Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
shukran kiongozi,tuendelee japo viwili basiMy Soulmate Sehemu ya 17.
Produced by; Equator Special.
#############Tulipoishia ######################
Mandoto alikuwa hatoki nyumbani kwake mchana anatoka usiku tu kukwepa kuonekana na Afande Stanley. Usiku mmoja alikwenda bar usiku alivyo enda chooni alishtukia kuona Afande stanley akiwa nae ndani ya choo hicho. Alibaki akimtumbulia macho ha amini kama ni amebambwa kirahisi hivyo.
Afande Stanley : "Mimi ni mwindaji Mandoto huwezi nikimbia nikakuacha...".
**** Endelea *******************
Ni kwenye club moja ilio changamka sana mida ya saa nane usiku. Mandoto anaelekea kwenye uwani kwa ajili ya kujisaidia. Mara Afande Stanley anaingia ndani ya choo hicho.
Afande Stanley : "Mimi ni mwindaji Mandoto huwezi nikimbia nikakuacha...".
Mandoto : “Umenipataje?”. Aliuliza akiwa ana tumbua macho.
Mara ghafla kuna mkaka na mdada wali ingia kwenye choo hicho na wakipiga kelele za shangwe wakiwa na dalili zote za kulewa. Mandoto alipo ona nafasi hiyo alitoka anakimbia mpaka nje.Mandoto anakimbia huku kichwa kikiwa na pombe tayari kwahiyo ana yumba yumba wakati huo Afande anamfatilia taratibu.
Afande : “Wewe una lala na mke wangu wewe?”.
Mandoto : “Nisamehe kaka..”. Mandoto alisema huku akikimbia kwa yumba yumba na kizungu zungu kiki msumbuwa anatamani kukimbia sana lakini mwili hauwezi.
Afande : “Huwezi nikimbia.” Huku akimfuata Mandoto taratibu kama mtu anaewinda sungura alie umia mguu!.
Mandoto : “Nisamehe ndugu sisi sote bina damu.”
Afande : “Hapana wewe unajua ninavyompenda Sara mimi?”
Mandoto : “Kuwa mpole haya mambo ya kawaida!”
Afande : “Mambo ya kawaida ?”.
Mandoto : “Ndio mkuuu kuwa mpole.”
Afande : “Niwe mpole na mtu nlie mkuta analala na mwanamke wangu? Mwanamke anae nifanya nijitoe vingi kwa ajili yake?. We ulikua wapi wakati anaumwa na saratani miezi sita?”
Mandoto: “Kaka kuwa mpole.”
Waliendelea kuongea mpaka kutoka nje ya club hiyo . Mandoto bado ana hangaika kutembea lakin hawezi kwa sababu ya pombe.
Afande : “Unajua nina vyo mpenda? Sara umelala nae kwenye kitanda changu kama ndio nyumba yako unadhani nimekufa ama?”.
Wakati huo wanapigana mke wa afande alifika maeneo hayo alikua akimfwata mumewe nyuma nyuma bila ya mumewe kujua anafuatiliwa.
Mandoto alisamama akasema hapa ama zangu ama zako siwezi kubali uni aibishe kisa ya mwanamke ninaye mpenda alianza nakurusha ngumi kumuelekea afande Stanley. Wakati huo sara ali ingia ndani ya pub akijua mumewe alingia humo muda sio mrefu akiwa ana angaza angaza kumtafuta mumewe.
Afande Stanley : “Hahahah inaoneka umeamua tuyamalize kiume sio?”.
Afande alisema huku akirusha ngumi za tumbo mfululizo kwa Mandoto . Mandoto alimkuatia wakawa wana garagara chini wakirushiana makonde ya kila maeneo. Mara ghafla sauti ya bunduki kufyatuliwa ilisikika . Sara alikuwa nje wakati huo na aliona sauti ilipotokea alimwona mumewe na mandoto wakiwa wamelaliana hakuna aliekuwa akisogea.
