Haki Huinua Taifa! Rais Samia kwa Kauli na Matendo ameonesha ni mtu wa Haki. Akitekeleza hili kama alivyosema, atabarikiwa, Tanzania itabarikiwa

Haki Huinua Taifa! Rais Samia kwa Kauli na Matendo ameonesha ni mtu wa Haki. Akitekeleza hili kama alivyosema, atabarikiwa, Tanzania itabarikiwa

Pascal Mayalla

Platinum Member
Joined
Sep 22, 2008
Posts
53,857
Reaction score
121,995
Wanabodi,
Kama kawaida yangu, huandika Makala za "Kwa Maslahi ya Taifa". Hii ni makala ya wiki hii, iliyotoka kwenye gazeti la Nipashe la Jumapili ya leo.
Screen Shot 2022-07-10 at 8.40.45 AM.png
Screen Shot 2022-07-10 at 8.41.09 AM.png

Karibuni.

Pasco
 
Samia anaweza kuwa na dhamira njema ya kuweka sheria zinazoleta usawa kwenye chaguzi, lkn kazungukwa na manyang'au yanayonufaika na hizi sheria kandamizi. Yatakubali?

Nasuburia kwa hamu kubwa mahojiano yako Pascal Mayalla na mhe Samia. Naamini maswali yako yatajikita kwenye masuala ya maslahi ya taifa tu na siyo kukijenga chama chako.
 
Hivi kwanini Pascal akimsifia mtu, mtu huyo huishia kufeli? Je, ana gundu?

Mfano:
Alianza na Lowassa
Akaja kwa Makonda
Akaja kwa Jiwe
Akaja kwa ...........

Sasa anajipenyeza kwa Hangaya 😃😃😃😃😃 (JUST JOKING)

 Kwa
hili la Samia kupenda haki naunga mkono amempita by far mtangulizi wake.
 
Kila kitabu na zama zake, hakuna cha kumpita mtangulizi wala huyu kafanya madogo au makubwa kuliko flani.

Hata nikichukua hiyo nafasi bado nitasifiwa na kusemwa kwa uzuri ni kwa sababu ni wakati wangu!.
 
Wahenga walisema 'Aisifiaye mvua imemnyea'. Bila shaka hata ndugu Pascal hajaandika makala hii kwa misingi ya methali hii ya wahenga.

Lakini alichokiandika ndugu Wakili mpya kiujumla mpaka sasa mama anatembelea madhaifu ya the great JPM ambayo yanawanufaisha wachumia tumbo wachache ambao wanaweza kuandika nyaraka mitandaoni. Lakini tunaofanya kazi huku vijijini bado mioyo ya wananchi ilishapandikizwa mbegu ya JPM ambayo kuikausha si rahisi.

Mama alisema hivi karibuni tutarudi uchumi wa kati, hiyo karibuni inaisha lini? Hapa ndo utajua record ya JPM ambayo wanatamani kuifuta kwa kutumia madhaifu yake lakini wananchi wanaojua alichokiacha baba.
 
Hivi kwanini Pascal akimsifia mtu, mtu huyo huishia kufeli? Je, ana gundu?

Mfano:
Alianza na Lowassa
Akaja kwa Makonda
Akaja kwa Jiwe
Akaja kwa ...........

Sasa anajipenyeza kwa Hangaya 😃😃😃😃😃 (JUST JOKING)

 Kwa
hili la Samia kupenda haki naunga mkono amempita by far mtangulizi wake.

Ni kweli kabisa Samia ni mpenda haki, ila iwapo kipimo cha haki itakuwa ni Magufuli tu. Lakini kutenda haki kama haki bado yuko kwenye level ya chini.
 
Heheheh endelea kupiga mapambio sie hatuna habari😂😂😂!!!

Kwa kifupi tu sio rahisi mtu kukata tawi la mnazi alilokalia, hizo ni ngonjera amabazo tushazizoea angeliongea hilo Magufuli ningewaza pengine kuna jipya ila sio huyo msambaza asali wenu.
 
Bimkubwa kachemka kinoma , kupanga kununua vichwa chakavu vya treni kwenye mradi mpya wa matrilioni ni ujinga wa karne! wanaomuuzia wanamdharau na kumcheka kwa ujinga huo!

Simple logic, vichwa vipya vichache tu vitapiga kazi kubwa regularly nenda rudi mwanzo mwisho na vitanunua hizo vichwa chakavu ila vichwa chakavu havitaleta pesa ya kununua vichwa vipya sababu ya kushinda karakaana daily for maintenance!

Mengine namkubali sana Bimkubwa!
 
Back
Top Bottom