Hai: Mbowe kaongea kwa hekima kidogo wakati Magufuli akizindua Barabara Kilimanjaro

Hai: Mbowe kaongea kwa hekima kidogo wakati Magufuli akizindua Barabara Kilimanjaro

Ghosryder

JF-Expert Member
Joined
Jul 6, 2014
Posts
10,403
Reaction score
4,373
Ni pale alipokuwa kwenye uzinduzi wa ujenzi wa barabara mkoani Kilimanjaro akiwa na Mhe. Magufuli,alisema, suala la maendeleo lisionekene au kuchukuliwa kuwa ni la siasa.

Ni kweli kabisa kuna baadhi ya wanasiasa hasa wasioelimika, wengi wao huzuia miradi mingi ya maendeleo mfano ujenzi wa maabara kwa kuleta siasa ndani ya shughuli za maendeleo!
=================
=

Hai.

Waziri wa Ujenzi, Dk John Magufuli jana aliungana na viongozi wenzake wa Serikali kuwamwagia sifa viongozi wa vyama vya upinzani baada ya kumwelezea Mbunge wa Hai na Mwenyekiti Chadema, Freeman Mbowe kuwa ni mpigania maendeleo ya wananchi na kwamba alitakiwa awe malaika.

Dk Magufuli alimuelezea kiongozi huyo wa upinzani bungeni kuwa ni mtu ambaye anafuatilia maendeleo ya watu bila ya kujali itikadi zao.

Waziri huyo ameungana na Rais Jakaya Kikwete na Waziri Mkuu Mizengo Pinda kusifu utendaji wa viongozi wa upinzani.

Februari 10, Rais Kikwete alisifu utendaji wa meya wa Manispaa ya Moshi, Jaffar Michael wa kuwaletea maendeleo wananchi, na siku 12 baadaye Waziri Pinda alimsifu mbunge wa Iringa Mjini (Chadema), Mchungaji Peter Msigwa kwa kuwa kiongozi wa kwanza kuchangia vitanda 30 kwenye Hospitali ya Frelimo.

Jana, Dk Magufuli alimmwagia Mbowe sifa hizo katika mkutano wa hadhara baada ya kukagua ujenzi wa barabara ya Kwasadala-Masama-Machame katika Jimbo la Hai inayojengwa kwa kiwango cha lami.

"(Mbowe)Unadhihirisha kwamba maendeleo hayana chama na kwa kweli tukienda hivi Tanzania itakuwa ni nchi ya kutolewa mfano. Sincerely (kwa dhati) nakupongeza Mbowe na Mungu akubariki," alisema.

Kabla ya Dk Magufuli kutoa pongezi hizo, Mbowe aliwataka wanasiasa kutekeleza ahadi zao kwa vitendo kwa kuwa maendeleo hayana itikadi.

"Mimi naamini maendeleo hayana itikadi. Jambo jema likifanywa na chama chochote cha siasa ama kiongozi wa chama chochote au Mtanzania, kama ni jema anastahili kupongezwa," alisema Mbowe.

"Hakuna aibu ya kukiri pale jambo jema linapofanyika. Ujenzi wa Barabara ya Kwasadala-Mula-Machame ni jambo jema," alisisitiza Mbowe.

Hata hivyo, alitumia mkutano huo wa hadhara uliofanyika Kijiji cha Masama kumuomba Dk Magufuli atoe maagizo ya kiserikali baada ya viongozi wawili wa CCM kutishia kuchoma moto greda lake.

"Nimenunua greda ili tusaidiane na Serikali, lakini juzi diwani na mwenyekiti wa kijiji walitishia kuchoma moto greda eti kwa sababu mbunge hajapewa kibali cha kuchimba barabara," alilalamika.

Mbowe alisema vyama vya siasa ni lazima vifanye pamoja kazi ya kuwaletea wananchi maendeleo.

Akihutubia mkutano huo, Dk Magufuli alisema Mbowe ni kiongozi mpole na mstaarabu na ndiyo maana kila ombi lake analoliwasilisha serikalini kwa ajili ya wananchi wake haligongi mwamba.

"Utapata wapi mtu mpole kama huyu? Alimuomba Rais pale kwamba niongezee kilometa tatu, (Rais) akatoa siku ile ile," alisema.

"Rais Kikwete ni mwenyekiti wa CCM, lakini ameleta barabara hapa kwa mwenyekiti wa Chadema. Huo ndiyo utanzania na haya ndiyo tunatakiwa viongozi tuige mfano."

Waziri Dk Magufuli alisema Mbowe ni miongoni mwa wabunge wachache wa upinzani ambao hawamsumbui bungeni na anapokuwa na jambo, huwa wanatoka nje na kuteta.

"Wako wengine wanapigaga kelele, lakini wewe unakuja tunazungumza. Unasema ndugu yangu, brother (kaka). Mbowe weweee! Ulitakiwa uwe malaika," alisema Dk Magufuli katika mkutano huo.

