Soulmate

Hadithi: My Soulmate

My Soulmate Sehemu ya 17.
Produced by; Equator Special.
#############Tulipoishia ######################
Mandoto alikuwa hatoki nyumbani kwake mchana anatoka usiku tu kukwepa kuonekana na Afande Stanley. Usiku mmoja alikwenda bar usiku alivyo enda chooni alishtukia kuona Afande stanley akiwa nae ndani ya choo hicho. Alibaki akimtumbulia macho ha amini kama ni amebambwa kirahisi hivyo.
Afande Stanley : "Mimi ni mwindaji Mandoto huwezi nikimbia nikakuacha...".
**** Endelea *******************
Ni kwenye club moja ilio changamka sana mida ya saa nane usiku. Mandoto anaelekea kwenye uwani kwa ajili ya kujisaidia. Mara Afande Stanley anaingia ndani ya choo hicho.
Afande Stanley : "Mimi ni mwindaji Mandoto huwezi nikimbia nikakuacha...".
Mandoto : “Umenipataje?”. Aliuliza akiwa ana tumbua macho.
Mara ghafla kuna mkaka na mdada wali ingia kwenye choo hicho na wakipiga kelele za shangwe wakiwa na dalili zote za kulewa. Mandoto alipo ona nafasi hiyo alitoka anakimbia mpaka nje.Mandoto anakimbia huku kichwa kikiwa na pombe tayari kwahiyo ana yumba yumba wakati huo Afande anamfatilia taratibu.
Afande : “Wewe una lala na mke wangu wewe?”.
Mandoto : “Nisamehe kaka..”. Mandoto alisema huku akikimbia kwa yumba yumba na kizungu zungu kiki msumbuwa anatamani kukimbia sana lakini mwili hauwezi.
Afande : “Huwezi nikimbia.” Huku akimfuata Mandoto taratibu kama mtu anaewinda sungura alie umia mguu!.
Mandoto : “Nisamehe ndugu sisi sote bina damu.”
Afande : “Hapana wewe unajua ninavyompenda Sara mimi?”
Mandoto : “Kuwa mpole haya mambo ya kawaida!”
Afande : “Mambo ya kawaida ?”.
Mandoto : “Ndio mkuuu kuwa mpole.”
Afande : “Niwe mpole na mtu nlie mkuta analala na mwanamke wangu? Mwanamke anae nifanya nijitoe vingi kwa ajili yake?. We ulikua wapi wakati anaumwa na saratani miezi sita?”
Mandoto: “Kaka kuwa mpole.”
Waliendelea kuongea mpaka kutoka nje ya club hiyo . Mandoto bado ana hangaika kutembea lakin hawezi kwa sababu ya pombe.
Afande : “Unajua nina vyo mpenda? Sara umelala nae kwenye kitanda changu kama ndio nyumba yako unadhani nimekufa ama?”.
Wakati huo wanapigana mke wa afande alifika maeneo hayo alikua akimfwata mumewe nyuma nyuma bila ya mumewe kujua anafuatiliwa.
Mandoto alisamama akasema hapa ama zangu ama zako siwezi kubali uni aibishe kisa ya mwanamke ninaye mpenda alianza nakurusha ngumi kumuelekea afande Stanley. Wakati huo sara ali ingia ndani ya pub akijua mumewe alingia humo muda sio mrefu akiwa ana angaza angaza kumtafuta mumewe.
Afande Stanley : “Hahahah inaoneka umeamua tuyamalize kiume sio?”.
Afande alisema huku akirusha ngumi za tumbo mfululizo kwa Mandoto . Mandoto alimkuatia wakawa wana garagara chini wakirushiana makonde ya kila maeneo. Mara ghafla sauti ya bunduki kufyatuliwa ilisikika . Sara alikuwa nje wakati huo na aliona sauti ilipotokea alimwona mumewe na mandoto wakiwa wamelaliana hakuna aliekuwa akisogea.
Sara alipiga ukunga kwa uoga aka anza kutetemeka akamkimbilia eneo la tukio ili ajionee kilichotokea. Akiwa akizidi kusogea aliona eneo hilo likiwa limejaa damu alishindwa kuamini kile alichokiona mbele ya macho yake.
Sara alifika pale akausogeza mwili wa mumewe uliokuwa ukimlalia mandoto. Kutahamaki ni Mandoto alikuwa akilala pale akiwa marehemu kutokana na risasi aliopgwa kifuani alianza kulia kwa uchungu kipindi hicho mumewe akiwa haamini kilichotokea alikuwa akitoa macho tu alipo rudi kwenye fahamu zake alimshika mkono wake aka anza kumburuta waondoke.
Sara : “Niache we muuwaji niache mimi.”.Alisema akiwa anahangaika kutoka kwenye mikono ya mumewe.
Afande : “Twende huku wewe na wewe nitakumalizia.”. Alisema akimburuza alipo ona haondoki almnyanyua na kumuweka begani na kutokomea nae pasipo julikana na mtu mmoja mmoja akianza kufika kwenye eneo la tukio.Ma askari hawakukawia kufika baada ya wasamaria kupiga simu polisi.
Mandoto alichukuliwa na gari ya hospitalini na kuwahishwa hospitalini kama jitahada za kuokoa maisha yake.
Rose dada yake na Mandoto alikuwa amelala wakati huo aliamshwa na simu kutoka hospitali akiombwa afike kwa ajili ya kumwona kaka yake aliekuwa amevamiwa . Wakati huo hakuna aliejuwa ukweli nini kilichotokea. Rose alipofika alijitambulisha akasema yeye ni nani.
Docta : “Rose nina habari mbaya kaka yako amekutwa akiwa amepigwa risasi ya kifuani na sidhani kama ni majambazi maana alikutwa na wallet yake na kila kitu.”
Rose : “Unaongea nini? Kaka yangu mimi hapa. Yuko wapi.” Rose aliongea akiwa anatoa macho bila kuamini amini anachosikia.
Docta : “Tafadhali kuwa mpole rose.”.Docta alisema kwa njia ya kiustarabu.
Rose : “Sio niwe mpollllee kaka yangu yukowapiiii….??”Rose alitoa sauti kali na kwa uwoga.
Docta : “Bahati mbaya tumejaribu kumuokoa lakini imeshindikana.”Docta aliendelea kuongea kwa huruma na upole.
Rose : “Una maaana gani imeshindikana nataka kumwona kaka yangu.”Rose alisema kwa sauti akianza kutoa machozi.
Docta : “Nataka uniahidi kuwa utakuwa mpole nikakuoneshe kaka yako.”Docta alisema kwa upole aki inuka tayari kwa ajili ya kuanza safari ya kwenda kumuona Bwana mandoto.
Rose : “Sawa.”Rose wakati huu alishindwa hata kutoa sauti.
Rose alifuatana mpaka mochwari na dactari pamoja na mfanya kazi wa mochuari. Docta alimwomba afungue kabati namba nne . Droo ilifunguliwa na mfuko wa kufunukia ulifunuliwa .
Rose : “Kakaaaa kaka jamani umeniacha kaka …”.Rose aliangua kilio baada ya kuona mwili katika droo hiyo ni kaka yake kweli aliona kama ndoto moja inayo tisha na kutesa sana alilia kwa uchungu ambao hata hauwezi kuandikika.
Upande mwingine Nickson akiwa anajiandaa kwenda kwenye mizunguko yake alikuwa pia ana sikiliza habari za asubuhi hakuamini alichokiona alimfuata Bertha moja kwa moja akamlazimisha aamke kabla ya taarifa hizo kuisha Bertha alipo ona hivyo hakuamini kuwa anaona kifo cha mumewe.
Bertha : “Mume wanguu jamani mume wangu jamani umeniacha nitabaki na nani mimi.”.Bertha alilia visivyo mfano aki mkumbatia Nickson aliekuwa akimpa matumaini kuwa yote ni maisha na ni mpango wa Mungu .Bertha hakuamini kuwa amampoteza mumewe tena aliekufa kikatili pamoja na kuwa alikuwa ni mkatili sana kwa bertha bado alimpenda hivyo hivyo .
Bertha aliamua kwenda alipo tokea kwa ajili ya kumzika aliekuwa mumewe.
Itaendelea…..
shukran kiongozi,tuendelee japo viwili basi
 
