Haijawahi tokea, ni kufuru! Yanga yachangiwa zaidi ya tiketi elfu 30 kutoka kwa Rais, Wizara, viongozi, Mabenki, na bado zoezi linaendelea

Mama katoa mpya kwaba Yanga wakibeba kombe litatembezwa kila kijiji cha Tanzania kama mwenge wa uhuru, kama utahisi kukereka ni ruksa kahamia Burundi.
Na sisi wana uchumi hatuwezi kuruhusu hilo litokee.

Hapo kuinusuru nchi isiingie kwenye hasara isiyokuwa na lazima solution ni moja, USM ALGER apewe motisha
 
Bwana wee mechi ya kitaifa itakuwa hii?

Nyie nendeni hiyo jumapili mkawatie hasara waliotoa hela zao za tickets baadaye mje na maneno ya "mpira una matokeo matatu"
Mkuu tafadhali usijivunjie heshima humu JF, kwa niaba ya Utopolo tunaomba tuungane pamoja kuiombea Yanga ifanikiwe kutwaa ubingwa wa CAFCCL 2023.

Sent from my CPH2387 using JamiiForums mobile app
 
Hao wana siasa ndio unawaona leo kwenye mechi za Yanga? Mara ngapi humu mlikuwa mnaleta uzi wa kupinga viongozi wenu kuwaletea viongozi wa kisiasa kama mgeni rasmi kwenye michezo yenu ya kimataifa? Kuna mechi ilichezwa ya Simba huku mabango na T shirt za raisi Samia zikiwa zitalindima uwanjani. Swala la siasa katika soka letu halianzia kwa Yanga na pia halijaanzia leo.

Hizo tiketi zimekuuma sana eeh? Yanga ni taasisi na taasisi yoyote inakuwa na viongozi ndio wanaratibu kila jambo. Viongozi wangekataa kununuliwa kwa tiketi, mashabiki wangejua nini cha kufanya. Hivyo mashabiki ni watu wa kusikiliza viongozi wamebariki jambo fulani au lah. Mbona unajitia aibu kwa mambo madogo hivyo! Ni hizo taasisi wametumia kama fursa kwao kujitangaza kupita mchezo mkubwa wa ngazi za vilabu Africa.
Haijaniuma kuona watu wazima mnashangilia kununuliwa tiketi za shingi 5000, imeniuma kuona watu wa mjini halafu mnafanyiwa uhuni wa waziwazi huku mmelala usingizi wa pono. Ilinishinda kunyamaza ila nimeshatoa stimu zangu, najiona mwepesiii.
 
Kwa Yanga jinsi ambavyo mmekuwa kero humu kwasababu ya ndondokela ya msimu mmoja tu basi imekuwa sababu ya wengine kukosa raha.

Aaah kwa hilo nakubali yote tu acha heshima ivunjike.

Kwanza mi heshima ya kazi gani umri huu hainiingizii hela zaidi ya sifa tu.

Mafanikio ya Yanga yatageuka kuwa fimbo kwangu yani nitatukanwa, nitasimangwa mpaka basi.

Sasa guarantee ya mimi kuwa na furaha ni Yanga isichukue ubingwa.

Lakini pia kuna mwana hapa aliwahi kuja na uzi kutupa pongezi sisi waminyaji kwa mchango wetu kuifanya Yanga ifikie haya mafanikio.

So miongoni mwenu kuna kundi lingine ambalo linatuona kwa jicho la kitofauti kama watu fulani ambao tuna influence ya kuifanya Yanga ipate haya mafanikio.

Tukiacha "uminyaji" maana yake kuna namna tutakuwa tumepunguza nguvu kazi ya kufikia mafanikio yenu.
 
Ndiyo point yangu ilipo hapo. Mechi nyingi tu za Yanga mlijaza uwanja hata kama siyo 60K, sasa kwa nini mnaona fahari sana kununuliwa tiketi na kwa nini hawa watu/taasisi wameona njia sahihi ni kuwanunulia tiketi watu ambao wameonyesha uwezo wa kujinunulia? Jibu unalo au kama hauna litafakari utalipata.

Mngekuwa wajanja mngewaambia BMT badala ya kununua tiketi ambazo mlikuwa na uhakika wa kuziuza, wasichukue makato yao katika mechi kubwa 3 mtakazoamua nyie, mngewaambia Wizara au Serikali hivyo hivyo lakini hamna ubavu wala labda kwa bahati mbaya akili hizo.

Kuna mengi zaidi ningekwambia ila ngoja nione kwanza haya utayapokeaje.
mtafute fainali yenu ndio mtoe mawazo yenu, sio kutegemea wanaume wavuje jasho huko misituni kuwinda huku nyinyi mnasubiria utoa mawazo.

