Mlemavu ana Economic disadvantages nyingi kuliko Advantages.
Tunazungumzia kukwamuka kiuchumi, mlemavu kupata nafasi katika Private Entity ni sawa na ngamia kupita katika tundu la sindano iwe Professional, iwe manual work mbinde sana mlemavu kupata nafasi huko...Private Entity wanaangalia faida ya kampuni zaidi kumpa kazi mlrmavu na kumuacha mzima kwao wanaona kama Charitable Activities na wao hawapo kwaajiri ya Charity.
Now, tunaona mlemavu hana nafasi serikalini hana nafasi Private, kimbilio pekee linalobaki kwake ni kujiajiri.
Swali: anajiajiri vipi hana mia mfukoni.
tukijiuliza swali hilo maana yake tunaangali mwanzo anaanzaje, tusiangalie kuna mlemavu anamiliki Gari, Hotel, Shule...Suala alipokuwa hana ata 100 Tzs mfukoni ilikuwaje.
Mimi sijui nyie mutakwamukaje mimi hilo halinihusu imetosha kuwatetea.
Walemavu munahitaji mkono kwakweli, ila kwahii Dunia ya sasa nafikiri inaenda kinyumenyume unaweza kuwa na haki yakupata kitu fulani ila utangoja ukipate mpaka unakufa hakuna atayekuja kukupa.
Maisha ya sasahivi Kama mvua yanamnyeshea kila mtu hayajari wewe mlemavu wewe Graduate, unategemewa, mgonjwa yenyewe yanachojua ni kutandika bakora tu bila huruma.