My Soulmate Sehemu ya 18.
Produced by: Equator Special.
Bertha amerudi alipokuwa anaisha na mumewe akakuta kweli kuna mazingira ya msiba hakuamini alianza kulia upya.
Alijikaza akaingia mpaka ndani akawa kuta ndugu zake na Mandoto wakiwa wanajadili alipofika alijaribu kuongea nao.
Bertha : “Jamani poleni.”. Wote walikaa kimya wakijifanya hawamwoni Bertha wakati huo Rose alikuwa amemgeuza familia nzima kinyume na Bertha.
Rose : “Samahani tunaomba utuache tuna kikao cha familia.”.Bertha aligeuka nyuma akiangalia kama kuna mwingine anae ambiwa hayo maneno.
Bertha : “Mimi ama?”.Bertha aliuliza kudhibitisha alichokuwa anasikia.
Rose : “Unazani naongea na nani we una kichaa si ndio?”
Bertha : “Naenda wapi huyu si mume wangu jamani?”
Rose : “Enhee ulikuwa wapi muda wote huo?”
Bertha : “Tuligombana nika amua kuondoka.”
Rose : “FOfofofofofo .”Alisema huku akibana pua yake.
Bertha : “Jamani.”
Rose : “Weeeee unadhani hatujui ulienda huko arusha kufanya umalaya wako.”
Bertha : “Jamani rose hayo maneno umetoa wapi?”.
Rose : “Unadhani sijui kuwa kaka alipokuja alikukuta ukifanya umalaya? Alikukuta umetoka hotelini na bwana wako.”. Wakati huo Bertha alitaka kumvamia Rose lakini ndugu waliokuwa karibu walimzuia. Waka mshika kwa nguvu wakampeleka mpaka nje ya nyumba hiyo. Wakati huo wakimtoa Hamida rafiki kipenzi wa Bertha aitwae Hamida alikuwa na ndo anafika maeneo hayo.Alimuwahi rafiki yake na kumkumbatia.Lakini wakati huo wote Bertha alikuwa analia anashindwa kuongea.
Hamida : “Basi rafiki yangu yote maisha.”Hamida ali jaribu kumpa rafikiye moyo katika wakati huu mgumu.
Bertha : “Hamida huyo ni mume wangu jamani wana ninyima kushiriki hata wanasema mimi malaya ahh jamani..”.Bertha alisema kwa uchungu aki ishiwa hata na nguvu ya kusimama.
Hamida : “We Nelson si unisaidie huoni au?”.Hamida alisema hivyo akimuashiria mpenzi wake aliekuja nae kumsaidia kumshikilia Bertha maana hawezi ata kusimama.
Nelson : “Mshike upande huo. ”. Walisaidiana pale kumshikilia na kumuingiza ndani ya nyumba hiyo ya mumewe.Kuna waliomuona Bertha akirudishwa wakawafuata ili kuwa rudisha nje. Hamida alijua dhamira yao kabla hawajawafikia akawa nyooshea mkono aki wa ashirie wasi sogee.
Hamida : “Weeeee sogeeni muone kichaa changu!.”.Walipo ona hivyo walisimama na kuondoka wakampeleka Bertha akaenda kukaa ambapo wageni wengine wame ekewa kuketi kwenye uwanja wa nyumba hiyo.
Hamida : “Jamani pole shoga yangu jamani watu wana roho ya nyoka.”
Nelson : “Wewe acha hizo tupo kwa watu..”
Hamida : “Wacha wasikie mimi sijali.”
Nelson : “Mh haya!.”
Watatu hao waliendelea kukaa mpaka jioni wakati wa chakula watu wote waligawiiwa chakula kasoro hao wa tatu . Hamida alichukua sheria mkononi akazunguka nyuma ya nyuma ambapo wanapika na akapakua chakula akawaletea wote walikula kasoro Bertha aliekuwa katika majonzi kiasi cha kwamba kalia mpaka anashindwa kulia tena amebaki kinyonge.
Jinsi muda ulivyo kuwa una songa ndugu za marehemu Mandoto walikuwa wakipita kwenda kulia na kushoto lakini walikuwa wakimpita Bertha kama sio mkwe wao.
Bertha : “Hamida tuondoke.”
Hamida : “Haaa hubaki hapa?”
Bertha : “Hamida huoni kuwa wananitenga sasa nakaa hapa kufanyaje?”
Hamida : “Hawa ma mbwa hawa walivyo kuwa wanajifanya wanakupenda wakati unateska na mume wako kutafuta utajiri huu saivi wanajifanya hawakujui.”
Bertha : “Hamida we achana nao. Watakusikia!.”
Nelson : “Msikilize mwenzako usipayuke kwa watu jamani Hamida!.”
Hamida : “Wacha wanisikie hawa wanafiki wakubwa wananikera sana!”
Bertha : “Hamida basi imetosha.”
Hamida : “Kwanza huyu Rose ile siku haukumbonda vizuri. Alipo kuwaga anaumwa TB uli hangaika nae huku na huku kama yeye ni mzigo wako. Mende yule saivi anajifanya sana ungemwacha angekufa yule mtu mwenye afya goigoi…..”
Nelson : “We twende bhana ukianza kuongea huachagi. ”.Nelson alisema akimsukuma Hamida waondoke ama sivyo watakaa hapo muda mrefu na Bertha alishasema waondoke.
Bertha : “Twende shoga wangu hawa watu hawana maana .”Betha alijikaza akasimama macho yakiwa mekundu.
Hamida : “Haya sasa tunaenda wapi?”.
Betha : “Nimeacha vitu vyangu hotelini nilipo fikia.”
Hamida : “Nelson tumuache shoga yangu leo akalale kwetu. Analalaje hotelini wakati mimi hapa nipo?”