Tiketi zimenunuliwa na pesa za mauzo zimeingia vile vile tu kama ambavyo tiketi zinavyonunuliwa mechi zilizopita, kilichofanyika ni kwamba amiri jeshi mkuu, mabenki makubwa, mkuu wa jiji kubwa zaidi Tanzania, na Wizara ya Michezo wameamua kuonyesha uzalendo, huwezi kuwazuia watu kuonyesha uzalendo.
 
Haijaniuma kuona watu wazima mnashangilia kununuliwa tiketi za shingi 5000, imeniuma kuona watu wa mjini halafu mnafanyiwa uhuni wa waziwazi huku mmelala usingizi wa pono. Ilinishinda kunyamaza ila nimeshatoa stimu zangu, najiona mwepesiii.
Una upeo mdogo sana wa kufikiria sijajua ndio uwezo wako au Yanga ndio inayokuchanganya mpaka uwe na akili za ovyo kiasi hiko.
Yaani wewe taasisi kununua tiketi kwako umeona ni jambo la ajabu sana utafikiri mgeni kwenye mpira.
Halafu cha ajabu sana unasema eti mashabiki wanaibiwa, haya nikuulize wanaibiwa na nani? Kwani ela za viingilio huwa kuna mgao kwaajili ya mashabiki? Gate collection ni faida ya muwekezaji ambaye ni GSM asa kama kwake kaona ni sahihi kwa taasisi kununua tiketi kwaajili ya mashabiki, wewe kinachokuumiza kichwa ni nini kama sio uhayawani huo?
 
Hao wana siasa ndio unawaona leo kwenye mechi za Yanga? Mara ngapi humu mlikuwa mnaleta uzi wa kupinga viongozi wenu kuwaletea viongozi wa kisiasa kama mgeni rasmi kwenye michezo yenu ya kimataifa? Kuna mechi ilichezwa ya Simba huku mabango na T shirt za raisi Samia zikiwa zitalindima uwanjani. Swala la siasa katika soka letu halianzia kwa Yanga na pia halijaanzia leo.

Hizo tiketi zimekuuma sana eeh? Yanga ni taasisi na taasisi yoyote inakuwa na viongozi ndio wanaratibu kila jambo. Viongozi wangekataa kununuliwa kwa tiketi, mashabiki wangejua nini cha kufanya. Hivyo mashabiki ni watu wa kusikiliza viongozi wamebariki jambo fulani au lah. Mbona unajitia aibu kwa mambo madogo hivyo! Ni hizo taasisi wametumia kama fursa kwao kujitangaza kupita mchezo mkubwa wa ngazi za vilabu Africa.
we jamaa ndio huna unachokijua...

hiyo fainali, itasemwa si tu na vyombo vya habari vya ndani bali hata vya nje... juzi tu hapa habari zilikuwa ni kuhusu marumo kununua tiketi zote, hayo yametokea huko ila habari zipo afrika yote...

sasa basi hiyo fainali baadhi ya taasisi wanatumia kama marketing, ni kama kulipia tangazo la kutangaza biashara yako kwa gharama hizo... hivyo ni jambo la kawaida sana katika masuala hayo ya soka kuona taasisis inanunua tiketi badala ya mashabiki.... acha uzwazwa na kufikiri kimaskini maskini kwamba watu hawana uwezo wa kununua tiketi hadi wanunuliwe kichwa panzi wewe
Kabisa mwananchi unaruhusu taasisi kubwa za fedha zitumie platform kubwa kama mechi ya fainali ya CAF kujitangaza kwa kutoa tu milioni 25 wakati wangeweza kutoa milioni 300? Mngeweza kuwaambia badala ya kununua tiketi ambazo naendelea kusisitiza mlikuwa na uhakika wa kuuza, embu wapeni wachezaji wote fixed deposit account ya milioni 12 kila moja. Hapo kuna benki tatu, kila mchezaji milioni 36. Ipi dili bora?
 
Punguza kidomo domo hicho, hayo mawazo yako yapeleke fainali yenu utayoiota ndotoni.

Tiketi zimenunuliwa na pesa kama kawaida imeingia Yanga, kilichofanyika ni kwamba amiri jeshi mkuu, mabenki makubwa, mkuu wa jiji kubwa zaidi Tanzania, na Wizara ya Michezo wameamua kuonyesha uzalendo, huwezi kuwazuia watu kuonyesha uzalendo.
Kidumu Chama cha Mapinduzi! Na Zidumu Fikra za Mwenyekiti!
 
Kwa Yanga jinsi ambavyo mmekuwa kero humu kwasababu ya ndondokela ya msimu mmoja tu basi imekuwa sababu ya wengine kukosa raha.