Sara alipiga ukunga kwa uoga aka anza kutetemeka akamkimbilia eneo la tukio ili ajionee kilichotokea. Akiwa akizidi kusogea aliona eneo hilo likiwa limejaa damu alishindwa kuamini kile alichokiona mbele ya macho yake.
Sara alifika pale akausogeza mwili wa mumewe uliokuwa ukimlalia mandoto. Kutahamaki ni Mandoto alikuwa akilala pale akiwa marehemu kutokana na risasi aliopgwa kifuani alianza kulia kwa uchungu kipindi hicho mumewe akiwa haamini kilichotokea alikuwa akitoa macho tu alipo rudi kwenye fahamu zake alimshika mkono wake aka anza kumburuta waondoke.
Sara : “Niache we muuwaji niache mimi.”.Alisema akiwa anahangaika kutoka kwenye mikono ya mumewe.
Afande : “Twende huku wewe na wewe nitakumalizia.”. Alisema akimburuza alipo ona haondoki almnyanyua na kumuweka begani na kutokomea nae pasipo julikana na mtu mmoja mmoja akianza kufika kwenye eneo la tukio.Ma askari hawakukawia kufika baada ya wasamaria kupiga simu polisi.
Mandoto alichukuliwa na gari ya hospitalini na kuwahishwa hospitalini kama jitahada za kuokoa maisha yake.
Rose dada yake na Mandoto alikuwa amelala wakati huo aliamshwa na simu kutoka hospitali akiombwa afike kwa ajili ya kumwona kaka yake aliekuwa amevamiwa . Wakati huo hakuna aliejuwa ukweli nini kilichotokea. Rose alipofika alijitambulisha akasema yeye ni nani.
Docta : “Rose nina habari mbaya kaka yako amekutwa akiwa amepigwa risasi ya kifuani na sidhani kama ni majambazi maana alikutwa na wallet yake na kila kitu.”
Rose : “Unaongea nini? Kaka yangu mimi hapa. Yuko wapi.” Rose aliongea akiwa anatoa macho bila kuamini amini anachosikia.
Docta : “Tafadhali kuwa mpole rose.”.Docta alisema kwa njia ya kiustarabu.
Rose : “Sio niwe mpollllee kaka yangu yukowapiiii….??”Rose alitoa sauti kali na kwa uwoga.
Docta : “Bahati mbaya tumejaribu kumuokoa lakini imeshindikana.”Docta aliendelea kuongea kwa huruma na upole.
Rose : “Una maaana gani imeshindikana nataka kumwona kaka yangu.”Rose alisema kwa sauti akianza kutoa machozi.
Docta : “Nataka uniahidi kuwa utakuwa mpole nikakuoneshe kaka yako.”Docta alisema kwa upole aki inuka tayari kwa ajili ya kuanza safari ya kwenda kumuona Bwana mandoto.
Rose : “Sawa.”Rose wakati huu alishindwa hata kutoa sauti.
Rose alifuatana mpaka mochwari na dactari pamoja na mfanya kazi wa mochuari. Docta alimwomba afungue kabati namba nne . Droo ilifunguliwa na mfuko wa kufunukia ulifunuliwa .
Rose : “Kakaaaa kaka jamani umeniacha kaka …”.Rose aliangua kilio baada ya kuona mwili katika droo hiyo ni kaka yake kweli aliona kama ndoto moja inayo tisha na kutesa sana alilia kwa uchungu ambao hata hauwezi kuandikika.
Upande mwingine Nickson akiwa anajiandaa kwenda kwenye mizunguko yake alikuwa pia ana sikiliza habari za asubuhi hakuamini alichokiona alimfuata Bertha moja kwa moja akamlazimisha aamke kabla ya taarifa hizo kuisha Bertha alipo ona hivyo hakuamini kuwa anaona kifo cha mumewe.
Bertha : “Mume wanguu jamani mume wangu jamani umeniacha nitabaki na nani mimi.”.Bertha alilia visivyo mfano aki mkumbatia Nickson aliekuwa akimpa matumaini kuwa yote ni maisha na ni mpango wa Mungu .Bertha hakuamini kuwa amampoteza mumewe tena aliekufa kikatili pamoja na kuwa alikuwa ni mkatili sana kwa bertha bado alimpenda hivyo hivyo .