Nelson : “Sawa kabisa twende sasa!.”
Hamida : “Haya twende tupitie vitu vyako tukalale kwetu hawa ma ng`ombe Mungu atawalipa.”
Bertha : “Sawa!”.Bertha wakati wanaondoka aliona bustani ambayo walikuwaga wana cheza na mumewe marehemu aka anza kuangusha machozi tena.
Walitoka hapo waka fika kwenye hotel vitu vya Bertha vilipokuwa waka vibeba na kuelekea nyumbani kwa Nelson na Hamida . Wakala na wakalala Bertha hakuwa na hamu ya kula lakini rafiki yake alimlazimishia kula alikua kama robo sahani aka shindwa kuendelea.
Ilipo fika kesho yake Bertha aligoma kwenda kule kwenye msiba asije korofishana na wakwe zake. Alimwomba Hamida akafuatilie ni lini mazishi ili ahudhurie kwenye mazishi japo hapo atakuwa ameshiriki. Hamida alienda aka pata taarifa kuwa Mandoto atazikwa kesho ya siku hiyo alimweleza Bertha.
Siku ya mazishi iliwadia Hamida ni mtu wa watu alipo wambia marafiki zake kuwa ni mazishi ya shemeji yake hawakubisha kumsindikiza kwenye msiba Huo.
Bertha alifika asubuhi na mapema walijaribu kumfukuza lakini Hamida alisimama kidete kumtetea waka mwacha.Mazishi yaliendelea na ulipofika muda wa kufukia udongo hawakutaja kuhusu swala la mke wa madoto ambaye ndie Bertha hawakutaja.Muda wa mazishi ulifika wakati wa kuweka udongo ndugu jamaa na marafiki wa Mandoto walitajwa kasoro mke wake hakuitwa kueka udongo aliweka kama watu wengine wa kawaida. Hiki kipindi kilikuwa kigumu sana kwa Bertha asijue cha kufanya isingekuwa ya rafiki yake kusimama na yeye walau hata nafasi ya kuwepo msibani ingekuwa ngumu lakini mumewe ali fariki ndoa ikiwa matatani alikimbia kuokoa maisha yake alikuwa anaishi kuzimu ya duniani.
Mazishi yalifanyika salama watu walitawanyika Bertha alibaki nyuma kwenye kaburi la mumewe kwa ajili ya kumuaga. Ndugu za Rose walikaa ndani wakiwa wanakunywa pombe kana kwamba hakukua na mazishi . Walipanga kugawa mirathi ya bwana Mandoto baada ya wiki moja . Bertha aliondoka sehemu hiyo na kurudi alipokuwa na Hamida.
Ilipofika siku ya kugawa mirathi hiyo Betha alienda kwa ajili ya kuhudhuria kikao cha kugawa mirathi alipo fika alishangaa kukuta askari migambo wa tatu mlangoni kitu ambacho sio kawaida.
Mgambo : “Samahani dada unaelekea wapi?”
Bertha : “Mimi ni mke halali wa Mandoto nadhani labda hunifahamu.”
Hamida : “Kwani hamumfahamu mkuu wenu?”
Mgambo : “Samahani dada tume pewa agizo la kuzuia mtu asi ingie humu ndani bila ruhusa.”
Hamida : “Makuubwa!.”
Bertha : “Umeambiwa na nani?”
Mgambo : “Wakuu waliopo humo ndani. ”
Bertha : “Basi naomba kuongea nao labda watanielewa.”
Mgambo : “Wamepiga simu dada wamesema mtu yeyote asi ingie!”
Bertha : “Basi naomba zao niwapigie niwa ambie mimi ni nani!.”
Mgambo : “Namba zao nimepoteza.”
Hamida : “We kaka ni mjinga eeeh?. Hauna akili unasema umepigiwa afu hauna namba unaongea na mashetani ama?”
Mgambo : “Mdada naomba tuheshimiane mimi nipo kwenye kazi yangu tafadhali usilete madharau na kazi yangu. “
Hamida alimshika mkono Bertha akasema “Twende na watuguse watuone”. Hamida alianza ku angaika kupenya katikati ya wana migambo hao bila mafanikio.
Hamida : “Niacheni niacheni nyie.” Hamida alipiga kelele kwa sauti huku walinzi wakiwa wana pambana kumzia asi ingie.
Hamida : “Afu unanishika wapi huko?”.Hamida alianza ku gombana na mgambo waliokuwa waki mzuia asi ingie alijikuta akimshika hamida kifuani. Hamida alirusha kibao mara ugomvi ukawa una kolea zaidi .
Rose aliposikia sauti za kelele walitoka na kukuta kukiwa na mparangano wa ugomvi.
Rose : “Watoeni hao malaya waambie wame sababisha kifo cha kaka yangu wanakuja kuchukua mali gani kwa mfano?“.Rose alisimama kwa mbali akiwa anasema maneno hayo. Akiwa mbali wagambo hao hatimae waliweza kuwatoa nje . Waka bamiza mlango .
Bertha alikaa chini aka anza kulia aka sema “kama ni mali nita pata upya kama nilivyo pata hizi na mume wangu”. Alijisemea hivyo huku akisimama na kujifuta machozi.
Bertha alikaa kwa rafiki yake kwa takribani wiki mbili aka amua kufunga safari na kurudi arusha . Angalau kule kuna Nickson ambae ana mpenda kama ndugu japokuwa ni marafiki tu. Bertha aliwaza akasema angekua na Nickson kama mume angekuwa na faraja sana! . Alipo mkumbuka Nickson alitabasamu mwenyewe kwenye basi kama kichaa.
Itaendelea ……………….
 
