Haiwezekani Mungu asimuue Shetani halafu aamuru Watu waue wanaofanya mambo ya kishetani; Haiingii akilini

Na hapohapo tunaambiwa hakuna wa kusujudiwa ila Mungu, iweje Mungu amuamuru Shetani kumsujudia Adam? Contradictions juu ya contradictions argghhh 😬😬😬
 
Mtoa mada umejiabisha kwa hiki ulicho kiandika! Nadhani hujui lengo la kuwepo hapa katika hii Dunia ?? That why unaandika Kila kinachokujia katika akili yako bila kuchuja???

Watatokea watu kukupongeza kwa ulicho andika ila na wao ni pia sio watu wanaofikiria sawa sawa

Hapa tatizo lako ni Moja tu .ni kuwa humjui mungu WA mweli uwezo wake upoje ???

Hapa shetan anaepoteza wanadamu ni yule aliekataa kumsujudia NABII adamu na Sio mwengine na huyo baada ya kufukuzwa na Allah aliomba kwamba Allah asimuue Hadi mwisho WA ulimwengu ( kama Kuna kitu nimekosea naomba kurekebishwa)!

Huyu shetan au ibilis alimuapia Allah kuwa atawapoteza Wana adamu ili waingie wote moton siku ya kiyama . Ila Allah alimwambia waja wake hawawezi kupotezwa na ibilisi yaan shetwan

Note
Hadi hapa kama akili yako Ina akili basi utakuwa umeshaelewa SoMo hapa

Kwa mfano

Mwalimu anatoa mtihani labda form six
Kuna watakao Fanya vyema na Kuna watu watafanya average na Kuna watakao fell pia
Na lengo la mtihani watu wafaulu na Sio kufeli


Kwahiyo hapa Duniani ni kama mtihani tu Kuna watu watapatia na Kuna wengine watafeli

Na kufeli kunachagizwa na mambo mengi kama ulaji WA pombe ,kamari,zinaaa,wizi,fitna, ubasha, n.k


Mtoa mada unaposema shetani ndio mungu mwenyewe unakuwa unafeli pakubwa sana
Mungu hawez kuwa shetan na shetan hawezi kuwa mungu na hata ww unalijua Hilo sema tu unajizima data.

Hoja yako nyingine eti unataka watu wote tuwe aina Moja Yani wote tuwe wema ????

Hili hata mtoto wa darasa la kwanza anakuweka kando ! Ukishawai kwenda sokon ukakuta wanauza nyanya tu soko zima.????

Au ukakuta soko zima wanauza Infinix tu.???

Ni lazima utakuta mixer hapa Wala tusimsingizie mungu

Binadamu wote hatuwezi kuwa na fikra Moja kuwa tunawaza kitu kimoja ili tuwe wema wote
Na ndio maana Kuna moto na pepo

Ukifauli pepo ni yako na ukifeli moto ni wako

Maana tayar tulishaletewa manabii na mitume kuja kutuonya usimtaje shetani tu.

Note.

Rejea mfano WA mwalimu anapotoa mtihani lengo sio watu wafeli lengo ni kuwapima wanafunzi wake .kama lengo angetaka wafaulu wote basi huo mtihani angeutunga na kufanya mwenyewe .kama unavyotaka ww eti mungu amuue shetani ambae ndio huo mtihani alio wapa bina adamu ili kuwapima.


Alafu vijana WA siku hizi Wala hamna hamsomi visa vilivyopita kabla hili suala unaloleta ww lilishawai kuulizwa Enzo hizo za manabii na kama sikosei alikuwa NABII Musa.
 
Na hapohapo tunaambiwa hakuna wa kusujudiwa ila Mungu, iweje Mungu amuamuru Shetani kumsujudia Adam? Contradictions juu ya contradictions argghhh 😬😬😬
Hii ni kwamba alitaka kuonyesha malaika kwamba binadamu ni kiumbe bora zidi yao ...Ibilisi ndo alipogoma na kuona huyu kiumbe ana ubora gani sisi Mungu tunakuabudu leo hii tusujudie hili dongo ... Huyo dongo ntamkalia kila pande kama msalaba duniani ili asimuabudu Mungu na kusahau kuhusu Mungu.

Ni kweli binadamu ni mkubwa kwa vile angalia ni khalifah (kiongozi) wa vitu vyote duniani anaatawala
 
Ujuaji utakuponza
 
Mkuu huoni ni kipimo cha utii wa mema na mabaya? maana haiwezekani mwalimu wa chekechea akalipwa sawa na mwalimu wa chuo kikuu utalipwa kutokana na uelewa wako na ulivyotenda.
 
Nimesoma vizuri uzi huu changamoto kwamba auna elimu ya koroho ila umesoma sana theory. Watu wengi wanaopinga uwepo wa Mungu mmoja aliyeumba mbingu na nchi(Simaanishi wewe ila ni baadha ya watu) cha hajabu hao watu wengi ni madevil worshiped waabuduMashetani. Wanakataa uwepo wa Mungu lakini wanakubali uwepo wa shetani ambaye ndie baba yao.