Bertha aliamua kwenda alipo tokea kwa ajili ya kumzika aliekuwa mumewe.
Itaendelea…..
SafiiiiMy Soulmate Sehemu ya 18.
Produced by: Equator Special.
Bertha amerudi alipokuwa anaisha na mumewe akakuta kweli kuna mazingira ya msiba hakuamini alianza kulia upya.
Alijikaza akaingia mpaka ndani akawa kuta ndugu zake na Mandoto wakiwa wanajadili alipofika alijaribu kuongea nao.
Bertha : “Jamani poleni.”. Wote walikaa kimya wakijifanya hawamwoni Bertha wakati huo Rose alikuwa amemgeuza familia nzima kinyume na Bertha.
Rose : “Samahani tunaomba utuache tuna kikao cha familia.”.Bertha aligeuka nyuma akiangalia kama kuna mwingine anae ambiwa hayo maneno.
Bertha : “Mimi ama?”.Bertha aliuliza kudhibitisha alichokuwa anasikia.
Rose : “Unazani naongea na nani we una kichaa si ndio?”
Bertha : “Naenda wapi huyu si mume wangu jamani?”
Rose : “Enhee ulikuwa wapi muda wote huo?”
Bertha : “Tuligombana nika amua kuondoka.”
Rose : “FOfofofofofo .”Alisema huku akibana pua yake.
Bertha : “Jamani.”
Rose : “Weeeee unadhani hatujui ulienda huko arusha kufanya umalaya wako.”
Bertha : “Jamani rose hayo maneno umetoa wapi?”.
Rose : “Unadhani sijui kuwa kaka alipokuja alikukuta ukifanya umalaya? Alikukuta umetoka hotelini na bwana wako.”. Wakati huo Bertha alitaka kumvamia Rose lakini ndugu waliokuwa karibu walimzuia. Waka mshika kwa nguvu wakampeleka mpaka nje ya nyumba hiyo. Wakati huo wakimtoa Hamida rafiki kipenzi wa Bertha aitwae Hamida alikuwa na ndo anafika maeneo hayo.Alimuwahi rafiki yake na kumkumbatia.Lakini wakati huo wote Bertha alikuwa analia anashindwa kuongea.
Hamida : “Basi rafiki yangu yote maisha.”Hamida ali jaribu kumpa rafikiye moyo katika wakati huu mgumu.
Bertha : “Hamida huyo ni mume wangu jamani wana ninyima kushiriki hata wanasema mimi malaya ahh jamani..”.Bertha alisema kwa uchungu aki ishiwa hata na nguvu ya kusimama.
Hamida : “We Nelson si unisaidie huoni au?”.Hamida alisema hivyo akimuashiria mpenzi wake aliekuja nae kumsaidia kumshikilia Bertha maana hawezi ata kusimama.
Nelson : “Mshike upande huo. ”. Walisaidiana pale kumshikilia na kumuingiza ndani ya nyumba hiyo ya mumewe.Kuna waliomuona Bertha akirudishwa wakawafuata ili kuwa rudisha nje. Hamida alijua dhamira yao kabla hawajawafikia akawa nyooshea mkono aki wa ashirie wasi sogee.
Hamida : “Weeeee sogeeni muone kichaa changu!.”.Walipo ona hivyo walisimama na kuondoka wakampeleka Bertha akaenda kukaa ambapo wageni wengine wame ekewa kuketi kwenye uwanja wa nyumba hiyo.
Hamida : “Jamani pole shoga yangu jamani watu wana roho ya nyoka.”
Nelson : “Wewe acha hizo tupo kwa watu..”
Hamida : “Wacha wasikie mimi sijali.”
Nelson : “Mh haya!.”
Watatu hao waliendelea kukaa mpaka jioni wakati wa chakula watu wote waligawiiwa chakula kasoro hao wa tatu . Hamida alichukua sheria mkononi akazunguka nyuma ya nyuma ambapo wanapika na akapakua chakula akawaletea wote walikula kasoro Bertha aliekuwa katika majonzi kiasi cha kwamba kalia mpaka anashindwa kulia tena amebaki kinyonge.