Safiiii
 
My Soulmate Sehemu ya 19

Produced by : Equatorstory Specials.

Ni mida ya saa mbili asubuhi Bertha alikuwa kwenye gari tayari la kuelekea Arusha . Katika mawazo yake alimkumbuka Nickson akasema sio vibaya nimpigie.

Bertha : “Hallo”.

Nickson : “Habari bertha za kupotea?”

Bertha : “Nimepotea wapi? Mimi nipo wewe ndo upo kimya!.”

Nickson : “Karibu kila siku nakutafauta haupokei simu.”

Bertha : “Samahani jamani ni mambo ya mazishi yaliniyumbisha.”

Nickson : “Poleni na msiba vipi mumezika salama?”

Bertha : “Ndiyo tulizika juma lililopita saivi nakuja huko!.”

Nickson : “Karibu sana Arusha kwa wa janja wan chi hii.”

Bertha : “Hahahaaaa usha anza.”.Bertha aliachia tabasamu la nguvu akiyumbisha yumbisha shingo yake.

Nickson : “Kwani sisi sio wajanja?”

Bertha : “Mh labda…’

Nickson : “We jifanye mjanja. Lakini jua sisi pia ni watanashati mbaya mbovu!.”

Berta : “Hilo sikatai mwaya .”Bertha aliendelea kuongeza tabasamu.

Nickson : “Jamani ufike salama.baadae tutaongea!.”

Bertha : “Sawa utaki zawadi?”

Nickson : “Nataka chochote zawadi kubwa nikuone wewe!”.

Bertha : “Haya kwaheri mwaya.”

Nickson alikata simu na aka endelea kujiandaa kwenda chuo ambapo alipeleka pendekezo lake la mfumo anaona mda umepita sana!.

Nickson bila kujua hiyo ndio ilikua siku ambayo Sambeke na rafiki yake Eric alie msaliti. Nickson ali maliza kujiandaa akafika chuoni alipofika alimkuta yule secretary Rita.

Nickson : “Habari za asubuhi?”. Rita hakuitikia Nickson akarudia “Dada za asubuhi?”.

Rita : “Salama shida yako?”.Rita aliuliza kwa madharau.

Nickson : “Mh leo una shida gani?. Lakini isiwe tabu nimekuja kufuatilia ule mradi niliopendekeza.”

Rita : “Kaka kwani hujapata taarifa tumepata mtu mwingine aliesema huo mradi wako umeibiwa ”.

Nickson : “Hahahah yani umeibiwaje? Mimi mbona ninao?”.

Rita : “Naomba usinichekee huo mradi ni wazo la mtu mwingine wewe ndo ume iba!”

Nickson : “Unasemaje? Nimeiba kwa nani?”.

Rita : “Acha kujifanya hujui!”.

Nickson : “We dada kuwa siriazi jamani ”.

Rita : “Mi nimeanza matani na wewe?”.

Nickson : “Ah bhana we unani changanya ngoja nimsubirie mkuu wa chuo labda huyo nita elewana nae!”.

Rita : “Ungejua ndo yupo humo anaongea na hiyo kampuni ambao uliwa ibia hilo wazo.”

Nickson: “Wako wapi?’

Rita :”Wapo kule kwenye bwalo la chakula ndo wanaonyesha huo mradi kwa wanafunzi!.”

Nickson : “Acha kunitania basi.”

Rita : “We kaka acha kuni sumbua mi sio mtani wako si uende kule ukaone?”

Nickson : “Sawa ngoja niende.”

Nickson alianza ku changanyikiwa asielewe kinachotokea mbele ya macho yake. Alijikaza na aka anza kelekea kwenye bwalo hilo. Alikuta kuna wanafunzi wengi wakiwa kwenye mkutano huo alijipenyeza mpaka kufika karibu na mbele . Ali shangaa kuona Eric ndo ana fanya maonesho ya mfumo huo na isitoshe ulikuwa unafanana kama walio kuwa waki tengeneza ha amini macho Eric kamsaliti.

Ali baki kasimama na macho yaki mtirirka kama maji kichwa kiki anza kumu uma . Akijiuliza kweli eric kamsaliti?. Ali geuka nyuma na kuamua kuondoka eneo hilo.

Baada ya Eric kumaliza alipigiwa makofi sana kwa maonyesho mazuri na kwa wazo zuri la kusuluhisha matatizo ya maelfu ya watu. Yamkini watu wangejua nyuma ya pazia kilichotokea mambo yasingekua kama yalivyo sasa hivi.

Baada ya Eric kumaliza maonyesho na kushuka jukwaani wadada walikua wakiomba kupiga nae picha na wengine waki uliza maswali japo wapate mawaidha ya namna ya kufanikiwa kwenye maisha kama yeye hapo alipofikia.

Mandoto na Mkuu wa chuo waliondoka moja kwa moja kwenda kwenye ofisi ya mkuu wa chuo na wakiwa na wakuu wengine wa vyuo vingine ambao walikuja kupata kujionea walio ya sikia .

Mkuu wa chuo : “Bwana Mandoto.”

Mandoto : “Naam mkuu.”

Mkuu wa chuo : “Wanafunzi wameonekana kupenda sana wazo lako. Hongera sana hivi ndo vitu tuna vyo hitaji kwenye taifa letu mawazo kama haya maisha yana kuwa yana leta maendeleo chanya.”.Alisema hivyo huku wakuu wengine waki tikisa vichwa kuonesha kukubaliana na kilicho semwa.

Mandoto : “Asante mkuu jambo dogo hilo huna haja ya kunipongeza sana!.”

