Haki Huinua Taifa! Rais Samia kwa Kauli na Matendo ameonesha ni mtu wa Haki. Akitekeleza hili kama alivyosema, atabarikiwa, Tanzania itabarikiwa

Samia anaweza kuwa na dhamira njema ya kuweka sheria zinazoleta usawa kwenye chaguzi, lkn kazungukwa na manyang'au yanayonufaika na hizi sheria kandamizi. Yatakubali?
Mkuu Sexless, kikawaida hao manyang'au huwa wanakwenda na tempo ya rais aliyepo madarakani, hivyo watabadilika.
Nasuburia kwa hamu kubwa mahojiano yako Pascal Mayalla na mhe Samia. Naamini maswali yako yatajikita kwenye masuala ya maslahi ya taifa tu na siyo kukijenga chama chako.
Rest assured tunaposema ni kwa maslahi ya Taifa, we mean Maslahi ya Taifa na sio Maslahi ya Chama.
P
 
Kwa upande wangu mimi nafurahi sana kuona mama ameweza kwenda na siasa za kizazi kilichopo sasa.
Na sio siasa zile za kishamba na kikoloni.
 
Hivi kwanini Pascal akimsifia mtu, mtu huyo huishia kufeli? Je, ana gundu?.

Mfano:
Alianza na Lowassa
Akaja kwa Makonda
Akaja kwa Jiwe
Akaja kwa ...........
Duh...!. Ila japo una joke lakini inafikirisha!.
Sasa anajipenyeza kwa Hangaya 😃😃😃😃😃 (JUST JOKING)
Hapa unanionea bure!.
angalia terehe za haya mabandiko, aliyesifiwa ni Nani na lini na leo ni Nani! Siku ya Wanawake Duniani: Je, tuna Wanawake wenye sifa za Presidential Material? na hapa Siku ya Wanawake Duniani: VP Samia Suluhu: "Womanly, Genuine, Humble, Simple na Down To Earth!” na hapa "Watu waachwe Huru kuujadili Muungano"- VP, Samia Suluhu Hassan. Huyu mama anaongea vizuri kwa Unyenyekevu mpaka raha. Huchoki kumsikiliza

 Kwa hili la Samia kupenda haki naunga mkono amempita by far mtangulizi wake.
Tawire.
P
 
Kila kitabu na zama zake, hakuna cha kumpita mtangulizi wala huyu kafanya madogo au makubwa kuliko flani.

Hata nikichukua hiyo nafasi bado nitasifiwa na kusemwa kwa uzuri ni kwa sababu ni wakati wangu!.
Naunga mkono hoja, kila zama na Zama zake, zama zile zimepita, twende na zama zilizopo.
P.
 
Sijaona cha maana zaidi ya kumsifia, SS anapita njia ile ile kama waliomtangulia, ila kwa ujanja na mbinu nyingine.
Hakuna ubaya wowote kumsifia mtu yoyote as long as ni sifa za kweli and she is doing great!.
P
 
Ukiweza kupamba maua kadiri iwezekanavyo ili watu wasifie eneo lako fanya hivyo na inawezekana ukapata kipato kwa wapita njia kutaka kupigia picture hapo.
☝🏾
That's!.
naunga mkono hoja
P
 
Eti, mkuu Pascal. Nikuulize swali. Unafikiri utulivu wa nchi hii kwa sasa ni kwa hisani ya nani na nini!?
Mkuu blogger, asante kwa swali zuri. Kwanza tutofautishe hisani na wajibu, hisani ni vitu vinavyofanywa kwa favours na sio wajibu. Mfano wewe unawajibika kwa matunzo ya familia yako ikiwemo chakula, mavazi, malazi etc huo ni wajibu wako, kutimiza wajibu wako is not favours, its a responsibility. Ila kutokana na hali yako ukiamua badala ya kuwanulia mkate wewe utanunua keki, mayai na sausages for breakfast, hapo ndio umefanya hisani, au umeamua kununua chakula na kumgawia na jirani yako.

