Haiwezekani Mungu asimuue Shetani halafu aamuru Watu waue wanaofanya mambo ya kishetani; Haiingii akilini

Mungu hayupo, hizo habari za kuwepo Mungu mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote na upendo wote ni hadithi za uongo kuridhisha wasiotaka kuhoji mambo kwa kina kimantiki.

Ukianza kuhoji kimantiki kidogo tu unagundua huyo Mungu katungwa na watu, tena kijingajinga tu.

Mungu ukishaingiza habari za mantiki hawezi akawepo.
Na hui ni Kutokana na upeo mdogo wa Akili zetu wanadamu hauwezi kujadili baadhi ya vitu hasa za MIUNGU.
 
Naona sasa watu wana anza kumwelewa Kiranga anaposema "Mungu hayupo"

Watu wanafunguka kiakili sasa, Ila mwanzoni walikuwa wabishi kweli[emoji23][emoji23]

Hapo kwenye hayupo bado sijafikia hitimisho, Kwa sasa Acha ibaki yupo,
Kiranga huenda yeye keshafikia Hilo hitimisho lakini Kwangu bado, na safari yangu ya Maisha sijui itanifikisha wapi.
 
Mungu hayupo, hizo habari za kuwepo Mungu mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote na upendo wote ni hadithi za uongo kuridhisha wasiotaka kuhoji mambo kwa kina kimantiki.

Ukianza kuhoji kimantiki kidogo tu unagundua huyo Mungu katungwa na watu, tena kijingajinga tu.
Watu wanafunguka kiakili sasa wana anza kuku elewa.

Walikuwa bado hawaja kua kiakili kuelewa Hoja zako za kutokuwepo Mungu..

Sasa wana anza kuelewa[emoji3][emoji3]
 
Hapo kwenye hayupo bado sijafikia hitimisho, Kwa sasa Acha ibaki yupo,
Kiranga huenda yeye keshafikia Hilo hitimisho lakini Kwangu bado, na safari yangu ya Maisha sijui itanifikisha wapi.
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] unahofia kwamba ukisema Hayupo kwa sasa huwezi kubarikiwa..

Siku ukitoboa kimaisha utakuwa Full Atheist ni swala la muda tu...
 
Mungu ukishaingiza habari za mantiki hawezi akawepo.
Na hui ni Kutokana na upeo mdogo wa Akili zetu wanadamu hauwezi kujadili baadhi ya vitu hasa za MIUNGU.
Unajuaje hawezi kuwepo kutokana na uwezo mdogo wa akili zetu, na si kwamba hawezi kuwepo kwa sababu hayupo tu?

Kwa kanuni yako hiyo, hata mimi naweza kukuambia mimi Kiranga wa JF ndiye Mungu mwenyewe, ila wewe huwezi kuelewa hilo tu kwa sababu uwezo wako mdogo wa kibinadamu haukuruhusu kuelewa.

Kwa kutumia kanuni yako hiyo utanibishiaje?

Itabidi ukubali kila ujinga, kwa maelezo kwamba 'kwa akili yako ndogo ya kibinadamu huwezi kuelewa".
 
HAIWEZEKANI MUNGU ASIMUUE SHETANI ALAFU AAMURU WATU WAUE WANAOFANYA MAMBO YA KISHETANI; HAIINGII AKILINI!

Anaandika, Robert Heriel
Kuhani

Kwenye nyumba za ibada tangu tukiwa Watoto tulifundishwa kuna Wahusika Wawili mahasimu, wakwanza anaitwa MUNGU na wapili anaitwa SHETANI.

Mhusika Mungu huyu tuliambiwa ndiye Muumbaji wa Mbingu na Nchi, na ndiye Baba yetu (Chanzo chetu). Huyu tukaambiwa pia ni Mwema, mwenye upendo, nguvu na uweza. Chanzo chake hatujaelezewa, na hata wanaotuelezea habari zake hawajawahi kumuona. Hii ni kumaanisha hawajui anafananaje.