Mkuu wa chuo : “Kidogo?Teh teh. Hapana lazima ukweli usemwe.”

Mandoto : “Asante sana mkuuu.”

Mkuu wa chuo : “Sawa sasa hawa unaowaona ni wakuu wa vyuo kadhaa hapa Arusha na kwenye maongezi wamesema wanataka kupata mfumo kama huu.”

Mandoto : “Aaahaa sawa… Jamani nafurahi kuwa fahamu.”. Mandoto alitamani kuruka ruka seama kwa sababu yupo na watu wa heshima hakuweza.

Mkuu wa chuo : “Sasa mimi nitakupa mawasiliano nao na tutajadili haya mambo kwa ujumla.”

Mandoto : “Jamani wakuu nafurahi sana kupata muda nikaongea nanyi. Naombeni niwa ache na majukumu najua mnayo mengi.”

Mkuu wa chuo : “Sasa wewe baada ya kama masaa sita utakua usha pata malipo ya awali. Nitamwagiza Secretary afanye mpango wewe cha kufanya kamu achie namba yako ya akaunti ya benki.”

Mandoto : “Sawa mkuu nashukuru sana.”Mandoto aliamka na kuanza kuondoka wakati huo mkuu wa chuo alikua akiendelea kumsifia bwana Mandoto kwa wazo hili Mandoto alipunguza mwendo kidogo japo aendelee kusikiza anavyo sifiwa.

Mandoto alimkuta Eric amekaa pale kwenye kiti cha wageni kusubiria. Alikuwa amekaa na Rita wakiwa karibu.

Eric : “Mkuu kume endaje huko?”.Eric aliuliza kwa shauku akitaka kujua kama amefanikiwa.

Mandoto : “Mambo yame enda vizuri sana isitoshe kuna wakuu wengine wametaka huu mfumo.”

Eric : “Acha utani.”

Mandoto : “Sasa mimi nina utani na wewe?”.

Eric : “Yaaaaaaaaasssssss!”.Alipiga makelele ya furaha akijua kuna dalili za hela nyingi sana.

Mandoto : “We tuliza munkari.”

Eric : “Sawa sawa boss.”. Ali geuka akataka kumkumbatia Rita .

Rita : “We ni vipi? Una akili kweli mxxxxheww.”.Alisema akimsukuma Eric na kuondoka kwa hasira.

Eric : “Samahani nilisahau kama ni kazini hapa.”

Rita : “Mxxxxhew we jisaulishe tu.”

Eric : “Samahani.”

Rita : “Nini?”.Rita aliendelea kuonesha hasira na kuondoka hapo.

Mandoto : “Sasa kuna mahali naenda shika hii utatumia kama nauli sitoweza kukupa lifti.”

Eric : “Sawa asante haina shida.”

Mandoto aliondoka bila kusema chochote kuhusu hela .Eric kwa sababu ya mazoea alijua ata mpata kule ofisini kwake.

Upande mwingine nyumbani kwa kina Nickson ali mkuta Bertha amesharudi tokea safarini.

Bertha : “Waaooooow”.Bertha alsiema kwa furaha huku akimpa rafiki yake kumbatio lenye upendo wa hali ya juu.

Nickson : “Ah jamani nimekumiss sana.”

Bertha : “Unaendeleaje? Mbona kama huna raha?”

Nickson : “Aah ni ukubwa!.”

Bertha : “Niambie bhana.”

Nickson : “Mh mimi usiniwaze niambie mambo yame endaje?”.

Bertha : ”We jifanye mgumu tu!.”

Nickson : “Niambie na mimi nitakwambia.”

Bertha : “Haya tume enda nimefika salama . Ndio hivyo nime mzika mume wangu.”.Bertha aliacha kuongea kwa muda akitiririsha machozi . Nickson alimkumabatia kumpa faraja.

Nickson : “Jikaze najua sio virahisi.”

Bertha : ”Nickson nimemzika mume wangu kama mtu baki!. Wamekataa hata kuniona!.”. Bertha alianza kutoa kilio upya alilia kwa uchungu sana.

Nickson : “Basi basi jamani Mungu yupo na wewe!.”

Bertha : “Nickson wamemzika hata sijapewa hata nafasi ya kuweka mchanga kwenye kaburi la mume wangu…..”

Nickson : “Basi pole jamani..”. Nickson alishindwa kujizuia aka anza kutoa machozi lakini ana jitahidi sana kujikaza.

Bertha : “Dah jamani Mungu ni mimi tu?”.Bertha aliendelea kulia hapo kwa takribani dakika 20 huku Nickson akimkumbatia . Nickson alitoa ushauri kwamba watoke waka pate chakula japo mazingira yataeza kupata ahueni.

Walitoka wakaenda kwenye sehemu yao pendwa na wakala chakula. Walijikuta wakianza kunywa pombe mara wasimame wakaacheze mara wacheke kana kwamba hakuna shida tena ilifika muda wakaona kurudi nyumbanin wakaenda kulala chumba kimoja .

Ilipofika asubuhi Nickson aliamka akajikuta yupo mtupu na Berha kwenye kitanda kimoja huku Bertha kamkumbatia .

Wapi Comment mdau!
Itaendelea………………..
 
My Soulmate Kipande cha 20.

Produced by EquatorStory Specials.

##############Tulipoishia######################

Nickson na Bertha walitoka wakaenda kwenye sehemu yao pendwa na wakala chakula. Walijikuta wakianza kunywa pombe mara wasimame wakaacheze mara wacheke kana kwamba hakuna shida tena ilifika muda wakaona kurudi nyumbanin wakaenda kulala chumba kimoja .

Ilipofika asubuhi Nickson aliamka akajikuta yupo mtupu na Berha kwenye kitanda kimoja huku Bertha kamkumbatia .

*********Endelea nayo ********************

Nickson alianza kuona moyo ukienda mbio na kichwa kilikuwa kina muuma ilikuwa ni mara yake ya kwanza kutumia pombe lakini jana yake alijikuta ana kunywa. Wakati anaendelea kushangaa Bertha alishtuka usingizini na kuona kuwa yupo utupu na Nickson. Alisimama nduki na shuka akakimbila kanga akajifunga akiwa ana shangaa nini kimetokea?.

Nickson na Bertha wali baki wakishangaana ni nini kimetokea?.