Usalama, amani na utulivu is a responsibility and it's not a favour, ni wajibu na jukumu la kila mtu to maintain that.

Hivyo ili nchi iwe na Amani na utulivu, piece and tranquility kuna vyombo vya kuhakikisha hilo na kuna viongozi wa kusimamamia hilo, hivyo whoever responsible for this ni wajibu wake na sio hisani.
P
 
Wahenga walisema 'Aisifiaye mvua imemnyea'. Bila shaka hata ndugu Pascal hajaandika makala hii kwa misingi ya methali hii ya wahenga.
Mkuu Mbekenga , asante kwa hili,
Lakini alichokiandika ndugu Wakili mpya kiujumla mpaka sasa mama anatembelea madhaifu ya the great JPM ambayo yanawanufaisha wachumia tumbo wachache ambao wanaweza kuandika nyaraka mitandaoni.
JPM hakuwa malaika so does Mama, hivyo sii kweli kuwa anatembelea madhaifu ya mtangulizi, bali Mama anarekebisha makosa yaliyofanyika huko nyuma.
Lakini tunaofanya kazi huku vijijini bado mioyo ya wananchi ilishapandikizwa mbegu ya JPM ambayo kuikausha si rahisi.
Hakuna yeyote anayetaka kuikausha mbegu yoyote iliyopandwa na yeyote.
Mama alisema hivi karibuni tutarudi uchumi wa kati, hiyo karibuni inaisha lini?
Hivi karibuni ni neno relative la kuashiria muda, linalofuata kanuni za relativity kutegemeana na muktadha husika. Hivi karibuni ya siku ni few days, hivi karibuni ya weeks ni few weeks, hivi karibuni ya months ni few months, hivi karibuni ya years ni few years, hivyo hivi karibuni ya kutengemeza uchumi wa kati ni few years. Na kuna Ile hivi karibuni ya centuries and centuries ya kumsubiria "atakapo rudi Mwana wa Adamu", tunaambiwa "kesheni mkiomba kwa maana hamjui siku".
Hapa ndo utajua record ya JPM ambayo wanatamani kuifuta kwa kutumia madhaifu yake lakini wananchi wanaojua alichokiacha baba.
Naendelea kusisitiza hakuna yeyote anayetamani kuifuta record ya yeyote.
P
 
Unatafuta uteuzi, huchoki tu! Rubbish!
Sitafuti uteuzi wowote!, for what?!. Ushauri wangu wa bure kwako, next time ukikutana na rubbish, just ignore and move forward, don't stop and waste your precious time to read rubbish and reply. Time is money, save your precious time, save your money!.
P
 
Ni kweli kabisa Samia ni mpenda haki, ila iwapo kipimo cha haki itakuwa ni Magufuli tu. Lakini kutenda haki kama haki bado yuko kwenye level ya chini.
Tuwe na shukrani kwa madogo ili tutendewe makubwa!. Safari ni hatua, na lazima uanzie chini mdogo mdogo kuenenda huku aki gain momentum, tutafika, Kwa mwendo huu alioanza nao, atabarikiwa na Tanzania Itabarikiwa.
P
 
Nani atampa kesi lofa huyu
Kwanza asante kuniita lofa! kwasababu kwa sasa hapa nilipo mimi ni lofa kweli, ila ulofa sio kitu permanent, mtu anaweza kuwa lofa leo, na kesho akawa sio lofa, halafu wewe ambaye leo sio lofa, bali unawaita wengine ma lofa, kesho wewe ndio unaweza kuwa lofa au hata...!. Heshima ya mtu itokane na mchango wake kwa jamii na sio kutumia vigezo vya ulofa.

Sio kila wakili ni wakili mtafuta kesi. Nimemaliza LL.B UDSM, 2007, sijawahi kuomba kuwa wakili. Hata huu uwakili wangu sio uwakili wa kusubiria kupewa kesi. Uwakili wangu ni more strategic than kwenda mahakamani.
P
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…