Mhusika Shetani huyu amepewa uhusika mbaya Kwa kusemekana alimuasi Mhusika MUNGU, asili ya Shetani wapo waliosema ni Jamii ya Malaika waitwao Makerubi, ambaye jina lake ni Lucifer. Wakati wengine wakidai Shetani au Ibilisi asili yake ni Kutoka Koo za majinni. Hii ni kusema Shetani ni kiumbe kilichoumbwa na Mungu. Ingawaje Stori hizi mbili hazijakamilika na zinaacha maswali mengi kuliko kilichoelezwa.

Lusifa kama aliasi, aliasi sheria ipi miongoni MWA sheria za Muumba wake huko Mbinguni?

Kabla hajaasi hiyo sheria ilitamka kuwa adhabu ya kuasi ni ipi?

Stori za Shetani zimeanzia juujuu na kuishia juujuu kama Stori za masela WA vijiweni. Yaani Stori imeanzia Kati na kuishi katikati.

Tukirudi kwenye Hoja.
Wasimulizi WA hizi dini zakuletwa na Waandishi wa vitabu vyao ambavyo vimeandika habari za huyo Mungu na Shetani Kwa uchache Mno, wakaja na sheria, ni kama sheria za biashara ya Market zile za Qnet. Unawekeza Kwa Imani pasipo kuuliza maswali yenye kufikiri, ATI hivyo ndio namna ya Kupata faida kwenye biashara.

Vitabu vya Dini vinaeleza kuwa Shetani ndiye chanzo cha dhambi, inakazia zaidi kuwa kila dhambi ifanywayo na binadamu chanzo chake ni Shetani kwani Shetani ndiye anayeshawishi Watu au viumbe kufanya Uasi.

Ukisoma kwenye Quran au Biblia yapo Makosa MTU akifanya anatakiwa kuuawa kama adhabu.
Mfano WA Makosa hayo ni kama kuua, kuwa Shoga au msagaji, kulala na mnyama, kuzini na mama mzazi au Baba mzazi au mkwe au mtoto wako. Kumkufuru Mungu na kuwa mchawi au mshirikina. Na Makosa mengine mengi yenye kustahili adhabu ya kifo Kwa mujibu wa vitabu vya Dini.

Swali linakuja, Ikiwa mhusika Mungu wa kwenye vitabu hivyo vya Dini, aliamuru Watu kuwaua Watu wenzao wanaofanya Makosa au dhambi nzito kama zilivyotajwa, ni Kwa nini huyu Mungu asingeshughulika na Shetani mwenyewe ambaye ndiye anawafanya Watu WAUE, wawe mashoga, na kufanya zinaa chafu ya kiwango cha juu?

Kwa sababu kama kweli Mungu hakutaka Dunia iwe na uovu kama ni kweli Kabisa basi ni dhahiri angedili na chanzo ambacho vitabu vya Dini vinamtaja ni mhusika Shetani.

Haiingii akilini badala ya kumuua Shetani ambaye ndiye chanzo cha Watu kufanya uovu mkubwa, ATI uwaamuru hao Watu wawaue Watu wenzao wanaofanya Matendo ya kishetani yaani wanaomfuata Shetani ambaye wamezaliwa wamemkuta na watakufa watamuacha. Hakuna mantiki kabisa ya Jambo Hilo.

Nafikiri Vitabu vya Dini vinashindwa kueleza ukweli Kati ya huu;
1. Binadamu ndio Shetani wenyewe. Lakini wametafuta Shetani bandia asiyeonekana ili wamsingizie.
Hoja hii haina nguvu Kwa sababu Mwanadamu hawezi kupambana na Mungu au Shetani yaani hawezi kupambana na matamanio yake yaliyomo katika Akili yake. Kwani matamanio na utashi ndio humuongoza MTU.

2. Mungu na Shetani ni Mhusika mmoja. Yaani Mungu ndiye Shetani na Shetani ndiye huyohuyo Mungu.
Vitabu vya Dini vinashindwa kuelezea ukweli huu labda Kwa kuogopa kuyafanya Maisha yataonekana hayana maana. Jambo ambalo nikweli kuwa Maisha ni ubatili.

Kama Mungu ndiye muumba wa yote na muweza WA yote tafsiri yake Ipo wazi kabisa.
Hii ni kusema, Mungu hawezi kumuua Shetani Wakati yeye ndiye huyohuyo Shetani. Na Shetani hawezi kumuua Mungu Wakati yeye ndiye huyohuyo Mungu.