Bertha : “Tuta shangaana mpaka saa ngapi sasa?”.

Nickson : ‘Sijaua kuhusu ratiba yako mimi nipo huru hata siku nzima.”

Bertha : “Hahahahaha .We kaka unapenda utani wewe!.”

Nickson : ”Unakumbuka kilichotokea jana?.”

Bertha : “Hapana vipi we unakumbuka?”.

Nickson : “Hapana sikumbuki hata tumefikaje!”

Bertha : “Au uliniekea dawa kwenye kinywaji?”.

Nickson : “Unasemaje?”. Aliuliza aki kunja sura kuonesha kukasirika.

Bertha : “Nakutania wewe nae.”.Bertha alisema kwa kucheka kwa mbali kuashiria amani.

Nickson : “Hapa naskia tumbo linakwaruza na kichwa kinauma nasikia kizungu zungu.”

Bertha : “Hata mimi najisikia ovyo sijui ndo mimba.”

Nickson : “Heheheh Acha zako wewe.”

Bertha : “Nikwambie kitu twende tukanywe supu labda itatupa nguvu.”

Nickson : “Hapo umenena. Sasa twende. ”

Wakajiandaa na kuondoka kwenda kunywa supu lakini kwa leo hawakuwa waongeaji kama ilivyo kawaida yao. Walikuwa wakitupiana macho ya kiu wizi huyu akimwangalia mwenzie kwa kupokezana.Mpaka wanarudi wali kuwa kimya kama watu wanaotafakari mambo mazito sana.Njiani Nickson aliamua kuvunja ukimya.

Nickson : “Niku ulize?’

Bertha : “Uliza tu usijali.”

Nickson : “Una mpango gani wa mahusiano?”

Bertha : “Hata mimi nataka niku ulize.”

Nickson : “Hapana usiulize swali juu ya swali.”

Bertha : ”Sawa. Nakujibu.”

Nickson :”Nafikiri hili swala tunatakiwa kujua kabla hatuja endelea we jibu na mimi ntakujibu.”

Bertha : “Sawa.”. Alishusha pumzi kabla ya kuongea.

Nickson : “We ongea usiwe na wasi.”

Bertha : “Kusema kweli ndoa nliokuwa nayo imenitesa sana!. Yani bado siamini kama sipo kwenye ule uhusiano. Nilipata tabu sikupendwa pamoja na kumpenda sana!.”

Nickson : “Pole.”

Bertha : “Asante. Nilichukulia wanaume wote ni walewale walghai wanakupenda sana kabla ya ndoa ukifika huko anatoa makucha na kukuparua bila huruma.”

Nickson : ‘Hao ni wao sio mimi.”

Bertha :”Lakini kweli wewe ni mtu mmoja wa muhimu sana yani sijawai kuona mwanaume ana tabia kama zako mpaka najiuliza ulikuwa wapi kabla sijaolewa. Nisinge kubali kuolewa na yule shetani mkubwa au ninge kufanya uwe mchepuko wangu uni poze moyo.”

Nickson : “Mimi huyo mchepuko kabisa?”.

Bertha : ”Ndio kwani we nani?. Lakini naomba unisamehe nickson sina uwezo wa kukubali huu uhusiano usonge mbele. Nimepitia machungu sana nataka nikae bila mtu mpaka nitakapo amua kuwa niko tayari natamani sana kama utaheshimu hilo swala.”

Nickson : “Afadhali umesema ukweli mimi ntakupa nafasi unayo taka naheshimu maamuzi yako.”

Bertha : “Enhee na wewe mpango wako?”.

Nickson : “Mimi nilikwambia nina yule mpenzi wangu Stela?”.

Bertha : “Ndio nakumbuka uliniambia. Bora uwe mwaminifu kwake.”.

Nickson : “Ndio nataka kuwa mwaminifu kwake! . Japo kuwa ni pasua kichwa.”

Bertha : “Sasa ndo hicho tu ulikuwa unaogopa kuongelea.?”

Walicheka huku wakiondoka wakicheka kuhusu hili na lile wakishikana mikono mara wakimbizane. Siku hiyo ilipita.

Nickson aliamuwa kwenda kwenye ofisi ya mandoto ofisi yake ya zamani alipokuwa ana fanya kazi.

Alipofika alikutana na mlinzi pale mlangoni.

Mlinzi : “Bwana Nickson karibu sana za kupotea.”

Nickson : “Asante mkuu. Za masiku huyu mkuu nimemkuta?”

Mlinzi : ”Yupo ngoja nikamwambie secretary kuwa umekuja .”Mlinzi alienda kumuita stela .

Stela alipo fika akajitenga pembeni na Nickson.

Stela : “Acha zako wewe unanifuata kisa nini mimi sikutaki nipo na mume mpya boss mandoto.”Stela alianza kuropoka bila kutaka kujua Nickson amekuja mipango gani.

Nickson : “Unasemaje?”.Nickson ali shangaa kutoamini alicho kisikia.

Stela : “Ndio hivyo kama umekuja hapa kujifanya unanipenda mi sitaki umeona hii pete? Ni ya uchumba jana Mandoto kanivisha.”

Nickson : “Attyy?. Stela acha utani unajua nakupenda ety?”.

Stela : “Acha kunisumbua mimi bure wewe uhusiano wa maneno matupu napeleka wapi? ”

Nickson : “Daaah stela umeamuwa kunitenda? Mimi nilikuwa mwaminifu kwako.”

Stela : “Mi hicho sijakuomba!.”

Nickson : “Stela stela…”.

Stela : “Kama huna cha kusema sema mi nirudi nikafanye kazi yangu.”

Nickson : “Mhh haya Stela mi sikuja kwa ajili ya hicho nilikuja kumwona mandoto.”Nickson alisema kwa huzuni huku maumivu ya moyo yaki mnyongonyeza.

Stela : “Kumbe ni huyo? Hajafika bado unaeza kukaa pale umngojee!.’

Nickson : “Mi naondoka ntakuja mda mwingine.”

Stela : “Utajua mwenyewe . Lakin usinitafute sijui unanipenda mara sijui nini nini…. Umesikia?”.

Nickson : “Sawa.”

Stela : “Kwaheri.”

Nickson aligeuka kwa uchungu aanze kuondoka hakuamini kama yule stela aliempenda kapendwa na mtu mwingine na hamtaki tena.Wakat ana karibia kutoka kwenye jingo hilo alikutana na Eric na Mandoto waki ingia ofisinin hapo.