Ukisoma Biblia kwa theory hasa Agano la kale utakuja kuona Mungu ni katili sana. Changamoto inakuja pale neno moja limetumika kwa maana tofauti tofauti kwenye biblia za kishwahili na kingeleza Tofauti ukisoma Biblia ya kiebrania utakuja kuona tofauti mkubwa sana hasa neno Mungu. Kwa asilimia kubwa agano la kale liliongozwa na malaika ndio walikuwa wakihitwa nano Mungu au Bwana,Yehofa au elohiym. Hata Musa mwenyewe hakukutana na Mungu bali alikutana na Malaika uso kwa uso.
Agano jipya kwa njia ya Yesu Kristo ndio aliyekuja kumfunua Mungu halisi katika tabia zake. Ndio maana ukisoma Agano jipya unakuja kuona Mungu ambaye siye katili na ni tofauti wa agano la kale katika Tabia ambazo kristo Yesu alivomfunua.
Tunaposema Yesu atumaanishi mwili bali ni roho ya Mungu iliyokuja kuvaa mwili wa kinadamu kwaiyo aijalishi angekuwa mweusi au mweupe lakini utabaki kua ni mwili tu.

Tunaposema Mungu ni Mungu mwenye haki wala yeye sio kigeugeu wala ajipingi wala kubadilika. Sio Mungu aliyluhusu watu wauwane au watu wawauwe wale wanaompinga yeye na kumkubali shetani.

Mungu aliwaumba wanyama na malaika pamoja na mbingu na nchi kwa ajiri ya kumiliki na kutawala binadamu only. Malaika aitwae Lucifer kabla ajawa shetani alikuwa ni malaika mwema tu aliyemfanya Mungu kwa ajiri ya kumtumikia binadamu lakini kwa utashi wa lusifa aliasi yaani alitoka kwenye nafasi yake ya kutumika kwa wanadamu bali yeye ndio alitamani atumikiwe na viumbe vingine kitu ambacho akiwezekani.

Binadamu pekee ndio aliyepewa uwezo mkubwa wa akili kuliko viumbe vyote. Ndiomaana hao malaika walioasi yaani walioacha wajibu wao wa kumlinda binadamu wanatumia hila kumlubuni binadamu lakini kiukweli hata hao waabudu mashetani ni wajinga na wapumbavu sanaaana wanawaabudu wafanya kazi wao.
Shetani anauwezo wa kutoa utajiri isipokuwa anatumia uwezo wa mwanadamu uwo uwo kukutengenezea wewe utajiri.

Kwaiyo ndugu mtoa uzi tafuta biblia na tafsiri za kiebrania, kiyunani na kigiriki ndio utakuja kupata majibu kamili.

Sent from my SM-A105F using JamiiForums mobile app
 
Hamna kufuru yoyote hapo sema imani yako ulivyo fundishwa ukiwa mtoto ndio inakupa fikra hizo. Ukweli ni kwamba Mungu na shetani ni pande mbili za sarafu moja. Mfano wake ni kama betri au kifaa cha kutunzia umeme lazima kuwe na positive na negative charge hivo hivyo ni kama mungu hawezi kuwepo bila shetani kwaiyo ni juu yako kuchagua unataka kwenda upande upi.
 
Hivi ulisha wahi kujiuliza kwanini wazungu wanagawa biblia bure, siyo tuu kugawa bali pia wametafsiri biblia kwa lugha zote mpaka za makabila yetu? Kwanini waarabu nao wanagawa misahafu au quran bure? Kwanini wasinge gawa na kutafsiri bure vitabu vya biolojia, kemia vitabu vya sayansi na hisabati? Usiamini sana hizo stori kaka wewe una uhakika huyo musa anakujua? Au musa atakusaidia nini ukifa kirefu cha biblia unakijua? Unajua hiyo biblia vitabu vingapi vimeondolewa na kwanini wameviondoa. Kuwa open minded kaka huyu mtu ameweka hii mada ili akukomboe ki fikra, emancipate yourself from mental slavery kaka
 
Na sisi inawezekana ni mifugo kwa viumbe wenye mamlaka juu yetu,,,na ndio maana wanachukua roho zetu na uhai kama sisi tunavyofanya kwa hao wanyama tulio na mamlaka juu yao,,,Duniani hapa na sisi ni mifugo kwa hao viumbe walio na mamlaka juu yetu
 
Na sisi inawezekana ni mifugo kwa viumbe wenye mamlaka juu yetu,,,na ndio maana wanachukua roho zetu na uhai kama sisi tunavyofanya kwa hao wanyama tulio na mamlaka juu yao,,,Duniani hapa na sisi ni mifugo kwa hao viumbe walio na mamlaka juu yetu
πŸ˜‚πŸ˜‚
 

Atamsujudiaje Adamu Wakati sheria inasema wakusujudiwa ni MUNGU pekee?

Nini kilimfanya akatae, je Mungu hakujua atakataa,
Au Mungu ndio aliweka kukataa ndani ya Shetani?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…