Aaah kwa hilo nakubali yote tu acha heshima ivunjike.

Kwanza mi heshima ya kazi gani umri huu hainiingizii hela zaidi ya sifa tu.

Mafanikio ya Yanga yatageuka kuwa fimbo kwangu yani nitatukanwa, nitasimangwa mpaka basi.

Sasa guarantee ya mimi kuwa na furaha ni Yanga isichukue ubingwa.

Lakini pia kuna mwana hapa aliwahi kuja na uzi kutupa pongezi sisi waminyaji kwa mchango wetu kuifanya Yanga ifikie haya mafanikio.

So miongoni mwenu kuna kundi lingine ambalo linatuona kwa jicho la kitofauti kama watu fulani ambao tuna influence ya kuifanya Yanga ipate haya mafanikio.

Tukiacha "uminyaji" maana yake kuna namna tutakuwa tumepunguza nguvu kazi ya kufikia mafanikio yenu.
Umetapika ya ndani kabisa, hapo umefikia stage mbaya sana ya kukereka. Yaani hapo ulipofikia upo kwenye stage ya uchawi. Kama ukiambiwa kuwa kuna mtu anauwezo wa kuizuia Yanga isichukue kombe bila shaka utakuwa upo tayari kwenda.
 
Una upeo mdogo sana wa kufikiria sijajua ndio uwezo wako au Yanga ndio inayokuchanganya mpaka uwe na akili za ovyo kiasi hiko.
Yaani wewe taasisi kununua tiketi kwako umeona ni jambo la ajabu sana utafikiri mgeni kwenye mpira.
Halafu cha ajabu sana unasema eti mashabiki wanaibiwa, haya nikuulize wanaibiwa na nani? Kwani ela za viingilio huwa kuna mgao kwaajili ya mashabiki? Gate collection ni faida ya muwekezaji ambaye ni GSM asa kama kwake kaona ni sahihi kwa taasisi kununua tiketi kwaajili ya mashabiki, wewe kinachokuumiza kichwa ni nini kama sio uhayawani huo?
GSM! GSM! GSM!
 
Umetapika ya ndani kabisa, hapo umefikia stage mbaya sana ya kukereka. Yaani hapo ulipofikia upo kwenye stage ya uchawi. Kama ukiambiwa kuwa kuna mtu anauwezo wa kuizuia Yanga isichukue kombe bila shaka utakuwa upo tayari kwenda.
Hiyo uchawi ni wewe jinsi unavyoamua kuiita.

Ila umri huu sio wa kulazimishana kushangilia timu yako wakati na mimi nina yangu.

Nyie mlikuwa mnasema wachambuzi hawapaswi ku base kwenye upande kwasababu wao sio mashabiki

Sasa naona hata sisi mashabiki tumeanza kuingiliwa uhuru wetu yani tuache timu yetu afu tuwe pro wa timu nyingine?
 
Kabisa mwananchi unaruhusu taasisi kubwa za fedha zitumie platform kubwa kama mechi ya fainali ya CAF kujitangaza kwa kutoa tu milioni 25 wakati wangeweza kutoa milioni 300? Mngeweza kuwaambia badala ya kununua tiketi ambazo naendelea kusisitiza mlikuwa na uhakika wa kuuza, embu wapeni wachezaji wote fixed deposit account ya milioni 12 kila moja. Hapo kuna benki tatu, kila mchezaji milioni 36. Ipi dili bora?
Mashabiki hawafanyi biashara bali muwekezaji jukumu lake. Hilo la milioni 25 badala ya 300 sio kipaumbele cha shabiki. Shabiki kipaumbele chake cha kwanza kushuhudia timu yake ya pili ni kuona timu yake inafikwa taji la ufalme (kombe) habari za pesa hazimuhusu mshabiki kwasababu hakuna pesa atakayogaiwa shabiki. Akili yako ielewe hilo, mwwnye maslahi ya hilo ni muwekezaji ni bila shaka kwavile yeye yupo katika kitengo cha kuona ni namna gani michuano inarudisha pesa hata kwa kiwango fulani ni lazima kaishatengeneza mifumo ya kuingiza pesa kupitia fainali anayocheza Yanga. Hizi unazosikia ni ya nje tu ila makubaliano mengine haujui.
 
Msisahau ya Stars, tiketi zote zilinunuliwa. Tulichoambulia sasa, ni aibu.
 
Waache wacheze wakishinda washangilie watubeze tani yao

Ila na sisi matokeo yakija kwa namna inayotufurahisha basi tupewe uhuru wetu.

Hii nchi yetu wote
 
Back
Top Bottom