Nickson: “We jamaa kumbe msaliti??.”.Nickson alitaka kumvamia Eric na ngumi lakini Mandoto alimzuia kabala ya kumfikia.

Mandoto : “Weweeee naomba uheshimu ofisi hii huezi kuja na kutaka kupiga watu kama una uwazimu.”

Nickson : “Mmeshirikiana kuni ibia wazo langu?. Saivi mnakula kwa jitahada zangu.”

Mandoto : “Weweee huyu Rafiki yako alikuja kwangu na kusema kuwa wazo lilikuwa kubwa sana kwako usingeweza mshukuru sana maana kakusaidia ku hakikisha wazo lako lina fanya kazi.”

Nickson : “Hapana huo ni uwizi mumeiba wazo langu .”

Mandoto : “Unaweza kudhibitsha wazo ni lako? Ama unaropoka tu?”.

Nickson : “Dah Eric mkuu nilikuamini!”

Eric : “Uliniamini una dhani mimi mama yako ama nimekuwa Yesu?. Kwanza sitaki hata kuongea na mjinga kama wewe.” Eric alipitiliza akamsukuma Nickson na kuondoka kama ofisi ile ni yake na madoto alimalizia kwa kumualika Nickson kwenye sherehe ya kuvishwa pete stela.

Nickson aliondoka kuelekea nyumbani kwa unyonge sana akijua amekosa kila kitu rafikiye kipenzi kamsaliti. Mpenzi wake stela anaolewa na boss wake wa zamani.
Neno moja kwa Nickson.
Itaendelea…….
 
My Soulmate / Mwenzi wa roho yangu

Sehemu Ya 21

#### Tulipoishia ####
Nickson amepata mapigo mawili kwa mpigo mmoja. kwanza amesalitiwa na rafiki ya Eic na mpenziwe Stela anaolewa na boss wake wa zamani . Bwana Mbekure.

******* Tuendelee ************

Ni wiki takribani ya pili sasa kwanzia Eric afanye maonyesho na watu kukubali kazi yake lakini mambo yamebadilika ghafla baada ya bwana sambeke haonekani kwenye ofisi yake takribani muda wote na bahati mbaya au nzuri hana namba zake. Akienda ofisini anarudishiwa getini na mlinzi akingoja boss aonekane atakaa hapo mpaka jioni bila mafanikio.

Baada ya kumsumbua sana RIta ali fanikiwa kuongea nae kwenye simu.

Rita : "Helo . Enhee shida yako?".

Eric : "Mbona umebadilika hivyo mpenzi wangu."

Rita : "Bhana usinisumbue mimi nipo kazini bhana."

Eric : "Jamani mpenzi huo ni ubize gani?"

Rita : "Naomba uache kuni ita ita mpenzi bila mpangilio."

Eric : "Heee yamekuwa hayo?".

Rita : "Kwani sikukuambia mpenzi wangu alikua uganda au umejisahaulisha?".

Eric : "Jamani acha zako."

Rita : "Ndio hivyo hubby wangu mfalme wangu amekuja usije ukajileta kwenye hii nyumba tena!".

Eric : "Yamekua hayo?. Jamani kama nimekukosea niambie!.".

Rita : "Heeee yani wewe mwanaume mjinga kweli uli dhani ntakua na lofa kama wewe?. Nimemkosea Mungu nini mimi?."

Eric : "Dah acha kuleta maringo ya kijinga uwe na adabu bhana!."

Rita : "Maringo ya nini?".

Eric : "Maringo na madharau mimi sipendagi. Isingekua ni kuhusu hela nisingekutafuta hata upite mdada mwenye ndo wewe?."

Rita : "Hahahahahahahahahahhha."

Eric : "Unacheka nini sasa?".

Rita : "Ety hella.....".Alisema kwa sauti ya kubana pua.

Eric : "Una dhani mimi nina na shida na kinyago kama wewe."

Rita : "Masikini ungejua.."

Eric : "Kujua nini?"

Rita : "Kwamba umesha tapeliwa na Sambeke.". Moyo wa Eric ulipasuka na aka anza kuhisi baridi na bado alihisi jasho likaribia kutoka. Mara ahisi tumbo linauma mara ahisi kwenda kukojoa. Mara kizunguzungu.

Eric : "Mhhhhhh."

Rita : "Eti hela fofofofofofofo! Hela utasikia bombani."

Eric : "Unasemaje wewe mwanamke?".

Rita : "Ndo hivyo babu we!."

Eric : "Wacha uongo wewe."

Rita : "Utajua mwenyewe. Kwani Sambeke umempata?".

Eric : "Hapana yupo bize kidogo."

Rita : "Hahahahah We mjinga kweli huna msimamo mwanaume mbwa wewe una acha marafiki kisa mwanamke na tamaa ya hela?. Hapa ndo umefika!."

Eric : "Tafadhali kuwa na heshima."

Rita : "Ama utanifanya nini wewe?. Utakuja kunikumbuka wacha ujinga jifunze adabu."

Eric : "Sambeke hawezi kuni tapeli nina mwamini."

Rita : "Huachagi kunishangaza! Kwa upumbavu wako utakae muoa ana taabu sana labda uka oe mpumbavu mwenzako. "

Eric : "Acha zako!. Mimi msomi unajua?"

Rita :"Msomi kiuno changu!. We mjinga tu unadhani haya maisha bila kujiongeza na akili za kuzaliwa utafanikiwa."

Eric : "Duh nisaidie basi nimpate Sambeke."

Rita : "Hata nikikupeleka kwa Sambeke utamfanyaje?. Kwani umesaini nae mkataba? We ni mfanya kazi wake ama?. Kwanza aliniambia anaenda mozambique kula maisha. "

Eric : "Acha uongo wewe."

Rita : "Unanipotezea muda wangu bure . Usinitafute tena nisije nika achwa na mume wangu mwanaume jitu miraba minne we mwembamba kama njiti."

Eric : "Unasema".Hapo RIta alikuwa amesha kata simu na kumuweka kwenye orodha ya waliozibwa wasieze kumpigia.

