Hai: Mbowe kaongea kwa hekima kidogo wakati Magufuli akizindua Barabara Kilimanjaro

Hai: Mbowe kaongea kwa hekima kidogo wakati Magufuli akizindua Barabara Kilimanjaro

Tatizo kubwa la Mbowe ni kwamba alikimbia shule,hapo viongozi wanajaribu kumuelimisha ili asiendelee kutumia vibaya nafasi ya KUB.

Nyie mliosoma miaka 53 mmefanya nini zaidi ya kupita na mifuko kwenye nchi za watu kuombaomba kama mayatima huku mkiwa hamjui kwa nini wananchi mnaowaongoza ni masikini huku mkiwa na kila ngekewa ya rasilimali nyambafu kabisa eti alikimbia shule wewe ni tondo kabisa.
 
Waziri wa Ujenzi, Dk John Magufuli jana aliungana na viongozi wenzake wa Serikali kuwamwagia sifa viongozi wa vyama vya upinzani baada ya kumwelezea Mbunge wa Hai na Mwenyekiti Chadema, Freeman Mbowe kuwa ni mpigania maendeleo ya wananchi na kwamba alitakiwa awe malaika.

Dk Magufuli alimuelezea kiongozi huyo wa upinzani bungeni kuwa ni mtu ambaye anafuatilia maendeleo ya watu bila ya kujali itikadi zao.

Waziri huyo ameungana na Rais Jakaya Kikwete na Waziri Mkuu Mizengo Pinda kusifu utendaji wa viongozi wa upinzani.

Februari 10, Rais Kikwete alisifu utendaji wa meya wa Manispaa ya Moshi, Jaffar Michael wa kuwaletea maendeleo wananchi, na siku 12 baadaye Waziri Pinda alimsifu mbunge wa Iringa Mjini (Chadema), Mchungaji Peter Msigwa kwa kuwa kiongozi wa kwanza kuchangia vitanda 30 kwenye Hospitali ya Frelimo.

Jana, Dk Magufuli alimmwagia Mbowe sifa hizo katika mkutano wa hadhara baada ya kukagua ujenzi wa barabara ya Kwasadala-Masama-Machame katika Jimbo la Hai inayojengwa kwa kiwango cha lami.

“(Mbowe)Unadhihirisha kwamba maendeleo hayana chama na kwa kweli tukienda hivi Tanzania itakuwa ni nchi ya kutolewa mfano. Sincerely (kwa dhati) nakupongeza Mbowe na Mungu akubariki,” alisema.

Kabla ya Dk Magufuli kutoa pongezi hizo, Mbowe aliwataka wanasiasa kutekeleza ahadi zao kwa vitendo kwa kuwa maendeleo hayana itikadi.

“Mimi naamini maendeleo hayana itikadi. Jambo jema likifanywa na chama chochote cha siasa ama kiongozi wa chama chochote au Mtanzania, kama ni jema anastahili kupongezwa,” alisema Mbowe.

“Hakuna aibu ya kukiri pale jambo jema linapofanyika. Ujenzi wa Barabara ya Kwasadala-Mula-Machame ni jambo jema,” alisisitiza Mbowe.

Hata hivyo, alitumia mkutano huo wa hadhara uliofanyika Kijiji cha Masama kumuomba Dk Magufuli atoe maagizo ya kiserikali baada ya viongozi wawili wa CCM kutishia kuchoma moto greda lake.

“Nimenunua greda ili tusaidiane na Serikali, lakini juzi diwani na mwenyekiti wa kijiji walitishia kuchoma moto greda eti kwa sababu mbunge hajapewa kibali cha kuchimba barabara,” alilalamika.

Mbowe alisema vyama vya siasa ni lazima vifanye pamoja kazi ya kuwaletea wananchi maendeleo.

Akihutubia mkutano huo, Dk Magufuli alisema Mbowe ni kiongozi mpole na mstaarabu na ndiyo maana kila ombi lake analoliwasilisha serikalini kwa ajili ya wananchi wake haligongi mwamba.

“Utapata wapi mtu mpole kama huyu? Alimuomba Rais pale kwamba niongezee kilometa tatu, (Rais) akatoa siku ile ile,” alisema.

“Rais Kikwete ni mwenyekiti wa CCM, lakini ameleta barabara hapa kwa mwenyekiti wa Chadema. Huo ndiyo utanzania na haya ndiyo tunatakiwa viongozi tuige mfano.”

Waziri Dk Magufuli alisema Mbowe ni miongoni mwa wabunge wachache wa upinzani ambao hawamsumbui bungeni na anapokuwa na jambo, huwa wanatoka nje na kuteta.





chanzo mwananchi
 
hatimae mawaziri wa jk waanza kuwakubali wapinzani
 
Angalieni tu asije akawa anamwaga sifa hizo ili apatiwe shirika na nyie
 
mbowe ni moja ya wanasiasa wenye hazina sana ndani ya nchi hii
 
Nampongeza sana Mbowe kwa kununua greda kwa hela yake binafsi kwa ajili ya kujenga barabara jimboni mwake. Maendeleo ya Kili yataletwa na wanakili wenyewe kama ilivyokuwa tangu zamani Nyerere alipokataa kupeleka bajeti maeneo ya Moshi kwa madai kuwa tuwasubiri watanzania wengi na KNCU waliamua kuanza kujenga barabara na madaraja kwa hela zao wenyewe
 
Ngeleja kaenda shule lakini ni bora kinyesi kuliko thinking zake..JK na degree yake ya pass ya UD bado vitu vinamshinda ..by the way mbowe pampja na kukimbia shule yuko successfull kuliko hata baba yako

 
Last edited by a moderator:
Mbowe anajali sana maendeleo jimboni kwake na anatoa ushirikiano mkubwa kwa serikali

 
tapatalk_1489851838987.jpeg
Mbowe anajali sana maendeleo jimboni kwake na anatoa ushirikiano mkubwa kwa serikali

 
Back
Top Bottom