Jinsi muda ulivyo kuwa una songa ndugu za marehemu Mandoto walikuwa wakipita kwenda kulia na kushoto lakini walikuwa wakimpita Bertha kama sio mkwe wao.
Bertha : “Hamida tuondoke.”
Hamida : “Haaa hubaki hapa?”
Bertha : “Hamida huoni kuwa wananitenga sasa nakaa hapa kufanyaje?”
Hamida : “Hawa ma mbwa hawa walivyo kuwa wanajifanya wanakupenda wakati unateska na mume wako kutafuta utajiri huu saivi wanajifanya hawakujui.”
Bertha : “Hamida we achana nao. Watakusikia!.”
Nelson : “Msikilize mwenzako usipayuke kwa watu jamani Hamida!.”
Hamida : “Wacha wanisikie hawa wanafiki wakubwa wananikera sana!”
Bertha : “Hamida basi imetosha.”
Hamida : “Kwanza huyu Rose ile siku haukumbonda vizuri. Alipo kuwaga anaumwa TB uli hangaika nae huku na huku kama yeye ni mzigo wako. Mende yule saivi anajifanya sana ungemwacha angekufa yule mtu mwenye afya goigoi…..”
Nelson : “We twende bhana ukianza kuongea huachagi. ”.Nelson alisema akimsukuma Hamida waondoke ama sivyo watakaa hapo muda mrefu na Bertha alishasema waondoke.
Bertha : “Twende shoga wangu hawa watu hawana maana .”Betha alijikaza akasimama macho yakiwa mekundu.
Hamida : “Haya sasa tunaenda wapi?”.
Betha : “Nimeacha vitu vyangu hotelini nilipo fikia.”
Hamida : “Nelson tumuache shoga yangu leo akalale kwetu. Analalaje hotelini wakati mimi hapa nipo?”
Nelson : “Sawa kabisa twende sasa!.”
Hamida : “Haya twende tupitie vitu vyako tukalale kwetu hawa ma ng`ombe Mungu atawalipa.”
Bertha : “Sawa!”.Bertha wakati wanaondoka aliona bustani ambayo walikuwaga wana cheza na mumewe marehemu aka anza kuangusha machozi tena.
Walitoka hapo waka fika kwenye hotel vitu vya Bertha vilipokuwa waka vibeba na kuelekea nyumbani kwa Nelson na Hamida . Wakala na wakalala Bertha hakuwa na hamu ya kula lakini rafiki yake alimlazimishia kula alikua kama robo sahani aka shindwa kuendelea.
Ilipo fika kesho yake Bertha aligoma kwenda kule kwenye msiba asije korofishana na wakwe zake. Alimwomba Hamida akafuatilie ni lini mazishi ili ahudhurie kwenye mazishi japo hapo atakuwa ameshiriki. Hamida alienda aka pata taarifa kuwa Mandoto atazikwa kesho ya siku hiyo alimweleza Bertha.
Siku ya mazishi iliwadia Hamida ni mtu wa watu alipo wambia marafiki zake kuwa ni mazishi ya shemeji yake hawakubisha kumsindikiza kwenye msiba Huo.
Bertha alifika asubuhi na mapema walijaribu kumfukuza lakini Hamida alisimama kidete kumtetea waka mwacha.Mazishi yaliendelea na ulipofika muda wa kufukia udongo hawakutaja kuhusu swala la mke wa madoto ambaye ndie Bertha hawakutaja.Muda wa mazishi ulifika wakati wa kuweka udongo ndugu jamaa na marafiki wa Mandoto walitajwa kasoro mke wake hakuitwa kueka udongo aliweka kama watu wengine wa kawaida. Hiki kipindi kilikuwa kigumu sana kwa Bertha asijue cha kufanya isingekuwa ya rafiki yake kusimama na yeye walau hata nafasi ya kuwepo msibani ingekuwa ngumu lakini mumewe ali fariki ndoa ikiwa matatani alikimbia kuokoa maisha yake alikuwa anaishi kuzimu ya duniani.