Hoja hii inanguvu Kwa sababu, hata vitabu vya Dini vinaeleza kuwa Mungu aliumba Mema na Mabaya (ushetani) lakini akamwambia Mwanadamu achague Mema ili aweze kuishi.

Kumaanisha upande mzuri au Mwema wa Muumbaji wetu ndio wanadini waliuita Mungu na upande Mbaya wa Muumbaji wetu wakauita Shetani. Ni kama vile USO na kisogo ambavyo vyote vipo Kwa mhusika mmoja.

Haiwezekani Lusifa Awe Muasi hivihivi, lazima tujiulize huo Uasi ulitoka wapi ikiwa sio Kwa Muumbaji wake? Kwa sababu kiumbe hakina uwezo wa kuumba Jambo lolote liwe zuri au liwe Baya.

Taikon pumzika sasa.

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Dar es salaam
Sijui ni Kitabu kipi kitakatifu unakizungumzia ila kwa biblia hakuna sehemu imeandikwa Shatani ni chanzo cha Dhambi hizi ni story za mitaani zinazofanana na ukweli lakini si ukweli
 
swali ni je kwnn mungu muweza wa yote amuumbe shetan na wkt alijua shatan atakuja kuw muasi
 
Wewe unasemaje mkuu, kwamba hakuna Mungu na chanzo chako ni nyani ambae umestaarabika?
 
Haya mambo ya rohoni yanasumbua sana
Ila ijulikane kwamba mambo yote yawe mema au mabaya huanzia rohoni

Nimekuacha kwa muda ila nitakua karibu nafuatilia[emoji28][emoji28][emoji28]
[emoji16][emoji16][emoji16][emoji16][emoji38]
 
SERIKALI HAIAMINI UCHAWI...
Hii ni kanuni Bora sana
[emoji2][emoji2][emoji2][emoji2]
 
Nitakujibu according to Christian theology which i believe is the only true theology, why i believe it to be true is a topic for another day.
About Lucifer
Lucifer kama walivyo malaika wengine wote jukumu lao lilikuwa ni kumtumikia Mungu na kumwabudu tu. They were created to do only that. Doing anything rather than obeying ni uasi mkubwa. Hapakuwa na haja ya written laws to show that he did wrong.
Unlike humans, angels and other heavenly beings have no hope for second chances. This is because humans may fail due to lack of faith because sometimes we cannot feel or see what we are supposed to believe in. God gives second chances to human because there is a possibility for them to know him and choose him. But what about angels? they live with God and commune with him on a day to day basis, they don't need faith in their life because they see God and His majesty everyday. So if they choose to rebel there is nothing that can change their minds. ONCE THEY REBEL AGAINST GOD THERE IS NO TURNING BACK.
So the question of aliasi kwa sheria ipi au iliandikwa wapi jibu ni kwamba Sheria zipo kwa viumbe wenye imani ndogo,waliokuwa kiimani hawahitaji sheria ziwaongoze. Since angels live with God they don't even need imani coz they are sure of God presence and they know who He is and what He desires from His creation. According to christian theology hata leo tuliookoka hatuongozwi kwa sheria bali kwa imani.(If you are a learned Christian iam sure you understand it)

Regarding Death Penalty
Again i will refer to the Christian theology which clearly it seems you are not familiar with. According to Christians theology which is bolded with the birth, death and resurrection of Jesus Christ the only emphasis is on love and forgiveness. The Bible teaches to forgive and pray for other people so that they can turn from their sinful life styles and surely not killing them. Go and take a look at the New Testament of the Holy Bible and you will see what i am trying to say here.

About allowing the Devil to exist and therefore Sins to exist
When God created the universe, He wanted His most valued creation to worship him willingly. Worshipping willingly requires to choose God first. Choice requires freedom and also requires options to choose from. Sin happen when we do not obey God, having ability of not obeying that's what we call freedom. This all comes down to the doctrine of FREEWILL.
Having this ability to choose is what makes us human. If we didn't have this ability we would have been like robots who are just programmed to respond to certain commands. GOD didn't want that. He wanted to be worshiped willingly.
In all this keep in mind that He created everything and he has put a choice in front of us and he made it very clear where every choice leads. His choice is simple choose Him and spend eternity with Him in Heaven or deny Him and spend eternity away from Him in Hell. Just as your short few years on Earth can earn you everlasting life the same short life can leads to everlasting torment. The scale is only fair. We can choose to put a finger on fire but we can't choose not to get burned. WE CAN CHOOSE WHAT TO DO BUT WE CAN'T CHOOSE CONSEQUENCES OF OUR ACTIONS.

