Synthesizer
Platinum Member
- Feb 15, 2010
- 12,699
- 22,598
Katika siku za mwisho za uhai wake, akiwa hospitali Uingereza na alipotembelewa na Mkapa, Nyerere alimwambia hivi Mkapa, "Benjamin, najua Watanzania watalia sana watakaposikia nimekufa"
Na Nyerere alipokufa ni kweli Watanzania tulilia sana. Tulilia pia alipokufa Waziri Mkuu wa enzi hizo, Edward Sokoine.
Watanzania tulilia sana pia alipokufa Dr. Omar Juma chini ya Raisi Mkapa, na tayari tulikuwa katika mfumo wa vyama vingi. Tulilia pia alipokufa Deo Filikunjombe wa CCM. Tulilia bila kujali itikadi zetu za siasa. Tumelia kifo cha Mkapa na Mwinyi, na tukijua hawakuhusikika na mambo ya sasa.
Katika uhai wake, akigusia uwezekano wa kifo chake, Magufuli hakusema Watanzania watalia sana, alisema mtanikumbuka. Naona alijitambua. Hapo ndipo mambo yalipoanza kubadilika. Magufuli alipokufa kuna Watanzania walilia sana, lakini pia wapo wengine walishangilia sana!
Na sasa imekuwa mtindo unaoendelea chini ya Raisi Samia. Kiongozi wa serikali au waandamizi wanapopoteza maisha au kujeruhiwa, tunashuhudia wananchi wengi wakishangilia sana!
Sasa ni bora serikali ya sasa chini ya Raisi Samia ijiulize sana, kwa nini imekuwa hivi? Kwa nini leo wananchi wakisikia polisi amepigwa au amekufa wanashangilia? Kwa nini wakisikia maofisa wa TRA wamepigwa na wengine kufa wanashangilia? Kwa nini wananchi wakisikia basi lililobeba wabunge limepata ajali na wabunge kuumia wanashangilia? Kwa nini wananchi wanatoa maoni kama kutamani kifo cha baadhi ya viongozi na waandamizi? Kwa nini hali hazikuwa hivi wakati wa Nyerere, Mwinyi, Mkapa na Kikwete?
Kuanzia Raisi wetu, tuje Makamu wa Raisi, Waziri mkuu, Mawaziri wote, Spika wa Bunge na wabunge wote, IGP, Polisi kiongozi wa kanda ya DSM, Ma RPC na askari Polisi wote kwa ujumla, TISS, TRA; juilizeni, hivi leo Watanzania wakisikia nimepoteza maisha, watashangilia au kulia sana? Kwa nini? Ndugu zenu mtakaowaacha watajisikiaje kuona watu watajisikiaje wakati wa msiba kuona watu wanashangilia kufa kwenu?
Karibu wote nyie, mtapata jibu kuwa mkifa watanzania wengi tu watashangilia sana! Si jambo jema lakini huo ndio ukweli. Jitafakarini na kutambua kuna kitu mnafanya hakipo sawa, mnapaswa kubadilika! Mnapaswa kuwarudisha wananchi wa Tanzania mahali ambapo wakisikia mmepoteza maisha basi walie sana, bila kujali itikadi zao za kisiasa! Huo ndio Utanzania halisi, na kama umetokweka wenye makosa ni nyie!