Eric ali ambulia patupu hakuweza kupata hela alizo ahidiwa aliachwa na Rita na bado hata akimpata Sambeke hawezi kumpeleka popote kwa sababu walifanya mkataba wa mdomo. Na nani atataka kusikiliza kesi ya tapeli alivyo tapeliwa?.

_____________________________________________________________________________

Upande mwingine mozambique Stela yupo na Sambeke wakiponda raha na Stela akijisifia kuwa bila yeye sambeke asinge weza kufikia hapo. Na pia akisema ukipata nafasi tumia vizuri. Kwa sababu ya hela waliopata waliamuwa kufanyia harusi yao huko mozambique sherehe nzuri tu ya watu kama kumi na ili faaana tu!.

___________________________________________________________________________

Upande mwingine Betha aliendelea kuishi maisha yake na baada mambo ya kuendelea kuwa magumu Nickson alikuwa akifanya kazi ya kubeba zege na zingine za mikono alimuradi ni sawa kisheria.Bertha alipata kazi za hapa na pale za kufua nguo kufanya usafi.

Bertha alikuwa ana penda sana kumwona tu Nickson . Wakae wapige stori wakienda kula mihogo lakini walikuwa wakicheka kama wanayo mamilioni. Walikuwa kama wapo kwenye ulimwengu wao.

Siku moja katika maongezi yao.

Bertha : "Nickson unajua maisha magumu sana lakini alimradi sipo kwa yule shetwani mi naona nina amani yangu kwa nini uolewe na usiwe na amani."

Nickson : "Kweli kabisa . Ndio maisha mwaya kikubwa amani hawa wadada wanaotaka watu wenye mihela yao wanaji weka vitanzi hawajui tu.".

Bertha : "Kweli lakini mimi nawaza kodi jamani."

Nickson : "Pole ni muda gani hujalipa ."

Bertha : "Mwezi wa nne huu!."

Nickson : "Mhh yule mama haja taka kukufukuza!?."

Bertha : "Kanipa wiki moja nihame sijui naenda wapi."

Nickson : "Hamia kwangu tukae pamoja!."

Bertha : "Mhhh utaeza kweli na Stela akijua atakubali kweli kukurudia?"

Nickson : "We usiwaze maisha kusaidiana bhana!. We hamia tuta ishi ki gheto gheto."

Bertha : "Hapana bhana watu watafikiriaje?".

Nickson : "Umekuwa TV wewe uwaze watu watakuonaje? We pambana bhana."

Bertha : "Mhh kuhamia kwako!.. Lakini unajua wewe ni rafiki yangu tu?".

Nickson : "Najua acha kujishaua sana!."

Bertha : "Mhh..."

Nickson : "We sikia wewe ni rafiki yangu wa karibu sana! Siwezi kubali eti ukalale mitaani wakati mimi nipo. Niachie mimi nikulinde niwezavyo."

Bertha : "Mhhh wewe unaweza mikito mikito ya kulinda mtu!?"

Nickson : "Unanionaje?. Wacha utani njoo ujichange utahamia tu kwako maisha ni kusaidiana!."

Bertha : "Sawa jamani Nickson unanijali sana na kujinyima sana kwa ajili yangu sijui nitakulipa na nini. "

Nickson : "Kipo we nisaidie kunifulia na kudeki deki na kupika na vingine we ishi pale kama kwako.'

Bertha alimkumbatia Nickson na kusema "Nakupenda sana wewe ni kama malaika mungu akubariki." Alisema huku aki angusha machozi ya furaha.

Baada muda Bertha walianza kuishi kwa pamoja kwa makubaliano kuwa marafiki lakini muda ulisonga mbele na hali zao ya kiuchumi ika anza kuwa ngumu mpaka ikafikia wakati Nickson ali shauri wauze vitu vya warudi kijijini. Wakakubaliana wakauza kila kitu mpaka simu zao .

Siku walipo uza kila kitu walibaki na mkeka tu na mabegi yao .

Nickson na Bertha waliamua kwenda kumuaga mama mwenye nyumba rasmi maana safari ina anza kesho asubuhi na mapema sana haitakuwa vyema kumuaga.

Nickson : "Mama kwa heri jamani umeitunza kama mwanao".

Mama Grace : "Naona umepata na mke kabisa tena anakufaa!."

Bertha na Nickson walicheka kuonesha kupingana na mama mwenye nyumba .

Nickson : "Hapana sisi ni marafiki."

Mama Grace : "aaaaaah wewe! Marafiki mnaishi pamoja?"

Nickson : "Hapana mama. Ni marafiki tumekuja kuku aga kesho tunaenda kijijini kuanza maisaha mapya. Tukalime hata na hela tuliopata yamkini tuta fanikiwa turudi mjini."

Mama Grace : "Haya wanangu Mungu awatangulie mka anze maisha na mufanikiwe jamani. Najua nyie ni wapambanaji."

Nickson na Bertha : "Amina mama!."

Mama Grace : "Haya kwaherini we Nickson acha funguo humo ndani mimi nitauona!."

Nickson : "Sawa mama kwaheri.."

Nickson walianza kurudi walipokuwa wanarudi walikuwa wakipiga stori mbili tatu wakicheka mara washikane mikono.

Hatimae wakafika kwenye nyumba waliopanga. Nickson aliomba aende chooni mara moja ili akilala asirudi tena!.Bertha alitangulia na kwenda kuingia chumbani alipofika alizibwa puani na watu wasionekana sura zao. Baada ya kama dakika mbili nickson alifika akakuta chumbani kuna giza aka anza kushangaa kwanini Bertha hajawasha taaa akae mwenyewe gizani?.

Akawasha taa kuhamaki kuna mtu aliejificha sura akiwa na mavazi meusi amekaa kwenye mkeka waliokuwa wamebakia baada ya kuuza kila kitu bertha akiwa katika hali ya kulala asijulikane kama ni mzima ama laaah. Nickson aka anza kumfuata aliepo kitandani akiuliza wew ni nani. Wakati alipopiga hatua mbili alivamiwa na aliekuwa nyuma yake akamziba mdomo mpaka kupoteza fahamu.

Ni kina nani hawa?. Ni yule mpelelezi aliekuwa anawafatilia ?. Ni majambazi?. NI maaadui wa Bertha au wa marehemu mumewe na Bertha ? .

Itaendelea..........
 
Doh!..
Kweli ngombe wa maskini hazai, na akizaa....
 
Back
Top Bottom