Hata hivyo, Dk Magufuli aligeukia siasa na kusema ustaarabu na upole alio nao Mbowe unatokana na malezi mazuri ya CCM kwa vile wazazi wake walikuwa wana-CCM na kwamba pongezi anazitoa kwa dhati. Alimpongeza Mbowe kwa kununua greda, akisema fedha hizo angeweza kuzitumia kwa shughuli nyingine lakini akaamua kulinunua ili kusaidia wananchi wake.


Chanzo: Mwananchi
 
Taratiibu umeanza kuelewa somo ingawaje kwa kebehi. Usipoziba ufa utajenga ukuta nje ya nchi mwezi novemba .Kaa chonjo kifo chaja.
 
Mbowe bhna akiongea utaskia tunaiagiza serikal sjuh nn na nn? Mara nasema wametuhujumu hahaha kuongea point ni mara moja moja
 
Ukweli ni kuwa mbowe huwa anaongea kisomi sana na vizuri zaidi.
Ni Mwanasiasa wa kipekee Tanzania nzima. Ukiwapanga wa5. Lazima umweke kwenye listi.
Sikumbuki vizuri nani anayemzidi?

Labda mbatia... Napo inategemea..
Kwenye listi yangu yupo pia Lowassa, nilikuwa nimweke mizengo pinda lakini siku hizi amepwaya kidogo.
Pia Mkapa, hayati nyerere.nuff said.
 
Mbowe bhna akiongea utaskia tunaiagiza serikal sjuh nn na nn? Mara nasema wametuhujumu hahaha kuongea point ni mara moja moja

Ndio wananchi lazima waiagize serikali!! lakini sasa hivi viongozi wetu ni wafalme,ni wenye dhuruma na kiburi!! wanataka waaabudiwe ndo walete maendeleo; tunaviongozi aina ya makengeza hawataki hata kuonywa!!!

misingi ya nchi imeharibika!!!
 
Wewe nawe vipi? Kwani Mbowe ameongea leo? UVCCM tunawategemea,msituangushe kama hivi.

Mzee Tupatupa

We nani kakwambia mimi ni UVCCM? Usinichanganye hapa sijui ukoje? mtu akisema jambo likiwagusa mnakimbilia kumpachika chama fulani! badilika wewe, mimi ni mjenzi huru wa nchi.
 
Wanaoleta siasa ni CCM wanaojidanganya maendeleo yapo kwa hela zao kumbe ni kodi zetu za wafadhili. Akili kidogooo
 
Ni kweli suala la maendeleo si la kisiasa,nilihuzunika sana pale mbunge wa Mchinga (CCM) Bw Said Mtanda alipowakataza wananchi wasichangie maabara huku akijua fika kuwa tatizo namba moja kwa wananchi wake ni suala la elimu.Kwani hata hiyo gesi bila kuwa na vijana waliosomea masomo ya sayansi ili kuweza kufanya kazi katika sekta hiyo.Itakuwa ni ndoto na kuishia kuandamana kudai upendeleo.
 
Angekuwa anakubali mambo mazuri ya nayofanywa na serikali angekuwa wa maana. Kila siku yeye anajifanya kuiagiza serikali.
 
Kama leo ndiyo umeweza kutambua kwamba Mbowe ana busara na huwa anaongea point. Basi wewe ni mmojawapo wa watoto waliokaa tumboni mwa mama yako hadi ukaota MENO na MAVUZI!
 
Mbowe huwa anababatiza vipoint kama mchezaji anapofungia goli kwa kutumia ugoko au tumbo.

Wakati nyie wenye upeo mdogo mnapokuwa na mawazo finyu viongozi wenu wanamwomba Mbowe atulize mambo pale yanapokuwa mazito kwa serikali. Huyu ni kiongozi kwa talanta alizopewa na Muumba kejeli zenu ni maneno kama ya kwenye kanga.
ImageUploadedByJamiiForums1425532572.255280.jpg
 
Asante Mungu kakufungua akili leo na umejua kipawa cha ajabu alichonacho inspekta na jemedari wa Anga hon Mbowe,
 
Wee jamaa vp???
Mbowe alikuwa anaongelea miradi ya ujenzi wa Barabara na sio ujenzi wa maabara, Tanzania nchi pesa na rasilimali kibao namba hii wanafaidi akina Change et al hafu mie mlalahoi ndo nilale njaa kuchangia maabara.. ptuuuuuu
 
Swala la siasa litabakia pale pale na swala la maendeleo pia litabakia pale pale,siwezi amini na sintaweza kuelewa serikali ya yenye watu wanaosema hela milioni kumi ni ya kununulia mboga sokoni,alafu wavuja jasho na walipa kodi wa nchi hii kulazimishwa kuchangia maabara,mimi kama mimi bado sikubaliani nalo kabisa,

maabara zilikuwepo tena zenye hali na kiwango cha juu kabisa,tangu omba omba waingie kwenye uongozi imekuwa ni shida,watu wamefanya ulaya ndo sehemu ya kwenda kufanya shopping,kwenda marketing na warembo,just to misuse the govn funds,alafu leo unasema swala la maabara lisiwe la kisiasa kivipi?
 
Back
Top Bottom