HAKI JINAI: Inachohitaji Afrika ni viongozi waaminifu na sheria zisizopendelea

HAKI JINAI: Inachohitaji Afrika ni viongozi waaminifu na sheria zisizopendelea

kavulata

JF-Expert Member
Joined
Aug 2, 2012
Posts
13,778
Reaction score
14,214
Hakuna demokrasia inayoweza kuletwa kwa magunia kutoka sehemu nyingine kwenda sehemu nyingine. Hakuna demokrasia inayopatikana kwa mazungumzo bali kwa uhalisia wa mambo. Mfano, China wako karibia watu bilioni 2 chini ya matawala mmoja, serikali moja na nchi moja, ni demokrasia gani inafaa kwenye mazingira ya aina hiyo?

Afrika ina watu wengi ambao hawana elimu kubwa, maskini sana, miundombinu mibovu, chakula kidogo, hospitali chache na techologia hafifu. Je, ni aina gani ya demokrasia inayofaa katika mazingira ya aina hii?

Demokrasia inamtofautisha vipi kati ya mzalendo na kibaraka, mkweli na muongo, mwenye nia mbaya na nia njema, adui na rafiki, ukweli na propaganda?

Je, demokrasi ni kumshawishi mtu mwingine ambae hana tatizo akubaliane na wewe kuwa ana tatizo? Yaani mtu anaetaka kuandamana anapita mitaani kuwaambia watu wengine wamuunge mkono waandamane?

Unavyotakiwa kuishi vitatokana na vile ulivyozaliwa, ulivyolelewa, unavyokula, mnavyooanana, mnavyolima, mnavyofuga, mnavyosaidiana, nk. Je, kumlazimisha mtoto asiyetaka kwenda shule aende shule ni demokrasia?

Mtoto kuzaliwa na mzazi masikini au mwenye sura asiyoipenda, au kupewa jina bila idhini yake ni demokrasia gani? Nani kanipa mimi jina la Kavulata bila idhini yangu mimi? Nani alikubatiza bila kukuuliza?

Ndugu zangu, sisi binadamu na hata wanyama na viumbe wengine hawaahitaji demokrasia ya kuletewa bali wanahitaji mfumo ambao haubagui uwe mzuri au mbaya lakini unatenda vilevile kwa watu wote kulingana na mazingira yao, umri, jinsia, hali ya afya yake, nguvu zake alizonazo, akili yake, hekima zake, uzuri wake, eneo alipo, sababu za kufanyiwa, nk. (Survival of the fittest).

Ulaya na Marekani wana aina ya demokrasia ambayo sio demokrasia bali mifumo ya maisha yao ilisababisha itokee vile.

Yaani walipigana sana kupita kiasi, walidhulumiana sana kupita kiasi, waliuana sana kupita kiasi, walibaguana sana kupitiliza, walikerana sana kupitiliza, wengine walitajirika sana na wengine wakawa masikini sana hadi maisha yalikuwa magumu sana hadi wakafikia enough ikawa enough kweli, watu wakaacha woga wakapambana hadi wakafikia equilibrium.

Sisi waafrika tatizo letu la msingi sio ukosefu wa demokrasia au haki, bali tuna tatizo la viongozi wezi, waio waadilifu na wanaotenda kazi kwa kupendelea.

Shida yetu kubwa sisi kwa sasa ni kupata hwea safi, maji, chakula, nyumba, na mavazi. Kisha tunahitaji usafiri, matibabu na elimu bora, kisha tunahitaji masoko huru na uhakika ya kuuzia bidhaa zetu, kisha tecnolojia na uwezo wa kuvunia rasilimali zetu zote kikamilifu.
 
Back
Top Bottom