Haki ya Mungu nimejikuta namkumbuka Magufuli ghafla tu

Kuna watu watakuja hapa watakwambia wewe ni sukuma gang.
 
Jibu swali kwa nini hakusema ni mkopo akasema ni pesa za ndani stupid
Kaangalie hotuba zake , alikuwa anasema fedha za ndani pamoja na mkopo , ila mama anajenga shule kwa mikopo , je fedha za ndani zinafanya kazi gan?
 
Kaangalie hotuba zake , alikuwa anasema fedha za ndani pamoja na mkopo , ila mama anajenga shule kwa mikopo , je fedha za ndani zinafanya kazi gan?
Niangalie hotuba za nani?bora kuangalia mpira au mieleka ila sio uongo wa yule jamaa
 
Sio rahisi akatokea kama Magufuli
 
Kwenye maeneo mengine yote ukitoa siasa nilimpenda! Sana na ninamkumbuka sio siri!
Ila kwenye siasa hapana
 
Personally simkubali Magufuli Ila pamoja na yote haimaanishi kwamba hajawahi kufanya mambo mazuri ambayo nimeweza kuyakubali.

Magufuli jambo la kwanza na la muhimu akirudisha nidhamu ya kazi kwa watumishi wa umma na kuhakikisha kwamba fedha za umma zinatumika ipasavyo pamoja sasa alikuwa hajui nini kiwe kipaumbele na kipi aache alikuwa anasoma kila kitu bila hata plan.

Nidhamu ya kazi kwa watumishi wa umma umeanza kuzorota siku Hadi siku kwakweli hii inasikitisha sana.

Tunaweza kujikuta kwenye kukusanya Kodi na mapato matrilioni kwa trillions Ila Kama Ile nidhamu alivyoweka Magufuli hatutaiendeleza basi itakuwa kazi bure.

Rais wa Sasa anaweza kujenga madarasa mengi Ila Kama nidhamu ya kuyatunza haitakuwepo na kuwandisha vijana wetu kwa moyo wa kizalendo basi itakuwa kazi bure kabisa.

Lazima tukubali kuendeleza mazuri ya viongozi waliopita, yale yenye mapungufu turekebishe .
 
Mpaka mkiri....
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…