Mazishi yalifanyika salama watu walitawanyika Bertha alibaki nyuma kwenye kaburi la mumewe kwa ajili ya kumuaga. Ndugu za Rose walikaa ndani wakiwa wanakunywa pombe kana kwamba hakukua na mazishi . Walipanga kugawa mirathi ya bwana Mandoto baada ya wiki moja . Bertha aliondoka sehemu hiyo na kurudi alipokuwa na Hamida.
Ilipofika siku ya kugawa mirathi hiyo Betha alienda kwa ajili ya kuhudhuria kikao cha kugawa mirathi alipo fika alishangaa kukuta askari migambo wa tatu mlangoni kitu ambacho sio kawaida.
Mgambo : “Samahani dada unaelekea wapi?”
Bertha : “Mimi ni mke halali wa Mandoto nadhani labda hunifahamu.”
Hamida : “Kwani hamumfahamu mkuu wenu?”
Mgambo : “Samahani dada tume pewa agizo la kuzuia mtu asi ingie humu ndani bila ruhusa.”
Hamida : “Makuubwa!.”
Bertha : “Umeambiwa na nani?”
Mgambo : “Wakuu waliopo humo ndani. ”
Bertha : “Basi naomba kuongea nao labda watanielewa.”
Mgambo : “Wamepiga simu dada wamesema mtu yeyote asi ingie!”
Bertha : “Basi naomba zao niwapigie niwa ambie mimi ni nani!.”
Mgambo : “Namba zao nimepoteza.”
Hamida : “We kaka ni mjinga eeeh?. Hauna akili unasema umepigiwa afu hauna namba unaongea na mashetani ama?”
Mgambo : “Mdada naomba tuheshimiane mimi nipo kwenye kazi yangu tafadhali usilete madharau na kazi yangu. “
Hamida alimshika mkono Bertha akasema “Twende na watuguse watuone”. Hamida alianza ku angaika kupenya katikati ya wana migambo hao bila mafanikio.
Hamida : “Niacheni niacheni nyie.” Hamida alipiga kelele kwa sauti huku walinzi wakiwa wana pambana kumzia asi ingie.
Hamida : “Afu unanishika wapi huko?”.Hamida alianza ku gombana na mgambo waliokuwa waki mzuia asi ingie alijikuta akimshika hamida kifuani. Hamida alirusha kibao mara ugomvi ukawa una kolea zaidi .
Rose aliposikia sauti za kelele walitoka na kukuta kukiwa na mparangano wa ugomvi.
Rose : “Watoeni hao malaya waambie wame sababisha kifo cha kaka yangu wanakuja kuchukua mali gani kwa mfano?“.Rose alisimama kwa mbali akiwa anasema maneno hayo. Akiwa mbali wagambo hao hatimae waliweza kuwatoa nje . Waka bamiza mlango .
Bertha alikaa chini aka anza kulia aka sema “kama ni mali nita pata upya kama nilivyo pata hizi na mume wangu”. Alijisemea hivyo huku akisimama na kujifuta machozi.
Bertha alikaa kwa rafiki yake kwa takribani wiki mbili aka amua kufunga safari na kurudi arusha . Angalau kule kuna Nickson ambae ana mpenda kama ndugu japokuwa ni marafiki tu. Bertha aliwaza akasema angekua na Nickson kama mume angekuwa na faraja sana! . Alipo mkumbuka Nickson alitabasamu mwenyewe kwenye basi kama kichaa.
Itaendelea ……………….
Asante sana kiongoziJamani hapo ndio mwisho wa season ya kwanza. Mwendelezo utatoka muda sio mrefu kaa chonjo!
Sawa mkuuJamani hapo ndio mwisho wa season ya kwanza. Mwendelezo utatoka muda sio mrefu kaa chonjo!
Sawa mkuu!Fanya makeke mkuu...
Mkuu vipi mbona kimya?Sawa mkuu!