Haikuwa uamuzi sahihi kusitisha ajira hata kwa Walemavu, hili kundi linataabika sana mtaani

Haikuwa uamuzi sahihi kusitisha ajira hata kwa Walemavu, hili kundi linataabika sana mtaani

Nahis kama ungeacha kuchangia hapa. Unavuruga michango mizuri inayotolewa na wengine.
Siachi...tumejilea vby sana watz..tunapenda mteremko....lazima tuambizane ukwel...siku serikali ikikupa huo msaada uje useme hapa umepewa bure mamilion mangapšŸ˜,kwan ukiwa mlemav wa mwili na akili nayo inakua lemavu?
 
Mlemavu ana Economic disadvantages nyingi kuliko Advantages.

Tunazungumzia kukwamuka kiuchumi, mlemavu kupata nafasi katika Private Entity ni sawa na ngamia kupita katika tundu la sindano iwe Professional, iwe manual work mbinde sana mlemavu kupata nafasi huko...Private Entity wanaangalia faida ya kampuni zaidi kumpa kazi mlrmavu na kumuacha mzima kwao wanaona kama Charitable Activities na wao hawapo kwaajiri ya Charity.

Now, tunaona mlemavu hana nafasi serikalini hana nafasi Private, kimbilio pekee linalobaki kwake ni kujiajiri.

Swali: anajiajiri vipi hana mia mfukoni.

tukijiuliza swali hilo maana yake tunaangali mwanzo anaanzaje, tusiangalie kuna mlemavu anamiliki Gari, Hotel, Shule...Suala alipokuwa hana ata 100 Tzs mfukoni ilikuwaje.

Mimi sijui nyie mutakwamukaje mimi hilo halinihusu imetosha kuwatetea.

Walemavu munahitaji mkono kwakweli, ila kwahii Dunia ya sasa nafikiri inaenda kinyumenyume unaweza kuwa na haki yakupata kitu fulani ila utangoja ukipate mpaka unakufa hakuna atayekuja kukupa.

Maisha ya sasahivi Kama mvua yanamnyeshea kila mtu hayajari wewe mlemavu wewe Graduate, unategemewa, mgonjwa yenyewe yanachojua ni kutandika bakora tu bila huruma.
Mkuu ahsante sana kwa kutambua hilo, pia ahsantebkwa ushauri na mtazamo mzuri.
Bora tulipigie kelele hili kuliko na kukaa kimya ukizingatia hali ya utawala ilivyo. Ipo siku hizi kelele zitasikika na kuzaa matunda.
 
Lakini mbona anaandika fresh..labda uono hafifu....lakini bado anaweza sana kuanza na chichote then akawa pushed....
Alisema anatumia kisoma screen yani App yenye uwezo wa kutamka herufi ukiigusa. Akipapasa screen akaigusa A, kisoma screen kinatoa sauti inatamka hiyo A na yeye anagusa tena hapo ndio herufi inaandikwa.
 
Inasikitisha sana, ivi sheria inasemaje kuhusu hili suala la ajira kwa walemavu hata kama haifuatwi.

Hili kundi haitakiwi kusahaulika kiasi hiki hata kama mambo mengi makubwa yanatekelezwa
Sheria ya watu wenye ulemavu sura ya 183 imeweka masharti mazuri sana kwa waajiri,pia sheria ya Utumishi wa umma na ile kanuni (gn 326/2021) zimeweka mazingira mazuri sana kwao.Tatizo: wachache sana wanaomba kazi au wanapata minimum qualifications.Kuna part yao waicheze vizuri kwanza.
 
Sheria ya watu wenye ulemavu sura ya 183 imeweka masharti mazuri sana kwa waajiri,pia sheria ya Utumishi wa umma na ile kanuni (gn 326/2021) zimeweka mazingira mazuri sana kwao.Tatizo: wachache sana wanaomba kazi au wanapata minimum qualifications.Kuna part yao waicheze vizuri kwanza.
Tuna tatizo sana na kufuata sheria nchi hii
 
Back
Top Bottom