Haji Manara abubujikwa machozi akimuelezea aliyemtweza sababu ya rangi ya ngozi yake,asema anamuachia Mungu

Sikia, aliyemtweza kapatia anastahili tuzo.

Mi hufurahia sana kushuhudia mbabe yeyote akifikia hatua ya kukwamishwa na kupelekea hadi kulia kiuhalisia.

Huyo bwana kwa mdomo hawezekani na kama kawezekana, basi hasimu wake anastahili pongezi.

Ukipigana naye vita vya maneno ni lazima akudhalilishe tu ni fundi sana wa kuuchongoroa mdomo wake na ukisema umpige, umepiga mlemavu, umepiga albino unafungwa.

Sasa kuona leo naye mambo yamemgeukia kalizwa kwa kudhalilishwa, mambo yameenda vizuri, hapo ni win win stuation.

Huwa kama naangalia jambo lolote huegemeza huruma zangu kulinda haki za aliye upande wa mnyonge na huumizwa sana na ukandamizaji wa kibabe.

Hata kama naangalia documentary ya wanyama pori, huumia sana kuona mnyama mbabe akidhalilisha myama mwenziye anayeshindwa kujitetea!

Nikiona mdhalilishaji, mfano fisi ama simba kazingirwa kakamatwa anaanza kuliwa huku akipiga kelele, hujikuta nafarijika na kukazia macho kuangalia mpaka mwisho.

Ndiyo haya ya Manara, muosha kaoshwa.
 
Sijaelewa ni kwa nini watu wanadhani kumwita mtu zeruzeru ni tusi ila albino si tusi.

Kusema ana uzeru zeru inaonekana kuwa ni lugha ya kudhalilisha ila albinism ni sawa.

Kwa mtazamo wangu zeru zeru ni nzuri zaidi kwa kuwa ni kwa binadamu tu, wakati albino na albinism ni hadi kwa wanyama na mimea.

Sisi zeru zeru si maelezo ya udhaifu/upungufu bali ni maelezo ya muonekano wa mtu ila Albino na Albinism ni maelezo ya udhaifu ama upungufu.

Tunautukuza Sana uzungu.

cocastic
 
Nakazia, tena kwa herufi kubwa.
ZERU ZERU. πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…