About God being all powerful (OMNIPOTENCE OF GOD)
God has many attributes one of them is being all powerful but also Has many other attributes. God's wisdom exceeds all wisdom of man or anything created for that matter. Sometimes being powerful is allowing your enemy to exist so that your people can be able to choose. Remember a choice to obey or not to obey was there before even the snake lied to Eve and then Adam. The Devil came and inspired them not to obey but the choice was always there.

One final issue is about Sin. God didn't create Sin as many of you thinks. Sin is a by product of not obeying. Lets take this example, God created food to be eaten by man, but not eating will result to starvation. He didn't create starvation but starvation is a result of not taking food.
 
Hapo kwenye hayupo bado sijafikia hitimisho, Kwa sasa Acha ibaki yupo,
Kiranga huenda yeye keshafikia Hilo hitimisho lakini Kwangu bado, na safari yangu ya Maisha sijui itanifikisha wapi.
How about the existance of jesus christ, do you believe on it?
 
Nakuona moyo wako una uchungu kama nyongo, kwa uchungu huo moyo wako umejaa kufuru kwa kudhani kuwa kukufuru huko kutapunguza maumivu na uchungu wa moyo wako!! Unaikalia hukumu ya kutisha ya MUngu ambayo nafsi yako inajua kabisa kuwa unastahili hukumu!! Lakini nina habari njema kwa ajili yako!! ni kwamba YESU anakupenda na yuko tayari kukusamehe dhambi zako zote kama ukikubali kuja kwake na kutubu uovu wa moyo wako wote! Ukitubu na kumkaribisha Yesu kwenye moyo wako atakusamehe dhambi zako zote na ataingia moyoni mwako kama Bwana na Mwokozi wa maisha yako!! Atakupa furaha, amani na burudiko la moyo ambalo hujawahi kulipata japo umelitafuta sana!! Vinginevyo hayo makufuru utowayo kwa muumba wako hayatakusaidia siku ya hukumu ambayo dhamiri yako inakushuhudia daima kuwa unastahili hukumu!!

Kama uko tayari kutubu omba kwa dhati sala hii ya toba: Bwana Yes, naja kwako, mimi ni mwenye dhambi. Ninakuomba unisamehe dhambi zangu zote ninazozijua na nisizozijua, ninazozikumbuka na ambazo sizikumbuki. Tangu sasa namkataa shetani na kazi zake zote. Ninamkubali Yesu na kumkaribisha moyono mwangu awe Bwana na Mwokozi wa maisha yangu. Bwana Yesu naomba ulifute jina langu kwenye kitabu cha hukumu na uliandike kwenye kitabu cha uzima. Asante Yesu kwa kunisamehe na naomba unipe nguvu ya kuishi maisha matakatifu. Ninaomba katika Jina la Yesu-Amina..

Kama umeomba sala hiyo ya toba kwa moyo wa dhati, haya ndiyo maombi yangu kwa ajili yako: Baba katika Jina la Yesu Kristo, namleta kwako ndugu huyu aliyetubu mbele zako. Ninaomba mkono wako wa uweza umguse na damu yako ya thamani imwoshe dhambi zote. Namwombea rehema zako zilizo nyingi sana! Ninavunja nguvu za giza ndani yake kwa Jina la Yesu Kristo, na minyororo ya uovu iliyomtesa kwa miaka mingi ikatike na awe huru kukuabudu na kukutukuza. Yalinde maisha yake tangu sasa na ujidhihirishe kwake katika namna utakayoona vema. Ninaomba katika Jina la Yesu -Amina.

Nenda zako kwa amani na Mungu akubariki. Nakukaribisha kwenye kanisa la TAG (Tanzania Assemblies of God lililo karibu na wewe kwa msaada zaidi na mafundisho. Nenda kajitambulishe hapo na Mungu atakubariki!!
Kama Mungu angelikuwepo kweli bhasi tungelikiwa tushaweza Kummaliza. Totally
 
Back
Top Bottom